Tuesday, December 08, 2015

KAMPUNI YA BE FORWARD YAKABIDHI GARI AINA YA TOYOTA IST KWA MSHINDI JIJINI ARUSHA KATIKA PROMOSHENI YA JISHINDIE IST

DSC00871
Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Be Forward Geoffrey Mibaz akimkabidhi mshindi ambaye ni Mwalimu wa Shule ya St. Jude Mkoani Arusha aliyeambatana na familia yake,  Rasul Mngazija gari aina ya Toyota IST yenye thamani ya Sh. Milioni 12 katika promosheni ya jishindie IST iliyofanyika jana jijini Arusha iliyoendeshwa na kampuni ya uuzaji magari ya Be Forward Tawi la Tanzania
DSC00877
Muonekano wa Gari aina ya Toyota IST yenye thamani ya Sh. Milioni 12

DSC00875
Mshindi Rasul Mngazija akiwa na mkewe Hazina Msechu wakiwa na nyuso za furaha ndani ya gari aina ya IST walioshinda katika promosheni iliyokuwa ikiendeshwa na kampuni ya Be Forward Tanzania
DSC00874
Rasul Mngazi akiwa ndani ya gari akijaribu kuwasha huku akiwa na uso wa tabasamu
DSC00854
Afisa masoko kampuni ya Be Forward tawi la Arusha Gooluck Lyimo akiwa anamkabidhi mshindi documenti za gari ofisini kwao jijini Arusha jana mara baada ya kutembelea ofisi hizo

DSC00850
Meneja Masoko wa Kampuni ya Be Forward Geoffrey Mibaz akionyesha documenti za gari kwa waandishi wa habari pamoja na wadau waliofika jana katika promosheni hiyo ya Shinda Gari
DSC00837
Afisa Masoko Shufaa Kilango akiwa anatoa maelezo kwa ugeni uliotembelea ofisi zao jana jijini Arusha
DSC00842
Muonekano wa ndani wa ofisi za Be Forward jijini Arusha
DSC00884
Aliyeshika mfuko ni mkurugenzi wa jamiiblog Pamela Mollel akiwa na timu nzima ya Be Foward Arusha pamoja na mshindi wa gari IST akisindikizwa na familia yake
DSC00887
Familia ya Be Forward wakiwa katika picha ya pamoja na mshindi
DSC00881
Wafanyakazi wa Be Forward wakiwa katika nyuso za furahaaaa
SAM_6844
Rasul Mngazija akiongea katika halfa hiyo ambapo alisema kuwa “Sikutegemea kwanza kama ntakuwa mshindi kwani nilifika katika ofisi zao kwa ajili ya kuagiza gari nyingine,”
SAM_6822
Meneja Masoko wa Kampuni ya Be Forward Geoffrey Mibaz akiongea katika ofisi za Be Foward jijini Arusha
SAM_6841
Mwandishi wa habari  gazeti la Mwananchi na Citizen Musa Juma akiangalia zawadi alizopewa na kamapuni hyo
SAM_6794
Mshereheshaji wa halfa hiyo Akida ambaye pia ni mtangazaji wa kituo cha Radio 5 akifanya yake  katika ofisi za Be Forward jijini Arusha(Picha na 

Pamela Mollel wa Jamiiblog Arusha)
Mwalimu wa Shule ya St. Jude iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha Rasul Mngazija ameshinda gari aina ya Toyota IST yenye thamani ya Sh. Milioni 12 katika promosheni iliyofanyika jijini Arusha iliyoendeshwa na kampuni ya uuzaji magari ya Be Forward Tawi la Tanzania
Akizungumza Mara baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo jana katika ofisi za kampuni hiyo Mwl. Mngazija aliyekuwa ameongozana na famlia yake kupokea zawadi hiyo aliishukuru BE Forward  kwa kumchagua kuwa mshndi katika promosheni hiyo.“Sikutegemea kwanza kama ntakuwa mshindi kwani nilifika katika ofisi zao kwa ajili ya kuagiza gari nyingine,”
“Nikiwa hapo ndipo waliponijulisha pia kwamba kuna promosheni wanaendelea nayo kwa wateja wanaoagiza magari kupitia kwenye ofisi zao. Kwa hiyo nilijaza fomu na kuendelea kusubiria,”Mngazija aliendelea kusema kwamba kufanikiwa kuibuka mshindi wa zawadi hiyo gari kumemuongezea chachu ya kuhamasisha watu wengine zaidi kutumia huduma za kampuni hiyo kwa kuwa balozi wa Be Forward

Kwa upande wake Meneja wa Masoko wa Kampuni ya Be Forward Geoffrey Mibazalisema kwamba kampuni hiyo itaendelea kuwa karibu zaidi na jamii katika shughuli zake ikiwamo kurudisha sehemu ya faida inayopatikana.
Alisma baada ya kufungua ofisi zao jijini Dar es Salaam sasa wamefungua katika jiji la Arusha lengo likiwa ni kuwasogezea huduma zaidi wananchi.Katika uzinduzi huo ulioambatana na kumkabidhi gari mshindi, Geofrey aliwataka watanzania na watu wengine wanaopanga kununua magari kutumia zaidi kampuni hiyo kwa ajili ya usalama wa fedha na mali zao.
“Mtu yeyyote anayekuja kuagiza gari ofisini kwetu tunampa ushauri wa bure, wa aina gani ya gari anatakiwa kuagiza masuala ya kodi,”
Pia aliongeza kuwa wanatoa huduma ya ushauri kwa wateja wao kabla ya kuagiza gari huku akiwataka wananchi kutumia kampuni hiyo kuagiza magari kwakuwa usalama upo wa kutosha ukilinganisha na wajanja wa mjini

No comments: