Friday, November 28, 2014

MJADALA WA SAKATA AKAUNTI YA ESCROW BUNGENI LEO

Nchambi: Anailaumu serikali kwa kuchelewesha kuleta jambo husika bungeni, watanzania wana hamu ya kujua fedha ni nani? Wakili wa TANESCO (Mkono) alishauri kufunguliwa akaunti (ananukuu maandiko ya biblia kuhusu kuheshimu mamlaka), anasema kila mtu atawajibika kwa namna yake.

Mbunge wa Kishapu (CCM), Suleiman Masoud Nchambi.
Hasara nyingine tuliyoipta ni gharama za mawakili(bilioni 62) ambayo watuwengi hawaigusii, kesi imeenda miaka kumi hivyo haki kupatika ilionekana ni ngumi na bado tunadaiwa. Baada ya malipo tutakuwa tumepoteza bilioni 90 kwenye kesi.
Lazima tuangalie pande zote mbili, sehemu serikali inapotakiwa kuwajibika pia watu binafsi watatakiwa kuwajibika, fedha baada ya kutoka escrow na maamuzi(ruling) kutoka. Ilionekana bado TANESCO bado ingedaiwa lakini lazima serikali ituletee majibu dhidi ya mgogoro wa capacity charges.
Wizara ya nishati na madini ilikuwa na matatizo mengi kabla ya Prof Muhongo, tunapojadili hoja tujadili yenye mashiko. Tanzania ina kata 3804, Muhongo ameingia katika bajeti moja na kusambaza umeme vijiji vingi (ananukuu Quraan kuhusu kusema kweli).
Ananukuu Biblia watu wasiwe wakorofi(kumuingilia wakati anaongea), fedha za Escrow sio ugomvi ya ubadhilifu wa fedha pekee. Bei ya umeme tunaouziwa imeshika baada ya Muhongo, anasema kunaweza kuwa na chuki ya kibiashara hivyo tutumike kwa masilahi ya nchi na sio wafanyabiashara.
Kuwatisha wawekezaji sio jambo jema na tutapoteza imani na wawekezaji, waliotajwa kuhusika na fedha hizo serikali iwachunguze. Wapo watu wameingiziwa fedha kwenye akauti zao. Ananukuu Quraan kuhusu haki na batili, anapata mashaka mbunge kwenda kukagua wakati yeye pia anatiliwa mashaka.
Kuna list ya watu itakuja hapa bungeni, kuna watu wa kambi ya pili wametetea hili jambo kwa upole na unyonge. Wabunge tusimamie haki na tuseme ya kweli, tulianza na Mungu na tuendelee na Mungu. Anamsifu Muhongo kwa kazi anayoifanya wizarani. Waziri mkuu ametajwa, ametajwa kwa namna tofauti na kuna watu ni majeruhi. Ananukuu Quraan kuhusu wajuzi, niwatie moyo mjadala uende vizuri.
Mwigulu Nchemba: Ukububwa wa jambo tunaongelea maadili na maslahi ya watanzania, nitajikita eneo linalogusa wizara ya fedha. Nazipongeza taasisi zote zilizoshiriki kwenye ripoti hii(anazitaja). Tangu utaratibu huu uanze, chimbuko la ripoti hii ni serikali yenyewe.
Kodi, imegawanyika maeneo matatu, VAT haikukatwa na kukatokea mkanganyiko, TRA inashughulikia na ni ilikua ni bilioni 26.97 lakini baada ya kugundua kuna kodi ya wananchi haijakusanywa ndipo wakakusanya bilioni 4.1 na ukaguzwa ni wa kwenye Escrow na sio IPT. Niwahakikishie watanzania kuwa kodi hii italipwa, hatuwezi kuacha kodi kwa tajiri halafu tukimbizane na mama mjane anaeuza mchicha barabarani.
Kodi ya pili ni iliyotokana na kukosewa kwa mahesabu na ni lazima ilipwe, TRA imeshaandika barua ya Novemba 2014 ya kufuta cheti(certificate). Brela wameshapewa notice ya kufuta capital gain certificate iliyotolewa kipindi kilichopita. Hatua imechukuliwa na serikali na tuko makini. Kuna watu wasio waaminifu, kuna mtu badala ya kuandika $ milioni 6 akaandika Tshs milioni 6 na badala ya kuandika $milioni 20 ameandika Tshs 20.
Naagiza mamlaka ya TRA ifanye uwajibishaji wa ndani na akafanye kazi nyingi na hakuna uchunguzi juu ya uchunguzi. Mtu aliyeiba ukimfukuza kazi ni kumpa likizo akatumie fedha alizoiba hivyo mamlaka husika wachukue hatua. Tumeambiwa kuhusu pesa zilizogawiwa, na wenyewe walipie kodi kabla ya tarehe 31/12/2014. Baada ya tarehe hio TRA wafatilieni mmoja mmoja. Kuna taarifa pesa zilitoka kwenye mafurushi na magunia, nimefatilia na wamefata sheria.
Anatoa agizo kwa Stanbic na Mkombozi watoe matamko, wateja wao wana haki ya kujua reputation ya benki yao. Niwaombe wabunge, kuna kuongea na kuchukua hatua na watanzania wanasubiri kuchukua hatua. Tumekua tunawachukulia hatua wanasiasa lakini wataalamu waliosomeshwa kwa kodi hawajibiki popote.(Muda umeisha)
Kafulila: Benki ya stanbic wamemfukuza kazi aliefungua akauti ya PAP amefukuzwa kazi asharudi kwao Uganda hivyo hizi ni dalili kuwa kuna makosa yalifanyika ndo maana hatua zimechukuliwa.
Mnyaa: Nampongeza Nchemba kwa kusimama katika ukweli, economic hitman ni kama Mafia, na washawahi kuziangusha nchi (anazitaji) na miradi mikubwa wanayohusika nayo ni kama ya umeme, tujiulize kama hawajaingia Tanzania.
Nyaraka nyingi zilizothibitishwa akatoa mbunge kuzikanusha ni kosa, Muhongo anasema ana nyaraka muhimu kwannini hakuzipeleka kwa CAG, maadili ya viongozi ambayo katika maazimio ya Richmond yaliazimiwa. Mwanasheria wa RITA leo yupo katika IPTL na mgao. CAG anapinga wabunge kuwa wajumbe wa bodi, leo hii sio conflict of interest? Wahusika ni IPTL na TANESCO na BoT NI MSIMAMIZI.
Imekuwaje BOT kutuma pesa PAP badala ya IPTL, kwa nini imekiuka akouti ya Escrow.
Mchangiaji: Ni dhambi kudhania PAC ni chombo cha wapinzani, kama kuna mapungufu ni bora tuyarekebishe, wanaofanya haya wanakula na viongozi wetu wa juu. Katika hili wananchi wameathirika sana kutokana na balaa hili la overcharge.
Haiwezekana watu kuchukua pesa za dhulma na sisi wanyonge kuzilipa. Hakuna yoyote aliye alie juu ya sheria, uwajibikaji ni la lazima. Mbona alijiuzulu kwa mzigo wa watu wengine kwakuwa walikuwa chini yake.
Ashumta Mshana: Kuna taarifa tatu, ya serikali, PAC na CAG ila ukisoma zote zimetofautiana hivyo kutufanya tusielewe vizuri, taarifa ya PAC ina mapungufu mengi. Mbowe ametajwa kupokea pesa lakini haijataja.
Taarifa: PAC inafanyia kazi taarifa ya CAG, hayo majina unayoyasema hayakuwepo.
Asumpta: Kwani mapendekezo ya PAC yapo kwenye taarifa ya CAG
Mwenyekiti: Si vizuri kutaja majina ambayo hayapo kwenye ripoti.
Asumpta: Benki ya Mkombozi pekee majina yake ndio yameletwa, tunataka na majina ya Stanbic. Waziri mkuu hawezi kuondoka, tunao uhakika mbele yetu. Ripoti ya CAG hakukuwepo kuwa Muhongo amehusika moja kwa moja.
Waziri wa nchi: Kwa mujibu wa kanuni, nasogeza muda wa bunge mpaka saa nane mchana.
Nkumba: Serikali lazima ichukue hatua, haiwezakini ukapewa bilioni na Lugemalila lazima aseme alitoa hizo fedha kwa ajili ya nini. Nimshukuru Lugemarira ametusaidia sana kumaliza hili jambo hili. Hata kama ni chama cha mapinduzi tuwashughulikie.
Ole Sendeka: Hapa hamna uwajibikaji wa pamoja bali mtaje wahalifu, wahalifu lazima wabebe, hakuna majina ya watu kwenye mauzo, huhitaji akili kubwa kujua kuwa hapa kuna uhalifu, watu wamekwepa kodi bilioni 8.7 kwa watu kughushi, haihitaji upoteze muda, utajua hapa kuna utapeli tangu mwanzo, kusimama na kusema ofisi ya CAG ni uongo mtaiambia nini dunia kwamba vyombo vyetu vyetu tulivyoviweka ni uongo. Hii ni dhambi, watu wanaopata fadhila za wizara wanakaa kwenye kamati.
Muhongo kafanya kazi ya udalali, watanzania ni vyema wakapata majibu kama ni kweli ama la, kwenye mkataba unamtaja mheshimiwa Muhongo(anaunukuu)
Muhongo anaomba taarifa kuwa anachosema Sendeka ni uongo na kilichoandikwa si lazima awe sahihi, niwahakikishie watanzania hakuna mwekezaji yeyote nchi hii ambae hajaja kuonana na mimi.
Zitto Kabwe: Nyaraka za CAG zimekua verified lakini za Muhongo alizozitoa uongo, mkataba unasema walikutanishwa na Sendeka.
Ole Sendeka: Nimesoma kwenye mkataba ambao pia uko ofisini kwako na wewe umeshiriki, profesa aliita nyaraka nilizozileta ni za kufungia maandazi, hakuna shaka kuwa Muhonga alikua dalali katika dili hili, nina uhakika miongoni walionufaika ni waliowezesha dili hili. Ingekuwa haunizidi umri ningesema ulichofanya ni ukuwadi.
Kodi la ungezeko la mtaji kila mmoja anajua tulivyoibiwa, ushauri wa nwanasheria mkuu umekwepesha kodi nchi hii, tunamlinda kwa sababu gani, Muhongo na Maswi pia bodi ya TANESCO inabaki kwa sababu gani! Tulimwajibisha, waziri leo anapewa masaa mawili kuitetea serikali ambayo si ya serikali bali wake mwenyewe.
Mlienda Kunduchi kugawana fedha kwa njaa. Isaidieni nchi hii, hamuwezi kukwepa kodi alafu mkaja kutetea. Mwisho tupige kura juu ya mambo haya. Hatujakokotoa na bado tukampa Lugemalira lakini alilipa mabilioni ya kodi wakatiSeth mmemuacha.
Mkono mlimpa dili wenyewe na mwanasheria wa TANESCO mkamfukuza bila haya, mi naomba waziri mkuu arudishwe. Huitaji kuwa msomi kujua. (Muda umeisha)

SHEIKH PONDA ASHINDA RUFAA YAKE


  Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo huku wakipaza sauti baada Sheikh Ponda kushindarufaa ya kupinga hukumu ilitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kuvamia na kujimilikisha kwa nguvu kiwanja cha Markaz Chang’ombe jijini Dar es Salaam. Hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa, Mei 9, 2013. (Picha na Francis Dande)
 Wafuasi wa Sheikh Ponda.
 Wafuasi wa Sheikh Ponda Issa wakitoka Mahakamani.
  Wafuasi wa Sheikh Ponda Issa wakitoka Mahakamani.
 Gari la Polisi.
 Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti.
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda (wa pili kushoto) akitoka katika chumba cha Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kushinda rufaa ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kuvamia na kujimilikisha kwa nguvu kiwanja cha Markaz Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa chini ya ulinzi wa askari wa Magereza wakati  akitoka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda akitoka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya kushinda rufaa ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kuvamia na kujimilikisha kwa nguvu kiwanja cha Markaz Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
 Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikimakabili.
 Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti baada ya Sheikh Ponda kushinda kesi iliyokuwa ikimakabili.
  Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti baada ya Sheikh Ponda kushinda kesi iliyokuwa ikimakabili.
Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti baada ya Sheikh Ponda kushinda kesi iliyokuwa ikimkabili.
Mfuasi wa  Sheikha Ponda akitoka Mahakamani.

 Ulinzi ukiwa umeimarishwa nje ya Mahakama Kuu Dar es Salaam wakati wa kesi ya Ponda.
  Wafuasi wa Sheikh Ponda Issa wakiwa wamelizunguka basi la Magereza alilokuwa amepanda Sheikh Ponda wakati akielekea mahabusu ya gereza la Keko.
  Wafuasi wa Sheikh Ponda Issa wakilifukuza basi la Magereza alilokuwa amepanda Sheikh Ponda wakati akielekea mahabusu ya gereza la Keko.

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE TANDAHIMBA


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitembelea maghala ya kuhifadhia korosho wilayani Tandahimba, Mtwara wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi na kupkea kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
 Kinana akisaidia kumtwisha gunia la korosho mmoja wa wapagazi wa maghala ya kuhifadhia korosho, wilayani Tandahimba.
 Kinana akikagua mradi wa maji wa Mkupete katika Kata ya Mahuta.
 Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la Ofisi ya CCM Kata ya Mdimba, wilayani Tandahimba
 WANANCHI wakisikiliza kwa makini wakati Kinana akihutubia katika Kata ya Mahuta, wilayani Tandahimba
 Kinana akitembelea baadhi ya nyumba 100 zilizoezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa katika Kijiji cha Nanyanda, wilayani Tandahimba


Kinana akiwafariji baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Nanyanda ambao wameathirika baada ya nyumba zao kuezuliwa na upepo wa mvua

 Kinana akiendelea kukagua nyumba hizo zilizoezuliwa
 Kinana akipandisha bendera katika Shina la CCM la wakereketwa mjini Tandahimba 
 Kwaya ikitumbuiza wakati wa mkutano wa hadhara Mjini Tandahimba
Aliyekuwa Katibu wa Chadema Wilaya ya Tandahimba, Jaffari Hassan ambaye amehamia CCM,  akielezea sababu zilizosababisha ahamie chama hicho wakati wa mkutano wa hadhara, mjini Tandahimba.Hassan hivi sasa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wa wilaya hiyo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF wa Kata ya Kitama akipongezwa na Kinana baada ya kuhamia CCM katika mkutano huo wa hadhara. Hivi sasa ni Mkobo ni Green Guard wa CCM Wilaya ya Tandahimba
  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Tandahimba ambapo alimtaka Katibu Mkuu wa CUF, Seif Shariff Hamad aache kuwahadaa wananchi kwamba wasiipigie kura Katiba inayopendekezwa akidai ni ya CCM na kwamba akitaka kuwa mkweli aachie ngazi nafasi ya Umakamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya CCM inayoongozwa na CCM
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano huo wa hadhara, ambapo ameahidi kukutana wadau na viongozi wa mikoa ya inayolima korosho nchini, ili wajadili kero mbalimbali za wakulima wa zao hilo na kuzipatia ufumbuzi wa kudumu
Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, akielezea utekelezji wa miradi mbalimbali jimboni humo wakati wa mkutano huo wa hadhara.

Thursday, November 27, 2014

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AMALIZA ZIARA YAKE NEWALA, LEO YUKO TANDAHIMBA

1
10
Wafanyakazi wa kiwanda hicho wakiendelea na kazi ya kubangua korosho
6
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mhandisi wa Maji Newala Bw. Nsajigwa Said wakati alipotembelea chanzo cha maji cha Malatu mjini Neawala.
7
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua mradi wa maji katika kata ya Malatu kushoto ni mkuu wa mkoa wa Mtwara B. Halima Dendegu.
8
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kusuka nondo katika ujenzi wa tanki la maji la kijiji cha Kilidu kwa pamoja na wafanyakazi wa katika mradi huo wa tatu kutoka kulia aliyesimama ni Mbunge wa jimbo la Neawala Mh. George Mkuchika.
9
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Dr Yudas Ndugile Mganga mkuu wa wilaya ya Newala wakati alipokagua jengo jipya la Kituo cha Afya Mkwedu kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa wilaya ya Newala BwMarx Simon Kamaoni na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendegu.
11
Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishuhudia aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Wilaya ya Newala Chadema Bw. Adam Nangwanda Sijaona akivua shati la CHADEMA na kuvaa la CCM mara baada ya kuondoka katika chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mahakama mjini Newala.
12
Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitupa shati hilo
13
Aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Wilaya ya Newala Chadema Bw. Adam Nangwanda akiwa amekabidhi kadi yake na ya mke wake kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kujiunga na CCM mjini Newala kulia ni Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
14
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mahakama mjini Newala
15
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakisisitiza jambo katika mkutano huo.
16
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakikabidhi pikipiki kwa vijana ambazo zimekopeshwa kwao ili kujikomboa kiuchumi.
17
Umati wa watu wakisikiliza mkutano huo.