Tuesday, March 31, 2015

Waziri Lukuvi amaliza ziara ya siku mbili kushuhudia utendaji wa NHC

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akikagua mradi wa nyumba za gharama nafuu za makazi za Kibada, Kigamboni alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo.
 Nyumba za gharama nafuu za NHC Mwongozo, Kigamboni Dar es Salaam zinavyoonekana leo wakati Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi alipozitembelea.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akisikiliza maelezo ya Injinia wa NHC, Elisante Ulomi anayesimamia Mradi wa Mwongozo Housing Estate mchana wa leo.
 Mojawapo ya Nyumba za gharama nafuu za NHC Kibada, Kigamboni Dar es Salaam inavyoonekana leo wakati Waziri Lukuvi alipozitembelea.


  Nyumba za gharama nafuu za NHC Kibada, Kigamboni Dar es Salaam zinavyoonekana leo wakati Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi alipozitembelea.
  Waziri Lukuvi akikagua mradi wa nyumba za gharama nafuu za makazi za Kibada, Kigamboni alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo.

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akikagua mradi wa nyumba za gharama nafuu za makazi za Kibada, Kigamboni alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo.

  Waziri  Lukuvi akikagua mradi wa nyumba za gharama nafuu za makazi za Kibada, Kigamboni alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo.

Nyumba za mradi mkubwa wa NHC Morocco Square, Dar es Salaam zikiwa zinajengwa katika hatua ya msingi,  zinavyoonekana leo wakati Waziri Lukuvi alipozitembelea.

 Nyumba za mradi mkubwa wa NHC Morocco Square, Dar es Salaam zikiwa zinajengwa katika hatua ya msingi,  zinavyoonekana leo wakati Waziri Lukuvi alipozitembelea.
Nyumba za mradi mkubwa wa NHC Morocco Square, Dar es Salaam zikiwa zinajengwa katika hatua ya msingi,  zinavyoonekana leo wakati Waziri alipozitembelea.
Nyumba ya mfano itakayojengwa katika kitalu nambari 300 kona ya kuelekea kwenye Hospitali ya Mikocheni jijini, Dar es Salaam leo wakati Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi alipozitembelea.
Waziri Lukuvi akipata maelezo ya Nyumba ya mfano itakayojengwa katika kitalu nambari 300 kona ya kuelekea kwenye Hospitali ya Mikocheni jijini, Dar es Salaam leo.
Waziri Lukuvi akikagua mradi wa nyumba za NHC Victoria zinazojengwa na NHC alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo.
 Waziri Lukuvi akipata maelezo ya mradi wa nyumba za NHC Victoria zinazojengwa na NHC alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo.
 Waziri Lukuvi akipata maelezo ya mradi wa nyumba za NHC Victoria zinazojengwa na NHC alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo.
Waziri Lukuvi akipata maelezo ya mradi wa nyumba za NHC Victoria kutoka kwa Mkurugeni wa Ubunifu wa NHC, Issack Peter alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo.
Mmojwapo wa mafundi wajenzi wanaojenga nyumba hizo akiwa kazini wakati wa ziara ya Waziri.

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE ROMBO, AVUNA WANACHADEMA TARAKEA

1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika kazi ya kutandaza nyaya za umeme vijijini pamoja na wafanyakazi wa TANESCO wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro katika kijiji cha Kirongo Samanga wakati akiwa katika ziara yake katika jimbo la Rombo akikagua na kuhimiza ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2010  ya inayotekelezwa na serikali huku akihimiza uhai wa chama cha mapinduzi. Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa CCM Ndugu Nape Nnauye.(PICHA NA KIKOZIKAZI CHA FULLSHANGWE-ROMBO-KILIMANJARO)2Mafundi wa TANESCO wakiendelea na kazi ya kusa baza umeme katika kijiji cha Kirongo Samanga wilayani Rombo.018Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Bw. Shanel Ngowi Mkurugenzi wa kiwanda cha kutengeneza Juisi na Maji cha Bella View kilichopo katika Bella.019Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga picha na wafanyakazi wa kiwanda cha Juice Bella View.017Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kiwanda cha  juisi cha Bella View Bw. Shanel Ngowi alipokagua uzalishaji wa kiwanda hicho.020Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa heshima zake katika kaburi la pamoja la wanafunzi wa shule ya sekondari ya Shauritanga waliofariki katika ajali ya moto miaka kadhaa iliyopita mkoani Kilimanjaro. 3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya mradi wa maji wa Kahe kutoka kwa Mhandisi wa maji wilaya ya Rombo Bw.Tesha Andrew wakati alikagua mradi huo.4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na baadhi ya wananchi wakati alipokagua mradi wa maji wa Kahe wilayani Rombo.5Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiunganisha maji wakati alipokagua ujenzi wa  mradi wa maji wa Kahe wilaya ya Rombo.6Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifungua maji ya bomba wakati alipokagua ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Kahe wilayani Rombo.7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na injinia wa maji wilaya ya Rombo Bw. Tesha Andrew.8Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi mbalimbali wakati alipowasili katika uwanja wa Polisi Tarakea wilayani Rombo ambapo mkutano wa hadhara umefanyika.9Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo10Wananchi wa Tarakea wakinyanyua mikono yao juu  wakati mkutano huo ukiendelea.111213Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa polisi mjini Tarakea.1415Mmoja wa akina mama wa CCM akiwasili kwa pikipiki katika eneo la mkutano mjini Tarakea wilayani Rombo.16Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Bw. John Saimon aliyekuwa Katibu wa CHADEMA wilaya ya Rombo na Katibu wa Mbunge wa jimbo hilo Mh. Joseph Selasini akitangaza rasmi kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara mjini Tarakea.17Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikusanya kadi za vijana wa CHADEMA waliojiunga na CCM katika mkutano huo.18Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimvisha kofia Bw. John Saimon  mara baada ya kujiunga na CCM.19Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aki na Kijana John Saimon wakipigiana saluti mara baada ya kumalizika kwa mkuta no wa hadhara katikati anayeshuhudia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa.

TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA YAFANYA KIKAO CHAKE CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI

1
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambaye ni Katibu wa Tume Bi. Agnes Mgeyekwa akitoa hotuba fupi katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi TUMESHERIA.
2
Mwenyekiti wa Tume Mh. Jaji Aloysius Mujulizi akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi
3
Wajumbe wa Baraza wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa kikao cha Baraza.
4
Mwenyekiti wa TUGHE tawi la TUMESHERIA Bw. Fredy Kandonga akizungumza katika kikao cha Baraza.
5
Wajumbe wa Baraza wakiwa katika kikao hicho.
6
Katibu wa Kikoa cha Baraza Bi. Marlin Komba akitoa ufafanuzi wakati wa kikao cha Baraza.
7
Wajumbe wa Baraza pamoja na mgeni rasmi Mwenyekiti wa Tume wakiimba wimbo wa Mshikamano katika kikao cha Baraza la wafanyakazi TUMESHERIA .

SAKATA LA ASKOFU GWAJIMA MAASKOFU KUTINGA KWA IGP DAR ES SALAAM LEO KUMUOMBEA MSAMAHA

 Maaskofu na wachungaji wa makanisa ya kipentekosti wakiingia ukumbini katika Hoteli ya Tamari iliyopo Mwenge tayari kwa kutoa tamko lao.
Katibu wa Maaskofu wa makanisa ya Kipentekosti Dk. Damas Mukassa akisoma tamko la maaskofu hao Dar es Salaam jana, kuhusu sakata la kukamatwa kwa Askofu wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima ambalo leo hii wanatarajia kwenda kumuona Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Mangu kuzungumzia suala hilo. Kulia ni Askofu Dk.Mgullu Kilimba na Askofu Mwaviga Mwafululila.
 Askofu Dk. Paul Shemsanga akizungumza katika mkutano huo ambapo maaskofu hao walitoa tamko lao.
 Wachungaji mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wachungaji mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.


 Wanahabari wakisubiri kuchukua taarifa hiyo.
 Baadhi ya maaskofu wakiwa kwenye mkutano huo.

Mpiga picha wa gazeti la Mtanzania, Hamphrey Shao akipiga picha katika mkutano huo.
 Na Dotto Mwaibale MAASKOFU wa makanisa mbalimbali ya Kipentekoste nchini wamesema wanatarajia kwenda kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu ili kulimaliza sakata la Askofu Josephat Gwajima, kwani kuliendeleza ni kuleta mpasuko wa kidini katika jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa Maaskofu hao, Askofu Dk. Damas Mukassa alisema hakuna sababu ya jambo hilo kukuzwa, kwani mhusika amemsamehe Askofu Gwajima.
Dk. Mukassa alisema ni vema Serikali na vyombo vya usalama vikatumia weledi katika kushughulikia mambo ya kidini na viongozi, kwani yanaweza kusababisha chuki baina yao.
“Tunaomba Serikali isaidie kuondoa mkanganyiko huu, na busara itumike ili kuepusha uvunjifu wa amani katika jamii,” alisema Mukassa.
Katibu huyo alisema wanasikitishwa kukamatwa kwa wasaidizi wa Gwajima, kwa kisinginzio kuwa, walitaka kumtorosha, jambo ambalo haliwezekani.
Alisema wamekaa na kutafakari kilichomkuta Askofu Gwajima, kwani kiuhalisia afya yake ilikuwa salama, hivyo wamebaki na shaka, kama vyombo vya usalama si sehemu salama kama zamani.
Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Gwajima aliyelazwa katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam amejitokeza hadharani na kusema kuwa, hakuna njama  ya yeye kutoroshwa na wachungaji wake na amekiri kuwa, bastola iliyokutwa katika begi ni yake na anaimiliki kihalali.
Alisema iwapo angekuwa na lengo la kutoroka nchini angeondokea Arusha, ambapo alikuwepo, lakini aliamua kuitikia mwito wa jeshi la Polisi na kurejea Dar es Salaam.
Askofu Gwajima alisema baada ya wachungaji wake kupata taarifa  ya kuwa, amefariki ndipo walikwenda kumwona na kumpelekea silaha hiyo ili aweze kujilinda.
“Kwa kuwa, palikuwa na mpango huo nikawaambia wachungaji wangu waende nyumbani kwangu na kuchukua begi lililokuwa chumbani, ambapo ndani yake palikuwa na baadhi ya nguo na bastola  ninayoimiliki kihalali, kwani humo ndani kulikuwa na nyaraka zilizokuwa zikionesha umiliki na vitu vingine,” alisema Gwajima.
Alisema alishangaa kuona Askari wakiwavamia wachungaji wake na  kuwafikisha kituoni kwa kosa la kutaka kumtorosha, jambo ambalo si la kweli.
Gwajima alisema walipofika hospitalini usiku, wachungaji wake walimfikishia begi na kuliweka ndani ya chumba, lakini walitokea watu ambao walijitambulisha kuwa, ni askari na kuomba mzigo ulioingizwa ndani na hapakuwa na ushindani akawapa.
Kuhusu kuzimia kwake, alitoa taarifa ya kusumbuliwa na kichwa kwa muda mrefu bila ya kusikilizwa ili apatiwe huduma, ambapo kilichotokea ndiyo hicho walichokiona.
Gwajima alisema alikuwa akihojiwa na Kamanda wa Upelelezi wa Kanda (ZCO), ambapo aliendelea kumhoji huku akimpa taarifa ya kuumwa kichwa, lakini hakumsikiliza, hivyo mpaka anaanguka na kuzimia hakujua kilichoendelea hadi alipofikishwa hospitalini.
Askofu Gwajima alisema hana mgogoro wowote na Askofu mwenzake na anampenda, kilichotokea alikuwa katika kazi yake ya kukemea aliyoyasema.
Kwa upande, Dk. Willibrod Slaa, mara baada ya kumtembelea Askofu Gwajima hospitalini hapo, alisema haingilii ugomvi wa Askofu Pengo na Gwajima, bali anachokipinga ni upotoshaji unaofanywa na jeshi la polisi dhidi ya raia.
Dk. Slaa alisema polisi waache maneno yao ya kusema mtu anajifanya anaumwa, kwani ni kitendo ambacho kinaonesha kuwa, halithamini utu wa mtu.
Aidha, alisema mambo anayofanyiwa Askofu Gwajima hata yeye aliwahi kufanyiwa akiwa Arusha, baada ya umma kupotoshwa kuwa, alikamatwa na silaha kana kwamba yeye ni jambazi.
“Nilikamatwa na jeshi la polisi huko Arusha, ambapo kisheria unapokuwa na silaha unaisalimisha, nilifanya hivyo na nikaambiwa nijisajili, lakini siku iliyofuata taarifa ikatolewa kuwa, nimekamatwa na silaha, hivyo inaonesha jinsi gani jeshi la polisi linavyofanya hila kwa raia,” alisema.
Dk. Slaa alisema mahakama ndiyo itakayotoa ukweli wa jambo hilo kama ilivyotokea katika kesi ya ugaidi dhidi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakati fulani.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba alisema kinachoonekana kwa sasa ni ukiukwaji wa haki za binadamu ambao unaendelea kufanywa kwa vyombo vya usalama.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alisema anatarajia kufanya mazungumzo na Askofu Gwajima kutokana na kauli yake ili kujua nini kilimsukuma kutoa kauli hiyo.
Akizungumzia sakata hilo la kukutwa na silaha na kuendelea kuwashikilia wachungaji na wafuasi wa Gwajima, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema silaha hiyo haimilikiwi kihalali na Gwajima.
Kova
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kuwa, silaha zilizokamatwa hospitalini katika njama za kumtorosha Mchungaji Josephat  Gwajima hazimilikiwi kihalali.
Aidha, jeshi hilo lilisema kuwa, linaendelea na upelelezi wa watu 15 waliohusika na tukio la kufanya njama za kutaka kumtorosha Gwajima na uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi, Suleiman Kova alisema wanafanya uchunguzi ili kujua kwanini walikula njama na mbinu gani walitumia.
Alisema silaha hiyo ambayo ni bastola aina ya Berreta yenye namba CAT5802 ikiwa na risasi tatu iliyokamatwa juzi, imebainika kuwa, inamilikiwa kinyume cha sheria na wamiliki si halali.
“Silaha zilizokamatwa hazimilikiwi kihalali na wahusika akiwemo Gwajima, hawamiliki kihalali, hivyo kuna kesi ya kupatikana na silaha, ambapo ni kinyume cha sheria.”
“Pale ambapo tutagundua kuwa, kuna makosa yaliyotajwa atachukuliwa hatua kali za kisheria,” alisema.
Alisema kuhusu ni kwanini alipata mshtuko kuhusu suala hilo litajulikana na daktari kwa kushirikiana na mahakama.
Kamishna Kova aliongeza kuwa, upelelezi utakapokamilika na wakili wa Serikali akikubali,  washtakiwa hao watafikishwa mahakamani.
Wakati huohuo, Methusela Gwajima ambaye ni Mwanafamilia amekemea vikali kitendo cha kutukanwa kwa Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na kwamba ni kinyume cha sheria.
Alisema kitendo hicho ni cha fedheha, ni kinyume cha sheria ya nchi na kwamba, alitakiwa kumfuata na kumweleza na si kumtukana matusi makubwa na kumsababishia aibu kubwa.
Aliongeza, Gwajima abebe msalaba wake mwenyewe kwa kwenda kuomba msamaha, kwani aliamua kumchafua kiongozi huyo wa kiroho, na kwamba itamsaidia kurudisha heshima ya mwanzo aliyokuwa nayo. 
(Imeandaliwa na mtandao www.habari za jamii.com)