Monday, August 31, 2015

MAGUFULI MKOANI RUVUMA




















WATUMIAJI WA MITANDAO VIBAYA SHERIA KUWADHIBITI KUANZA LEO SAA 6:00 USIKU.

NNa Magreth Kinabo 

………………………………….
Sheria mpya   ya Makosa ya Mtandao ya mwaka   2015 na Sheria ya Miamala ya Kielektroniki ya mwaka 2015 zitaanza kutumika rasmi kesho Septemba Mosi mwaka huu, hivyo watumiaji   na watoa huduma waaswa kuzingatia sheria hizi ili kuepuka mkondo wa sheria.
 Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.
“Sheria hizi ni nzuri zitaanza kutumika Septemba Mosi mwaka  huu,kuanzia saa 6.00 usiku . zina maslahi katika nchi yetu. Ninatoa wito kwa wananchi kuzingatia matumizi salama ya mtandao kwa manufaa yako na maendeleo ya Taifa letu,” alisema Profesa Mbarawa.
 Aliongeza kuwa sheria hiyo ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 hazihitaji utungaji wa kanuni kwa kuwa iko wazi.
 Alisema tayari wizara imeanza kuelimisha watu kuhusu sheria hiyo na itendelea kuwajengea uwezo wadau mbalimbali.
Profesa Mbarawa alisema sheria ya makosa ya mtando ya mwaka 2015 na Tanzania sio nchi ya kwanza kuwa nayo, bali nchi mbalimbali zina sheria kama hiyo ,ambapo alitolea mfano Uingereza,India,Malaysia, Uganda na Korea ya Kusini.
 Akizungumzia kuhusu  madai sheria hiyo kuhusika na suala la Uchaguzi Mkuu, alisema si kweli, bali imekamilika katika kipindi hicho ndio maana baadhi ya watu wanadai hivyo.Aliongeza kwamba sheria hiyo imetunga ili kudhibiti matumizi ambayo  si mazuri. 
“ Mtu akitumiwa ujumbe akiupokea hapaswi kuisambaza  kwani atakapousambaza atakuwa na amefanya kosa,”alisisitiza.
Aliyataja baadhi ya makosa kuwa ni usiri, usalama wa upatikanaji wa taarifa za kompyuta na mifumo  kama vilekuingilia mawasiliano ya kompyuta au mifumo ya kompyuta kinyume cha sheria na wizi wa taarifa kimtandao.
Makosa  dhidi ya kompyuta ikiwa ni pamoja na,udanganyifu kwa kutumia kompyuta,kugushi kwa kutumia kompyuta wizi wa utambulisho wa mtu binafsi  mtandaoni, matumizi ya vifaa kinyume cha sheria.
Makosa yanayohusiana kimaudhui kama vile usambazaji wa ponografia, ponografia za watoto makosa dhidi ya ubaguzi wa rangi na chuki, michezo ya kmari mtanadaoni kiunyume cha sheria, kashfa na habari za uongo na makosa dhidi ya haki na hati miliki.
Pia inatambua muungano wa makosa inajumuisha kama vile utakatishaji wa fedha haramu na ugaidi kwa kutumia mtandao.
Kwa upande wa sheria ya miamala ya kieletroniki ya mwaka 2015, baadhi ya makosa likiwemo la wajibu wa watoa huduma kwa walaji, bidhaa ,huduma au mawasiliano ambayo hayajaombwa na uhalali wa Muamala wa elektroniki.
Aliongeza kuwa kanuni za sheria hiyo zinatayarishwa zikiwa tayari zitangazwa  na zitaanza kutumika wakati wowote.

JESHI LA POLISI TANZANIA LAWAITA KWENYE USAILI WAHITIMU WA SHAHADA, STASHAHADA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
wwwwww
TANGAZO KWA UMMA.
JESHI LA POLISI TANZANIA LINAWAITA KWENYE USAILI WAHITIMU WALIOORODHESHWA WA SHAHADA, STASHAHADA NA ASTASHAHADA. USAILI UTAFANYIKA KUANZIA TAREHE 03.09.2015 HADI TAREHE 04.09.2015 KUANZIA SAA MBILI ASUBUHI HADI SAA KUMI JIONI KATIKA MAENEO YAFUATAYO:-
• FANI YA UTAWALA, UCHUMI, USIMAMIZI WA SHERIA NA UTEKELEZAJI [BALE], UALIMU, UANDISHI HABARI, UHANDISI MADINI [MINING ENGINEERING], UGAVI, LUGHA, USHAURI NASIHI, KATIBU MUKTASI, LAND SURVEY CATHOGRAPHER NA GEOMATICS WATAFANYA USAILI KATIKA CHUO CHA TAALUMA YA POLISI DAR ES SALAAM [DPA] KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM.
• MAFUNDI MAGARI, MATENGENEZO YA PIKIPIKI, MAFUNDI MATENGENEZO YA UMEME WA MAGARI [AUTO ELECTRICAL], MAFUNDI RANGI ZA MAGARI, MAFUNDI MAGARI, MAFUNDI USHONAJI,MAFUNDI BODY ZA MAGARI NA MADEREVA. USAILI WA KADA HIZI UTAFANYIKA KIKOSI CHA POLISI UFUNDI KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.
• MATENGENEZO YA KOMPYUTA, FAX & PHOTOCOPY MACHINES NA MAWASILIANO YA REDIO [DIPLOMA IN RADIO COMMUNICATION], USAILI WAO UTAFANYIKA NYUMA YA KIKOSI CHA UFUNDI YAANI TEHAMA KEKO CHINI.
• WAKEMIA, BAILOJIA [MOLECULAR BIOLOGY] USAILI UTAFANYIKA MAKAO MAKUU YA POLISI YALIYOPO MAKUTANO YA BARABARA YA OHIO NA GHANA JENGO LINALOTAZAMANA NA POSTA HOUSE.
• KADA ZA AFYA USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA AFYA KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.
• MANAHODHA NA MAFUNDI MITAMBO WA MELI, USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA WANAMAJI KILICHOPO KARIBU NA JENGO LA MAHAKAMA YA RUFAA.
• DAKTARI WA WANYAMA, USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA MBWA NA FARASI KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.
• MAFUNDI AC ZA MAJUMBANI, ARCHITECTURE DRAFTMAN, QUANTITY SURVEYORS, CIVIL ENGINEER, WELDING & FABRICATION, UMEME WA MAJUMBANI, PAINTING, ALUMINIUM & GLASS WORK, PLUMBING, MOSONRY, MOTOR REWINDING, HYDRO GEOLOGY DRILLING WELL, REFRIGERATION & AIR CONDITIONING. USAILI WA KADA HIZI UTAFANYIKA KIKOSI CHA POLISI UJENZI NDANI YA KAMBI YA POLISI BARRACKS KURASINI KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.
• FANI ZA BENDI, BRASS BENDI, WOODWIND, STRING JAZZ NA PERCUSSIVE, USAILI WAO UTAFANYIKA KIKOSI CHA BENDI KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.
• FANI YA URUBANI,USAILI UTAFANYIKA KIKOSI CHA ANGA KILICHOPO UWANJA WA NDEGE NDOGO WA ZAMANI WA J.K.NYERERE DSM.
MUHIMU:
1. MWOMBAJI AFIKE KWENYE USAILI AKIWA NA NAKALA HALISI YA VYETI VYOTE VYA MASOMO/TAALUMA [ACADEMIC TRANSCRIPT (S)/CERTIFICATE (S) YAANI KIDATO CHA NNE, SITA, CHUO NA CHETI CHA KUZALIWA. KIAPO CHA KUZALIWA HAITAKUBALIWA.
2. MWOMBAJI ALIYEITWA KWENYE USAILI ATALIPIA GHARAMA ZA UPIMAJI AFYA SHILINGI ELFU KUMI (10,000/=), USAFIRI, CHAKULA NA MALAZI KWA MUDA WOTE WA ZOEZI LA USAILI.
3. AMBAYE HATAHUDHURIA USAILI KUANZIA SIKU YA KWANZA HATAPOKELEWA.
ILI KUPATA/KUONA ORODHA YA MAJINA, TEMBELEA www.policeforce.go.tz
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA NATIONAL DEFENCE HEADQUARTERS

H
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ulinzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi muda mfupi baada ya kuwasili eneo la Lugalo kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa National Defence Headquarters.
P
Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika hafla ya kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa National Defence Headquarters huko Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
O
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Makamanda wa Jeshi la Ulinzi wakati wa uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi.
i
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua kitambaa wakati wa uwekaji jiwe la msingi la Ujenzi wa National Defence Headquarters huko Lugalo jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Mkuu wa majeshi ya Ulinzi  Jenerali Davis Mwamunyange,Watatu Kushoto ni Waziri wa Ulinzi Dkt.Huessein Ali Mwinyi na kulia ni Bwana Hu mwakiklkishi wa kampuni ya ujenzi kutoka China.
t
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa National Defence Headquarters Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
e
k
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange akimuonyesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mchoro wa majengo ya Makao Makuu ya Ulinzi yatakayojengwa eneo la Lugalo jijini Dar es Salaam leo.Wapili kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
(Picha na Freddy Maro)

RELI YA KATI KUANZA KARABATIWA HIVI KARIBUNI

 Waziri wa Uchukuzi Samwel Sitta akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kuchukua hatua kubwa kuanza  kufufua reli ya kati muda wowote, ujenzi wa reli hiyo utaanza ili kuongeza kasi ya maendeleo  hapa nchini leo Jiji Dar es Salaam.
Waandishi wa habari walio hudhulia  katika mkutano na Waziri wa Uchukuzi Samwel Sitta, wakimsikiliza kwa makini.
 (Picha na Emmanuel Mssaka.

Na JenikisaNdile –Maelezo
SERIKALI  kwa kushirikiana na kampuni ya reli Asset holding imejizatiti kuimarisha miundo mbinu ya reli itakayogharimu Tsh. Trilioni 16 katika kuleta maendeleo endelevu hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam waziri wa uchukuzi Mhe. Samweli sitta amesema kuwa  mkakati ni kuimarisha  reli  katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Aliongeza kuwa maeneo yatakayonufaika na uboreshwaji wa miundo mbinu hiyo ni pamoja na Songa Mpiji. Mtwara hadi Mbambabay, Songea hadi Mchuchuma na mradi mpya wa reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Bagamoyo.

“Lengo  la miradi hii ni kuhakikisha kuwa tunaleta maendeleo ya kiuchumi  kwa kujipatia fedha za kigeni ambazo  zitatokana na usafirishaji wa mizigo nje ya nchi “ amesema Mhe. Sitta.

Aliongeza kuwa miradi hiyo inatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi wa tisa  ambapo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Jakaya Kikwete ataweka jiwe la msingi tayari kwa utekelezaji.

Aidha alibainisha kuwa kwa kuimarisha miundo mbinu ya reli kutasaidia katika kurahisisha usafirishaji wa mizigo yenye uzito mkubwa kama mafuta, makaa ya mawe na chuma ndani na nje ya nchi.

TASWA DAR HOI TAMASHA LA WAANDISHI JIJINI ARUSHA


 kikosi cha timu ya mchezo wa mpira wa pete ya Taswa Dar mara baada ya mechi kuisha.



Siku moja kabla ya bonanza waandishi wa habari wa mkoa wa Arusha walipata fursa ya kutembelea kiwanda cha bia ya TBL Arusha hapa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo akiwa anawapa maelekezo ya jinsi kiwanda hicho kinavyoweza kufanya kazi  ya kutengeneza beer kwa kutumia mashine na komputa
 nikiwa na waandishi wa habari wakogwe mara baada tu ya kuwasili ndani ya kiwanda cha bia cha Tbl Arushawa kwanza kushoto ni Gwandu  akifuatiwa na Woinde shizza,Mr mchau wakwanza kulia ni Salma Mchovu pamoja na Yasinta..


RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA NATIONAL DEFENCE HEADQUARTERS

 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua kitambaa wakati wa uwekaji jiwe la msingi la Ujenzi wa National Defence Headquarters huko Lugalo jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Mkuu wa majeshi ya Ulinzi  Jenerali Davis Mwamunyange,Watatu Kushoto ni Waziri wa Ulinzi Dkt.Huessein Ali Mwinyi na kulia ni Bwana Hu mwakiklkishi wa kampuni ya ujenzi kutoka China.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange akimuonyesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mchoro wa majengo ya Makao Makuu ya Ulinzi yatakayojengwa eneo la Lugalo jijini Dar es Salaam leo.Wapili kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa National Defence Headquarters Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
(Picha na Freddy Maro).

RC ARUSHA AVIOMBA VYOMBO VYA HABARI KUSAIDIA UCHAGUZI MKUU KUWA WA AMANI


Na Woinde Shizza,Arusha
 Mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda, amevitaka vyombo vya habari nchini kusaidia uchaguzi mkuu mwaka huu umalizike kwa amani na utulivu ili Tanzania iendelee kuwa na sifa ya amani Barani Afrika.

Akizungumza katika tamasha la 10 la vyombo vya habari mkoani hapa, lililowashirikisha wanahabari kutoka mkoa wa Arusha, Manyara na jijini Dar es Salaam, Ntibenda, alisema vyombo vya habari ni wadau wakubwa wa amani na utulivu.

Alisema kama wanahabari wote watafanyakazi kwa weledi, wanaweza kusaidia Taifa kupita salama katika uchaguzi Mkuu wa mwezi Octoba mwaka huu.
Ntibenda alisema kwa mkoa wa Arusha, suala la amani ni la kipekee hivyo ni muhimu kila mdau kuhakikisha amani inakuwepo, kwani Arusha ndio kitovu cha utalii nchini.Alisema anaunga mkono kauli mbiu za Tamasha hilo, kuwa Uchaguzi mkuu bila vurugu inawezekana.

Hata hivyo, alisema kama wa wanahabari wakifanya kazi kwa ushabiki wa vyama bila kujali maadili wanaweza kuchangia kulitumbukiza taifa katika vurugu.

Awali Mkuu wa Idara ya Matukio ya kampuni ya Bia nchini(TBL), Chris Sarakana aliwataka wanahabari kutumia vyema kalamu zao kuhamasisha amani na utulivu nchini.Naye mmoja wa waandaaji wa Tamasha hilo, Mussa Juma alisema waliamua kauli mbiu katika tamasha hilo la 10, kuwa ni uchaguzi bila vurugu inawezekana, ili kuweza kuhamasisha amani na utulivu kuelekea uchaguzi mkuu.


Katika kuhamaisha amani na kukuza utalii wa ndani, wanahabari kutoka Jijini Dar es Salaam walipata fursa kutembelea hifadhi ya Taifa ya Arusha na wanahabari wa mkoa wa Arusha, walitembelea kiwanda cha bia nchini TBL

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA LAANDAA SHEREHE ZA KUMUAGA AMIRI JESHI MKUU MHE. DKT KIKWETE

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Simu ya Upepo   : “N G O M E”        Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM  22150463     Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                      DAR ES SALAAM,  31 Agosti, 2015,
Tele Fax                : 2153426
Barua pepe               : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz
                    

     Taarifa kwa Vyombo vya Habari
          Vyombo vya Ulinzi na Usalama vinaandaa sherehe ya kumuaga Amiri Jeshi Mkuu tarehe 01 Septemba 2015 kwa gwaride rasmi litakalofanyika katika viwanja vya Uhuru, kuanzia saa 2.00 Asubuhi hadi saa 6.30 mchana.
Waandishi wa Habari mnakaribishwa katika uwanja wa Taifa kwa ajili ya Coverage ya tukio hilo la kihistoria.   

Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0756 - 342279
                                         0783- 309963.