Sunday, May 31, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA MARIAN BAGAMOYO

B2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015. Picha na OMR
ba1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo,  kwa pamoja wakikata utepe kuzindua Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015. Picha na OMR
ba3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo, kwa pamoja wakifunua kitambaa kama ishara ya kuweka Jiwe la Msingi la uzinduzi  wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015. Picha na OMR
ba4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na baadhi ya waumini wa dini ya Kikristu, katika Ibada maalum ya uzinduzi  wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015. Picha na OMR
ba5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian, baada ya uzinduzi wa Chuo hicho uliofanyika leo Mei 31, 2015 mjini Bagamoyo. Picha na OMR
BA7
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo, baada ya uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015. Picha na OMR
BA8
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo, baada ya uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015. Picha na OMR
BA9
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo na baadhi ya viongozi na waumuini  baada ya kuzindua rasmi Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015. Picha na OMR
BA10
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisikiliza maelezo kutoka kwa mkandarasi wa majengo ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian wakati akitembelea kujionea ramani ya Chuo hicho baada ya uzinduzi wa Chuo hicho uliofanyika leo mjini Bagamoyo. Picha na OMR
BA11
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na baadhi ya waumini wa Dini ya Kikristu, baada ya uzinduzi wa Chuo hicho uliofanyika leo chuoni hapo mjini Bagamoyo. Picha na OMR

STEPHEN WASSIRA ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS


Stephen Wassira akitangaza nia ya kuwania Urais kwenye Ukumbi wa wa BOT jijini Mwanza leo.
WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira leo ametangaza nia ya kuwania Urais kwenye Ukumbi wa wa BOT jijini Mwanza.
Wassira anawania nafasi ya kugombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Katika hotuba yake wakati wa kutangaza nia yake, Wassira amesema amepata kuteuliwa kuongoza sehemu mbalimbali nchini maana marais wote wa awamu nne walikuwa na imani naye.
Pia amewashukuru wageni waalikwa waliofika kwenye ukumbi kutoka sehemu mbalimbali kwa kuweza kufika na kumuunga mkono huku wakiwa na imani naye.
Kauli mbiu yake ni katika mbio hizo ni Uchumi Imara kwa Tanzania mpya.

MWIGULU NCHEMBA NAYE ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS


Mwigulu Nchemba akitangaza nia ya kuwania nafasi ya kugombea Urais kupitia CCM jioni hii mkoani Dodoma.
NAIBU Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, ametangaza nia ya kuwania nafasi ya kugombea Urais jioni hii kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwa katika Ukumbi wa Mwl. Nyerere uliopo kwenye Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.
Kauli mbiu ya Mwigulu ni ‘Mabadiliko ni Vitendo Wakati ni Sasa.’
Katika hotuba yake Mwigulu ameanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, wazee, ndugu zake, wananchi wake wa Iramba na wananchi wote waliohudhuria hafla hiyo ya kutangaza nia.
Mwigulu pia amempongeza Rais Kikwete kwa kumuamini na kumteua katika nyadhifa mbalimbali.
Amesema ameamua kutangaza nia akiwa mkoani Dodoma ili kuondoa dhana ya ‘ukwetukwetu’ iliyozoeleka miongoni kwa viongozi. Aongeza kuwa Dodoma ni makao makuu ya taifa na chama chake ndiyo maana amefanya hivyo.
Aidha Mwigulu ameeleza mambo matatu yaliyomsukuma kutangaza nia kuwa ni pamoja na:
-Kutaka Mabadiliko
-Kujua mbinu za mabadiliko
-Utayari wa kufanya mabadiliko.
Pia kiongozi huyo amekemea viongozi wanaochaguliwa kwa mazoea wakisingizia uzoefu kwa kueleza kuwa kiongozi anayechaguliwa kwa mazoea ataongoza kwa mazoea na atafanya kazi kwa mazoea maana uzoefu ni mazoea.
Kiongozi huyo ameeleza jinsi anavyozijua fika shida za Watanzania na umasikini walionao hajausoma kwenye vitabu bali ameishi maisha ya umasikini.
Mwigulu ameeleza pia alivyobeba zege baada ya kumaliza chuo kikuu na mke wake akiwa mama ntilie akiwapikia yeye na vibarua wengine wa ujenzi.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MAALIM SEIF IKULU DAR ES SALAAM

2
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad ikulu jijini Dar es Salaam
(picha na Freddy Maro)
1
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad ikulu jijini Dar es Salaam.

EDWARD LOWASSA ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS WA TANZANIA, JIJINI ARUSHA


 Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya jana, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. SOURCE:http://issamichuzi.blogspot.com/
 Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya jana, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola akisalima umati wa watanzania uliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya jana, kumsikiliza  Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa (kulia).
 Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa, kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya jana.
 Mh. Lowassa akiwapungia wananchi.
 Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akihutubia katika mkutano wa hadhawa wa kutangaza nia yake hiyo,  kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya jana.
Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mkewe Mama Regina Lowassa wakati wa mkutano uliofanyika jioni ya Jana. kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Mh. Edward Lowassa akipongezwa na baadhi ya Wabunge waliohudhulia mkutano huo, baada hotuba yake.

UJUMBE WA MAOFISA WA UMOJA WA BENKI ZA AKIBA DUNIANI KANDA YA AFRIKA WAKITEMBELEA ZANZIBAR


Meneja wa Tawi la Benki ya Posta Zanzibar Ndg Justin S.Nandonde akisalimiana na kumkaribisha wageni wake walipotembelea Tawi hilo Zanzibar kujionea utendaji wa Benki ya Posta Tawi la Zanzibar wakiwa katika ziara yao Zenj.
MKURUGENZI
Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Ndg. Sabasaba Moshingi, akitoa maelezo ya
Ujumbe wa Maofisa wa Benki wa Umija wa Mabenki Duniani Kanda ya Afrika,
walipotembelea Benki ya Posta tawi la Zanzibar.
Wajumbe wa Mkutano wa Wanachama wa Umoja wa Mabenki Duniani na Kanda ya Afrika wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania wakati walipofika Tawi la Benki ya Posta Zanzibar,
MKURUGENZI
Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Ndg. Sabasaba Moshingi, akitowa maelezo ya
Ujumbe wa Maofisa wa Benki wa Umija wa Mabenki Duniani Kanda ya Afrika,
walipotembelea Benki ya Posta tawi la Zanzibar
Mkurugenzi wa Tekohama na Uendeshaji wa Benki ya Posta Tanzania Ndg Jema Msuya akitowa maelezo ya kiufundi kwa ujumbe huo.walipotembelea Benki ya Posta Tawi la Zanzibar Mchangani  
Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Zanzibar Ndg. Justin SNdandonde akitowa maelezo kwa ujumbe huo ulipotembelea Tawi hilo na kuagalia ufanisi wa huduma za Benki hiyo kwa wateja wao
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Ndg Sabasaba Moshingi akiwa na wakeni wake wakitoka katika moja ya sehemu ya historia ya Kanisa la Mkunazi Zanzibar.  
Mtembeza Watalii katika Mji Mkongwe seif Ali akitowa maelezo kwa Ujumbe huwa sehemu za historia za Mji Mkongwe wa Zanzibar. 
Maofisa wa Umoja wa Benki za Akiba Duniani Kanda ya Afrika wakiwa katika ziara yao katika mji mkongwe na kupata kuonja Ubuyu wa Kwaissa sokomuhugo Zenj wakiwa katika ziara ya siku mbili Zanzibar baada ya kumaliza Mkutano wao Dar.
Mtembeza Watalii Zenj akitowa maelezo kwa Ujumbe huo wa Maofisa wa Mabenki ya Akiba wakiwa katika ziara yao kutembelea sehemu za historia za mji Mkongwe Zanzibar wakipata maelezo ya Mlango wa Zanzibar