Thursday, April 30, 2015

Shirika la Nyumba la Taifa lang'aa maonyesho ya Mei Mosi Mwanza

 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Julius Ntoga kwenye maonyesho yanayoshirikisha taasisi, asasi na vitengo mbalimbali vya umma na watu binafsi mjini Mwanza jana. Maonyesho hayo ya wiki moja ni sehemu ya sherehe za Mei Dei yanayofanyika kesho kitaifa mkoani humo.

Mhandisi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Julius Ntoga  akiwaelekeza jambo wageni waliofika kwenye banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC) akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo  kwenye maonyesho yanayoshirikisha taasisi, asasi na vitengo mbalimbali vya umma na watu binafsi mjini Mwanza jana. Maonyesho hayo ya wiki moja ni sehemu ya sherehe za Mei Dei yanayofanyika kesho kitaifa mkoani humo. Wa tatu kutoka kushoto ni Meneja wa NHC mkoa wa Mwanza Benedict Kilimba.
 Mhandisi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Julius Ntoga  akiwaelekeza jambo wageni waliofika kwenye banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC) akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo  kwenye maonyesho yanayoshirikisha taasisi, asasi na vitengo mbalimbali vya umma na watu binafsi mjini Mwanza jana. Maonyesho hayo ya wiki moja ni sehemu ya sherehe za Mei Dei yanayofanyika kesho kitaifa mkoani humo. Wa pili kutoka kulia ni Meneja wa NHC mkoa wa Mwanza Benedict Kilimba.
Baadhi ya wageni waliotembelea kwenye banda banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC) jana.
 Baadhi ya wageni waliotembelea kwenye banda banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC) jana.
 Baadhi ya wageni waliotembelea kwenye banda banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC) jana.
 Baadhi ya wageni waliotembelea kwenye banda banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC) jana.

 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Julius Ntoga kwenye maonyesho yanayoshirikisha taasisi, asasi na vitengo mbalimbali vya umma na watu binafsi mjini Mwanza jana. Maonyesho hayo ya wiki moja ni sehemu ya sherehe za Mei Dei yanayofanyika kesho kitaifa mkoani humo.

TIMU YA NYOTA FC YAIBUKA KINARA KOMBE LA NDONDO CUP

Wachezaji wa timu ya Umbrella Garden wakielekea katika lango kupiga mikwaju ya Penalti mara baada ya kutoka sare ya goli 1-1
mchezaji wa Nyota Fc akipiga Penelti katika lango la Umbrela Garden
Naibu Meya wa jiji la Arusha Prosper Msofe akifurahia mashindano ya Ndondo Cup katika Viwanja vya Aicc Jijini Arusha.
.Mashabiki waliojitokeza Uwanjani hapo wakifuatilia meza kuu ambayo haipo Pichani
Mashabiki wa Nyota Fc wakishangilia Ushindi mara baada ya timu yao kuinyuka Umbrella garden magoli 6-5
Mlinda mlango wa timu ya Nyota Fc Hamis maarufu kama Dida akiwa anatizama mpira wavuni.

Ashura Mohamed-Arusha

Timu ya  Soka ya Nyota  Fc imeichapa timu ya Ambrella Garden Fc  kwa  Magoli  Sita kwa Matano na kufanikiwa kuondoka na kombe la Ndondo Cup  Sambamba na Kitita cha Shilingi  Laki  Tano Taslimu  katika fainali za Ndondo Cup zilizofanyika katika viwanja vya Aicc vilivyopo Jijini Arusha.

Akizungumza wakati wa fainali hizo Naibu meya wa Jiji la Arusha Prosper Msofe alisema kuwa mashindano hayo ya ndondo Cup yamewakutananisha vijana wengi ambao wamepata fursa ya kuonesha vipaji  vyao.

Prosper Msofe alisema kuwa mkoa wa Arusha una sifa nyingi lakini katika upande wa Soka kwa sasa Hakuna timu ambayo ipo imara ambao inafanya vizuri katika ligi mbali mbali hapa nchini.

Aidha Msofe alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa wanaibua vipaji zaidi na kutengeneza timu moja ya mkoa Jiji la Arusha limepanga kununua eneo la kiwanja nje ya mji na kutengeneza uwanja bora wa kisasa ambao utawawezesha vijana wanaopenda kandanda mkoani Arusha kupata sehemu za kuonesha vipaji vyao na badae kuchuja vijana 20 ambao wataunda timu moja ambayo itawakilisha mkoa wa Arusha katika mashindano mbalimbali hapa nchini.

Kwa sasa hatuna maeneo ya wazi na hili ni changamoto kwetu vijana wetu wana vipaji lakini hawana sehemu ya konesha tumepanga kununua viwanja na kuvitengeneza ili tuanzishe mashindano mbalimbali ambayo yatapelekea tuapte timu bora itakayotuwakilisha vizuri mkoa wetu wa arusha alisema Msofe

Kwa upande wake waandaaji wa  Ndondo Cup ambayo ni kampuni ya Tan Communication Media wamiliki wa redio 5, Mathew Philip alisema kuwa lengo la mashindano hayo ya ni kutoa burudani ya soka la Mchangani kwa wakazi wa Jiji la Arusha lakini pia kuwapa vijana nafasi ya kuonesha vipaji vyao katika mchezo wa soka.

Mathew alisema kuwa kampuni hiyo itaendelea kutoa burdani mbali mbali kwa wakazi wa Jiji la Arusha huku akisema kuwa mkoa wa Arusha kwa muda mrefu hakukuwa na Soka la Mchangani ambalo lina vijana wengi ambao wana vipaji na kuwawezesha kuonesha uwezo wao kwa kuwa sasa mpira ni Ajira.

Timu zilizoshiriki ni Pamoja na Nyota Fc ambao waliibuka washindi,Ambrella Garden ambao walishika nafasi ya Pili na kujinyakulia shilingi laki tatu,F.F.U Oljoro Fc,Njiro Sports,Tanzanite Fc,Red Star Fc,Lemara Boys,

CLOUDS FM YASHINDA TENA TUZO YA UBORA YA SUPERBRAND KWA MARA YA TATU AFRIKA MASHARIKI

 Picha ya pamoja ya baadhi ya makapuni binafsi waliopewa tuzo bora za viwango,kutoka shoto ni Bi.Dorothy Mashamsham kutoka kampuni ya Mafuta ya PetrolFuel,Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One Bi Joyce Mhaville,Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group Bw. Ruge Mutahaba,Meneja Masoko Bw. Elisa Ernest kutoka kampuni ya bima ya Alliance Insurance.
 Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana Jawad Jaffer akiwa na baadhi ya viongozi wa juu wa kampuni ya Clouds Media Group,kutoka kulia ni Mkuu vipindi wa Clouds FM Sebastian Maganga,wa tatu ni Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji Ruge Mutahaba na Mkuu wa kitengo cha huduma,Promosheni na Tamasha Clouds Media Group.Bi Fauzia Kullane.
 Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana Jawad Jaffer akimkabidhi tuzo bora ya viwango Mkurugenzi wa Uzalishaji na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba,kwenye hafla fupi ya utoaji tuzo bora za viwango hizo iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
 Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akizungumza jambo  na Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana Jawad Jaffer.
 Mkurugenzi wa Uzalishaji na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba akiishukuru taasisi ya SUPERBRAND East Africa mbele ya wageni waalikwa na waaandishi wa habari kwa kutambua ubora wa kituo cha redio hiyo na kuipa tuzo bora za viwango katika Afrika Mashariki kwenye hafla fupi ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
 Baadhi ya Wageni waalikwa na wanahabari wakifuatilia jambo kabla ya utoaji tuzo bora za viwanga a.k.a SUPERBRAND kwa makampuni binafis nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akiwa amepozi na Mtangazaji wa ITV Bwa.Godwin Gondwe

KAMPUNI ya Clouds Media Group imeendelea kuwa kinara kwa ubora wa SuperBrand kwa mara ya tatu katika nchi za Afrika Mashariki.

 Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa Viwango Afrika Mashariki,Jawad Jaffer amesema kuwa matokeo ya utafiti huo ulizingatia maoni ya watalaam wazoefu wa masoko na walengwa wa huduma za bidhaa ambao wanahaki ya kuamua aina ya haki ya viwango bora vya superbrands na kupongeza makampuni ambayo yamefanikiwa kuingia 20 bora.

Utafiti huo umefanywa na idara ya uchambuzi wa viwango  makao makuu nchini  Uingereza kutokana na kuzingatia ushauri wa wataalam wa masoko  na maoni ya watumiaji bidhaa zaidi ya 600 wa huduma hizo.

Amesema kampuni nyingi zilizoingia katika ubora wa superbrands ni 1000 zikapambanishwa na kufanya kampuni 20 ziingie katika ubora superbrands na kufanya kampuni Clouds Media Group kuendelea kushikiria nafasi ya jsu  kwa mwaka wa 2015 -2016.

DKT. MAGUFULI AMWAGIZA MTENDAJI MKUU TANROADS KUKABIDHI BARABARA YA “DART”

Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

WAZIRI wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli amemwagiza  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale, kukabidhi barabara  ya magari yaendayo kasi kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo kasi(DART) ili zianze kutumika wakati sehemu zilizobaki zikiendelea kukamilika.

Hayo ameyazungumza Waziri wa Ujenzi Dkt. Magufuli katika hafla uzinduzi wa barabara ya Uhuru ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam iliyofanyika jana katika viwanja vya Karume.

Pia Dkt. Magufuli amemwaagiza  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo kasi(DART), Bi. Asteria Mlambo aharakishe kutafuta mabasi yaendayo kasi ili ifikapo Octoba Mwaka huu yawe yameanza kufanya kazi katika barabara ya Morogoro Road,jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick, amekemea vitendo vyote vya uhujumu wa miundombinu na uchafuzi wa mazingira ambavyo vinaathiri taswira ya jiji la Dar es salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick, amekemea vitendo vyote vya uhujumu wa miundombinu na uchafuzi wa mazingira ambavyo vinaathiri taswira ya jiji la Dar es salaam.

“Tatizo la wananchi wa Dar es salaam ni kutokutunza miundombinu pamoja na kutupa taka ovyo hali inayosababisha uharibifu wa miundombinu na kupelekea mafuriko wakati wa mvua”, alisema Meck Sadick.

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mitambo ya ujenzi wa barabara ya Uhuru km 3 huku akiwa pamoja na viongozi wengine wa mkoa wa Dar es Salaam jana jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mitambo ya ujenzi wa barabara ya Uhuru km 3 huku akiwa pamoja na viongozi wengine wa mkoa wa Dar es Salaam jijini Dar es Salaam jana.
Sehemu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza katika uzinduzi wa barabara ya Uhuru jijini Dar es Salaam jana.
Picha ya Pamoja ya Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi mbalimbali wa Dar es Salaam pamoja na wananchi wa Manispaa ya Ilala waliohudhuria katika uzinduzi wa barabara ya Uhuru leo jijini Dar es salaam.Picha zote na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA DHARURA WA VIONGOZI WA NCHI NA SERIKALI WANACHAMA WA SADC

AD1

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Hoteli ya Rainbow, jijini Harare, Zimbabwe kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa SDC, uliofunguliwa jana Aprili 29, 2015 na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Jijini unaojadili kuhusu Uendelezaji wa Viwanda. Picha na OMRAD2AD3Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati), akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake katika Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa SDC, uliofunguliwa jana Aprili 29, 2015 na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Jijini Harare, Zimbabwe, kuhusu Uendelezaji wa Viwanda. Picha na OMRAD4Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe akihutubia mkutano huo.AD5Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifuatilia hotuba ya Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, wakati akifungua rasmi Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa SDC, uliofunguliwa leo Aprili 29, 2015, kuhusu Uendelezaji wa Viwanda. Picha na OMR

AD7AD8AD9Baadhi ya Mawaziri wa Tanzania, waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, wakati akisoma hotuba ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa SDC, uliofunguliwa leo Aprili 29, 2015, kuhusu Uendelezaji wa Viwanda. Picha na OMR/
………………………………………………………………………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo Jumatano Aprili 29, 2015, ameiwakilisha Tanzania katika mkutano wa dharura wa Umoja wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika jijini Harare, chini ya Uenyekiti wa Rais Robert Mugabe, Rais wa Zimbabwe, Mwenyekiti wa sasa wa SADC pamoja na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU). Mkutano huo wa siku moja pia umehudhuriwa na Rais Seretse Ian Khama, Rais wa Botswana na Makamu Mwenyekiti wa SADC, Mfalme Muswati III wa Swaziland, Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi, Rais wa Namibia Hage Geingob, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa Lesotho Pakalitha Mosisili, Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma na Rais wa Zambia Edgar Lungu.
Awali akifungua mkutano huo Rais Mugabe alisisitiza umuhimu wa nchi za SADC kuwa na mpango madhubuti wa Viwanda kwa kuwa uwepo wa viwanda utasaidia kupunguza tatizo kubwa linalozikabili nchi hizi hasa ajira, pamoja na uchumi duni unaotokana na ukosefu wa viwanda vya kuboresha bidhaa zinazozalishwa katika nchi za ukanda huu. Mkakati huu uliopitishwa na Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaanza mwaka huu 2015 hadi mwaka 2063. Katika mkakati huu nchi za SADC zinalenga kutanua uhuru wa soko katika utatu wa kanda za Kibiashara yaani SADC, EAC na COMESA ikiwa ni pamoja na kutenga eneo huru la ukanda wa kiuchumi wa nchi za kanda hizi, huku lengo likiwa kufanikiwa upatikanaji wa eneo huru la ukanda wa biashara kwa nchi za Afrika. Masuala mengine ni pamoja na kukuza bidhaa zinazozalishwa katika nchi hizi katika masoko ya Asia ambao ni walaji na watumaji wakubwa wa malighafi zinazozalishwa katika nchi hizi.
Rais Mugabe alifafanua pia kuwa, nchi hizi kwa umoja wake zikiunganishwa utakuta ndizo zina rasimali kubwa ya madini ya Dhahabu, Almasi na hata Gesi na kwamba kama mtengamano huu utakamilika nguvu ya pamoja inaweza kugeuza hali ya maisha ya wananchi wa nchi hizi sambamba na maendeleo ya kiuchumi katika nchi hizo.
Awali akizungumza kabla ya hotuba ya ufunguzi ya Rais Mugabe, Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stargomena Lawrence Tax aliishukuru serikali ya Zimbabwe kwa maandalizi mazuri ya mkutano huu ambao ulikuwa ni mwendelezo wa ule uliofanyika Victoria Falls, Zimbabwe Agosti 17, 2014 mkutano uliotaka nchi wanachama wa SADC pamoja na kupitisha mkakati wake wa Kimaendeleo, upange dira ya utanuaji na uendedlezaji viwanda katika ukanda huu.
Matukio mengine katika mkutano huu ni pamoja na makabidhiano ya Kituo cha Mafunzo ya Utunzaji Amani katika nchi za SADC, makabidhiano yaliyofanywa na nchi ya Zimbabwe chini ya Rais wake Robert Mugabe kwa Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt Stargomena Tax. Kufuatia makabidhiano haya, Chuo hiki sasa kitakuwa kinamilikiwa na SADC na matumizi yake yatahusisha vyombo na wataalamu mbalimbali wanaohusika na masuala ya utunzaji amani ndani ya nchi hizi, ili kupata mafunzo ya kuboresha kazi zao kufuatia migogoro kuwa mingi katika nchi mbalimbali Afrika.
Pia Rais Mugabe alitumia muda huo kuutaka Mkutano huu wa Dharura kutoa heshima zao kufuatia kifo cha Brigedia Jenerali Hashim Mbita aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Kamati ya Ukombozi kwa kutambua mchango wake katika uhuru wa nchi zilizomo SADC na pia mchango wake kwa ajili ya maendeleo ya nchi hizi. Raia Mugabe alimtaja Hayati Brigedia Mbita kama mpiganaji mahiri na kiongozi aliyefanya kazi kwa maslahi ya watu wengi bila kuchoka na kwamba Afrika na SADC vitamkumbuka daima kwa mchango wake huo.
Imetolewa na:    Ofisi ya Makamu wa Rais
                                 Harare, Zimbabwe
                                       Aprili 29, 2015

SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA LAZINDULIWA RASMI NA MKUU WA WILAYA YA KISARAWE MH. SUBIRA MGALU KIJIJINI KISANGA.

 Mgeni Rasmi katika Sherehe za uzinduzi Rasmi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu akizindua Rasmi Mashindano hayo katika kijiji cha Kisanga Mashindano yatakapofanyikia.
 Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akielezea kwa kina kuhusu Shindano la Mama Shujaa wa Chakula
Diwani wa Kata ya Masaki Mh. Pily Kondo Changuhi akiongea na Wakazi wa Kisarawe pamoja na wageni waalikwa katika Sherehe hizo za uzinduzi wa Shindano la Mama  Shujaa wa Chakula
Kikundi cha sanaa cha Sanaa cha Dhahabu wakitoa Burudani ya Shairi wakati wa Sherehe za Uzinduzi wa Shindano la Mama  Shujaa wa Chakula
Mwenyekiti wa Mtandao wa Kijinsia Ngazi ya Kati Kisarawe Bi. Veronica
Sijaona akiwasihi wakina Mama wa Kisarawe kushiriki kwa wingi na
kuchukua fomu ili waweze kuungana na akina mama wengune pindi Shindano
la Mama Shujaa wa Chakula litakapo anza.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisanga Bwana Mohamed Mlembe Akiwashukuru Oxfam kwa kuleta Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 Kijijini kwake.
 Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Subira Mgalu akifurahi kwa Burudani ya Muziki pamoja na wananchi baada ya uzinduzi rasmi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kijijini Kisanga
Mwakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt. Eugania Kapanabo
Akiongea na wageni walikwa katika uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa
Chakula ambapo aliwashukuru Oxfam kwa Kuanzisha mashindano hayo pia
kuona umuhimu wa akina mama kuhusishwa katika kilimo, Umiliki wa Ardhi
na Haki zao za msingi na kusisitiza hii ni Njia moja wapo ya kumkwamua
Mama kiuchumi.
 Mh. Subira Mgalu akifurahi pamoja na Baadhi ya kinamama wa kijiji cha kisanga Baada ya Uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015
Mmoja wa wanakijiji cha Kisanga akijaza fomu za kushiriki katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015
 Baadhi ya Wageni waalikwa na wananchi wa Kisarawe wakiwa katika Sherehe za Uzinduzi Rasmi wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu amezindua Rasmi Shindano
la Mama Shujaa wa Chakula linaloendeshwa na Shirika la Oxfam kupitia
kampeni ya Grow lenye lengo la Kumuwezesha Mwanamke katika kilimo na
kumkwamua kiuchumi.
 
Akizungumza katika Sherehe hizo Mh.
Subira Mgalu amesema kuwa amefurahishwa na Mashindano hayo kufanyikia
wilayani kwake katika kijiji cha Kisanga na kuwasihi wakina mama wengi
kuchukua fomu za ushiriki, na kusisitiza kuwa wakina mama wa Kisarawe
sio wavivu na kuwataka washiriki ipasavyo ili zawadi na mshindi wa
kwanza atokee katika wilaya hiyo. Aliongeza kuwa Shindano hilo linampa
mwanamke uwezo wa kutambua haki zake hasa za umiliki wa Ardhi na
kuongeza kuwa ni shindano ambalo mshiriki anahitaji kuwa
mbunifu,mwenyeuzoefu ili waweze kubadilishana mawazo na kuwa na mbinu za
kisasa za kilimo bora.
 
Nae Mwakilishi kutoka Oxfam
Eluka Kibona alitambulisha rasmi kuwa kijiji cha Kisanga ndicho kitakuwa
wenyeji wa shindano hilo na kuwa shindano hilo linatarajia kuanza rasmi
mwanzoni mwa mwezi wa Nane na kurushwa moja kwa moja na Kituo cha
Televisheni cha ITV na zawadi ya Mshindi wa kwanza kuwa Shilingi Milioni
Ishirini za Kitanzania ambapo Mshindi atapata kwa njia ya kununuliwa
vifaa na zana za Kilimo.
 
Eluka  alizungumzia historia fupi
ya shindano hilo ambalo sasa ni mwaka wa nne kuendeshwa na kusisitiza
kuwa lengo kuu ni kumfanya mwanamke atambulike katika jamii kuwa nao
wakiwezeshwa katika kilimo wanaweza pia wanaweza kumiliki hata ardhi na
kuongeza kuwa shindano hilo linawapa wakina mama njia za kisasa za
kuendesha Kilimo.
 
Pia Diwani wa Kata ya Masaki Mh.
Pily Chamnguhi aliwasihi akina baba wa Kisarawe kuwaruhusu wake zao na
watoto wao wa kike kuchukua fomu kwa wingi na kushiriki katika shindano
hilo kwa kuwa hiyo ni moja ya Fursa ambazo watazipata kupitia Shindano