JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIABUNGE LA TANZANIA | ||
Simu Na. 022 2112065 Fax Na. (255) 022 2112538 E-mail: tanzparl@parliament.go.tz (Barua zote za kiofisi ziandikwe kwa (KATIBU WA BUNGE) Unapojibu tafadhali taja: | Ofisi ya Bunge S.L.P. 9133 DAR ES SALAAM |
Kumb. EB.155/172/01/300 31 Mei, 2011
YAH: WANAHABARI KWA AJILI YA BUNGE LA BAJETI
____________________
Tunayo furaha kukujulisha kuwa, Mkutano wa Nne wa Bunge la kumi la Jamhuri ya Muungano wa
Ofisi ya Bunge kila mara imekuwa ikitamani kupata toka kwako Wanahabari wenye uzoefu na uelewa wa kutosha juu ya masuala ya Bunge zikiwemo kanuni na taratibu zinazotawala chombo uendeshaji wa chombo hiki.
Aidha, ili kuwa na uratibu mzuri wa shughuli za utoaji Habari za Bunge, mwaka 2008 Wanahabari waliamua kuunda umoja wao kwa ajili ya kuwaunganisha katika shughuli hizi. Umoja huo uitwao Bunge Press Association of Tanzania (BUPAT) pamoja na mambo mengine unalenga kuwajengea uwezo Wanahabari na uwelewa mpana wa masuala ya Bunge.
Ni nia ya Ofisi ya Bunge kuuendeleza umoja huo ili hatimaye kujenga kada ya Wanahabari waliobobea katika utoaji wa Habari za Bunge. Katika kutekeleza azima hii, ofisi inaandaa mpango wa mafunzo utakaojumuisha semina, warsha na ziara za mafunzo katika Mabunge mbali mbali kwa Wanahabari husika.
Ni kwa misingi hiyo basi tumeona ni vyema tukapata ushirikiano wako katika hili na hivyo kukuomba kuwa kuanzia sasa unapoteua Wanahabari kwa ajili ya kwenda Bungeni wakidhi vigezo vifuatavyo:
- Wawe wamehudhuria Mikutano angalau mitatu
- Wawe na Press card inayotolewa na Idara ya Habari – Maelezo
- Wawe nadhifu, waadilifu na wenye nidhamu
Tunatanguliza shukurani zetu za dhati kwa ushirikiano wako katika jambo hili.
Pamoja na salaam toka ofisi za Bunge.
J.S. Mwakasyuka
Kny: KATIBU WA BUNGE
No comments:
Post a Comment