Friday, April 26, 2013

MTANDAO WA PR HABARI WAPATA MKOKO WAKE



Mwenyekiti wa  Mtandao wa kijamii wa http://prhabari.blogspot.com/, Spear Patrick akiwa amepozi na gari hilo




GARI HIYO INAVYO ONEKANA KWA NYUMA

MBUNGE GODBLESS LEMA AKAMATWA NA POLISI





















Baada ya mabishano ya muda mrefu nyumbani kwa kada huyu na Mbunge wa Arusha mjini na uvamizi wa Polisi wakati huu wa usiku; Mh. Lema amekamatwa na amechukuliwa na gari la polisi na kupelekwa kituo kikuu cha polisi Arusha yaani Central Polisi.Wananchi wengi wamejitokeza ku-support mbunge wao.
Baada ya kumfikisha Lema Central police Arusha amesachiwa na kuingizwa ndani. Lema alikuwa ameambatana na magari ya wafuasi waliomsindikiza ili kushuhudia kinachojili hapo kituoni.Hivi sasa polisi wamewafukuza wafuasi wote hapo kituoni na kuwaambia hawatakiwi kuonekana hapo. 
wafuasi wameondoka kwa amani na kwenda kupaki Safari hoteli wakisubiriana kupata mwongozo.03:41amWamekutana pembeni ya kituo cha polisi na wamekubaliana kuwa watawanyike. Hivyo, Lema yupo ndani na wananchi waliomsindikiza wametawanyika kwenda kulala. Tutaonana asubuhi kwa yale yatakayojiri.

SOURCE.JAMII FORUM

Thursday, April 25, 2013

Wabunge wa Chadema waliotimuliwa Bungeni Waunguruma Mbeya

  Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa akisindikizwa na Maelfu ya wanachama wa chadema muda mfupi baada ya kuwasili mkoani mbeya kuhutubia kwenye mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Ruanda-Nzovwe

Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) akihutubia maelfu ya wanachama wa chadema mkoani mbeya jana  katika Uwanja wa Ruanda-Nzovwe
 Mbunge wa Jimbo la Ilemela-Chadema Highness Kiwia akihutubia maelefu ya wanachama wa chadema mkoani mbeya jana katika Uwanja wa Ruanda-Nzovwe
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa akihutubia maelfu ya wanachama wa chadema kwenye mkutano wa hadhara Mkoani Mbeya Jana katika Uwanja wa Ruanda-Nzovwe katika mkutano huu uliudhuriwa na  Mbunge wa Iringa, Mchungaji Peter Msigwa (Iringa mjini), Ezekiel Wenje(Mwanza mjini) na Highness Kiwia wa Jimbo la Ilemela. Picha na Chadema

Wednesday, April 24, 2013

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe atoa majibu kwa Umma kuhusu Habari za mama yake Mzazi Bi. Shida kuvamiwa na kutishiwa bastola

Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema. Zitto Kabwe
--
Nimekuwa naulizwa kuhusu Habari za mama yangu Mzazi Bi. Shida kuvamiwa na kutishiwa bastola. Nawajibu watu Kwa ujumla kwamba 
“Moja, mie sio msemaji wa familia. Ni basi tu katika watoto wa mama yetu mie najulikana zaidi na hivyo mama anaitwa Mama Zitto. Kwetu Kigoma haitwi hivyo, ama Ni mama Salum au mama Lulu. 
Pili, hili Ni suala la polisi. Lipo polisi na linashughulikiwa na polisi. Nisingependa kulisemea wakati Ni suala linalochunguzwa na polisi. Mama yangu Ni mama wa kawaida wa kitanzania kama mama mwingine yeyote yule. Matukio ya namna hii yamezagaa nchi nzima. Hivyo suala lake litashughulikiwa kama yanavyoshughulikiwa masuala mengine yote ya Watanzania. Polisi wakimaliza uchunguzi wao naamini hatua mwafaka zitachukuliwa. 
Ushauri- tuwe makini na “Agente provocatuers” au in English “provocation agents” nyakati kama hizi. Calmness is the best protection against provocations. Nadhani mmenipata”
Nawatakia Kila la kheri katika kazi za ujenzi wa Taifa letu na kuimarisha Umoja na mshikamano wa Watanzania dhidi ya ufisadi, umasikini na ugandamizaji.
Majibu haya  ameandika kupitia mtandao wa Kijamii wa facebook.

Monday, April 22, 2013

Mkutano Mkubwa Wa Hadhara Uliyofanywa na Wabunge Wa Chadema Waliyosimamishwa Kuhudhuria Vikao Vitano vya Bunge na Naibu Spika Job Ndugai

Mbunge wa Ilemela-Chadema  Highness Kiwia akiunguruma mbele ya Maelfu ya Wanachama wa Chadema Mkoani Mwanza
Mbunge wa Iringa-Mjini-Chadema Mchungaji Peter Msigwa
Sehemu ya Maelfu ya Wanachama wa Chadema Mkoani Mwanza Wakiwasikiliza Mbunge wa Iringa-Mjini-Chadema Mchungaji Peter Msigwa na  Mbunge wa Ilemela-Chadema  Highness Kiwiawalipokua wakihutubia mkutano wa Hadhara Mwanza Jana.Picha na Chadema
 -- 
 Wabunge sita wa Chadema waliosimamishwa bungeni wameamua kwenda kuwashtaki Spika Anne Makinda na Naibu wake Job Ndugai kwenye majimbo yao.

Wakitangaza uamuzi huo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi ya Mbugani, Mwanza jana, walisema pia watakwenda kwenye majimbo ya wabunge wawili wa CCM, Mwigulu Nchemba (Iramba Magharibi) na Livingstone Lusinde (Mtera) ili kueleza jinsi wabunge wa upinzani wanavyokandamizwa bungeni.
Ndugai, ambaye ni Mbunge wa Kongwa (CCM), aliwasimamisha wabunge sita wa Chadema kuhudhuria vikao vitano vya Bunge kutokana na kile alichokiita kufanya vurugu bungeni. Hatua hiyo ya Ndugai aliyoichukua Aprili 17, mwaka huu ilipata baraka za Spika Makinda Ijumaa iliyopita.

Wabunge waliosimamishwa ni Tundu Lissu (Singida Mashariki), Godbless Lema (Arusha Mjini), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Mbeya Mjini), Highness Kiwia (Ilemela), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini) na Ezekiah Wenje (Nyamagana). Katika mkutano huo ulioanza saa 9.30 alasiri na kumalizika saa 12.00 jioni, ulihudhuriwa na wabunge wanne kati ya hao. Mbilinyi ndiye aliyekuwa wa kwanza kuhutubia akifuatiwa Mchungaji Msigwa, Kiwia na Wenje. Lissu na Lema hawakuhudhuria.

Akizungumzia ziara yao katika majimbo ya viongozi hao wa Bunge, Mchungaji Msigwa alisema itakuwa ya kuwashtaki kwa kuendesha Bunge kuwapendelea wabunge wa CCM hata wanapofanya makosa ya wazi.Kwa Habari Zaidi Bofya na Endelea.......>>>

Friday, April 19, 2013

MSIBA WA BILIONEA BABU SAMBEKE WAZUA GUMZO,VIGOGO WATAWALA MSIBANI


Jamal Sambeke mtoto wa marehemu akifunga jeneza la baba yake mara baada ya watu mbalimbali kutoa heshima zao za mwisho nyumbani kwake njiro Themi Mkoani Arusha
DSCF8840
Waombolezaji wakibeba jeneza la Bilionea Babu na kuweka kwenye gari maalumu tayari kwa 
safari kuelekea Moshi kwa mazishiDSCF8828

Watu wakitoa heshima za mwisho
DSCF8844
Watoto wa marehemu Sia na Getrude waliovalia nguo nyeupe
DSCF8834
Jamal akifunga jeneza la marehemu Babu Sambeke
DSCF8830
Jaji Aisha nyerere msibani pamoja na mkurugenzi wa kibo palace Vicent Laswai 
DSCF8832

DSCF8848
Baadhi ya magari ya kifahari yaliyofika katika msiba huo
DSCF8838
Mkurugenzi wa hoteli ya Kibo Palace Vicent Laswai akizungumza msibani mara baada ya watu mbalimbali kutoa heshima zao za mwisho
DSCF8847
Waombolezaji
Mamia ya vigogo pamoja na watu mbalimbali wafurika nyumbabi kwa marehemu Bilionea  “Babu Sambeke”Ernest Sambeke eneo la njiro jijini Arusha  kuaga mwili wake unaotarajiwa kuzikwa kesho nyumbani kwake eneo la Karanga mjini Moshi huku msiba huo ukiwa tofauti na misiba mingine iliyozoekeaka hapa Nchini
Marehemu,Sambeke alifariki hivi karibuni katika ajali ya ndege  aliyokuwa akiiendesha na pia mmiliki wa ndege hiyo ambapo ilianguka katika eneo la Kisongo na kusababisha  kifo chake Mkoani Arusha
Shughuli za kuaga mwili wa marehu zilikamilika majira ya saa 8:45 mchana huku mwili huo ukipakiwa katika gari maalumu la kifahari tayari kusafirishwa kuelekea nyumbani kwake Moshi kwaaajili ya mazishi
Taratibu za kuaga mwili wa marehemu zilianza majira ya saa 5 asubuhi  huku wafanyabiashara wa madini pamoja wafanyabiashara wengine kutoka hapa Arusha na Moshi walionekana kutawala msiba huo .
Katika zoezi hilo la kuaga mwili wa mareheu Padri Florentine Mallya ambaye ni mdogo wa marehemu  aliongoza misa ya kumuombea marehemu na baada ya kumaliza alitoa fursa kwa watu mbalimbali kupita mbele ya jeneza kwaajili ya kuaga mwili Ndani ya jeneza marehemu alivalishwa nguo zake za kirubani huku ,baadhi ya wanajeshi kutoka jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) walionekana jana katika zoezi la kuuaga mwili wa marehemu ambapo baadhi yao walikuwa wamevalia sare za jeshi hilo

Hatahivyo,baadhi ya watu  walionekana katika hali ya kawaida  huku watoto wakionekana na nyuso za huzuni mda wote
Tofauti na misiba mingine nchini watu mbalimbali walipata fursa ya kupata chakula na  vinywaji mbalimbali kwa kujihudumia vikiwemo vinywaji aina ya Bavaria ambapo watu waliohudhuria zoezi hilo walionekana wakijihudumia zaidi vinywaji vya bavaria Magari ya kifahari yalionekana kutawala msiba huo huku barabara ya njiro ikionekana kuwa na msongamano kubwa iliyosababishwa na zoezi hilo la uwagaji wa mwili Marehemu aliacha watoto watatu ambao ni Sia,Jamal,Getruda

Rais Kikwete, aongoza mamia kumzika Fatma Baraka 'Bi Kidude', katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja

 Rais wa jamhuri ya Muungao Dk Jakaya Kikwete akifuatiwa na Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein walipofika Kitumba yalipofanyika maziko ya Bi Kidude
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania , Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said sadiq akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
 Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Nasibu Abdul Juma (Diamond) akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
 Taratibu za Mazishi zikiendelea.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,(kutoka kulia) Rais wa jamhuri ya Muungano Dk. Jakaya Mrisho Kikwete,Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif,na Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi,wakiitikia dua baada ya maziko ya Msanii maarufu Fatma Binti Baraka (kidude) aliyefariki jana na kuzikwa leo Kijijini kwao Kitumba,Wilaya ya Katri Unguja.

Wednesday, April 17, 2013

Rais Mstaafu, Alhaj Ali Hassan Mwinyi akutana na Waandishi wa Habari Jijini Dar leo na kuzungumzia swala lenye utata wa Kuchinja hapa nchini

 
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Alhaj Ali Hassan Mwinyi akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) aliowaita leo nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam,wakati alipozungumzia swala uhalali wa kuchinja ambalo limekuwa ni gumzo sana hapa nchini kwa kipindi cha hivi karibuni.Mzee Mwinyi ametoa rai kuwa Swala hilo ambalo limekuwa na utata mkubwa na kupelekea kuzua vurugu kwa baadhi ya maeneo hapa nchini,kuwa liachiwe watu wenye dharula kama linavyoelekeza kwenye Moja ya Vitabu vya dini.…

 
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Alhaj Ali Hassan Mwinyi akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) aliowaita leo nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam,wakati alipozungumzia swala uhalali wa kuchinja ambalo limekuwa ni gumzo sana hapa nchini kwa kipindi cha hivi karibuni.Mzee Mwinyi ametoa rai kuwa Swala hilo ambalo limekuwa na utata mkubwa na kupelekea kuzua vurugu kwa baadhi ya maeneo hapa nchini,kuwa liachiwe watu wenye dharula kama linavyoelekeza kwenye Moja ya Vitabu vya dini.
 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wamsikiliza kwa Makini Rais Mstaafu,Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
 
Rais Mstaafu,Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiwa kwenye picha ya pamoja na Baadhi ya waandishi wa Habari waliofika nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam leo

WAGONJWA 316 WAPATA HUDUMA ZA MADAKTARI BINGWA MKOANI KIGOMA

1 
Dk. Vence (Katikati) akiwa katika chumba cha upasuaji kutoa huduma kwa mmoja wa watoto ambao walifanyiwa upasuaji mapema leo (jana)
Wagonjwa wakisubiri kuonana na madaktari bingwa wa magonjwa ya kawaida6 (2) 
Wagonjwa wakisubiri kuonana na madaktari bingwa wa upasuaji2
Daktari Bingwa wa akina Mama Dk. Mrema (wapili kutoka kulia) akimsikiliza kwa makini mmoja wa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo kwa lengo la kutoa ushauri wa tiba sahihi.
Na Grace Michael, Kigoma
JUMLA ya wagonjwa 316 ndani ya siku mbili katika Hospitali ya Rufaa ya Maweni mkoani Kigoma wamefanikiwa kuonana na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili ambao wapo mkoani humo kwa mpango unaoendeshwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Mbali na wagonjwa hao kuonana na madaktari hao, jumla ya wagonjwa 11 ndani ya muda huo nao wamefanikiwa kufanyiwa upasuaji na madaktari hao hali inayoonesha kuwepo uhitaji mkubwa wa madaktari katika mikoa ya pembezoni ambayo miundombinu yake bado haijaimarika.
Hayo yanafanyika katika Mkoa wa Kigoma ndani ya mpango wa NHIF ambao ulizinduliwa mapema Aprili mwaka huu mkoani Lindi ambako nako timu ya madaktari bingwa watatu waliweka kambi katika Hospitali ya Mkoa na kufanikiwa kutoa huduma kwa mamia ya wananchi.
Katika Hospitali ya Maweni, timu ya madaktari wanne kutoka Muhimbili ilianza kazi rasmi jana (Jumatatu) na itakaa hospitalini hapo kwa muda wa siku saba lengo ni kutumia wataalam hao kitaifa.
Wagonjwa wanaonufaika na mpango huu ni wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na wananchi kwa ujumla ambao wanapata huduma kupitia utaratibu wa kawaida.
Wagonjwa waliofanikiwa kujiandikisha kwa lengo la kupata huduma kutoka kwa wataalam hao ni kutoka katika wilaya zote za mkoa wa Kigoma ambapo wanaeleza kuwa ni fursa ya kipekee kuipata.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wagonjwa ambao wamepata huduma ambao walifikishwa hospitalini hapo wakiwa na hali mbaya waliushukuru Mfuko kwa kuanzisha mpango huo ambao moja kwa moja unawagusa wananchi hasa wa kipato cha chini.
Kwa upande wa watumishi hospitalini hapo, wanasema kuwa wataitumia fursa hii vyema hasa katika kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa madaktari hao bingwa ili waweze kuboresha huduma zao kwa wagonjwa hata watakapobaki wenyewe.
Idadi ya wagonjwa inazidi kuongezeka kila kukicha hatua inayowalazimu madaktari hao kufanya kazi kwa zaidi ya saa 15 bila ya kupumzika.
Akizungumzia mwitikio huo, Naibu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Hamis Mdee, alisema kuwa mwitikio huo ni faraja kwa Mfuko ambao lengo lake ni kutoa huduma kwa Watanzania na kuhakikisha afya zao zinaimarika.
“Sisi kama Mfuko tunaona faraja sana tunapoona wagonjwa wamefika hapa na kupata huduma hizi ambazo pengine wasingeweza kuzipata hivyo tutaendelea na mpango huu kwa kuwa unagusa moja kwa moja uhai wa wanachama wetu na wananchi kwa ujumla,” alisema Mdee.
NHIF imeanzisha mpango huu na utatekelezwa katika mikoa mbalimbali ya pembezoni ikiwemo Rukwa, Katavi, Pwani, Lindi na Kigoma.

TANZIA: Bi Kidude afariki dunia!

 
BI KIDUDE
Kwa Taarifa zilizopatikana punde, ni kuwa yule mwimbaji maarufu na mkongwe wa muziki wa Mwambao FATMA BINTI BARAKA alimaharufu kama Bi Kidude amefariki hii leo...

Taarifa hizo pia zimethibitishwa na ndugu wa karibu wa Bi Kidude! Chanzo cha umauti ni maradhi yatokanayo na uzee!


Bi Kidude amefariki ktk hospitali ya Hindu Mandal... Atakumbukwa kwa umahili wake ktk nyimbo za Taarabu ndani na nje ya nchi...alama ya Utamaduni wa Mzanzibar ktk matamasha ya muziki kama ZIF na Sauti za Busara.


...itakumbukwa hivi karibu Bi Kidude na baadhi ya Wanamuziki nguli kama Muhidin Ngurumo walitunukiwa Nishani ya heshima ktk mambo ya muziki pale Ikulu....

 

Wasifu Wake:


Mwanamuziki mkongwe katika Taarab Fatuma Bint Mbaraka maarufu kwa jina la Bi Kidude amefariki dunia muda mchache uliopita huko Bububu Zanzibar, sehemu alikokuwa anaugulia kwa kipindi sasa. Mwili wake utahamishiwa kwake Rahaleo na mazishi yatakuwa kesho. Bi Kidude alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo, alikuwa binti wa mchuuzi wa nazi, hakuna anayejua haswa Bibi huyu alizaliwa tarehe ngapi, kuna hata mawazo kuwa alikwishafikisha miaka 102.


Katika mwaka 1920 tayari alikuwa amekwisha anza kuimba katika vikundi vya sanaa kule kwao, mwaka 1930 alijiunga na Egyptian Musical Club ya Dar es Salaam na kuzunguka miji mingi ya Tanganyika wakati ule , mwaka 1940 alirudi Zanzibar ambako awali alikuwa amekimbia kwa kuwa aliozwa kwa nguvu na mtu aliyemzidi sana umri.



Bi Kidude pia liwahi kuimba na Sitti Binti Sadi wakati wa ujana wake, na katika maisha yake Bi Kidude amekwisha zunguka mabara yote akiimba katika majukwaa na wanamuziki maarufu ulimwenguni.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Nape Nnauye Wafanya Kweli Ifakara mkoani Morogoro

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akifungua Shina la Wakereketwa  wa CCM la tawi la Manjechanga, Ifakara mkoani Morogoro, Aprili 17, 2013.

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akivishwa skafu na chipukizi alipowasili  eneo la kivuko cha Kilombero tayari kuanza ziara ya kikazi ya kuimarisha uhai wa chama hicho katika Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro,Kinana alikuwa akitokea wilayani Ulanga.
 Katibu Mkuu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwa na watoto waliokuwa sehemu ya watu walioshuhudia  uzinduzi wa Tawi la CCM la Manjecha  eneo la Mahutanga, wilayani Kilombero.
 Katibu Mkuu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akipandisha bendera kuzindua rasmi Tawi la CCM la Manjecha  eneo la Mahutanga, wilayani Kilombero
 Aliyekuwa mwanachama wa Chadema, Julius Mogela akionyesha kadi yake, kwa wananchi kabla ya kumkabidhi Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) baada ya kutangaza kuhamia CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Aprili 17, 2013, kwenye stebdi ya mabasi, Ifakara mkoani Morogoro
Ranfred Majiji ambaye alikuwa mfuasi wa Chadema akikabidhiwa kadi ya CCM na Kinana
 Anna Mwakitosi aliyekuwa mwanachama wa Chadema, Anna Mwakitosi akishangiliwa na wafuasi wa CCM baada ya kujiunga CCM
 Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya Ifarakara Mjini

Sehemu ya umati wa wananchi uliofika kwenye mkutano huo
 Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Elias Masala (kulia), akijibu maswali mbele ya Kinana jinsi alivyopanga mikakati ya kuwaletea mandeleo wananchi wa wilaya hiyo.
.Baadhi ya wafuasi wa Chadema wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, alipohutubia mkutano mkubwa wa hadhara kwenye Stendi ya mabasi ya Ifakara mkoani Morogoro, Aprili 17, 2013.
Baadhi ya wafanyabiashara walilazimika kusitisha shughuli zao kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alipohutubia mkutano mkubwa wa hadhara kwenye stenbdi ya mabasi, Ifakara mkoani Morogoro. Pichani ni wauza ndizi wakiwa kwenye mkutano huo, Aprili 17, 2013.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga ngoma wakati wa uzinduzi wa Shina la Wakereketwa  wa CCM la tawi la Manjechanga, Ifakara mkoani Morogoro, Aprili 17, 2013.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), akimkabidhi ubani mtoto wa aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilombero, marehemu Oswald Mkokochela, Edward wakati uongozi wa chama hicho ulipokwenda jana  kuifariji familia kwa msiba wa uliotokea juzi. Ifakara Mjini,
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Innocenti Kalogaries akimkabidhi ubani Edward.Picha na Richard Mwaikenda na Bashir Nkromo