Sunday, March 31, 2013

Rais Kikwete Aifariji Familia ya Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TTCL Marehemu Adolar Mapunda

 Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa  TTCL Marehemu Adolar Enzi za Uhai Wake
 Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa  TTCL Marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam jana Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa  TTCL Marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam jana Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa  TTCL Marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam jana Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa  marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam jana Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alifariki usiku wa kuamkia jana.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiifariji familia ya marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam jana Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alifariki usiku wa kuamkia jana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mtoto wa  marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam jana Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alifariki usiku wa kuamkia jana.Picha na IKULU

uzinduzi wa mpango wa ushirikiano baina ya Vodacom, Benki ya CRDB PCL na Samsung

01 e3690
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa, wa pili kulia, akifafanua jambo kwa Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbawara, Dar es Salaam jana, wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa ushirikiano baina ya Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, Benki ya CRDB PCL na Samsung. Mpango huo unalenga kuwawezesha wateja wa CRDB nchini kujipatia simu za Samsung Galax S3,Samsung Galax note2 na Samsung Galax note 10 katika duka lolote la Vodacom na kuzilipia kwa awamu kwa kati ya miezi 12 na 24. Kulia ni Meneja wa huduma za kibenki wa CRDB, Farida Mbwana.
002 5ae66
Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbawara akimsikiliza Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa, wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa ushirikiano baina ya Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, Benki ya CRDB PCL na Samsung. Mpango huo unalenga kuwawezesha wateja wa CRDB nchini kujipatia simu za Samsung Galax S3,Samsung Galax note2 na Samsung Galax note 10 katika duka lolote la Vodacom na kuzilipia kwa awamu kwa kati ya miezi 12 na 24,kushoto ni Mkuu wa Vifaa vya Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bw.Mgopelinyi Kiwanga.


003 8c7a8
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Tenkolojia Profesa Makame Mbawara akihutubia wakati wa kampuni ya Vodacom,Tanzania, kampuni ya Samsung na Benki ya CRDB PLC walipokuwa wakizindua mpango wa ushirikiano wa kuwawezesha wateja wao kujipatia simu aina ya Samsung Galax S3,Samsung Galax note 2 na Samsung Galax note 10 kwa malipo ya awamu kati ya miaezi 12 hadi miezi 24 ambapo wateja wa benki ya CRDB PLC watajipatia huduma hiyo katika duka lolote la Vodacom nchini..Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam
004 cc46d
Naibu Mkurugenzi Mtendaji –Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB PLC,Bw. Saugata Bandyadhiyay akiongea na waandishi wa habari na baadhi ya wageni waalikwa waliofika katika halfa ya uzinduzi wa mpango wa ushirikiano baina ya Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, Benki ya CRDB PCL na Samsung. Mpango huo unalenga kuwawezesha wateja wa CRDB nchini kujipatia simu za Samsung Galax S3,Samsung Galax note2 na Samsung Galax note 10 katika duka lolote la Vodacom na kuzilipia kwa awamu kwa kati ya miezi 12 na 24.
005 5ae0b
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo..
006 7deed07 26b1d008 84dd4
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto), akigonganisha glasi na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (wa tatu), Meneja Mwandamizi wa Kampuni ya Samsung, Afrika Mashariki, Simon Kariithi (kulia) na Naibu Mkurugenzi Mwendeshaji, Undeshaji na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay, mara baada ya kuuzindua mpango wa ushirikiano wao, Dar es Salaam juzi, ambapo utamwezesha mteja kununua simu za Sumsung kwa malipo ya awamu

Rais Kikwete Atembelea Kujionea Mwenyewe Shughuli za Uokoaji Zinavyoendelea Baada ya Jengo la Ghorofa 16 Kudondoka Jijini Dar es Salaam na Kusababisha Vifo vya Watu 20

  Eneo la tukio ambapo jengo la ghorofa zaidi ya 10 liliporomoka jana asubuhi na hadi kufikia saa sita mchana jana maiti 18 zilikuwa zimeopolewa na watu wanne wakiwemo wakandarasi waliokuwa wanajenga pamoja na wahandisi wa halmashauri ya wilaya ya Ilala wanashikiliwa na polisi, wakati wawili wanaendelea kusakwa ikiwa ni pamoja na mjenzi ambaye kapewa masaa 12 kujisalimisha. Kuna habari kwamba jengo hilo refu kulia pia linajengwa na mkararasi aliyejenga hili lililoporomoka na kila aliye sehemu hii analiangalia kwa jicho la wasiwasi
  Rais Kikwete akiwa eneo la tukio tena leo, baada ya kutembelea jana,  akitoa maagizo kwa Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova kwamba kila aliyehusika na ujenzi wa jengo hilo kuanzia mchoraji, msimamizi na mjenzi wahojiwe na wawajibishwe wakipatikana na kosa
  Rais Kikwete akiongea na viongozi wa msikiti wa Shia ithnaasheri wakati anaondoka eneo la tukio
 Eneo la tukio ambapo jengo la ghorofa zaidi ya 10 liliporomoka jana asubuhi na hadi kufikia saa sita mchana leo maiti 18 zilikuwa zimeopolewa na watu wanne wakiwemo wakandarasi waliokuwa wanajenga pamoja na wahandisi wa halmashauri ya wilaya ya Ilala wanashikiliwa na polisi, wakati wawili wanaendelea kusakwa ikiwa ni pamoja na mjenzi ambaye kapewa masaa 12 kujisalimisha. Kuna habari kwamba jengo hilo refu kulia pia linajengwa na mkararasi aliyejenga hili lililoporomoka na kila aliye sehemu hii analiangalia kwa jicho la wasiwasi.Picha na IKULU

ODINGA AKUBALI KUSHINDWA, ATAKA AMANI IDUMU KENYA

Rais wa awamu ya nne wa Kenya Uhuru Kenyatta, (kushoto) akijadiri jaambo na mpinzani wake Raila OdingaPresident elect Hon Uhuru Kenyatta addresses a press conference after the Supreme Court upheld IEBC declaration as the duly elected president.
President elect Hon Uhuru Kenyatta addresses a press conference after the Supreme Court upheld IEBC declaration as the duly elected president.  NATION MEDIA GROUP
 


 
MGOMBEA wa Urais nchini Kenya kwa tiketi ya muungano wa Chama cha CORD Raila Amolo Odinga amekubali kushindwa katika kesi ya kupinga matokeo aliyofungua katika Mahakama ya Juu nchini humo.

Akihutubia taifa hilo muda mfupi uliopita,Odinga alisema kwamba anakubalina na uhumu hiyo iliyosomwa na Rais wa Mahakama hiyo Jaji Mkuu Willy Mutunga.

"Nimekubalina na matokeo hayo kwa sababu yakuheshimu Katiba ya Kenya ambayo inasema matokeo ya urais yapingwe katika Mahakama hiyo na maamuzi yatakayotolewa na Mahakama ndiyo ya mwisho"alisema Odiga.

Alisema, "Nilikwenda mahakamani kwa maslahi ya wakenya, hivyo natangaza rasmi kukubaliana na matokeo yaliyotangazwa na kuitakia amani serikali iliyoko madarakani,nitashikiana nao katika kujenga nchi yetu".

Odinga ametoa kauli hiyo ikiwa ni muda mfupi baada ya Rais wa Mahakama hiyo Jaji Mkuu Willy Mutunga kutoa hukumu ya kesi hiyo na kusema kwamba mahakama imekubali kwa kauli moja kuwa uchaguzi ulifanywa kwa huru na uwazi na kumfanya  Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto kuchaguliwa kihalali.

 hi yetu".

Wednesday, March 27, 2013

SIRI YA KUUWAWA ZITTO

Katika gazeti la Mtanzania toleo na. 7269 la Jumatano Machi 27, 2013 kuna habari yenye kichwa chenye maneno ‘ SIRI YA KUUWAWA ZITTO YAFICHUKA’ na vichwa vidogo ‘yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini’ dk. Slaa atajwa kumtuma Saanane kummaliza’.
 Habari hii imeniletea usumbufu mkubwa kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wangu, wamejazwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba ninaweza kuuwawa. Napenda kusema yafuatayo: Moja, sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu kunipa sumu hakijawahi kutokea. 
Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi kufanya kikao cha pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba mwandishi ahakikishe kuwa vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi. 
Pili, Siamini kamwe kuwa Katibu Mkuu wa chama changu anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya hivyo. Napenda kurudia kusema kwamba mimi ninaamini kuwa kila nafsi itaonja mauti. Kila mtu atakufa. Kama nitakufa kwa kuuwawa na mtu mwingine ndio itakuwa nimeandikiwa hivyo na Mungu. 
Ndio maana hata siku moja silalamiki kuhusu vitisho vya kuuwawa nk. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kumuua Zitto ndio furaha ya maisha yake atakuwa anajidanganya tu maana Zitto anaweza kufa kimwili lakini mawazo, fikra na maono ya Zitto yataishi tu. 
Siogopi kufa maana maisha niliyoyachagua ndio haya ambayo yamejaa vitisho. Muhimu kwangu ni kufanya kazi zangu kwa bidii, uhodari na uaminifu. Siku zote nitasimamia ukweli bila kujali uchungu wa ukweli huo. 
Tatu, nawashauri watu ambao wamehama CHADEMA na kuhamia vyama vingine watumie muda wao kujenga vyama vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya chama ambacho wao sio wanachama tena. Kama mtu kaamua kuhama CHADEMA anapoteza haki ya kujadili masuala ya CHADEMA maana kama angekuwa anapenda kuyajadili asingehama. 
Naonya mtu yeyote ambaye anatumia jina langu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa. CHADEMA sio pango la watesaji wala wauaji. Kama kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa anayedhani kuna mtu ndani ya CHADEMA anapanga mipango ovu aende kwenye vyombo vya sheria kumshtaki. 
Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi. Nne, Nawashauri viongozi wa CHADEMA na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya chama. Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama. 
Chama chetu lazima kiwe mfano bora wa kuheshimu demokrasia na haki za binaadamu. Wananchi hawawezi kutoa dola kwa chama chenye mifarakano. Tusiruhusu kugawanywa kwa matakwa ya watu wachache. Tusimamie misingi ya kuanzishwa chama chetu. 
-- Kabwe Zuberi Zitto, Mb Dar-es-Salaam Jumatano, Machi 27, 2013

HUYU NDIYE DEREVA ALIYEMGONGA TRAFIKI ENEO LA BAMAGA

   

ANAYEDAIWA kumuua askari wa kikosi cha usalama barabarani wiki iliyopita, Elikiza Nnko, Jackson Stephen Fimbo, jana alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na makosa ya matatu, likiwemo kosa la kuingilia msafara wa Rais. 
Mbele ya Hakimu Mkazi Kwey Lusema, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Lasdilaus Komanya, alilitaja kosa la kwanza kuwa ni la kusababisha kifo cha trafiki huyo kwa kumgonga na gari alilokuwa alikiliendesha.
Ilidaiwa kuwa Machi 18, mwaka huu, katika Barabara ya Bagamoyo kwenye taa za Bamaga jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa anaendesha gari lenye namba za usajili T328 BML aina ya Land Lover Discovery, alitenda kosa hilo.
Komanya alidai mshtakiwa huyo aliendesha gari hilo kwa mwendo wa hatari katika barabara hiyo jambo ambalo huhatarisha usalama wa raia, hivyo kumgonga askari huyo aliyezikwa Alhamisi iliyopita.
Alidai kosa la pili ni kuingilia msafara wa kiongozi, kuwa tarehe iliyotajwa hapo juu, mshtakiwa hakutii maelekezo yaliyokuwa yakitolewa kwa ishara na askari huyo (marehemu Elikiza) ambaye alikuwa na wajibu wa kuyasimamisha magari kwa njia ya ishara.
Komanya alidai shtaka la tatu ni la kushindwa kutoa taarifa za kusababisha ajali katika barabara hiyo.
Hata hivyo mshtakiwa huyo alikanusha mashtaka hayo na Komanya alidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, anaomba tarehe ya kuja kumsomea maelezo ya awali mshtakiwa.
Kwa upande wake hakimu Rusema alisema ili apate dhamana ni lazima awe na wadhamini wawili ambao kila mmoja atasaini bondi ya sh milioni 2 hata hivyo mshtakiwa alitimiza masharti hayo na kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 15 itakapokuja kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.
Katika hatua nyingine, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea kusikiliza kesi ya kuchapisha makala ya uchochezi inayomkabili aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima na wenzake, kwa sababu Kibanda bado amelazwa katika hospitali moja nchini Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu, hivyo kuahirishwa hadi Aprili 29 mwaka huu.

CHADEMA WASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO NA CHAMA CHA CONSERVATIVE CHA WATU WA DENMARK


 
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa (kushoto) akisaini mkataba wa ushirikiano na mwakilishi wa Chama cha Conservative cha watu wa Dermark.
 
Dk. Slaa akibadilishana nyaraka na mwakilishi wa Chama cha Conservative cha watu wa Dermark.

LOWASA AONGOZA VIONGOZI NA WANANCHI MAZISHI YA NYITI ARUSHA

Mh Lowassa akiongoza viongozi kwenda kwenda kuweka udongo kaburini,nyuma yake ni Waziri wa mambo ya nje Mh Bernard Membe.

Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa ameongoza maelfu ya Wakati wa mji wa Arusha na mikoa ya jirani katika mazishi ya mfanyabiashara na Kanda maarufu wa CCM Mkoani Arusha Henry Nyiti,nyumbani kwake Tengeru Arusha.

Nyiti alifariki ghafla wiki iliyopita akiwa katika mgodi wake wa madini,Mahenge Mkoani Morogoro.

Wengine waliyoudhuria Ni pamoja na Waziri wa Mambo ya nje Bernard Membe,Naibu Waziri wa maliasili na utaalii Lazaro Nyalandu,mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dr Reginald Mengi,Mkuu wa mkoa wa Arusha, mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Ridhiwani Kikwete.


 Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa pia alikwenda kutoa pole katika msiba wa Moja wa wazee maarufu eneo la Mto wa Mbu, mzee Athman.
Mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe akiweka udongo
Mh Lowassa akisalimiana na Mh Mbowe


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe akiweka shada la maua

Rais Jakaya Kikwete Afunga Mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi yumo mbunge wa Kigoma Kaskazini-Chadema Zitto Kabwe

Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi mbunge wa viti maalum Ester Bulaya jana katika kambi ya RUVU JKT.Rais Kikwete amefunga rasmi mafunzi hayo jana yaliyofanyika kwa wiki tatu.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, akipokea cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi kutoka kwa kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Muhingo Rweyemamu wakati wakimaliza mafunzo ya JKT, katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, akiapa mbele ya kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Muhingo Rweyemamu, hayupo pichani, wakati wakimaliza mafunzo ya JKT, katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani, akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya pamoja na wenzao wakila kiapo wakati wa kuhitimu mafunzo ya muda mfupi yaliyofanyika katika kambi ya jeshi la Kujenga Taifa Ruvu JKT huko kibaha Mkoani Pwani jana
Mbunge wa Biharamulo, Dk Athanas Mbassa, akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga
Mbunge wa Kiwani Pemba, Abdallah Haji Ali, , akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.

Wakwanza kushoto ni Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, ZItto Kabwe, wakihitimu mafunzo ya JKT katika kambi ya 835 Mgambo JKT iliyopo Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.

  Mbunge Viti maalum Raya Khamis , akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni.
wakwanza katika mstari wa kushoto ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe anayefuata ni Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani, wakiwa kwenye Paredi ya kumaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT Kikosi cha 835  Mgambo JKT kambi iliyopo katika Kata ya Mgambo ilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Mtera Mh. Livingstone Lusinde  Kibajaji"  (wa tatu toka kulia) akipiga kwata jana huko Ruvu
Baadhi ya Wabunge walikuwa wakichukua mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na waheshimiwa wabunge waliohitimu mafunzo maalumu ya JKT jana.Picha Zote za Tanga na Hussein Semdoe

Tuesday, March 26, 2013

TAARIFA JUU YA KANUSHO LA WATU WANAOTUMIA JINA LA FLAVIANA MATATA


Tunapenda kuutaarifu umma ya kuwa kuna genge la watu wanaotumia jina la mwanamitindo wa kimataifa Flaviana Matata katika mtandao wa kijamii wa Facebook ili kuwarubuni wasichana. Kuna ukurasa ujulikanao kama Flaviana Matata’s hutumika kama moja ya ukurasa wa Mwanamitindo huyu kitu ambacho si kweli. Watu hawa huwarubuni wasichana na kuwaahidi kuwatafutia kazi nje ya nchi kwa mgongo wa Mwanamitindo huyu.  Genge hili la uhalifu hudai kuwa kuna ‘kaka’ yake Flaviana ambaye hukutana na wasichana hawa na baada ya mazungumzo anawalaghai kwa njia mablimbali. Pia wahusika hawa hutoza kiasi cha pesa hata kufikia shilingi laki mbili (200,000 )kama tozo  kwa huduma hii ya kuwatafutia kazi nje ya nchi.
Compass Communications kama kampuni inayosimamia shughuli za Flaviana Matata inatoa tahadhari kwa umma kuwa Flaviana Matata hahusiki kwa njia yoyote na ukurasa huu au watu hawa.
 Pia tunawatahadharisha wananchi kuwa wawe waangalifu kwani Flaviana Matata hayuko katika biashara ya kumtafutia mtu yoyote kazi ya Uanamitindo popote pale.
Ukurasa halisi ya Flaviana Matata kwenye mtandaomwa Facebook ni “Flaviana Lavvy Matata” .
Hivi sasa tunaendelea kushirikiana na vyombo husika kwa kutoa taarifa kuhusu uhalifu huu na tunaomba ushirikiano wenu pia Wanajamii.
Imetolewa na
Compass Communications

Rais Kikwete na Rais wa China Xi Jinping Waweka Shada la Maua katika makaburi ya wataalamu wa China waliofariki wakati wa ujenzi wa Reli ya TAZARA

 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais wa China Xi Jinping wakiweka mashada ya maua katika makaburi ya wataalamu wa China waliofariki wakati wa ujenzi wa Reli ya TAZARA.Viongozi hao waliweka mashada hayo ya maua katika makaburi hayo yaliyopo katika kijiji cha Majohe,Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mke wa Rais wa China Mama Peng Liyuan wakiweka maua katika makaburi ya wataalamu wa China waliofariki wakati wa ujenzi wa Reli ya TAZARA huko katika kijiji cha Majohe,Ukonga nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam huku Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wa Rais Xi Jinping wakishuhudia.Picha na Freddy Maro-IKULU

Rais Jakaya Kikwete Apokea ufunguo kutoka kwa Rais Wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe.Xi Jinping wakati wa makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam

Rais Dkt.  Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ufunguo kutoka kwa Rais Wa Jamhuri ya  Watu wa China Mhe.Xi Jinping wakati wa makabidhiano ya Ukumbi wa  Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam  leo.Ukumbi huo umejengwa kwa ushirikiano kati ya Seriklai ya China na  Tanzania.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Xi Jinping wa China wakishangilia jambo wakati wa makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wageni waliohudhuria sherehe za  makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo  jijini Dar es Salaam.
 
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa China Mhe.Xi Jinping wakiangalia picha za  matukio mbalimbali yanayohusu historia ya ushirikiano kati ya China na  Tanzania katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo  wakati wa sherehe za makabidhiano ya ukumbi huo jijini Dar es Salaam  leo.