Saturday, January 30, 2016

UZIO WA HOTELI YA GOLDEN TULIP WATEMBEZEWA NYUNDOZZZ LEO

 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

SERIKALI imevunja uzio wa eneo la maegesho ya magari wa hoteli ya  Golden Tulip Jijini Dar es Salaam kutokana na umiliki wa eneo hilo kutolewa kwa njia zisizo halali.Hatua hiyo imefikiwa baada ya Serikali kushinda kesi dhidi ya mmiliki  wa hoteli hiyo.
Kazi ya kubomoa uzio huo imefanywa kwa ushirikiano wa Baraza la Mazingira (NEMC, Manispaa ya Kinondoni pamoja na Wizara ya Ardhi, Nyumnba na Maendeleo ya Makazi kutokana na mmiliki huyo kushindwa kubomoa mwenyewe kwa maelekezo ya aliyopewa na Serikali.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo la kubomoa uzio huo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema kuwa maeneo yote ya Ufukwe wa Bahari ni maeneo ya jamii hivyo hayatakiwi kuguswa kwa namna yeyote ile.
Waziri Lukuvi amesema serikali haitakubali kuona maeneo yanavamiwa na watu wachache kwa kuzunguka baadhi ya watendaji na kupata hati.

Amesema kuwa  katika kipindi hiki watafatilia maeneo yote ya ardhi kama yamevamiwa na yatarudishwa kwa ajili ya maendeleo ya jamii.

Uzio wa Golden Tulip mara ya kwanza uliombwa kwa ajili ya kuegesha magari kwa muda katika mkutano wa SADC baada ya hapo mmiliki wa hoteli akaweza kupata hati ya eneo hilo kwa kile kinachosemekana kuwa njia zisizo halali.
Baadhi ya wafanyakazi wa Hoteli ya Golden Tulip wakiendelea na zoezi la uondoshaji wa mabati yaliyoweka kama uzio katika eneo hilo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza na waandishi wa habari waliokuwepo kwenye eneo hilo.
 Msafara wa Rais Dkt. Magufuli ukipita wakati zoezi la kuuondoa uzio wa Hoteli ya Golden Tulip likiendelea.
Eneo hilo linavyoonekana baada ya kupita greda. PICHA NA OTHMAN MICHUZI

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU "UVUMI WA AJIRA ZA MADAKTARI JWTZ"



Hivi karibuni kumekuwa na uvumi unaoeleza kuwa JWTZ limetoa nafasi za kazi kwa vijana wenye fani ya Udaktari na kuwataka vijana hao kuripoti Makao Makuu na vyeti vyao kwaajili ya usaili.

Habari hizo si za kweli,JWTZ kama zilivyo taasisi nyingine za serilikali lina mfumo rasmi wa kutangaza habari zake hivyo jeshi linawaomba wananchi wazipuuzie taarifa hizo.

Aidha JWTZ linawataka wamiliki wa mitandao ya kijamii kutotoa taarifa za jeshi bila kuwasiliana na Makao Makuu ya jeshi kinyume na utaratibu huu,unawasababishia wananchi usumbufu usio wa lazima.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu JWTZ.

WAZIRI MKUU ATAKA MASHIRIKISHO YA MICHEZO KUMPA MPANGO KAZI

3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza mbio za  Wabunge  Hapa Kazi Tu Dodoma Half Marathon zilizoanzia Bungeni hadi uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Januari  30, 2016. Kushoyo kwake ni Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na  Michezo, Nape Nnauye na kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt Tulia  Ackson. Mwansasu (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………………………
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,Majaliwa ameyataka mashirikisho ya michezo mbalimbali kumpa mpango kazi wa muda mrefu na mfupi ili kuiwezesha Serikali kushirikiana nao kuleta maendeleo ya michezo nchini.
Mhe.Kassim Majaliwa,Majaliwa ameyasema hayo leo Mijini Dodoma wakati akifunga mashindano ya Hapa Kazi Tu Half Marathon yaliyoanzia katika Chuo cha Biashara (CBE) tawi la Dodoma na kumalizikia katika uwanja wa Jamhuri yenye lengo la kuadhimisha kilele cha  Siku 100 za uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Joseph Magufuli tangu aingie madarakani.
“ Serikali ya Awamu ya Tano tumejipanga kuendeleza michezo nchini kwani michezo ni moja kati ya sekta muhimu kwa maendeleo ya wanamichezo na nchi kwaujumla na pia ni moja ya kujitangaza kimataifa kupitia michezo mbalimbali”Alisema Mhe Majaliwa.
Aidha Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amesema kupitia wizara yake atajitaidi kuimarisha michezo hasa ukuzingatioa Serikali  imeweka mkazo katika michezo hivyo yeye kama waziri mwemye dhamana hiyo atalisimamia kwa karibu suala la maendeleo ya michezo yote .
“Naahidi kushirikiana na vyama vya michezo ili kuimarisha sekta ya michezo kwa kuweka mipango thabiti ya kusimamia na kuiendeleza michezo ili iweze kuleta tjia katika jamii ya watanzania”Alisema Mhe. Nnauye.
Mbio hizi za Hapa Kazi Tu Half Marathon zilmeshirikisha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Tulia Ackson,baadhi ya mawaziri, wabunge na watu wa rika zote kwa kukimbia umbali wa kilometa 2, kilometa5 na kilometa21 na washindi kupewa zawadi za pikipiki, mabati na fedha taslimu.
Mashindano haya ya hapa kazi Half Marathon yaliyoandaliwa na Chama cha Riadha Tanzania na kudhaminiwa na kampuni ya GSM, TANAPA, Kilimanjaro International Airport,East Teanders, CRDB Bank na DSTV yameandaliwa kwa nia ya kuandaa timu ya Riadha ya Tanzania kujiandaa na mashindano ya Olompiki yatakayofanyika Rio de Janeiro nchini Brazil.

SERIKALI YATOA VIPAUMBELE VYAKE KWA WANANCHI

10
11Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Benno Ndulu akisistiza wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu mapato na matumizi ya Serikali yalivyoboreshwa na uchumi wa nchi kuimarika na kutengemaa.
12
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile leo jijini Dar es salaam kuhusu Serikali ilivyojipanga kuboresha na kuhudumia sekta mbalimbali nchini ikiwemo elimu, umeme, maji na miundombinu.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango)
…………………………………..
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
NEMBO YA TAIFA
Serikali imetoa jumla ya Sh. Bilioni 318.406 kwa mwezi wa Januari mwaka 2016, kwa ajili ya miradi ya maendeleo nchini na Sh. Bilioni 538.5 kwa mishahara ya watumishi wa Umma.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Servacius Likwelile alisema kuwa Serikali inajivunia kufanikiwa kutumia fedha za ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambapo hadi sasa Serikali imetumia kiasi cha Sh. Bilioni 71.2 tu kutoka fedha za nje.
Dkt. Likwelile alisema mapato yanayokusanywa nchini yamewezesha kutekeleza sera ya elimu bure ambapo mwezi Desemba mwaka 2015 Serikali ilitoa kiasi cha Sh. Bilioni 18.77 kwa shule za msingi na sekondari kwa ajili ya ruzuku, ada na chakula kwa shule za bweni pamoja na mahitaji mengine ambapo mwezi wa Januari 2016 Serikali imetoa kiasi cha Sh. Bilioni 18.77 kwa ajili ya kutekeleza Sera hiyo.
Aliongeza kuwa katika ulipaji wa madeni ya wakandarasi nchini , Serikali imetoa Sh. Bilioni 130 kwa mwezi Januari mwaka 2016 ambapo mwezi Desemba mwaka 2015 ilitoa Sh. Bilioni 193.
Kwa upande wa Mfuko wa Barabara, Katibu Likwelile alifafanua mradi huo umetengewa kiasi cha Sh. Bilioni 47.89 na kuongeza kuwa Benki kuu ina fungu la mfuko huo ambapo nayo imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 76.3.
Dkt. Likwelile alisema kuwa Halmashauri zitapelekewa kiasi cha Sh. Bilioni 20.52 kwa ajili ya kuboresha barabara na jumla mfuko huo kufikia kiasi cha Sh. Bilioni 274.71.
Akifafanua kuhusu miradi ya umeme, Dkt. Likwelile alisema kuwa mwezi Desemba mwaka 2015 Serikali ililipa deni la TANESCO kiasi cha Sh. Bilioni 80 za mradi wa Kinyerezi II na kwa mwezi Januari mwaka 2016 kiasi cha Sh. Bilioni 40 zimetengwa kwa ajili ya mradi huo.
Hali hii imefikisha kiasi cha Sh. Bilioni 120 kwa ajili ya kulipa madeni na kuendeleza uzalishaji wa umeme nchini.
Alisema kiasi cha Sh. Bilioni 21.959 kimetengwa kwa ajili ya mradi wa umeme vijijini na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ina mfuko wa mradi huo ambao kwa sasa una kiasi cha Sh. Bilioni 21.9 na kuongeza kuwa huduma ya umeme kwa wananchi itaimarika.
Alifafanua kuwa Serikali imeanzisha mfuko wa maji Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambapo mpaka sasa mfuko huo una jumla ya kiasi cha Sh. Bilioni 46.3.
Aidha, BoT imetoa Sh. Bilioni 12.5 kuendeleza miradi ya maji ambapo kwa Januari mwaka 2016 Serikali imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 7.7.
Serikali imetenga kiasi cha Sh Bilioni 82.2 kwa mwezi wa Januari ili kuweza kulipa pensheni za wastaafu, na kwa wale wastaafu walio katika daftari la kudumu ambapo wametengewa kiasi cha Sh. Bilioni 33.3 kwa ajili ya malipo yao.
Wabunge wametengewa kiasi cha Sh. Bilioni 35.5 kwa ajili ya mkopo wa magari ambapo kila mbunge atapata kiasi cha Sh. Milioni 90, kiasi cha Sh. Milioni. 45 ni ruzuku na Sh. Mil. 45 ni mkopo ambao utalipwa ndani ya miaka 5.
Aidha, Serikali imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 784.3 kwa ajili ya kulipa deni la taifa.
Naye Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata alibainisha kuwa hali ya makusanyo ya mapato nchini iko vizuri ambapo kwa mwezi Januari 2016, makadirio yalikuwa Sh. Trilioni 1 na Bilioni 45 na hadi kufikia sasa kiasi cha Sh. Trilioni 1 na Bilioni 31 zimeshakusanywa.
Matarajio ya TRA ni kukamilisha kukusanya kiasi cha Sh. Billioni 14 zilizosalia.
Aidha, Kidata alibainisha kuwa uingizaji wa bidhaa kupitia bandarini bado uko vizuri licha ya minong’ono kuwa uzuiaji wa mianya ya ukwepaji kodi imepunguza uingizaji bidhaa ambapo kwa mwezi Januari Bilioni 111 zimekusanywa kutokana na ushuru wa forodha.
Kidata alitoa wito kwa kila mtanzania kulipa kodi na kutoa taarifa za wakwepa kodi ili kuweza kukuza mapato ya nchi.
Kwa upande wake Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Benno Ndulu amepongeza juhudi za ukusanyaji wa mapato na udhibiti wa matumizi ya fedha za Serikali.
Alisema kuwa uchumi umekua na unazidi kuimarika licha ya changamoto za kiuchumi duniani ambapo uchumi wa nchi umekua kwa asilimia 7 na unategemewa kukua miezi ijayo kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji nchini.
Mfumuko wa bei unaendelea kubaki ndani ya kiwango cha tarakimu moja, licha ya ongezeko dogo katika miezi ya hivi karibuni kutokana na kupanda kwa bei za vyakula.
Alisema kuwa mfumuko wa bei ulikuwa asilimi 6.8 mwaka 2015, ukilinganishwa na asilimia 6.1 kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 2015.
Wakati huo huo mfumuko wa bei usiojumuisha chakula na nishati uliendelea kubaki katika viwango vya chini ya asilimia 2.5 kutokana na hatua mbalimbali za kisera zilizochukuliwa na BoT.
Prof. Ndulu alifafanua mapato ya fedha za kigeni yanaendelea vizuri ingawa bei ya dhahabu imeshuka kutoka Bilioni 2.5 hadi Bilioni1.3.
Sekta ya utalii imesaidia kuimarisha fedha za kigeni kwani mapato yameongezeka kutoka Bilioni 1.5 hadi Bilioni 2.2.
Sekta ya viwanda nayo imeshika nafasi ya pili katika kuongeza fedha za kigeni nchini ambapo mwaka 2015 mapato yalikuwa Bilioni 1 na kwa sasa yamefikia Bilioni1.5.
Aidha, Prof. Ndulu aliongeza kuwa sekta ya usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi imesaidia kuimarisha fedha za kigeni ambapo mapato yamefikia Dola Bilioni11 kwa mwaka.
Hadi kufikia sasa Tanzania imenufaika kutokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika uingizaji bidhaa hiyo kwa asilimia 44.
Serikali inatarajia kuendelea kuimarisha uchumi ili kufikia azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati hadi ifikapo 2025.
Imetolewa na Wizara ya Fedha na Mipango
Kitengo cha Mawasiliano

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AHUDHURIA MKUTANO WA WAKUU WA AFRIKA ETHIOPIA LEO

sul1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea shada la Maua kutoka kwa Mtoto Yuthra Bawaid alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bolo Nchini Ethiopia leo Januari 30, 2016 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 26 kwa Wakuu wa Nchi za Afrika unaoanza leo mjini Addis Ababa Ethiopia
sul2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Gwaride la Heshima kutoka kwa Jeshi la Ethiopia alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 26 kwa wakuu wa Nchi za Afrika ulioanza leo Januari 30,2016 Mjini Addis Ababa
sul3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mwambata wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Nchini Ethiopia Meja Generali John Bishoge alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 26 kwa wakuu wa Nchi za Afrika ulioanza leo Januari 30,2016 Mjini Addis Ababa Ethiopia
sul4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 26 kwa wakuu wa Nchi za Afrika ulioanza leo Januari 30,2016 Mjini Addis Ababa Ethiopia.
sul5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifuatilia kwa Makini mkutano wa 26 wa Wakuu wa Nchi za Afrika ulioanza leo Mjini Addis Ababa Ethiopia. (Picha na OMR

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MNADHIMU MKUU WA JWTZ, BALOZI WA TANZANIA KUWAIT NA KATIBU TAWALA WA KATAVI NA MWANZA LEO IKULU DAR ES SALAAM

Q1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Dkt. 
Mahadhi Juma Maalim kuwa Balozi wa Tanzania  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Q3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha  Luteni Jenerali Venance Salvatory
 Mabeyo  kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Q5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi Clodwig Mathew Mtweve   kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Q8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi Paul Amani Moses  Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Q10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ MStaafu Luteni Jenerali (Rtd) Samuel Albert Ndomba baada ya shughuli ya kiapo Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Q12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na viongozi wa Jeshi la Wananchi na Jeshi la Polisi  katika picha ya pamoja baada ya kuapishwa Mnadimu Mkuu wa TPDF, Balozi wa Tanzania Kuwait na  Katibu Tawala wa Mikoa ya Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Q17
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  na viongozi wa Jeshi la Wananchi na Jeshi la Polisi   katika picha ya pamoja baada ya kuapishwa Mnadimu Mkuu wa TPDF, Balozi wa Tanzania Kuwait na  Katibu Tawala wa Mikoa ya  Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Q22
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  akifurahia jambo na viongozi wa Jeshi la Wananchi na Jeshi la Polisi  katika picha ya pamoja baada ya kuwaapisha  Mnadimu Mkuu wa TPDF, Balozi wa Tanzania Kuwait na  Katibu Tawala wa Mikoa ya Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Q23Q24Q25
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na msemaji wa JWTZ Luteni Kanali Ngeleba  Lubinga baada ya kuapishwa Mnadimu Mkuu wa TPDF, Balozi wa Tanzania Kuwait na  Katibu Tawala wa Mikoa ya Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Q26
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Abdulrahman Kaniki  baada ya kuapishwa Mnadimu Mkuu wa TPDF, Balozi wa Tanzania Kuwait na  Katibu Tawala wa Mikoa ya Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016.
PICHA NA IKULU

Rais Magufuli awateua Makatibu Tawala wa Mwanza na Katavi