Monday, October 31, 2011

NHC yatiliana saini ya makubaliano ya mikopo ya nyumba na benki saba za hapa nchini

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba nchini, Nehemiah Mchechu akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kutiliana saini ya makubaliano baina ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Mabenki ili kuwezesha kutoa mikopo ya Nyumba kwa wananchi hapa nchini. Hafla hii imefanyika leo kwenye hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Nyumba Tanzania, Injinia Kesogukewele Msita akihutubia katika hafla hiyo.
Waziri wa Ardhi, Profesa Anna Tibaijuka akihutubia wakati wa hafla ya kutiliana saini ya makubaliano baina ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Mabenki ili kuwezesha kutoa mikopo ya Nyumba kwa wananchi hapa nchini. Hafla hii imefanyika leo kwenye hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Tanzania,Nehemiah Mchechu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB,Mark Wiessing wakitiliana saini ya makubaliano kuwezesha kutoa mikopo ya Nyumba kwa wananchi hapa nchini .Waliosimama wakishuhudia tukio hilo ni Waziri wa Ardhi, Profesa Anna Tibaijuka na Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Nyumba Tanzania,Eng Kesogukewele Msita. Hafla hii imefanyika leo kwenye hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence Mafuru akisoma hotuba yake fupi kwa niaba ya Mabenki ya hapa nchini wakati wa hafla ya kutiliana saini ya makubaliano baina ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Mabenki ili kuwezesha kutoa mikopo ya Nyumba kwa wananchi hapa nchini .hafla hii imefanyika leo kwenye hoteli ya Hyatt Kilimanjaro,jijini Dar es Salaam.

Warioba amtembelea Pinda ofisini kwake

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu,Jaji Joseph Sinde Warioba kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Oktoba 31,2011. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

APPOINTMENT OF DR. MARINA A. NJELEKELA AS EXECUTIVE DIRECTOR OF MUHIMBILI HOSPITAL




DR. MARINA A. NJELEKELA

This is to inform the general public that the Muhimbili National Hospital Board of Trustees has appointed Dr. Marina Aloyce Njelekela as the Executive Director of the Hospital with immediate effect. Before her appointment, Dr. Njelekela was a Senior Lecturer and Head of the Department of Physiology at the Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS).

Dr. Njelekela has worked with MUHAS since 2001 and prior to that, she had worked at Kisarawe District Hospital as a Medical Officer and at the Muhimbili Orthopaedic Institute (MOI) as a Registrar until 1998 when she went for further studies in Japan.

Dr. Marina Njelekela holds a Doctor of Medicine Degree from the Univeristy of Dar es Salaam, and a PhD in Human and Environmental Studies from Kyoto University, Japan. Her area of specialization was Pathogenesis of Lifestyle Related Diseases in Developing countries.

As a team player, Dr. Marina Njelekela led the Medical Women Association of Tanzania (MEWATA) for six years. During her two terms as a MEWATA leader, she was in the forefront of health awareness among women and the general public, especially on Breast Cancer Awareness and Screening Campaigns that were conducted in Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Mtwara, Lindi, Dodoma, and Manyara.

She is also well known for her role in advocacy campaigns and has brought to light the real extent of the problem of breast and cervical cancers in Tanzania that led to significant improvement on the prevention and management of Cancers in the country.

Dr. Njelekela sits on various Boards, including the Aerial Glaser Paediatric AIDS Healthcare Initiatives (AGPAH) and Management Development for Health (MDH). She is a recipient of various awards in academia and social services, including the prestigious Martin Luther King Drum Major Award for Justice that was bestowed on her by the US Embassy in January 2010 for her efforts to improve women’s access to health care services.

Safari Miss Vodacom Tanzania 2011 katika Fainali za mrembo wa Dunia

Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa Tatu kutoka kulia akifurahia kwa Shangwe wakati wa Highland Games kuelekea kinyang'anyiro cha Mrembo wa Dunia
Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa kwanza kushoto aliye simama akiwa katika picha ya pamoja na wenzake

Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa Pili kutoka kulia akiwa anapiga Chiazi na wenzake .. katika safari ya kuelekea kumtafuta Mrembo wa Dunia.
Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa pili kutoka kulia akiwa Edinburgh Castle hivi karibuni katika safari ya kuelekea katika mashindano ya kumsaka Mrembo wa Dunia.
Miss Vodacom Tanzia 2011 Salha Israel aliye vaa Nguo za Njano katika Mazoezi ya nguvu kabisa wakati wa maandalizi ya shindano la Miss World Tanzania
Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa Kumi kutoka kulia akiwa na wenzake katika Dina la nguvu Huko Scottish maeneo ya Scottish Hydro.
Hapa Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa kwanza kushoto akiwa katika Vazi la Ufukweni na Wenzake katika maonesho ya Mavazi hayo hapo jana.
Kwa picha zaidi Tembelea: www.fredynjeje.blogspot.com

Saturday, October 15, 2011

HAJI RAMADHANI AKWAA USHINDI BSS, ANYAKUA MILIONI 40



Mshindi wa shindano la Bongo Star Search Second Chance 2011, Haji Ramadhani (katikati), akipunga mkono kwa mashabiki zake mara baada ya kutangazwa mshindi kwenye kinyang'anyiro hicho (kushoto), ni Mratibu wa mashindano hayo Rita Paulsen 'Madame Rita' akiwa katika pozi mara baada ya kumtangaza mshindi huyo, kulia ni mwakilishi kutoka Tigo ambao walikuwa wadhamini wakuu wa shindano hilo.
Habari na picha zaidi hebu cheki hapo chini
http://uniqueentertz.blogspot.com/2011/10/haji-ramadhani-ndiye-mshindi-bss.html

UDSM campus assumes new name

By Florence Mugarula
The Citizen Reporter

Dar es Salaam. The University of Dar es Salaam (UDSM) has decided to rename Mlimani Campus Mwalimu JK Nyerere in honour of Tanzania’s first PresidentThe move is a gesture to mark the 50th anniversary of the university, according to the UDSM vice chancellor, Prof Rwekaza Mukandala.

He said yesterday that the decision to rename Mlimani is also in recognition of Mwalimu Nyerere’s contribution towards the higher learning institution’s development. He told journalists in the city that it was the former president who selected the location of the UDSM way back in 1961.

Prof Mukandala said the new name will be officially used from October 21, this year, four days before marking the 50th birthday of the oldest university in the country.

“We are doing this in recognition of Mwalimu Nyerere’s contribution to the academic arena. This campus was known as Mlimani campus and now we have decided to rename it after the Father of the Nation, which brings more meaning to what he did,” said Prof Mukandala.

The university was established on October 25, 1961, two months before the country’s independence, starting with the faculty of law, as an affiliate of the University of London.It was later called the University College Dar es Salaam (UCD), as a constituent college of the University of East Africa (UEA). The UDSM was established in 1970.

Commenting on challenges facing it, Prof Mukandala said it was going to construct seven buildings that will have lecture rooms, offices and laboratories so that students may get quality education in a conducive environment. He said the UDSM would construct hostels capable of providing accommodation to 4,500 students and that their tenders have been already announced.

“We are planning to build hostels to minimize the problem of accommodation at the campus. The construction will be in three phases, and for each we will construct enough hostels to accommodate 1,500 students each,” said Professor Mukandala.

Meanwhile, the president of UDSM graduates, retired Judge Joseph Warioba, asked former UDSM students to attend a dinner which will be prepared by President Jakaya Kikwete next Tuesday to raise funds for the construction of a students’ centre at the campus.He said Uganda’s President Yoweri Museveni, who graduated from the UDSM in 1970, was also assisting to raise funds in his country. He asked members of the public to support the idea.

“I ask all wananchi to contribute to this University; we need to do more for the future of our children and Tanzania at large,” said Judge Warioba.He said the university was facing a lot of challenges, such as lack of enough lecture rooms, workers’ residential houses, students’ hostels and other important infrastructure.

Added Judge Warioba: “ The students’ centre is going to cost at least Sh17 billion. So far we have collected Sh5 billion and we look forward to reach all UDSM graduates through various means so that we succeed in this project.”

It was established that the number of students has increased from 14,000 to more than 20,000. Hostels at the campus accommodate less than 4,000 and the rest live outside it.

link

http://www.thecitizen.co.tz/news/4-national-news/16107-udsm-campus-assumes-new-name

Thursday, October 13, 2011

Prince Charles Kutembelea Tanzania



THE PRINCE OF WALES AND THE DUCHESS OF CORNWALL TO TOUR COMMONWEALTH AND GULF COUNTRIES
The British Government has asked The Prince of Wales and The Duchess of Cornwall to undertake official visits to South Africa and Tanzania from 2nd November to 9th November 2011 at the invitation of President Zuma and President Kikwete. The Prince of Wales will also visit Gulf countries on 31st October and 1st November. In Kuwait HRH will celebrate the 50th anniversary of Independence and 20th anniversary of liberation as the guest of the Amir and the Crown Prince. The Prince of Wales will stop briefly in Qatar for discussions with the Emir before departing for the Commonwealth countries.
Their Royal Highnesses’ Commonwealth tour will focus on trade and investment promotion to support Britain’s economic recovery and strengthen the economies of our partners; employment opportunities and development issues; education and practical support for disadvantaged young people; sustainability issues in the run-up to the Durban Climate Summit later in November; and shared heritage and conservation of traditional livelihoods and wildlife. In Tanzania the Royal visit will be part of the celebrations for the 50th anniversary of Independence. Bilateral ties including economic cooperation will also be to the fore in Kuwait and Qatar.
In both Commonwealth countries there will be a strong focus on The World Wildlife Fund’s (WWF) work to protect endangered species and fragile ecosystems. The Prince of Wales has recently become President of WWF UK. In South Africa Their Royal Highnesses will visit the Mandela Foundation in Johannesburg to see the legacy of former President Mandela.
The work of the Department for International Development (DFID) will assume particular prominence in South Africa and Tanzania given the UK Government’s commitment to the development of both countries.

JK aongoza mazishi ya Penza

Mzee Athumani Janguo akimzika rafiki yake mzee Penza leo jioni
Mwenyekiti wa mkoa wa Shinyanga Khamisi Mgejja akimzika bwana Penza

Nape Nnauye akishiriki katika Mazishi ya Penza
Rais Kikwete akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Juma Penza jioni hii
Waombolezaji wakiwasili kwenye makaburi ya kisutu kwaajili ya maziko ya mkongwe huyo
Rais Kikwete akiwa na wajukuu wa marehemu Juma Penda kwenye makaburi ya Kisutu jioni hii

********************

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, jioni ya leo, Alhamisi, Oktoba 13, 2011 ameungana na waombolezaji kumzika mwanahabari mkongwe, Ndugu Juma Fugame Penza katika makaburi ya Kisutu, mjini Dar es Salaam.

Ndugu Juma Penza alifariki dunia usiku wa kuamkia leo kwenye Hospitali ya Hindu Mandal, Dar es Salaam akiwa na umri wa miaka 63.

Marehemu Penza ambaye amekuwa katika tasnia ya habari kwa karibu miongo minne iliyopita na miongoni mwa walioshiriki mazishi yake katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam ni pamoja na viongozi waandamizi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) alichokifanyia kazi kwa zaidi ya miaka 20.

Katika salamu za rambirambi ambazo Mheshimiwa Rais Kikwete amempelekea Katibu Mkuu wa CCM, Mheshimiwa Wilson Mukama na kupitia kwake kwa familia na ndugu wa marehemu, Mheshimiwa Rais amemwelezea Hayati Penza kama mwandishi wa habari aliyefanya kazi zake kwa weledi na uzalendo akiongozwa na misingi imara ya taaluma yake na uzalendo kwa nchi yake.

“Nilimfahamu binafsi Ndugu Penza wakati tulipofanya kazi pamoja katika Chama cha Mapinduzi. Hakuna shaka kuwa Marehemu Penza aliitumia taaluma yake ipasavyo, akiongozwa na weledi wa kazi hiyo na uzalendo kwa nchi yake. Kamwe, hakupata kutumia ujuzi wa kazi yake kugawa wananchi kwa misingi ya aina yoyote ile.”

Katika maisha yake, marehemu Juma Fugame alishikilia nafasi za uandamizi katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni pamoja na kuwa Kaimu Mhariri wa Mazageti ya Serikali ya Daily na Sunday News, Kaimu Mkuu wa Shirika la Habari Tanzania (SHIHATA) kabla ya kujiunga na utumishi wa CCM.

Katika utumishi huo, Marehemu Penza alipata kuwa Mwandishi wa Habari wa Katibu Mkuu wa CCM, Mzee Rashid Mfaume Kawawa ambaye pia ni marehemu, Mwandishi wa Habari wa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Mzee John Malecela, Mkurugenzi wa Redio Uhuru na Afisa Mwandamizi wa masuala ya habari na vyombo vya habari katika makao makuu ya Chama.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,DAR ES SALAAM.

13 Oktoba, 2011



Monday, October 03, 2011

JK, Museveni kuharakisha ujenzi wa reli ya Tanga-Musoma-Uganda

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni muda mfupi kabla ya kuanza mazungumzo ikulu jijini Dare s Salaam leo mchana.Rais Museveni yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja (Picha zote na Freddy Maro)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere leo mchana kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
************
TANZANIA na Uganda zimekubaliana kuharakisha ujenzi wa reli ya Tanga-Musoma-Uganda ili kuhitimisha ndoto ya miaka mingi ya Mwanzilishi wa Taifa la Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ilieleza kuwa hayo ndiyo yalikuwa maamuzi makuu yaliyofikiwa jana, katika mkutano kati ya Rais, Jakaya Kikwete na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Nchi hizo mbili pia zimekubaliana kupanua bandari za Tanga na Musoma katika Tanzania, na kujenga bandari mpya nchini Uganda ili kuhudumia reli hiyo mpya kati ya nchi hizo mbili.

Rais Museveni ambaye amefanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini Tanzania aliwasili jana asubuhi na kupokea na mwenyeji wake Rais Kikwete kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Kiongozi huyo wa Uganda ameondoka kurejea nyumbani baada ya mazungumzo na mwenyeji wake.

Wakati wa mazungumzo yao, viongozi hao wawili wamekubaliana kuharakisha ujenzi wa reli hiyo kama njia ya kufungua mlango wa tatu wa Uganda kupitishia bidhaa zake kutoka na kwenda kwenye Bahari ya Hindi. Milango mingine inayotumiwa na Uganda kusafirisha bidhaa kutoka na kwenda Bahari ya Hindi ni bandari za Dar es Salaam na Mombasa, Kenya.

Katika kuhakikisha uamuzi wake wa kuharakisha ujenzi huo unaanza katika muda mfupi iwezekanavyo, viongozi hao wawili wameunda kikosikazi cha kusimamisha suala hilo. Kikosi kazi hicho kitaundwa na mawaziri wa wizara za usafirishaji na uchukuzi, fedha na mambo ya nje kwa kila nchi.

Chini ya mpango huo, bidhaa zitasafirishwa kwa reli kutoka Bandari ya Tanga hadi Bandari ya Musoma na kuwekwa kwenye pantoni maalum ya (wagon ferry) reli kutoka Bandari ya Musoma hadi bandari mpya ya Uganda kwa kuvushwa Ziwa Victoria.

Viongozi hao wamefanya uamuzi wa kuharakisha ujenzi huo kwa sababu ya faida za reli hiyo kwa chumi za nchi zote mbili lakini pia kwa kujua kuwa bila usimamizi wa karibu wa Tanzania na Uganda itachukua miaka mingi zaidi kwa reli hiyo kuweza kujengwa.

Wazo la kujenga reli ya kuunganisha Uganda na Bandari ya Tanga kupitia Bandari ya Musoma liliasisiwa miaka mingi tokea awamu ya kwanza ya uongozi wa Tanzania, lakini kwa namna moja ama nyingine, utekelezaji wa wazo hilo umekumbana na changamoto mbalimbali.

Katika mkutano wao wa leo, viongozi hao pia wamejadili masuala mengine yanayohusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili na masuala mengine ya kikanda na kimataifa.
SOURCE: IKULU

Kafumu atangazwa mshindi Igunga

Msimamizi wa uchaguzi Protace Magayane akimpongeza Dk Dalaly Kafumu baada ya kumtangaza na kumkabidhi cheti cha ushindi wa ubunge wa Jimbo hilo.
Wanachama na wapenzi wa CCM, wakifurahia ushindi wa chama hicho katika Uwanja wa Sokoine Igunga jana baada ya msimamizi wa uchaguzi wa uchaguzi kumtangaza mgombea wa chama hicho kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga jana. Picha na Emmanuel Herman.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza mgombea wa Ubunge kupitia (CCM) Dk Dalaly Kafumu kuwa mshindi wa kiti cha Ubunge wa Jimbo la Igunga, kufuatia uchaguzi mdogo uliofanyika juzi Jumapili.

Kafumu ameshinda kiti hicho kwa kupata kura 26,484 kati ya kura 52,487 halali zilizopigwa, sawa na asilimia 50.4 ya kura hizo, akiwashinda wenzake saba wa vyama vingine ambao pia walishiriki uchaguzi huo.

Msimamizi wa uchaguzi huo, Protase Magayane alimtaja mshindi wa pili katia kinyang’anyiro hicho kuwa ni Joseph Kashindye wa Chadema aleyapata kura 23,260 sawa na asilimia 44.3 akifuatiwa na mgombea wa CUF, Leopold Mahona aliyepata kura 2,104 sawa na asilimia 4.

Wagombea wengine walioshiriki uchaguzi huo na vyama vyao kwenye mabano ni Steven Mahuyi (AFP) aliyepata kura 235, Hassan Rutegama (Chausta) aliyepata kura 182, Said Cheni DP kura 76 na Hemed Ramadhani (SAU) kura 63.

Hata hivyo, CCM kimefanya vibaya katika jimbo la Igunga ikilinganishwa na uchaguzi wa mwaka jana wakati mgombea wake aliyeshinda, Rostam Aziz alipopata ushindi wa kura 35,674 sawa na asilimia 72.7 ya kura halali zilizopigwa.

Rostam aliyejiuzulu nafasi ya ubunge na kutoa nafasi ya kufanyika kwa uchaguzi wa juzi, alimshinda aliyekuwa mgombea wa CUF, Mahona ambaye alipata kura 11, 321 sawa na asilimia 23.1 ya kura halali. Mahona mwaka huu kura zake zimeshuka kwa asilimia 19 ikilinganishwa na matokeo hayo ya mwaka jana.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...