Friday, December 04, 2015

COSATO CHUMI AMALIZA TATIZO LA VITANDA HOSPITAL YA MAFINGA MJINI

 Pichani Mbunge wa jimbo la Mafinga mji ni Cotato Chumi akimkabidhi msaada wa vitanda ,magodoro pamoja na vifaa mbalimbali kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Mafinga Dk Abdul Msuya juzi
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatiliwa ugawaji wa vifaa hivyo wakati wa makabidhiano
Mbunge wa mafinga mjini Cosato Chumi akikabidhi vifaa hivyo kwa vitendo
Baadhi ya wadau na wanachama wa chama cha mapinduzi ccm walihudhulia tukio hilo .
…………………………………………………………………………………..
 
TATIZO la upungufu wa vitanda katika wodi ya
akina mama na watoto
 katika hospitali ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
ambalo kwa muda mrefu limekuwa chanzo cha msongamano na uwalazimu
baadhi ya wagonjwa kulala sakafuni sasa limepatiwa ufumbuzi baada ya
uongozi wa hospitali hiyo kupokea msaada wa vitanda na vifaa tiba kutoka
kwa mdau wa maendeleo katika sekta ya afya.

Mbunge wa Mafinga Mjini (CCM) Cosato Chumi alisema kuwa kwa muda mrefu hospitali hiyo ilikuwa ina upungufu wa vifaa mbalimbali ikiwemo vitanda hali iliyofanya kuandika maandiko mbalimbali kwa wahisani  wa nje ya nchi ili kuweza kumsaidia kupata vifaa hivyo .
  
Alisema kuwa umefika wakati sasa wadau mbalimbali, mifuko ya kijamii na makampuni kujenga utamaduni wa kusaidia watu wenye mahitaji mbalimbali wakiwemo watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na wagonjwa hospitalini kwani kufanya hivyo ni sehemu ya kurudisha kile wanachokitapa kwa jamii.
 
“Unajua afya ni kila kitu katika maisha ya binadamu hivyo lazima nitekeleze ahadi zangu nilizotoa wakati wa kampeni na wanachi lazima tufanye kazi kwa kujituma ili tumuunge mkono rais wetu ambaye anania ya ya kutuletea maendeleo na kuwataka wadau mbalimbali kusaidia jamii zenye mahitaji na kuacha kutegemea serikali pekee “ alisemaChumi aliwaomba wananchi wa jimbo hilo kuunga mkono kwa kufanya kazi kwa nguvu zote ili walete maendeleo kwa pamoja maana akifanya kazi pekee yake bila wao hawezi kuleta maendeleo pekee yake.
  
Msaada huo wa vitanda 16 na magodoro 11 na vitu
mbalimbali umetolewa
 na taasisi binafsi inayojishughulisha na masuala ya
afya ya nchini Astralia ijulikanayo kama “Rafiki Surgical Mission” kwa
uratibu wa ofisi ya mbunge wa jimbo la Mafinga mjini 
Alisema kuwa msaada huo aliopatiwa  na rafiki zao hawajatoa hata
senti
 tano bali huwa marafiki hao wanachangishana fedha na kununua vifaa
hivyo na kisha kuvisafirisha mpaka bandari kavu ambapo hapo ndio hutumia
garama kusafirisha vifaa hivyo mpaka sehemu husika
“Ndugu
zangu nadhani kila mmoja alikuwa akifahamu machungu waliyokuwa wakipata
mama zetu wanapokuja kujifungua kwa kukosa sehemu za
 kujifungulia lakini
 leo hii msaada huu utatusaidia sana na yoyote atakayeguswa na anaweza kuja na kuchangia chochote maana mufindi ni yetu sote na mufindi itajegwa na wanamufindi wenyewe”alisema

Alisema jambo kubwa lilokuwa likimuumiza kicha kila kukicha ni tatizo la vifaa
katika hospital, elimu  pamoja na tatizo la maji hivyo ni
 wakati
 wawanamafinga kushikana kwa pamoja katika kusumkuma mbele gurudumu la maendeleo ili kuendana na kauli mbiu ya sasa ya HAPA NI KAZI TU.
Akipokea msaada
huo kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Mafinga dk Abdul Msuya alisema
kuwa msaada wa vitanda hivyo na magodoro na  vifaa
 mbalimbali
 utakuwa umemaliza kabisa tatizo la vitanda hospitalini hapo licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kumalizika endapo kutatokea mdau mwingine kuwasaidi Kwa upande wake katibu wa ccm wilaya ya Mufindi Jimsoni Muhagama alimpongeza
mbunge huyo kwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo huku akimwambia kuwa
ni wakati wa kutekeleza kazi kwa vitendo na wala si
 maneno kwani
 wananchi wanapaswa kutatuliwa kero mbalimbali zinazowakabili badala ya kupiga porojo zisizo na msingi .
Mhagama
alisema kuwa kila mmoja anapaswa kuwajibika ipasavyo katika nafasi yake
kwani kasi anayokwenda nayo Rais John Magufuli si ya
 mchezo bali ni ya
 mchaka mchaka na ili nchi iweze kusimama katika mstari ulionyoka kila mmoja anapaswa kucheza wimbo wa mchaka mchaka
‘’Huuu si
wakati lelemama huu sio wakati mchezo mchezo ni wakati wa uwajibikaji
,hakika Tanzania tumepata kiongozi mchapa kazi tazama sasa
 ni siku ya 27
 nchi inaongozwa na watu wanne lakini kila sektaa imenyoka na mimi  nasemaa Magufuli wanyooshe tu kwa kuwa watu walikuwa wakifanya kazi kwa mazoeya bila ya kuangalia madhara wanayopata watanzania
swengi
Hata
hivyo Mhgama alisema kuwa kwa kuwa kipindi cha muda mchache nchi inaongozwa
na watu wachache na nchi imesimama haoni sababu ya kuwa na
 baraza kubwa
 la mawaziri bali Rais Magufuli achague baraza dogo kama la watu
10 ili kupunguza mzigo kwa serekali yake ya kuwa na mawziri wengi
wasiokuwa na tija  .

No comments: