Friday, January 30, 2026

RAIS SAMIA AMEJIPANGA KUFIKISHA UMEME VITONGOJI VYOTE




📌Bilioni 24.9 kupeleka umeme vitongoji 218 Njomb

📍Njombe

Imeelezwa kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameelekeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kufikisha umeme kwenye vitongoji vyote vilivyobakia nchini ambavyo bado havina huduma ya umeme ifikapo mwaka 2030.

Hayo yamebainishwa leo Januari 30, 2026 na Bw. Frank Mugogo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mha. Hassan Saidy wakati wa hafla fupi ya kumtambulisha mkandarasi kutoka kampuni ya Central Electricals International Ltd katika Mradi wa HEP 2B ambaye anaenda kutekeleza kwenye vitongoji 218 mkoani Njombe.

"Jumla ya vitongoji vyote mkoa wa Njombe ni 1,833 na vitongoji vyenye umeme ni 1,276. Vilevile vitongoji ambavyo havina umeme ni 557. Hivyo mradi huu unakwenda kupeleka umeme kwenye vitongoji 218 katika mkoa huu na vitabakia vitongoji 339 ambavyo havina umeme navyo vitakamilika, " Amesema Bw. Mugogo.

Ameongeza kuwa, gharama za kuunganisha umeme huo ni shilingi 27,000 tu na kuwataka wananchi wa mkoa huo kutumia fursa ya kuunganisha umeme kwa gharama nafuu iliyowezeshwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe.Rais Samia.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo mkoani Njombe, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Bw. Lewisi Mnyambwa amemshukuru Rais Samia kwa kuleta fedha nyingi zaidi ya bilioni 24 ili kupeleka umeme kwenye vitongoji vya mkoa wa Njombe.

"Serikali kupitia REA imefanya kazi kubwa. Tunasisitiza miradi hii ikamilike kwa muda uliopangwa na tutaendelea kuusimamia ipasavyo ili mkandarasi aweze kutekeleza majukumu yake pasipo changamoto yeyote katika kipindi chote cha utekelezaji wa mradi," Amesema Mnyambwa. 

Aidha, ametoa rai kwa wananchi wanaozunguka eneo la mradi kumpatia ushirikiano mkandarasi huyo na ametakiwa kutoa kipaumbele cha ajira kwa wazawa ili kufanya shughuli mbalimbali katika mradi huo ili uchumi wa wananchi uongezeke na wanufaike na uwepo wa miradi hiyo katika mazingira yao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Miradi kutoka kampuni ya Central Electricals International Ltd, Bw. Zameer Meghji ameishukuru Serikali kupitia REA kwa kupewa fursa ya kutekeleza mradi huo mkubwa. Amesema watahakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati, watashirikiana na wananchi na kutoa kipaumbele cha ajira kwa wazawa ili miradi hiyo ilete tija kwa wananchi na nchi kwa ujumla.

WITO KWA WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO KUCHANGAMKIA FURSA YA MIKOPO YA SERIKALI YENYE RIBA NAFUU



 

NGORONGORO SAKO KWA BAKO NA TAASISI ZA ELIMU KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII NA KUIMARISHA ELIMU YA UHIFADHI

 





Monduli, Arusha – Januari 30, 2026

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imeendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuwa mstari wa mbele katika kulinda rasilimali za asili na kuandaa kizazi kijacho chenye uelewa wa kina kuhusu uhifadhi endelevu, kupitia kampeni maalum ya utoaji elimu ya vivutio vya utalii na masuala ya uhifadhi kwa taasisi za elimu zilizopo Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha.

Katika kampeni hiyo iliyofanyika leo, NCAA ilikutana na wanafunzi pamoja na walimu kutoka Shule za Sekondari Manyara, Lowasa, Rift Valley pamoja na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Mto wa Mbu, ambapo washiriki walipata fursa ya kujifunza kwa kina kuhusu thamani ya kipekee ya Hifadhi ya Ngorongoro, mchango wake kwa uchumi wa taifa, na wajibu wa jamii katika kuilinda kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, mwakilishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro alisema kuwa lengo kuu la kampeni hiyo ni kujenga uelewa, uzalendo na hisia za umiliki miongoni mwa vijana kuhusu rasilimali za asili, hususan vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, ambalo ni miongoni mwa maajabu ya dunia yanayotambuliwa kimataifa.

“Ngorongoro si urithi wa Tanzania pekee, bali ni urithi wa dunia. Ili uendelee kudumu, ni lazima vijana waelewe thamani yake mapema na washiriki kikamilifu katika juhudi za uhifadhi,” alisema.

Kupitia mawasilisho, majadiliano na maswali ya wazi, wanafunzi walielimishwa kuhusu aina mbalimbali za vivutio vya utalii, ikiwemo Crater ya Ngorongoro, wanyamapori adimu, urithi wa kihistoria na kiutamaduni, pamoja na mchango wa utalii katika kuongeza mapato ya taifa na kuboresha huduma za kijamii.

Aidha, elimu ya uhifadhi iligusia masuala ya matumizi endelevu ya rasilimali, athari za uharibifu wa mazingira, mabadiliko ya tabianchi, na umuhimu wa jamii kushirikiana na taasisi za uhifadhi katika kulinda mazingira yao.

Walimu na wanafunzi walipongeza hatua hiyo ya NCAA, wakieleza kuwa elimu waliyoipata itaongeza motisha kwa vijana kuzingatia masomo yanayohusiana na mazingira, utalii na uhifadhi, sambamba na kuwa mabalozi wazuri wa kutunza mazingira katika jamii zao.

Mwalimu mmoja kutoka Shule ya Sekondari Lowasa alisema kampeni hiyo imewawezesha wanafunzi kuona uhifadhi si dhana ya darasani pekee, bali ni jukumu la kila mwananchi.

“Hii ni elimu inayogusa maisha ya kila siku. Wanafunzi wetu sasa wanaelewa kuwa kulinda mazingira ni kulinda maisha yao ya baadaye,” alisema.

Kupitia kampeni hii, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inaendelea kuimarisha uhusiano wake na taasisi za elimu, ikilenga kuandaa kizazi chenye maarifa, maadili na uwajibikaji katika kulinda na kutangaza vivutio vya utalii na rasilimali za asili za Tanzania.

Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati mpana wa NCAA wa kuwekeza katika elimu, uhamasishaji wa jamii na ushirikishwaji wa vijana kama nguzo muhimu ya uhifadhi endelevu na maendeleo ya sekta ya utalii nchini.

FURSA MPYA KWA VIJANA: BILIONI 2 KWA WATENGENEZAJI WA MAUDHUI



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda, amesema Wizara imepatiwa kiasi cha TZS bilioni 2 itakayowawezesha watengenezaji wa maudhui mbalimbali mitandaoni kuimarisha kazi zao na kuwaongezea kipato kupitia majukwaa ya kidijitali.

Amesema hayo Januari 29, 2026 jijini Dodoma na kubainisha kuwa, fedha hizo zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa lengo la kuyawezesha makundi yote ya watengeneza maudhui ikiwemo katika Sekta ya Utalii, Michezo, Habari, Jamii, Muziki, Filamu na sanaa nyinginezo. 

Amebainisha kuwa, zoezi la uandikishaji wa walengwa linaanza rasmi Januari 30 hadi Februari 15, 2026, ambapo watengenezaji wa maudhui wanatakiwa kufika katika ofisi za Halmashauri za Wilaya, Manispaa za Miji na Majiji kupitia vitengo vya habari, ili kuchukua na kujaza fomu za maombi, zikiainisha taarifa binafsi pamoja na shughuli wanazozifanya.

Thursday, January 29, 2026

MSAJILI WA HAZINA AZINDUA MPANGO MKAKATI WA NMB 2026-2030

Mwandishi wa OMH

Dar es Salaam. Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, amezindua Mpango Mkakati wa Muda wa Kati wa Benki ya NMB wa mwaka 2026 hadi 2030 (Agenda 2030).

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo unaolenga kuboresha utendaji kazi wa benki hiyo, Bw. Mchechu aliupongeza uongozi wa NMB na Bodi ya Wakurugenzi kwa kuifanya benki hiyo kuwa miongoni mwa benki bora zinazochangia kwa kasi ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

Alisema kuwa katika kipindi cha miaka mitano, Serikali, inayomiliki asilimia 31.8 ya hisa za NMB, imepata Sh670 bilioni kutokana na uwekezaji wake katika benki hiyo, ambapo kati ya kiasi hicho, Sh224 bilioni ni gawio.

Sanjari na hilo, aliipongeza Benki ya NMB kwa kuoanisha vipaumbele vyake na maono ya Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, hususan katika maeneo ya afya, elimu, ujasiriamali na mazingira.

Katika kusisitiza umuhimu wa mwelekeo huo wa maendeleo, Bw. Mchechu alisema anatamani kuona taasisi zote nchini, ikiwemo za sekta binafsi, zikioanisha mikakati yao na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. 

Alitaja Benki ya NMB kuwa mfano wa taasisi inayotekeleza mwelekeo huo kupitia utendaji wake wa kifedha na usimamizi makini wa mikopo.

“Benki ambayo imekuwa ikitoa wastani wa mikopo ya Sh5.6 trilioni kwa mwaka halafu inakuwa na wastani wa mikopo chechefu wa asilimia 2.5 ni kitu cha ajabu sana, hongereni sana NMB,” alisema.

Aidha, aliwataka wateja na wawekezaji kuendelea kuiamini na kupata huduma kutoka Benki ya NMB, akisisitiza kuwa ni sehemu salama kwa kuwekeza fedha zao.





WAFANYABIASHARA MSIWAUMIZE WANANCHI-DKT. MWIGULU





WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka wafanyabiashara nchini kutowaumiza Watanzania kwa kupandisha bei za bidhaa hususani kipindi hiki cha kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja na mfungo wa Kwaresma kwa kuwa nchi kwa sasa haina upungufu wa chakula.

Amesema licha ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) nchini kutangaza kuwepo kwa upungufu wa mvua katika maeneo mengi nchini lakini nchi inautoshelevu wa chakula hivyo hakuna sababu ya kupandisha bei za vyakula.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi, Januari 29, wakati akijibu swali la Nancy Nyalusi, Mbunge wa Viti Maalum katika kipindi cha Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu. Mbunge huyo alitaka kujua Serikali imejipangaje kuhakikisha nchi inakuwa na utoshelevu wa chakula na kuzuia mfumuko wa bei kuelekea kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Kwaresma.

“…Kwa sasa tunachakula cha kutosha, mahitaji ya chakula cha akiba kwa nchi ni takribani tani 150,000 na sasa nchi ina zaidi ya tani 400,000 za akiba ya chakula rai ambayo niliitoa hata nilipokutana na wakuu wa mikoa ni kuendelea kuwahamasisha wananchi  kuzingatia ushauri wa aina ya mazao ya kupanda.”

Pia, Waziri Mkuu amewaelekeza Wakuu wa Mikoa yote nchini wawaelimishe wananchi kuendelea kutumia vizuri chakula walichonacho kutokana na tahadhari ya upungufu wa mvua iliyotolewa na TMA. “Wananchi watunze chakula na kuwa na matumizi ya lazima tu, ili kuweza kuwa na akiba.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameielekeza Wizara ya Afya kuzingatia viwango rasmi vya gharama za huduma na kuharakisha mpango wa kutunga sheria itakayoweka viwango vinavyofanana nchini kote, ili kuondoa hali ya baadhi ya maeneo kuwa na viwango tofauti.

Ametoa maelekezo hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Ushetu, Emmanuel Cherehani ambaye alitaka kupata kauli ya Serikali kuhusu viwango wanavyotozwa wananchi kama gharama ya kumuona daktari ambaye ni mwajiriwa na analipwa mshahara na Serikali.

Waziri Mkuu amesema kwa mujibu wa utaratibu wa Taifa wa Bima ya Afya kwa Wote, wananchi wanahimizwa kujiunga na mifumo ya bima ili kupunguza changamoto ya kuchangia gharama wanapohitaji huduma hospitalini.

Waziri Mkuu amefafanua kuwa makundi yaliyoainishwa kisheria kama watoto chini ya miaka mitano, wajawazito, wazee na wenye magonjwa ya mlipuko yanaendelea kupata msamaha wa kuchangia gharama hizo.

Kuhusu changamoto ya mifumo hospitalini, Waziri Mkuu amesema Serikali itafuatilia kwa karibu ili kuondoa uzembe na visingizio vinavyochelewesha wagonjwa, huku taasisi husika zikielekezwa kurekebisha mapungufu ya kimfumo kwa kuwa huduma za afya hazipaswi kusubiri.

RAIS SAMIA AZINDUA MPANGO MKAKATI WA KISAYANSI WA KUJENGA UMAHIRI WA KUSOMA, KUANDIKA NA KUHESABU





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezindua Mpango Mkakati wa Kisayansi wa Kujenga Umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK), unaolenga kuboresha msingi wa elimu kwa watoto nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Rais Samia amesema mpango huo umeandaliwa kwa kutumia ushahidi wa kisayansi na uzoefu wa kitaalamu, ukiweka mkazo katika mbinu bora za ufundishaji, ufuatiliaji wa maendeleo ya wanafunzi, pamoja na kuwajengea walimu uwezo wa kitaalamu unaoendana na mahitaji ya sasa ya elimu.

Ameeleza kuwa umahiri wa kusoma, kuandika na kuhesabu ni nguzo muhimu ya maendeleo ya elimu na taifa kwa ujumla, akisisitiza kuwa watoto wanaopata msingi imara wa KKK hujifunza kwa ufanisi zaidi katika ngazi za juu za elimu na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Mpango huo pia unatarajiwa kuongeza usawa wa fursa za elimu, kupunguza ufaulu duni wa wanafunzi wa elimu ya awali na msingi, na kuchochea maendeleo endelevu kupitia elimu jumuishi na yenye ubora.

Mhe. Dkt. Samia, ameshiriki kucheza pamoja na kikundi cha ngoma za asili cha wanafunzi wa Shule ya Msingi Kisutu mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), jijini Dar es Salaam, tarehe 29 Januari, 2026.

Uzinduzi wa mpango huo unaakisi dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuwekeza katika elimu kwa vitendo, kwa misingi ya Kazi na Utu, ili kujenga rasilimali watu yenye maarifa, ujuzi na maadili kwa maendeleo ya Taifa.

#KaziNaUtuTunasongaMbele
#ElimuBoraKwaWote
#MaendeleoEndelevu
#Siku100ZaSamia

MKUTANO WA CATA UANGAZIE MIJADALA YA KUHAMASISHA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA UKUSANYAJI MAPATO - MAKAMO WA RAIS

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amesema matumizi ya mifumo ya kisasa ya teknolojia ni chachu kati...