Monday, October 31, 2016

ZIARA YA WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI KATIKA MRADI WA SAFARI CITY ARUSHA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Vangimembe Lukuvi akikagua mojawapo ya nyumba zilizojengwa na NHC katika eneo la Matevez maarufu kama #SafariCity, Kulia kwake ni Meneja wa NHC mkoa wa Arusha, James Kisarika, Waziri Lukuvi alitembelea mradi huo kujua maendeleo ya utekelezaji wa eneo hilo la kitovu cha mji cha #Safaricity.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Vangimembe Lukuvi akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoani Arusha. Waziri Lukuvi alitembelea mradi huo kujua maendeleo ya utekelezaji wa eneo hilo la kitovu cha mji cha #Safaricity.

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Vangimembe Lukuvi akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoani Arusha. Waziri Lukuvi alitembelea mradi huo kujua maendeleo ya utekelezaji wa eneo hilo la kitovu cha mji cha #Safaricity.

Afisa Mauzo wa Shirika la Nyumba Mkoani Arusha, Gibson Mwaigomole akitoa maelezo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Vangimembe Lukuvi aliyetembelea mradi huo kujua maendeleo ya utekelezaji wa eneo hilo la kitovu cha mji cha #Safaricity.

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Vangimembe Lukuvi aliyetembelea mradi huo kujua maendeleo ya utekelezaji wa eneo hilo la kitovu cha mji cha #Safaricity akizungumza jambo na Meneja wa NHC Arusha Kisarika.


 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Vangimembe Lukuvi akikagua mojawapo ya nyumba zilizojengwa na NHC katika eneo la Matevez maarufu kama #SafariCity, Kulia kwake ni Meneja wa NHC mkoa wa Arusha, James Kisarika, Waziri Lukuvi alitembelea mradi huo kujua maendeleo ya utekelezaji wa eneo hilo la kitovu cha mji cha #Safaricity.

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Vangimembe Lukuvi aliyetembelea mradi huo kujua maendeleo ya utekelezaji wa eneo hilo la kitovu cha mji cha #Safaricity akizungumza jambo na Meneja wa NHC Arusha Kisarika.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Vangimembe Lukuvi aliyetembelea mradi huo kujua maendeleo ya utekelezaji wa eneo hilo la kitovu cha mji cha #Safaricity akipata maelezo ya mradi kutoka kwa Meneja wa NHC Arusha Kisarika.

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Vangimembe Lukuvi aliyetembelea mradi huo kujua maendeleo ya utekelezaji wa eneo hilo la kitovu cha mji cha #Safaricity akizungumza jambo na Meneja wa NHC Arusha Kisarika.

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Vangimembe Lukuvi aliyetembelea mradi huo kujua maendeleo ya utekelezaji wa eneo hilo la kitovu cha mji cha #Safaricity akipata maelezo ya mradi kutoka kwa Meneja wa NHC Arusha Kisarika.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Vangimembe Lukuvi akikagua mojawapo ya nyumba zilizojengwa na NHC katika eneo la Matevez maarufu kama #SafariCity, Kulia kwake ni Meneja wa NHC mkoa wa Arusha, James Kisarika, Waziri Lukuvi alitembelea mradi huo kujua maendeleo ya utekelezaji wa eneo hilo la kitovu cha mji cha #Safaricity.

Friday, October 28, 2016

TUMIENI MISIKITI KUHUBIRI MISINGI YA UISLAMU-MAJALIWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya Sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Nunge mjini Dodoma Oktoba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Meya wa manispaa ya Dodoma, Jafar Mwanyemba na Sheikh Shabaan Kitila baada ya Sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Nunge mjini Dodoma Oktoba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam baada ya Sala ya Ijumaa kwenye msikiti wa Nunge mjini Dodoma Oktoba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Nunge mjini Dodoma Oktoba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika Dua ya kuwaombea wanafunzi wote wa Tanzania wanaotarajia kufanya mtihani wa Kidato cha Nne ili wafanye vizuri akiwa katika Sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Nunge mjini Dodoma Oktoba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………………………………………….. 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Waislamu watumie nyumba za ibada kuhubiri uislamu na misingi yake. 

Ametoa wito huo leo mchana (Ijumaa, Oktoba 28, 2016) wakati akishiriki sala ya Ijumaa katika msikiti wa Nunge mjini Dodoma. 

Amesema dini ya Kiislam inafundisha kwamba sala ndiyo msingi mkubwa unaopaswa kufuatwa na kila muumini hivyo ni lazima wafanye ibada kwa wakati. 

“Nasisitiza kwamba wote tutumie muda wetu vizuri pamoja na mambo mengine tufanye ibada kwani dini inatuekeza kuwa sala ndiyo msingi mkubwa kwenye Uislamu. Tunayo kazi ya kuimarisha misingi ya dini kwa kutumia nyumba za ibada,” amesema. 

Waziri Mkuu amesema Waislamu wana jukumu la kufundisha watoto wao na kuhakikisha wanakua kwenye imani na kujengeka katika maadili mema. 

“Dini inajenga maadili mema kwa mtoto na hata mtu mzima. Pia dini inajenga misingi ya uvumilivu na inamuwezesha mtu kumtambua Mwenyezi Mungu. “Tuendelee kuwafundisha vijana wetu umuhimu wa kushiriki kikamilifu kwenye masuala ya kidini ili wakikua waweze kuiendeleza kwa vizazi vijavyo,” amesema. 

Waziri Mkuu ambaye ametumia fursa hiyo kujitambulisha kwa waumini wenzake wa mkoa wa Dodoma baada kuhamia rasmi, ameahidi kutoa ushirikiano kwao na pia amewaomba wampe ushirikiano ili aweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo. 

“Nimekuja kujitambulisha. Mimi ni kijana wenu, ndugu yenu. Nimekuja Dodoma rasmi nyumbani na kikazi. Naomba mnipokee na naamini katika kipindi chote nitakachokuwa hapa nitapata ushirikiano nanyi na pia nitawapa ushirikiano,” amesema. 

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliwaomba waumini hao wawaombee dua wanafunzi wa kidato cha nne ambao wanatarajia kuanza mitihani ya kuhitimu Novemba Mosi, mwaka huu ili waweze kufaulu. 

Waziri Mkuu amewaomba waumini hao waendelea kuwaombea viongozi wa kitaifa wakiongozwa na Rais Dk. John Magufuli ili waweze kutekeleza vizuri majukumu yao na kufikia malengo yanayotarajiwa na wananchi. 

Aidha, Waziri Mkuu amechangia sh. milioni moja kwa ajili ya kuendeleza mradi wa ujenzi wa zahanati katika msikiti huo. Miradi inayojengwa na waumini wa msikiti huo kwa sasa ni zahanati, madarasa ya shule ya awali na shule ya ufundi.

CHAMA CHA MAPINDUZI CHAWAJIBU WAPINZANI WAKE, UZUSHI WA MITANDAONI

Ndugu Christopher Ole Sendeka, Msemaji wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa akizungumza kwenye mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo tarehe 28/10/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam. 

…………………………………………………………. 

Kwa muda sasa kumekuwepo na usambazaji wa taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa wakishirikiana na baadhi ya vyombo vya habari zinazolenga kukejeli, kudhihaki, kukatisha tamaa, kubeza na kudhoofisha jitihada zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi na Serikali zake katika kuleta maendeleo kwa Watanzania. 

Kumekuwepo na makala zinazoandikwa na magazeti mawili ya nje ambazo hutolewa kila baada ya miezi miwili na ambazo zinapotosha na kuandika habari zisizo za kweli kuhusu Tanzania. 

Pia, yapo magazeti mawili ya ndani ambayo yamekuwa yakitoa makala mfululizo kwa kila wiki zinazolenga kumchafua Mheshimiwa Rais na kuichafua taswira ya nchi yetu. 

Tumesikitishwa na waandishi wa makala hizo walioamua kujivua uzalendo na kushiriki mpango wa kuiharibu heshima na taswira ya nchi yetu kwa maslahi ya maadui zetu wa nje na baadhi ya wanasiasa. Tunafuatilia kujua nini kinawasukuma kufanya hivyo na kwa maslahi ya nani ilhali sote ni Watanzania. Je ni tamaa ya madaraka tu au mengine? Hakuna anayepinga ukosoaji bali unapaswa uwe ukosoaji wenye nia njema kwa nchi. 

Mtakumbuka hivi karibuni aliyewahi kuwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa, alisambaza taarifa kwa vyombo vya habari aliyoiita ya tathmini ya mwaka mmoja baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015. 

Katika taarifa yake hiyo, alidai kuwa alileta msisimko mpya katika siasa za Tanzania, kwamba ameshirikiana na wenzake kuionyesha nchi yetu maana ya demokrasia na kukosoa juhudi za serikali na wateule wa Rais. 

Demokrasia kimsingi ni dhana inayohusisha ushiriki na kuheshimu mawazo ya wengi katika kufikia uamuzi. Ikiwa maana halisi ni hii, tunajiuliza ni ipi demokrasia aliyoionyesha Lowassa ambayo leo anajisifu kuwa nayo? 

Tulishuhudia akiwa mgombea urais wa chama ambacho hakijui, hakushiriki kukijenga wala kutoa mchango wowote unaompa hadhi ya kupeperusha bendera huku katiba na kanuni ya chama hicho ikivunjwa. Kidemokrasia, anayepewa fursa ya kupeperusha bendera ya chama chochote makini duniani ni kiongozi au mwanachama aliyethibitika kwa imani na matendo, kuzielewa, kuzitekeleza, kuzitetea falsafa, itikadi na malengo ya msingi ya chama hicho. Mgombea ni taswira halisi na alama muhimu inayoakisi dhamira ya chama husika machoni kwa wananchi


Demokrasia ya kweli lazima ianzie ndani ya chama, ni demokrasia ipi iliyotoa mamlaka kwa vyama vinavyounda UKAWA kuwanyima wanachama wao haki ya kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera za vyama walivyoviasisi, kuvitetea, kuvigharamia na walivyovitumikia kwa kuamua kumteua mgombea “MTUNGUO” (ambaye hajapimwa wala hajawahi kuvipigania). Kitendo hicho cha kutowashirikisha wanachama na kuwanyima haki yao ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa kilidhihirisha usaliti wa hali ya juu wa misingi ya demokrasia. 

CHADEMA watuambie njia iliyotumika kuwapata wabunge wa viti maalumu. Ni demokrasia gani inayotoa fursa kwa baadhi tu ya viongozi kuteua wabunge ambao wanakiwakilisha chama chote. Ambapo kila kiongozi aliteua maswahiba zake na wengine kwa ugeni wao ndani ya CHADEMA walikosa watu wanaowafahamu na kuamua kuwateua wanawake maswahiba wao ndani ya CCM. Msingi wa kawaida wa kupata wabunge wa viti maalum ukiacha kura za maoni, kigezo kingine muhimu ni mchango wa mgombea/mwanachama huyo katika kukijenga na kukitumikia chama chake. Yaliyotokea kwa CHADEMA kwenye wabunge wake wa viti maalum ni mapya kwenye ulimwengu wa demokrasia. Inahitaji wataalamu wa sayansi ya siasa kufanya utafiti wa aina hii mpya ya demokrasia. 

Tulidhani baada ya mwaka mmoja kupita, wenzetu hawa wangelikuwa wamejifanyia tathmini, kujikosoa, kujisahihisha na hata kufanya uungwana wa kuwaomba radhi wanachama wao kwa uvunjifu mkubwa wa misingi ya demokrasia, katiba na kanuni za vyama vyao. 

Tunatoa wito kwa vyama vya siasa nchini kutochukulia kwa wepesi masuala ya demokrasia na mabadiliko, yasiwe ni nyimbo za kuburudisha au kutoa matumaini hewa kwa wanachama na wananchi. Kanuni mojawapo ya demokrasia ndani ya vyama ni lazima ionekane katika muundo wake na katika utekelezaji wa muundo huo. 

Umefika wakati vyama vya siasa vinapaswa kujifunza kuuza sera ili kujijenga na sio kusubiri matukio kwa ajili ya kupata huruma ya wananchi. Tunasubiri kushuhudia na kusikia demokrasia itakavyoendeshwa katika uchaguzi wa ndani wa vyama hivyo ambapo kuna taarifa mmoja wa vigogo amefanikiwa kupata kiasi cha dola milioni 15 zitakazomsaidia kupanga safu yake ya uongozi. 

Katika kutimiza mpango huo, tayari yapo mawasiliano ya mara kwa mara ya baadhi ya viongozi wakitoka Zanzibar na sehemu zingine za nchi kuja Dar es Salaam, na imeonekana dhahiri mazungumzo yao kutowashirikisha viongozi wenzao waandamizi kwani yanalenga kufanikisha mpango huo. 

Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli, ameendela kufanya juhudi kubwa katika kuijenga nchi kwa kuimarisha utendaji na nidhamu ya utumishi serikalini, kukusanya mapato na kusimamia matumizi sahihi ya fedha, kupambana na kuzuia mianya ya rushwa pamoja na kusimamia haki, usawa na wajibu kwa raia. Mwenzetu anayaona haya kuwa ni kuufanya utumishi wa umma kaa la moto. 

Juhudi hizi na nyinginezo ikiwemo ununuzi wa ndege mpya, ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, afya kwa kununua vitanda vya wazazi, kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari na nyinginezo hazipaswi kukatishwa tamaa kwa maslahi ya wachache, ni vyema kuziunga mkono kwa maslahi ya taifa letu. 

Katika kipindi hiki cha mwaka mmoja wa Rais Dk. Magufuli madarakani, CCM inawaomba wananchi kuendelea kumuunga mkono katika dhamira yake safi ya kuwaondolea kero, kuboresha huduma za jamii na kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii. 

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI 

Imetolewa na;- 

CHRISTOPHER OLE SENDEKA 

MJUMBE WA NEC NA MSEMAJI WA CCM 

28/10/2016.

WAZIRI PROFESA MBARAWA AZINDUA BODI YA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA JIJINI DAR ES SALAAM


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati), akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo.
Kaimu Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Fortunatus Kapinga, akizungumza kuhusu shirika hilo, kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Haruni Kondo, kuzungumza wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya shirika hilo jijini Dar es Salaam leo.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Kaimu Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta, Fortunatus Kapinga, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya shirika, Dk. Haruni Kondo.
Mameneja wa Shirika la Posta Tanzania, wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya shirika hilo.
Baadhi ya wajumbe wa bodi mpya ya Shirika hilo, wakiwa katika uzinduzi wa bodi hiyo.
Baadhi ya wajumbe wa bodi mpya wakiwa katika uzinduzi wa bodi hiyo.
Meneja Mkazi Zanzibar wa shirika la Posta, Mwanaisha Saidi (katikati), Meneja wa Huduma za Barua, Fadya Zam (kulia) na Meneja Utumishi wa shirika, William Makumba (kushoto), wakiwa katika uzinduzi wa bodi hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia matukio mbalimbali katika uzinduzi wa bodi hiyo.
Baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta wakiwa katika uzinduzi wa Bodi mpya ya Shirika hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo, akitoa maelezo mafupi kuhusu bodi hiyo mpya pamoja na shirika hilo kwa jumla kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati), kabla waziri Mbarawa hajaizindua rasmi bodi hiyo. Kushoto Ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo (Mawasiliano), Profesa Faustine Kamuzora.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, (Mawasiliano), Profesa Faustine Kamuzora, akitoa hutuba yake kabla ya kumkaribisha Waziri wa wizara hiyo, Profesa Makame Mbarawa (katikati), kutoa hotuba yake ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Shirika la Posta Tanzania leo, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta wakinukuu hotuba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa, akizungumza wakati alipoizindua rasmi bodi mpya ya Shirika la Posta Tanzania, leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa bodi hiyo, Dk. Haruni Kondo.
Baadhi ya wajumbe wa bodi ya Shirika la Posta wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa, alipokuwa akitoa hotuba yake ya uzinduzi wa bodi hiyo, leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa, akizungumza wakati akiizindua rasmi bodi mpya ya Shirika la Posta Tanzania, leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa bodi hiyo, Dk. Haruni Kondo.
Kaimu Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta, Fortunatus Kapinga (kushoto), akifuatilia hotuba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya shirika hilo, leo jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Bodi, Stella Nghambi, akitoa neno la shukurani baada ya Waziri Profesa Mbarawa kuizindua bodi hiyo.
Picha ya Pamoja ya Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati waliokaa), mara baada ya kuizindua bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.  
Picha ya Pamoja ya viongozi wa Shirika la Posta na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto waliokaa), mara baada ya kuizindua bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.  


HOTUBA YA MHESHIMIWA PROFESA MAKAME MBARAWA (MB) WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO WAKATI WA UZINDUZI WA BODI MPYA YA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA,TAREHE 20 OKTOBA, 2016, KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO, GHOROFA YA 12, POSTA HOUSE MAKAO MAKUU.

·         Katibu Mkuu wa Mawasiliano,
·         Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania,
·         Wakurugenzi wa Bodi, 
·         Kaimu Postamasta Mkuu,
·         Viongozi wa Menejimenti,
·         Wageni waalikwa,
·         Mabibi na Mabwana,

·            PONGEZI NA SHUKRANI
          
Awali ya yote napenda nitumie fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutujalia uhai na afya  njema ya kuweza kujumuika hapa leo na kushiriki katika uzinduzi huu wa Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania.

Pia nawapongeza Wajumbe wote wa Bodi na Mwenyekiti kwa kuteuliwa kuongoza Shirika hili.

Ninawashukuru kwa kunikaribisha ili niungane na kuzungumza nanyi wakati huu wa kuzindua Bodi mpya.  Fursa hii ni adimu kwani imetuwezesha kufahamiana pamoja na kutafakari kwa kina juu ya changamoto zilizopo na kuanza kubuni njia ya kuzitatua.

·            MAJUKUMU NA CHANGAMOTO ZA SHIRIKA

                   Mwenyekiti wa Bodi,

Leo hii nitawakabidhi baadhi ya nyenzo na nyaraka za majukumu ya Shirika na Bodi ya Wakurugenzi kama yalivyoainishwa katika Sheria ya Bunge Na. 19 ya mwaka 1993.

Sina haja ya kutaja majukumu haya lakini ni vyema kuanzia sasa mzingatie kuwa mawasiliano haya kwa njia ya Posta ni kichocheo  na kielelezo muhimu cha ukuaji wa uchumi wa Taifa lolote duniani.

Kwa bahati nzuri Wajumbe wa Bodi hii ni wataalamu wenye uzoefu na waliobobea katika nyanja muhimu ikiwa ni pamoja na uhamasishaji wa biashara, usimamizi wa rasilimali watu na rasiliamali fedha, sheria, TEHAMA, ubunifu katika biashara, usalama na uendeshaji wa sekta binafsi.

·            HALI YA HUDUMA ZA POSTA KITAIFA NA KIMATAIFA

Mwenyekiti wa Bodi,

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Posta Duniani (UPU), mtandao wa mawasiliano kwa njia ya Posta unajumuisha Ofisi za Posta laki sita na sitini elfu (660,000).

Huu ni mtandao mkubwa zaidi duniani ambao pamoja na huduma nyingine una uwezo wa kusambaza wastani wa barua zipatazo 450 bilioni na vifurushi 6 bilioni kwa mwaka.

Hapa Tanzania Shirika hili linaendesha mtandao wa Ofisi za Posta zipatazo 400. Kwa mujibu wa takwimu zilizopo wastani watu 120,000 katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanahudumiwa na ofisi moja ya Posta.  Kuhusu ufikishaji barua na vifurushi katika ofisi na makazi  ya watu (physical delivery of mail) kiwango ni kidogo sana.  Wastani wa 98% ya barua zinazohudumiwa na Shirika hili hupitia katika masanduku ya barua yalioko katika ofisi za Posta.

Kiwango hicho kinaonyesha wazi kuwa tunalo jukumu la msingi la kupanua na kuboresha mtandao wa huduma za Posta hapa nchini ili kufikisha huduma za kisasa za kimtandao karibu na jamii.  Ningependa kusisitiza hapa kuwa ni lazima Shirika hili liongeze kasi zaidi katika kuboresha na kuanzisha huduma zinazozingatia matakwa ya wateja.

·              SERA YA TAIFA YA POSTA
          Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi,

Kwa hivi sasa Wizara yangu inaendelea kuhuisha Sera ya Taifa ya Posta ili kuzingatia mahitaji ya sasa na baadae. Utekelezaji wa sera hii ni eneo mojawapo ambalo inabidi tulizingatie.

Mwelekeo wa sera hii kwa muhtasari ni:-

·         Kuwezesha Shirika la Posta ambalo ni mtoa huduma kwa umma (Public Operator) kutoa na kufikisha huduma bora kwa jamii yote na kwa gharama nafuu.

·         Kuliendesha Shirika la Posta kwa misingi ya kibiashara.

·         Kuzifanya huduma za Posta kuwa za kisasa zaidi kwa kutumia teknolojia maridhawa ili kukidhi mahitaji mapya ya wateja ambayo  yanabadilika mara kwa mara.

·         Kushirikisha sekta binafsi katika kuendesha na kuwezesha shughuli za Posta ili kuchochea maendeleo ya sekta hiyo na sekta nyingine kama za fedha, biashara,  afya, elimu, habari n.k

·         Wizara yangu inapenda kuona utekelezaji wa masuala yaliyoainishwa katika sera ya Posta na kuhakikisha uhuishwaji wa sera hii ambayo ni ya muda mrefu 2003 ili kuwezesha malengo yanafikiwa.

·            MATUMIZI SAHIHI YA FURSA NA RASILIMALI ZA SHIRIKA

Kwa bahati nzuri Shirika la Posta ni moja ya Taasisi zenye rasilimali na fursa nyingi ambazo kama zikitumiwa vizuri zinaweza kusaidia kuliendeleza Shirika.  Rasilimali na fursa hizo ni pamoja  na:-

·         Viwanja na majengo ya kuishi na ya ofisi ambayo yako sehemu mbalimbali hapa nchini na hasa yaliyopo maeneo ya mijini.  Kwa mfano, Shirika lina viwanja 178 na kati ya hivyo viwanja 153 vimeendelezwa na 25 havijaendelezwa.

·         Mtandao mpana wa ofisi za Posta zipatazo 400 hapa nchini ambao umeunganishwa katika ofisi za Posta zipatazo 660,000 duniani kote (Global Connectivity).

·         Uwezo mkubwa wa kutoa huduma unganishi za kimtandao (Integration of physical and digital solutions).

·         Uwezo mkubwa wa kuboresha huduma na biashara zilizopo na hapo hapo kuanzisha mpya .  Kwa bahati nzuri hata Sheria iliyoanzisha Shirika hili  inasisitiza juu ya jambo hili.

·         Mna uwezo wa kurejesha imani kubwa ya kihistoria (Historical Loyalty) waliyonayo wateja na wadau mbalimbali wa Posta.

Naamini mnafahamu kuwa  mkakati huu wa kutumia vizuri fursa na rasilimali kama hizi umefanywa na mashirika mengi ya Posta hapa duniani na umeyawezesha mashirika hayo kuwa na mafanikio makubwa.  Hali ni hivyo hivyo hapa nchini kwani, baadhi ya mashirikia kama hili la Posta yametumia vizuri fursa na rasilimali zilizopo na kuweza kufanikiwa.

Jambo la msingi  ni kuangalia maeneo yote hasa sheria zenye ukiritimba zinazozuia Shirika kutumia rasilimali zake kwa ajili ya uzalishaji mfano, sheria ya Shirika kuwa chini ya uangalizi wa Consolidated Holding Corporation (CHC)  ambapo haliwezi kukopa au kuweka rehani vitega uchumi vyake ili kuendeleza huduma na biashara.

·            MFUMO WA ANUANI ZA MAKAZI NA SIMBO ZA POSTA

Mwenyekiti na Wajumbe,

Anuani za makazi na simbo za posta (Physical Address and Post code System) ni moja ya mradi mkubwa wa kitaifa ambao mwezi Septemba mwaka huu Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa alizindua muongozo wake mkoani Dodoma.

Aidha, kuwepo kwa anuani zinazotambulisha makazi ya watu na rasimali za kudumu kutatoa fursa nyingi zaidi katika utoaji na uendeshaji wa huduma za posta nchini.

Ingawa wadau wa utekelezaji wa mfumo huu ni wengi lakini Wizara yangu na taasisi zilizoko chini yake hususani Shirika hili la Posta, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) zina wajibu mkubwa zaidi katika kuhakikisha manufaa ya mfumo huu yanawafikia watumiaji wa mwisho ambao ni pamoja na wananchi wa kawaida (last mile Users).  Manufaa hayo ni pamoja na:-

·         Kuwezesha huduma za usambazaji na logistiks.  Hili ni eneo linalopanuka kwa haraka sana hapa nchini na duniani kote.

·         Kuwezesha huduma jumuishi za kimtandao hususani za biashara (E-business), elimu (E-education), afya (E–medicine), utawala  serikalini (E – governance) na nyinginezo.

·         Uboreshaji wa huduma za dharura na usalama kama zima moto na uokoaji, polisi, magari ya wagonjwa, majanga kama matetemeko, mafuriko na vimbunga.

·         Kurahisisha usajili wa huduma, biashara, na mifumo mbalimbali kama vizazi, vifo, ndoa na talaka.

·         Kukuza utalii wa ndani na nje pamoja na kurahisisha utambuzi wa sehemu kwa wageni.

·         Kuboresha utendaji wa taasisi nyingine kama za Ugavi wa Nishati na Maji, Mabenki, Mamlaka za mapato, Bima na Hifadhi ya Jamii.

Kwahiyo lazima tuzingatie kuwa watu wote na taasisi zote hizo zinatutegemea katika kufanikisha mfumo huu wa Anuani za Makazi na Postikodi.  Tafadhali tusiwaangushe.

7.0 HUDUMA YA POSTA MLANGONI

Mwenyekiti na Wajumbe,

Kwa kuzingatia mwelekeo huu, Shirika hili limeanzisha huduma mpya ijulikanayo kama “POSTA MLANGONI”.  Huduma hii tajwa imeanzishwa hapa Dar es Salaam, Dodoma na Arusha.

Ni mwanzo mzuri, lakini ningependa mwongeze jitihada katika jambo hili.  Mwelekeo wetu uwe ni kuzingatia maslahi mapana ambayo ni pamoja na:-

·         Kujenga nchi ya viwanda.

·         Kufikiwa malengo ya Dira ya Taifa ya mwaka 2025 (Vision 2025).

·         Kupunguza umaskini na kurahisisha utoaji wa huduma za kiuchumi na kijamii.

8.0 UTEKELEZAJI WA MIUNDOMBINU MINGINE

Mwenyekiti na Wajumbe,

Pamoja na utekelezaji wa mfumo wa Anuani za Makazi na Postikodi ili kufanikisha dhamira yetu ya kitaifa, kwa bahati nzuri nchi yetu imefikia hatua ya kuridhisha katika kusimika miundombinu mingine muhimu ya kufanikisha dhamira hii.

Miundombinu hii ni pamoja na:-

·         Upanuzi wa Mkongo wa Taifa na Ujenzi wa mikongo ya mijini (Metro fiber network).

·         Ujenzi wa kituo mahiri cha kutunza kumbukumbu (Data – Centre).

·         Uboreshaji wa mtandao wa barabara, viwanja vya ndege na bandari.

·         Usambazaji wa huduma za nishati ya umeme katika maeneo yote ya nchi yetu.

          Nawaagiza Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti, na Wafanyakazi wote wa Shirika hili           changamkieni fursa za miundombinu hii.

9.0 HITIMISHO

Mwenyekiti,

Kabla ya kumaliza hotuba yangu ningependa kusisitiza juu ya maeneo yafuatayo:-

·         Uwajibikaji, uchapakazi na ubadilishwaji wa mtazamo (change of mind sets) ya wafanyakazi wa Shirika hili.  Tuondokane na kuendesha shughuli zetu kwa mazoea (business as usual).  Hii ni pamoja na kuwajengea uwezo katika teknolojia ya kisasa.

·         Kuongeza udhibiti wa usalama katika mtandao wa Shirika.  Tuwe macho na uhalifu wa kimtandao kama usafirishaji wa madawa ya kulevya, utakatishaji wa fedha na uzingatiaji wa jumla wa sheria za nchi na Kimataifa.

·         Kuanzisha huduma ya “One Stop Community Centre”.  Hii iende sambamba na kuimarisha huduma za uwakala kwa kutumia TEHAMA ikiwa ni pamoja na kuwa na “Payment Switch”.

·         Eneo lingine ni kutoa huduma bora zinazowaridhisha wateja (customer satisfaction).  Hii ni pamoja na kuimarisha shughuli zenu za masoko.

·         Kupanua wigo wa biashara, kuongeza mapato, kupata faida na hatimaye kutoa gawiwo kwa mwenye hisa ambaye ni serikali.

Nafahamu baadhi ya mambo haya yako katika mipango yenu ila la muhimu ni ufuatiliaji na  utekelezaji wenu. Kwa upande wa Serikali tunatambua na kuzingatia changamoto za msingi za Shirika hili ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mtaji na mzigo wa kulipa pensheni za wastaafu wa Jumuiya ya zamani ya Afrika Mashariki.

Baada ya kuyasema hayo, sasa natamka kuwa – Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania, IMEZINDULIWA RASMI.


Ahsanteni kwa kunisikiliza