Saturday, November 30, 2013

SHABIKI MKUBWA WA SOKA, RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE APOKEA KOMBE LA DUNIA!!

D92A7946Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akilifunua na kulinyanyua Kombe la Dunia katika uwanja wa michezo Kirumba mjini Mwanza (picha na Freddy Maro)D92A7955D92A7966Rais Dkt. Jakaya Kikwete ni shabiki mkubwa mno wa michezo, na kila timu ya Taifa inapofanya kazi nzuri huwa anafarajika sana

Mhe Angela Kairuki afungua mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 30 ya Tume



Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Angelah Kairuki akifungua Mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 30 ya Tume
 Mwenyekiti wa Tume Mhe Jaji Aloysius Mujulizi akisoma taarifa yake wakati wa kufungua mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 30 ya Tume
  Baadhi ya Wastaafu wa Tume wakiwa katika mkutano wa maadhimisho ya miaka 30 ya Tume.
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ambaye sasa ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Mhe Jaji Mstaafu Damian Lubuva akichangia mada wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya Tume
 Spika Mstaafu Mhe Pius Msekwa akiwasilisha mada wakati wa mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 30 ya Tume
  Aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa na Kamishna wa Tume Bw. George Liundi akichangia mada katika Mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 30 ya Tume
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ambaye sasa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Jaji Profesa Ibrahim Juma akitunukiwa Cheti na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angelah Kairuki
 Picha ya pamoja ya Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Angelah Kairuki na Wenyeviti wastaafu wa Tume
 Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Angelah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Watendaji wastaafu wa Tume waliokaa Bw. Nathaniel Issa (Kulia) na Bw. Japhet Sagasii (wa pili kulia).
Picha ya Pamoja baina ya Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angelah Kairuki na washiriki wa Mkutano wa maadhimisho ya miaka 30 ya Tume.  Picha zote na Munir Shemweta LRCT

TOVUTI KUU YA SERIKALI YAZINDULIWA RASMI, TAARIFA NA HUDUMA MBALIMBALI SASA KUPATIKANA KWA NJIA YA MTANDAO



Waziri Mkuu Mizengo Pinda (katikati) akiwa ameambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Celina Kombani wakiwasili katika Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao kupata maelezo ya Tovuti Kuu ya Serikali kabla ya kuizindua tovuti hiyo  jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa Tovuti Kuu ya Serikali www.tanzania.go.tz itakayowawezesha wananchi kupata taarifa na huduma mbalimbali za serikali kwa urahisi, haraka na kwa wakati. Wanaoshuhudia kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Celina Kombani na Dkt. Jabiri Bakari ,Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao ambao ni wasimamizi wa Tovuti hiyo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akifurahia jambo mara baada ya kuzindua Tovuti Kuu ya Serikali na kuwataka wananchi kuitumia katika kupata taarifa mbalimbali za serikali.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo kuhusu uundwaji wa Tovuti Kuu ya Serikali na namna inavyoendeshwa kutoka kwa Mkurugenzi wa Msaidizi wa Mifumo Shirikishi ya Umma Bw. Fratern Hassani (kulia) katika Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao wasimamizi wa Tovuti Kuu ya Serikali. Wengine wanaosikiliza kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo Dkt. Jabiri Bakari, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Celina Kombani,Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa, Makatibu wakuu na watendaji wengine wa serikali.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza jambo mara baada ya kupata maelezo kuhusu mifumo ya uendeshaji wa Tovuti Kuu ya Serikali alipokutana na wataalam wanaosimamia Tovuti hiyo katika Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao jijini Dar es saalam. Picha na 6. Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakitekeleza makumu yao wakati wa uzinduzi wa Tovuti Kuu ya serikali katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Jabiri Bakari akitoa ufafanuzi kwa wadau mbalimbali juu ya wa namna Tovuti Kuu ya Serikali inavyofanya kazi na namna ya kupata taarifa za serikali wakati wa uzinduzi wa Tovuti hiyo jijini Dar es salaam.
Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao waliofanikisha uzinduzi wa Tovuti Kuu ya serikali.
Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambayo ndiyo msimamizi wa maudhui ya Tovuti Kuu ya Serikali kupitia Idara ya Habari –MAELEZO waliohudhuria Uzinduzi wa Tovuti Kuu hiyo.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Bw. Raphael Hokororo akifuatiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Assah Mwambene.
Waandishi wa habari wakiwajibika. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO,Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda amesema kuwa kuanzia sasa wananchi wanaweza kupata taarifa na huduma mbalimbali za serikali kwa urahisi zaidi  kwa njia ya mtandao katika maeneo wanayoishi bila hata kulazimika kufika kwenye ofisi husika.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tovuti Kuu ya Serikali jana jioni jijini Dar es salaam, Mh Pinda amesema kuwa tovuti kuu ya serikali sasa itawawezesha wananchi kupata taarifa ya huduma mbalimbali za serikali na namna ya kupata huduma hizo kwa njia ya mtandao na kupunguza usumbufu wa kulazimika kusafiri eneo moja hadi jingine kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali.

 Alisema tovuti hiyo inayopatikana sasa kwa anuani ya www.tanzania.go.tz ni mojawapo  ya juhudi za Serikali  katika kuhakikisha kuwa taarifa na huduma zinazotolewa na Serikali zinapatikana na kuwafikia wananchi kwa urahisi,  wakati wowote na mahali popote ndani na nje ya nchi.

Alieleza kuwa tovuti  hiyo  ni moja ya mafanikio makubwa katika kutimiza dira ya muda mrefu ya kuwa na dirisha moja linalotoa taarifa na huduma zinazotolewa na Taasisi  za Serikali kwa urahisi na kuongeza kuwa licha ya kurahisisha upatikanaji wa taarifa itawapunguzia Wananchi usumbufu kwa kuokoa muda wa kufuatilia taarifa hizo kutoka eneo moja hadi jingine.

Alisema kuwa taarifa za masuala mbalimbali kuhusu Kilimo, Biashara, Viwanda, Ufugaji, Masoko, Elimu na nyingi zinazohusu taifa la Tanzania sasa zinapatikana kupitia Tovuti Kuu ya Serikali na kutoa wito kwa wananchi kuitumia tovuti hiyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani akizungumza wakati wa uzinduzi huo alisema kuwa uzinduzi huo umekuja kwa wakati muafaka kutokana na kuwepo kwa mahitaji makubwa ya taarifa mbalimbali za serikali zinazowahusu wananchi katika masuala ya biashara, uwekezaji, kilimo, ufugaji, uhamiaji, nishati na madini na masuala mengine yanayohusu maisha ya kila siku.

Alisema kuwa Menejimenti ya Utumishi wa Umma itaendelea kufanya kazi bega kwa beg na Wakala ya serikali Mtandao kuhakikisha inaijengea uwezo ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo ya kuwahudumia wananchi.

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao ambao ndio wasimamizi wa tovuti hiyo Dkt. Jabiri Bakari akizungumza wakati wa uzinduzi huo alisema kuwa Wakala ya serikali anayoisimamia itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali  katika kutoa huduma zake kwa wananchi.

Alisema wakala kwa kushirikiana na Wizara, taasisi, mikoa na Halmashauri za wilaya itaweza kuwahudumia wananchi kwa kuhakikisha kuwa taarifa za serikali zinapatikana kwa urahisi na kwa kuzingatia muda na kuongeza kuwa italitekeleza jukumu hilo kwa ufanisi mkubwa kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Idara ya Habari –MAELEZO ambao ndio wasimamizi wa maudhui wa tovuti hiyo.

 Kuhusu taarifa na huduma zilizomo katika Tovuti Kuu ya serikali Dkt. Jabiri alisema zimegawanywa katika maeneo makuu sita ambayo ni Serikali, Wananchi, Taifa letu, biashara, Sekta na Mambo ya Nje.

Alisema maeneo yote yanalenga kurahisha utoaji wa huduma mbalimbali zikiwemo za upatikanaji wa nyaraka zote za Serikali, huduma zinazotolewa na Serikali kwa njia ya simu na mtandao, Viwango vya fedha, Hali ya Hewa, na Soko la Hisa.

Alisema huduma nyingine katika Tovuti Kuu hiyo imetengwa katika ukarasa wa Nifanyeje unaopatikana ndani ya tovuti hiyo ambao  unamjengea uwezo mwananchi kufahamu taratibu za upatikanaji wa huduma zinazotolewa na taasisi mbali mbali za Serikali kama upataji wa hati ya kusafiria, kibali kazi, TIN, cheti cha kuzaliwa na mikopo ya vyuo.

Aliongeza kuwa tovuti hiyo pia inalenga kuziunganisha Tovuti na mifumo ya Taasisi mbali mbali inayotoa taarifa na huduma kwa wananchi na wafanyabiashara katika dirisha moja.

Tovuti Kuu hiyo ilianza kutengenezwa mwaka 2009 na kupatikana kwa anuani ya www.egov.go.tz chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Tovuti hiyo iliboreshwa na kuunganishwa na iliyokuwa Tovuti ya Taifa kwa anuani ya www.tanzania.go.tz  mwaka 2012 chini ya Wakala ya Serikali Mtandao.

Thursday, November 28, 2013

Rais Jakaya Kikwete Akagua na Kuzindua Miradi Mkoa Mpya wa Simiyu

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bwana Saguda Kasili mlemavu ambaye pia ni mtendaji wa kijiji cha Ng’wang’wali jana  wakati aliposimama kijijini hapo kuwasalimia wananchi wa eneo hilo
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Old Maswa muda mfupi baada ya kuzindua ujenzi wa barabara ya kilometa ya Bariadi-Lamadi 71.8 huko eneo la old Maswa, Mkoani Simiyu.
 Msanii wa kundi la sanaa kutoka Bariadi akicheza na nyoka aina ya Chatu wakati wa uzinduzi wa Ujenzi wa Barabara ya Bariadi –Lamadi  Jana 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli(watatu kushoto),Mbunge wa Bariadi  Mhe. Andrew Chenge(kushoto)pamoja na viongozi wengine wakifunua kitambaa kuashiria kuweka jiwe la msingi na kuzindua ujenzi wa Barabara ya Bariadi-Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8 huko enelo la Old Maswa mkoa mpya wa Simiyu jana
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Mradi wa Umeme katika kijiji cha Nkololo wilayani Bariadi, Mkoa wa Simiyu  Jana.Weninge katika picha kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mh. Steven Masele, Mbunge wa Bariadi Mhe.Andrew Chenge(wapili kushoto),Paroko wa Nkololo Padri Paulo Fegan(wanne kushoto) na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Pascal Mabiti.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi waliohudhuria ufunguzi wa Barabara ya Bariadi Lamadi jana.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli(pembeni ya Rais kulia) pamoja na viongozi wengine akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi ujenzi wa Barbara ya Bariadi Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8 huko eneo la Old Maswa jana.Picha na Freddy Maro-IKULU

Wednesday, November 27, 2013

Serikali yatangaza nafasi mpya za kazi 2,748


Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia watanzania  wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 2,748 kwa ajili ya waajiri mbalimbali Nchini. Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya waajiri mbalimbali wa Ofisi za Umma.
 Daudi alitaja nafasi za kazi zinazotangazwa kuwa ni Afisa Uvuvi daraja la ii, Mvuvi msaidizi daraja la ii, Afisa Mifugo msaidizi daraja la ii, Afisa mifugo daraja la ii, Mteknolijia wa samaki daraja la ii, Daktari wa mifugo daraja la ii,Afisa utafiti Mifugo daraja la ii, Daktari utafiti Mifugo daraja la ii, Fundi sanifu Maabara Mifugo daraja la ii, Mkufunzi Mifugo daraja ii, Mkufunzi wa Mifugo msaidizi na Daktari Mifugo.

Kada nyingine ni Mkufunzi daraja la ii, Mtekinolojia wa Samaki msaidizi daraja la ii, uunda boti daraja ii, nafasi 2, Dereva wa vivuko daraja la ii, msaidizi mifugo,afisa kilimo daraja la ii, Afisa kilimo msaidizi daraja la ii, Mhandisi kilimo daraja la ii, Fundi sanifu daraja la ii, Afisa utafiti kilimo daraja la ii, Mkufunzi wa kilimo msaidizi, Afisa kilimo msaidizi daraja la iii,Dereva daraja la ii, mlinzi, Mhasibu mkuu daraja ii, Msanifu lugha mkuu iii  na Afisa vipimo.

Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira nafasi hizo za kazi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kiteto, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mlele, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kalambo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mpanda, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nkasi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Sumbawanga na Mkurugenzi Manispaa ya Kinondoni.

Nafasi nyingine ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kyerwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chato, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Misenyi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ngara, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Muleba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bukoba, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Handeni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mkinga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kilindi, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Korogwe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Pangani, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Handeni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Korogwe na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Muheza.

Nafasi hizo pia ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ulyankulu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Sikonge, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Uyui, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nzega, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Nzega, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Igunga, Mkurugenzi Manispaa ya Tabora, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ikungi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mkalama, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Iramba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Manyoni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Singida, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Itilima na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ushetu.

Waajiri wengine ni Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Msalala, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kishapu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bukombe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Meatu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Shinyanga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Maswa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kahama, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bariadi, Mkurugenzi Manispaa ya Shinyanga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nyasa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Namtumbo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbinga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Tunduru, Mkurugenzi Manispaa ya Songea, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nyang`wale, Mkurugenzi Manispaa ya Ilemela, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Misungwi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ukerewe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Geita na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Magu.

Nafasi hizo za kazi pia ni kwa aajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Tandahimba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Newala, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Masasi, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Masasi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Gairo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mvomero, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kilombero, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ulanga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Morogoro, Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Tunduma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Momba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbarali, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ileje, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kyela, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chunya, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbozi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbeya, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Rorya,

Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Serengeti, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bunda, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Tarime, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Butiama, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa ya Musoma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ruangwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nachingwea, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Lindi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mwanga na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Hai. Katika nafasi hizo waajiri wengine ni Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Rombo, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa ya Moshi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kahama, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Uviza,  Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Monduli, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Babati, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Hanang, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Simanjiro, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bagamoyo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kisarawe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Rufiji, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mafia, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mkuranga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Iringa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mufindi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Makete, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Karatu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chamwino,

Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mpwapwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kondoa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kongwa na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bahi,  Waajiri wengine katika nafasi hizo za kazi ni Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chemba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Njombe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kongwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kilolo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Makambako, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ludewa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Wanging`ombe, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa ya  Kigoma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kigoma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kasulu,


Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kakonko, Katibu Tawala Mkoa Arusha, Katibu Tawala Mkoa Pwani, Katibu Tawala Mkoa Dodoma, Katibu Tawala Mkoa Iringa, Katibu Tawala Mkoa Kilimanjaro, Katibu Tawala Mkoa Mtwara, Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Katibu Tawala Mkoa Ruvuma, Katibu Tawala Mkoa Tabora, Katibu Tawala Mkoa Kagera, Katibu Tawala Mkoa Dar es salaam, Katibu Tawala Mkoa Rukwa, Katibu Tawala Mkoa Katavi, Katibu Tawala Mkoa Njombe, Katibu Tawala Mkoa Njombe, Katibu Tawala Mkoa  Simiyu na Katibu Tawala Mkoa Geita. Daudi amesema mwisho wa kupokea barua za maombi ya kazi ni tarehe 10 Desemba, 2013.

Aidha amewataka waombaji wote wa fursa za ajira kutambua kwamba Kila mwombaji kazi atapangwa katika kituo chochote cha kazi bila kujali eneo au mahali alipoomba kutokana na mahitaji ya mwajiri pamoja na idadi ya waombaji katika eneo husika. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 27 Novemba, 2013.

Majengo ya nyumba za makazi za NHC Mchikichini yakiwa hatua za mwisho





Majengo ya nyumba za makazi za NHC Mchikichini yakiwa katika hatua za mwisho za ujenzi, yatakapokamilika yatakaliwa na familia 48, ambapo katika kila nyumba ina vyumba vitatu jiko na choo pamoja na parking ya kutosha.

WAZIRI DK.NCHIMBI AZINDUA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITATU WA KUBORESHA MADAWATI YA KIJINSIA NA WATOTO NDANI YA JESHI LA POLISI

IMG_2363
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou akisalimiana na Kamanda wa Kanda Maalum Dsm, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Suleiman Kova alipowasili kwenye uzinduzi wa Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi. Tukio hilo lilifanyika Kituo cha Polisi Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam.
IMG_2364
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou akibadilishana mawazo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema.Kulia ni Kamanda wa Kanda Maalum Dsm, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Suleiman Kova. Kushoto ni Wanamawasiliano kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Hoyce Temu na Sangita Khadka.
IMG_2370
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema akimtambulisha mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi kwa baadhi ya maafisa wa Jeshi la Polisi nchini mara baada ya kuwasilia eneo la tukio.
IMG_2374
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akibadilishana mawazo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema (kushoto) na Kulia ni Kamanda wa Kanda Maalum Dsm, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Suleiman Kova wakati wakielekea jukwaa kuu.
IMG_2377
Balozi wa Ireland nchini Fionnuala Gilsenan (katikati) akiteta jambo na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou (kushoto) Kulia ni Mkuu wa Mabalozi wa EU nchini Filiberto Sebregondi.
IMG_2381
Pichani juu na chini Maandamano yakiwasili kwenye uzinduzi wa Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi.
IMG_2384IMG_2385
Taasisi mbambali zikiwa zimebeba mabango yenye jumbe mbalimbali za kutokomeza ukatili wa Kijinsia.
IMG_2398
Burudani kwenye uzinduzi wa Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi.
IMG_2459
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akitoa hotuba yake kwa Askari na Maofisa wa Jeshi la Polisi, Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali pamoja na wakazi wa Temeke kabla ya kuzindua Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi. Tukio hilo lilifanyika Kituo cha Polisi Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Waziri Nchimbi akatika hotuba yake alilishukuru Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali kwa kusaidia masuala ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia nchini.
IMG_2438
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic KacouIMG_2409
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema akizungumza kwenye uzinduzi wa Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi.
IMG_2419
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi akizungumza kwenye hafla hiyo.
IMG_2431
Balozi wa Ireland nchini Fionnuala Gilsenan akizungumza kwa niaba ya nchi yake ambapo amesema Ireland itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa ukaribu zaidi.
IMG_2460
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizindua kitabu cha Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa kuboresha madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi katika uzinduzi uliofanyika Kituo cha Polisi Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema, wa pili kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou, wapili kushoto ni Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi na Kushoto ni Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova. Waziri Nchimbi akatika hotuba yake alilishukuru Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali kwa kusaidia masuala ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia nchini
IMG_2465
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikionyesha kitabu cha Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa kuboresha madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi katika uzinduzi uliofanyika Kituo cha Polisi Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam.
IMG_2469
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akimshukuru Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dr. Alberic Kacou mara baada ya kuzindua Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa kuboresha madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi ulio chini ya Umoja wa Mataifa.
IMG_2471
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikata utepe kuzindua ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto katika Mkoa wa Kipolisi Temeke. Kushoto ni Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi.Waziri Nchimbi katika hotuba yake alilishukuru Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali kwa kusaidia masuala ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia nchini.
IMG_2481
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali baada ya waziri huyo kuzindua Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi. Tukio hilo lilifanyika Kituo cha Polisi Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam leo. Wapili kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema.
IMG_2486
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dr. Alberic Kacou akiteta jambo na mmoja wa maafisa wa Jeshi la Polisi mara baada ya uzinduzi huo.
IMG_2497
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dr. Alberic Kacou akifanya mahojiano na mwandishi wa habari wa redio wa BBC. Katikati ni Afisa Habari wa kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Usia Nkhoma Ledama.
 IMG_2499
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akiagana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini, Dr. Alberic Kacou mara ya uzinduzi.