Friday, February 28, 2014

Tanzania Yafunguka Kuhusu Michepuko

Kila Kona ya Nchi,Jambo Kuu linaloongelewa sasa ni MICHEPUKO! Kwa mara ya kwanza Tanzania imefunguka kuhusu mambo yanayosababisha Michepuko kwenye mahusiano na namna Michepuko hiyo inavyofichwa!

Kupitia FACEBOOK Page ya Michepuko www.facebook.com/Michepuko ,Twitter @Michepuko na Instagram @Michepuko... WaTanzania wamepata Nafasi ya kuongea kwa uwazi kabisa kuhusu Sababu za Michepuko, Namna ya kuivumbua na Jinsi ya kuiepuka Michepuko katika Mahusiano yako.

Ni vituko vitupu kwenye Social media, Umewahi Kusikia mtu kaseviwa kinukta "." kwenye simu? Wengine wameseviwa "Nani?" au "Fundi Choo"... Tembelea Facebook,Twitter na Instagram za Michepuko ujionee

Tanzania Bila Ukimwi,inawezekana. Baki Njia Kuu,Michepuko Sio Dili. Epuka Ukimwi

Tume ya Taifa ya uchaguzi imetangaza ratiba ya uchaguzi mdogo wa jimbo la CHALINZE kama ifwatavyo:-

 Tume ya taifa ya uchaguzi imetangaza ratiba ya uchaguzi mdogo wa jimbo la CHALINZE, mtakumbuka kuwa jimbo hilo limekuwa wazi baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo bwana Said Bwanamdogo kufariki dunia tarehe 22 Januari 2014 kwenye hospitali ya MOI jijini Dar es salaam. 

Ratiba ya uchaguzi kwenye jimbo hilo iko kama ifuatavyo:-
 
1. Uteuzi wa wagombea  - Tarehe 12 Machi 2014
 
2, Kampeni na Uchaguzi - Tarehe 13 Machi 2014
 
3. Siku ya Uchaguzi - Tarehe 6 April, 2014
 


Tarehe ya wagombea ubunge kuchukua Fomu za uteuzi kwa msimamizi wa uchaguzi ni kuanzia tarehe 03 Machi, 2014 hadi tarehe 12 Machi, 2014(Siku ya uteuzi) Kabla ya saa 10:00 Alasiri.
 

Wagombea wanatakiwa kuwasilisha fomu za uteuzi kwa msimamizi wa uchaguzi siku ya uteuzi si zaisi ya saa 10:00 Alasiri.

MWIGULU AZINDUA RASMI KAMPENI ZA CCM KALENGA KWA KISHINDO


Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Godfrey William Mgimwa akibebwa Juu na Wanachama/wapenzi wa CCM mara baada ya Kuwasili Viwanja Vya Stendi-kata ya Ifunda.

Mapokezi Mazito yakiendelea ya Naibu Katibu Mkuu CCM-Bara na Kijana Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey William Mgimwa kwenye uwanja wa Stedi-Kata ya Ifakara hii leo wakati wa Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni za Ubunge Jimbo la Kalenga.


Mh:Naibu Katibu Mkuu CCM-Bara akisaini Kitabu akiwa na Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey William Mgimwa mara baada ya kuwasili Viwanja Vya Stendi Kata ya Ifunda.
Chief Wa Wahehe, Chief Mkwawa ambaye pia ni Kada Mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi akishikana Mikono ya Baraka na Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga Godfrey William Mgimwa,Pia akisalimana na Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu Nchemba hii leo kwenye Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni kata ya Ifunda-Kalenga.Kubwa zaidi CHIEF MKWAWA ambaye ni Mtoto wa Marehemu Mkwawa alikuwa anakanusha taarifa kuhusu Yeye Kuunga Mkono Chadema,Amesema hawezi kuunga Mkono chama ambacho hakieleweki kuanzia muundo wake na hata maamuzi yake ndani ya Chama.Yeye ni MwanaCCM damu damu,na ameapa atafia CCM.

 
Msanii Dokii ambaye ni kada wa Chama Cha Mapinduzi akitumbuiza kwenye ufunguzi wa kampeni wa Jimbo la Kalenga kwa Chama Cha Mapinduzi.Dokii ametunga wimbo rasmi kwaajili ya Kalenga na Umuhimu wa Kijana Godfrey William Mgimwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo,

 
Katibu Msaidizi wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini Ndugu Mtatulu akionesha baadhi ya Mitego inayodaiwa kuwekwa na Vijana wa CHADEMA kwenye njia ili Magari ya CCM yanayozunguka kwenye Kampeni yapata matatizo.Pia Ndugu Mtatulu alitaja majina ya Wahusika na ameshayapeleka Polisi kwa hatua zaidi za kisheria.

Naibu katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu Nchemba akiteta Jambo na Kijana Godfrey William Mgimwa ambaye ni Mgombe Ubunge Jimbo la Kalenga.

Wabunge wa Iringa(Wilaya+majimbo) wakitoa neno la kuomba Kura kwa Wananchi Wa Ifunda ili wamchague Mgombe wa CCM Kijana Godfrey William Mgimwa.

 
Ni Naibu Katibu Mkuu CCM_Bara Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na mamia ya Wananchi waliofurika Viwanja Vya Stendi Kata ya Ifunda hii leo kuhudhuria Mkutano wa hadhara wa ufunguzi wa Kampeni za Ubunge Jimbo la Kalenga(CCM).Mh:Mwigulu Nchemba amewaomba Wananchi wa Kalenga kumchagua Kijana Godfrey William Mgimwa kwa sababu anakila sifa za kuwatumikia Wananchi wa Kelenga,Lakini pia  ni Kijana aliyependekezwa na Chama kuanzia ngazi ya Chini hadi Taifa kwa mtindo wa Kura za maoni na amewashinda wenzake 9.

Mh:Mwigulu Nchemba amesisitiza kuwa Kwa namna Marehemu Mgimwa alivyolitumikia Jimbo lake na kuiletea Heshima Nchi yetu na Jimbo la Kalenga,kuna kila sababu ya Kuipa nafasi CCM iendelee kutekeleza Ilani yake ndani ya Jimbo hilo.Mh:Mgimwa tangu kufariki kwake Vyama vya siasa vimekuwa mstari wa mbele kumsifia kutokana na Utendaji wake Kuanzia Wizara ya Fedha hadi Jimboni kwake hasa upande wa Miundombinu,Maendeleo yote yaliyofanyika ndani ya Jimbo la Kalenga ni Matunda ya sera nzuri za CCM na Ilani ya CCM ndani ya Jimbo hilo.

Pia Mwigulu amezungumzia kuhusu Amani na Mshikamano ulipo kwa Wananchi wa Kalenga ni lazima uendelee kudumishwa,Kitendo cha kukaribisha wapinzani kwenye jimbo hili ni sawa na kukaribisha Vurugu kwasababu Wapinzani hasa Chadema katika Taifa hili hawana rekodi nzuri ya kudumisha amani kwenye maneo wanayoongoza. 

Kubwa zaidi Mh:Mwigulu Nchemba ameendelea kuwaomba Wanakalenga kufanya Kampeni za  Ustaarabu,Kampeni za Amani na Utulivu.Kwa MwanaCCM kufanya Vurugu sio Jambo jema,bali tutumie Amani tuliyonayo kuwaelimisha hata wenzetu wa Upinzani kufanya siasa za kistaarabu,Waache michezo ya Kusababisha Vifo kwa Wananchi wasio na hatia yoyote ile.Siasa safi ni zile za Kupambanisha Sera na Uwezo wa Kujenga hoja majukwaani.

Hivyo tar.16/03/2014 Wanakalenga Wote wanajitokeze Kupiga Kura na Kumchagua Mgombea wa CCM Kijana Godfrey William Mgimwa kwa maendeleo ya Wote Wanakalenga.


Kijana huyu ameamua kurudisha Kadi ya Chadema baada ya Somo zuri Kutoka kwa Mh:Mwigulu Nchemba kwenye Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni Jimbo la Kalenga.

Naibu Katibu Mkuu CCM_Bara Mh:Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea wa Ubunge Jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey Mgimwa hii leo kwenye Ufunguzi wa Kampeni Jimbo la kalenga.Uchaguzi unategemewa Kufanyika tar.16/03/2014.

Picha zote  na Habari kwanza Blog

Rais Kikwete azindua Rasmi Mtambo Maalum wa Usimamizi na Uhakiki wa mawasiliano ya Simu


  Mgeni Rasmi Kuwasili Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho kiwete ,  Rais wa Serikari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizindua Rasmi Mtambo Maalum wa Usimamizi na Uhakiki wa mawasiliano ya Simu kwa kukata utepe ambapo sherehe hizo zilifanyika  Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya  Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) aliouzindua leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam. Kulia niWaziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pro, Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ProfJohn Nkoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadick na wadau wengine wa tehama.

 


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe  kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam.


 Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho kiwete ,  Rais wa Serikari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa akiwa katika 'Laptop' kwa ajili ya kubofya ili kuruhusu Rasmi mtambo huo kuanza kufanya kazi.

 
 


 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Profesa John Nkoma akitoa Maelezo ya kina kwa Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho kiwete ,  Rais wa Serikari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jinsi Mtambo huo unavyofanya kazi


 Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho kiwete , Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  akizungumza Jambo wakati wa uzinduzi Rasmi  wa Mtambo huo.

SKYLIGHT BAND YAZIDI KUKONGA NYOYO MASHABIKI ZAKE, NI IJUMAA HII TENA PALE THAI VILLAGE‏

DSC_0303
Joniko Flower akiongoza safu ya Skylight Band kutoa burudani kwa mashabiki wa Bendi hiyo Ijumaa iliyopita kwenye kiwanja chao cha Nyumbani Thai Village Masaki jijini Dar.... Ni kila Ijumaa zote za wiki wanakuwa hapo kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki wake!!!
DSC_0229
DSC_0244
Meneja wa Band Aneth Kushaba AK47 na Winfrida Richard wakiwajibika jukwaani kuwapa utamu mashabiki wa Skylight Band.
DSC_0253
Hashim Donode na Winfrida Richard wakitawala jukwaa huku wakisindikizwa na Digna Mbepera pamoja na Mary Lucos.
DSC_0173
Madiva wa Skylight Band wakisaka Dough....... Kutoka kushoto ni Winfrida Richard, Mary Lucos na Digna Mbepera.
DSC_0284
Babu Athumani akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band.
DSC_0163
Joniko Flower, Sony Masamba na Sam Mapenzi wakisebeneka taratibu bila jasho..!!!
DSC_0322
Mheshimiwa Bundala akiwa na kijana wake Emmanuel Francis (wenye vest) wakisebeneka na midundo ya Skylight Band.
DSC_0366
Hapo ni Yachuma chuma mwanzo mwisho...!!
DSC_0334
Skylight Band ndio habari ya mujini usiku wa leo ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0337
Pananogaje......Picha inaongea...!!
DSC_0347
Wadau wakishow love na Ukodak.
DSC_0361
Wadau wa Skylight Band wakipata Ukodak.
DSC_0385
Mchezaji mkongwe wa Kabumbu John Mwansasu akishow love na Lubea wa Skylight Band pamoja na mdau ndani ya kiota cha Thai Village Ijumaa iliyopita.
DSC_0353
Mdau Dagma (mwenye miwani), Pacha wa Customer Care, Lubea pamoja na Mdau wakipata Ukodak.

Ziara Rasmi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe Nchini China

 Mhe. Membe akiagana na Mhe. Yuanchao mara baada ya mazungumzo yao.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao alipokutana nae kwa mazungumzo kwenye Jumba la Mikutano la Kitaifa la China maarufu kama People's Great Hall mjini Beijing, China. Mhe. Membe yupo nchini humo kwa ziara ya kikazi ya siku tano kuanzia tarehe 24 hadi 28 Februari, 2014.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akiwa katika mazungumzo na Mhe. Wang Hanning, Makamu Waziri wa Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China alipokutana nae mjini Beijing wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Membe nchini China tarehe 26 Februari, 2014.
 Mhe. Membe akiendelea na mazungumzo na Mhe. Hanning huku Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Abdulrahman Shimbo (kulia kwa Mhe. Membe) na wajumbe waliofuatana na Mhe. Hanning wakisikiliza.
 Mhe. Membe na Mhe. Yuanchao wakiendelea na mazungumzo.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Mhe. Li Jinzao, Makamu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China kabla ya kufanya mazungumzo rasmi na Waziri huyo wakati wa ziara yake nchini China.
Mhe. Membe (kulia) na Ujumbe wake wakiwa kwenye mkutano wa pamoja na Mhe. Jinzao (kushoto) na ujumbe wake.