Tuesday, October 30, 2012

Usafiri wa Treni Dar es Salaam waanza Rasmi

USAFIRI wa kutumia treni jijini Dar es Salaam kutokea eneo la Ubungo Maziwa kuelekea katikati ya Jiji la Dar es Salaam (Stesheni ya Treni) umeanza jana . Treni ya kwanza imeondoka Ubungo majira ya saa 12:00 asubuhi kuelekea katikati ya jiji, ambapo kwa mujibu wa maofisa wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) imetumia wastani wa dakika 30 kufika katikati ya jiji. 
Treni ilioanza kazi jana iliyokuwa na injini mbili (vichwa vya traini) moja ikiwa imefungwa nyuma na nyingine mbele huku ikiwa na mabehewa sita, yaani matano ya abiria wa kawaida (watu wazima) na moja likiwa ni maalumu kwa ajili ya kubeba wanafunzi. Abiria mmoja ni sh. 400 kwa tripu huku wanafunzi wakitakiwa kulipa sh. 100 kwa kila mmoja. 
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ndiye aliyezindua usafiri wa leo ambao ni wamajaribio, akiwa pamoja na viongozi waandamizi kutoka TRC, Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), TAZARA pamoja na Polisi Kitengo cha Reli. 
Treni hiyo pia imezinduliwa pamoja na treni ya TAZARA ambayo itafanya kazi kama ya Ubungo, lakini yenyewe ikianzia eneo la TAZARA kuelekea Mwakanga. Akizungumza mara baada ya ufunguzi huo Waziri Mwakyembe alisema atahakikisha treni hiyo inaendelea kufanya kazi ili kuwasaidia kiusafiri wananchi wa Dar es Salaam ambao wamekuwa wakisumbuliwa na kero ya usafiri hasa kwa foleni, ambapo utumia muda mrefu njiani kuingia na kutoka jijini. 
Alisema jumla ya mabehewa ya treni 14 pamoja na injini mbili zimekarabatiwa na mafundi wazalendo nchini, ambayo ndiyo yatakayokuwa yakifanya kazi ya kusafirisha abiria kuingia na kutoka jijini kila asubuhi na jioni. Alisema kwa sasa inafanya treni moja kwa majaribio lakini baada ya uzinduzi mkubwa zitafanya kazi treni mbili, na zitakuwa zikipishana njiani moja ikirudi na nyingine ikienda. 
Akifafanua zaidi alisema kitendo cha mafundi wazalendo kufanya ukarabati kwa mabehewa na injini kimeokoa kiasi kikubwa cha fedha za umma kwani ukarabati wote umetumia sh. bilioni 2.1 tu, ilhali kama Serikali ingelazimika kukodi injini gharama ingekuwa kubwa zaidi kwani bei ya kukodi injini moja ya treni ni sh. milioni moja kwa siku. 
Hata hivyoDk. Mwakyembe amewataka Watanzania hasa abiria kuwa wavumilivu kwa upungufu utakaojitokeza kwa safari za mwanzo kwani bado wanaendelea kufanya marekebisho kadhaa, lakini baada ya muda mambo yatakaa sawa. 
Mwandishi wa habari hizi alikuwa ni mmoja wa wasafiri walioizindua treni hiyo leo. Awali akizungumza mmoja wa viongozi waandamizi wa TRC, alisema treni hiyo itafanya kazi kila siku isipokuwa kwa siku za jumapili na siku kuu na itaanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa sita mchana na kupumzika hadi saa 9:00 za jioni, itakapoendelea tena na safari zake hadi majira ya saa nne usiku. 
Uchunguzi uliofanywa na muandishi wa habari hizi umebaini kuwa behewa moja la treni linauwezo wa kuchukua abiria 66 wakiwa wamekaa, lina milango minne, feni, taa, muziki/redio, pamoja na mikanda maalumu ya kujishikia kwa abiria ambao watakuwa wamesimama. Aidha mabehewa yote yana madirisha ya kutosha kuingiza na kutoa hewa ya kutosha. 
Treni ilioanza kazi leo, ikitokea Ubungo ilikuwa ikisimama vituo vya eneo la Mwananchi (relini), Tabata Relini, Buguruni Miamani, Tazara, Kariakoo Gerezani (Kamata), na mwisho Kituo Kikuu cha Treni kilichopo jirani na Kituo cha Polisi Kati (Katikati ya Jiji).
Abiria wa Usafiri wa Treni uliozinduliwa rasmi jana kwa ajili ya safari za ndani ya Jiji la Dar wakipanda usafiri huo.
Abiria Wakisubiri Treni Kituoni.
Treni ikiwa safarini.

Abiria wakiwa ndani ya Treni hiyo huku wakiwa ni wenye furaha na usafiri huo.
Waziri wa Uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe akiongozana na baadhi ya viongozi waandamizi kutoka TRC, Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), TAZARA pamoja na Polisi Kitengo cha Reli wakati wa uzinduzi wa Safari za Treni ndani ya Jiji la Dar es Salaam jana.
Waziri wa Uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe akiwa nadni ya treni hiyo sambamba na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi pamoja na viongozi waandamizi kutoka TRC, Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), TAZARA pamoja na Polisi Kitengo cha Reli wakati wa uzinduzi wa Safari za Treni ndani ya Jiji la Dar es Salaam jana. SOURCE:MICHUZI

SIKU YA IBADA YA KUOMBEA AMANI KWA TAIFA MCH. DK RWAKATARE AIBUKA NA UJUMBE MZITO

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni Mh. Dkt. Getrude Rwakatare akitoa Ujumbe kwa Watanzania waliohudhiria Ibada Maalum ya Kuliombea Taifa ambapo ametaka watu kutobaguana kwa misingi ya Dini, Ukabila wala Siasa na kusema pamoja na Utawala bora pia tunahitaji maombezi ili tuweze kufikia Malengo yaliyokusudiwa kulipeleka Taifa linapotakiwa kufikia.
Dkt. Rwakatare amesema nia kubwa ya kufanya Ibada hiyo ya Maombezi ni kutaka kuweka usawa kutokana na siku za hivi karibuni kuibuka kwa Matamko mbalimbali kutoka kwa watu tofauti wakiwemo viongozi wa Kitaifa, Kidini na wa baadhi ya Makundi yanayohitilafiana na kusema tukiomba kwa jina la Mungu kila kitu kitakwenda kama tulivyomuomba ili Tanzania iendelee kuwa nchi ya Amani na Utulivu kama ilivyokuwa miaka yote ambayo ni kimbilio la watu wa Mataifa mbalimbali kwa sababu Watanzania hawajui kuchukiana na wamekuwa watu wa kushikamana kwa miaka yote.
Picha Juu na Chini ni Waumini waliohudhiria Ibada Maalum ya kuliombea Taifa wakinyanyua bendera juu kuimba na kuabudu kwa furaha bila kuonyesha tofauti ya matabaka.
Msanii wa Kimataifa wa muziki wa nyimbo za Injili wa Tanzania Rose Muhando akiimba na kumtukuza Mungu sambamba na wachezaji wake wakati wa Ibada hiyo maalum ya kuliombea Taifa letu liendelee kuwa na Amani, Upendo na Utulivu.
Nimeonja Utamu wa Yesu Weeeeee........!!!
Mchungaji Kiongozi Dkt. Rwakatare akijumuika sambam

Monday, October 29, 2012

Chadema yailiza CCM udiwani

 




Mpaka sasa matokeo ya kata 14 yalnaonyesha kuwa CCM imerejesha kata zake saba, huku CHADEMA ikinyakua kata sita, ambapo mbili zilikuwa za kwao na nne imewanyang’anya CCM na CUF ikiwa na kata moja.

Matokeo
Wakati hali ikiwa hivyo, matokeo ya udiwani katika baadhi ya kata yalikuwa yakiendelea kutolewa huku CHADEMA ikiendelea kuiliza CCM kwa kuzitwaa baadhi ya zilizokuwa kata zake.

Jijini Arusha katika Kata ya Daraja Mbili, CCM ilipoteza kata hiyo kwa CHADEMA iliyozoa kura 2192 dhidi ya 1315 za chama tawala.

CHADEMA wameweza kuzirejesha kata zao mbili za Nangerea jimboni Rombo, ambapo mgombea wao Frank Sarakana alijizolea kura 2370 dhidi ya 1134 za Dysmas Silayo wa CCM pamoja na ile ya Mtibwa, mkoani Morogoro.

Wilayani Sikonge katika kata ya Ipole, CCM walipoteza kata hiyo kwa CHADEMA iliyopata kura 577 dhidi ya 372 za washindani wao, na vilevile kuitwaa kata nyingine ya Lengali wilayani Ludewa iliyokuwa ya CCM.

CHADEMA pia ilikuwa ikiongoza katika kata ya Mpwapwa, mkoani Dodoma, hadi tunakwenda mitamboni usiku.

Nayo CCM ilifurukuta kwa kuzirejesha kata zake za Msalato ya mkoani Dodoma, Bang’ata ya Arumeru Magharibi kwa kuwa 1177 dhidi ya 881 za CHADEMA, Mletele ya Songea CCM ilishinda kwa kura 950 na CHADEMA ilipata 295.

Pia CCM iliweza kutetea kata zake za Mwawaza mjini Shinyanga, Lwenzela mkoani Geita, Bungala wialayni Kahama na Bagamoyo mkoani Pwani kwa kuibwaga CHADEMA wakati Chama cha Wananchi (CUF) kilishinda kata ya Newala.

Sunday, October 28, 2012

CCM YAIBWAGA CHADEMA BUGARAMA, KAHAMA


Chama cha Mapinduzi kimefanikiwa kuibwaga Chadema katika uchaguzi mdogo wa Udiwani uliofanyika katika Kata ya Bugarama wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Habari zilizopatikana zimesema,  katika uchaguzi huo ulifanyika leo CCM imepata kura 1145
Chadema: 772 na TADEA: 156 wagombea wakiwa Nixon Igoko (CCM) Erasmus Francis (Chadema) na Clement Michael (TADEA) 
Pia habari zilizopatikana kutoka Kata ya Shinyanga mjini ambako pia uchaguzi mdogo wa Udiwani umefanyika, zinasema CCM imeshinda. Hata hivyo hatukuweza kupata mizania ya ushindi huo kwa kura.
SOURCE: http://bashir-nkoromo.blogspot.com/2012/10/ccm-yaibwaga-chadema-bugarama-kahama.html

Friday, October 26, 2012

RAIS DK SHEIN ASHIRIKI SALA YA EID EL HAJJ



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein,pamoja na Viongozi wengine
wakijumuika na waislamu na wananchi katika swala ya EID el Hajj
katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar Leo.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
Baadhi ya Waislamu na wananchi wakisikiliza Hotuba,baada
ya Swala ya Eid el Hajj iliyotolewa na Sheikh Soraga,katika Msikiti wa
Mwembeshauri Mjini Zanzibar Leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na waumini ya Dini ya
Kiislamu baada ya kuswali swala ya EID el Hajj katika Msikiti wa
Mwembeshauri Mjini Zanzibar Leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Mzee wa Mshitu wishes you all the best on Eid al Adha

The Management and Staff of Mzee wa Mshitu Blog would like to congratulate all Muslims all over the World for successful celebrations of Eid Al Adha.
 We would like to assure our esteemed readers and viewers of Mzee wa Mshitu Blog will strive to serve you better by bringing you current and well- researched news, analyses and photos by our competent staff.

MAKAMU WA RAIS DKT. GHARIB BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI MSIKITI MPYA WA JIHAD WILAYA YA MWANGA-KILIMANJARO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi katika Jengo la Msikiti mpya wa Jihad, baada ya kuzindua rasmi Msikiti huo uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro, leo Oktoba 26, 2012 wakati wa Sikukuu ya Eid El Hajj, iliyofanyika sambamba na uzinduzi wa Mfuko wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini wa Dini ya Kiislam katika Swala ya Idd El Hajj, iliyofanyika Kitaifa katika Msikiti mpya wa Jihad, uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro. Ibada hiyo ilifanyika sambamba na uzinduzi wa Msikiti huo na uwekaji wa Jiwe la Msingi pamoja na uzinduzi wa Mfuko wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre, leo Oktoba 26, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa Swala ya Idd El Hajj, iliyofanyika Kitaifa katika Msikiti mpya wa Jihad, uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro. Ibada hiyo ilifanyika sambamba na uzinduzi wa Msikiti huo na uwekaji wa Jiwe la Msingi pamoja na uzinduzi wa Mfuko wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na mmoja wa waumini wa Kiislam wa Kijiji cha Vuchama wakati akiondoka eneo hilo baada ya kuzindua na kuweka Jiwe la Msingi na kuchangisha fedha za ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre. leo Oktoba 26, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wananchi na waumini wa dini ya Kiislam, wakati akiondoka eneo hilo.Picha na Ofisi ya  Makamu wa Rais 

Wednesday, October 24, 2012

UMOJA WA MATAIFA WATIMIZA MIAKA 67


Waziri wa Afrika Mashariki akishuhudia upandishwaji wa bendera ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni ishara ya kusheherekea miaka 67 ya Umoja huo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar leo.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Raphael Muhuga aliyemwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Tanzania katika sherehe za maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja wa Mataifa tangu kuzaliwa kwake.

Mgeni rasmi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta akiwasili katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo katika Kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Mataifa Tanzania kusheherekea miaka 67 tangu uanzishwe.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akimlaki na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaa leo.
Pichani Juu na Chini ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou (katikati) akimtambulisha Mh. Samwel Sitta kwa baadhi ya Wakurugenzi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa hapa nchini.
Waziri wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta akipokea heshima ya wimbo wa Taifa baada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo kuhudhuria kilele cha maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa baada ya kutimiza miaka 67 ya UN tangu kuanzishwa.
Mh. Samuel Sitta akikagua gwaride maalum katika kilele cha wiki ya maadhimisho ya Umoja wa Mataifa.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou, Mgeni rasmi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meha Jenerali Raphael Muhuga wakiwa Meza kuu.
Pichani Juu na Chini ni viongozi wa Madhehebu ya Dini nchini wakiomba Dua kwa ajili ya kubariki sherehe za kutimiza miaka 67 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta akizungumza katika sherehe za kutimiza miaka 67 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UN) katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Sitta aliipongeza Umoja wa Mataifa kwa kuisaidia Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo ili kutokomeza umaskini.Waziri Sitta alisisitiza kwamba bado Umoja wa Mataifa unakabiliwa na changamoto nchini kama vile amani na usalama, tatizo la njaa, mabadiliko ya tabia nchi na uwepo wa silaha za maangamizi.
Katibu wa UNA Tanzania Fancy Nkuhi akizungumza kwenye hafla hiyo alisema umoja wa mataifa imefanya kazi kubwa katika kuwaunganisha vijana wa bara la Afrika. Nkuhi alisema kupitia YUNA walitoa elimu ya afya ya uzazi na ugonjwa wa Ukimwi kwa vijana katika mikoa kumi hapa nchini Tanzania katika harakati ya kuelimisha vijana madhara ya ugonjwa huo na afya ya uzazi kwa vijana.
Wanafunzi kutoka shule ya mchepuo wa kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium Schools) ambao walikuwa kivutio wakati wa maadhimisho ya miaka 67 ya wiki ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania wakiwa katika gwaride maalum kupamba sherehe hiyo.
Meza kuu ikifurahia jambo wakati wa gwaride la watoto wa shule ya Heritage baada ya kuonyesha mbwembwe katika kupamba sherehe hiyo.

Mauzo ya Nyumba za Mindu

 

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA


 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UUZWAJI WA NYUMBA ZA MRADI WA UJENZI WA MINDU, DAR ES SALAAM


Kwa mara nyingine tena Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo 24 Oktoba, 2012  limezindua rasmi mauzo ya nyumba katika mradi wake mpya wa Mindu, jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huu ulianza rasmi mwezi Novemba mwaka 2011,  na unatarajiwa kukamilika rasmi Aprili 2013 na mteja kuweza kukabidhiwa nyumba yake mwezi Mei  2013, ikiwa ni miezi 18 baada ya kuanza ujenzi.

Mradi unatarajiwa kugharimu kiasi cha zaidi ya Shilingi bilioni 11 mpaka utakapomalizika, fedha zinazogharamiwa na Shirika kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwemo fedha za mikopo ya benki.

Mradi huu uliopo  mtaa wa Mindu eneo la Upanga, takribani mita 100 kutoka Hospitali Kuu ya Taifa Muhimbili, una sehemu ya nyumba 60 za kuuzwa zilizopo kwenye majengo pacha ya ghorofa 15, uko sehemu zenye huduma zote muhimu za kijamii  zikiwamo hospitali, shule, maduka, na masoko.

Pia Mradi unatarajiwa kuboresha maisha ya wanunuzi wa nyumba hizi kwani upo karibu kabisa na katikati ya jiji na kwamba mnunuzi anaweza kwenda kazini bila kutumia gharama yoyote ya usafiri wa gari.  Aidha, nyumba zipo ndani ya uzio kwa ajili ya usalama wa wakaazi wake  na kuna maegesho ya magari ya kutosha.

Nyumba 60 tu zinazouzwa ambapo kila nyumba ina vyumba vitatu vya kulala, vyo vinajitegemea. Kila nyumba ina ukubwa wa mita za mraba 141 (sq.m), sebule iliyoungana na eneo la kula chakula, choo cha umma, jiko kubwa la kisasa na eneo la kufulia na kuanikia nguo.

Sifa za ziada za mradi huu ni kuwa na eneo maalum la kukusanyia taka, sehemu iliyotengwa maalum kwa ajili ya kufanyia mazoezi (gym), bwawa la kuogelea (swimming pool) na eneo kubwa la ziada la maegesho ya magari.

Kila nyumba itauzwa kwa bei ya TZS  272,050,673.08 bila kodi ya ongezeko la thamani (VAT )  na  TZS  321,019,794.24 ikiwa na kodi ya ongezeko la thamani (VAT).
Tunawahamasisha na kuwakaribisha watanzania wote walio nchini na nje ya nchi kujitokeza ili kununua nyumba hizo. Wanaweza kufanya mawasiliano na Makao Makuu ya Shirika, Ofisi zetu za Mikoa au kupitia barua pepe na kukamilisha taratibu mapema kwa ajili ya kuweza kuingia kwenye mchakato ulio wazi wa manunuzi.
Katika kutekeleza miradi ya ujenzi wa nyumba, Shirika linajenga nyumba za gharama ya juu, kati na chini ili kuwahudumia watanzania wa kada zote. Katika azma hiyo, nyumba 10,000 zitakazojengwa kufikia 2015 zitahusu watu wa  kipato cha juu na nyumba 5,000 zitakazojengwa kufikia mwaka huo zitakuwa ni nyumba za watu wa kipato cha chini.

 Shirika limeanza kujenga nyumba za gharama ya kati na juu ili kupata faida itakayoliwezesha kuwajengea watu wa kipato cha chini nyumba za gharama nafuu. Hii inatokana na ukweli kuwa Shirika halipati ruzuku toka serikalini ya kujenga nyumba kwa ajili ya wananchi wa kipato cha chini. Mradi huu wa Mindu tunaouzindua hii leo, ni moja ya miradi ya ujenzi wa nyumba za watu wenye kipato cha juu..
Ukiwa mdau na mnunuzi mtarajiwa, ama una ndugu/rafiki anayetamani kununua nyumba katika mradi huu, tafadhali waweza kutumia akaunti nambari : …….. au wasiliana na Kitengo cha Mauzo simu namba 0754 444 333; barua pepe: sales@nhctz.com na pia tembelea tovuti ya Shirika www.nhctz.com  kwa maelezo zaidi.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA JAMII
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA







SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) LAZINDUA MAUZO YA NYUMBA ZA MAKAZI MINDU PLACE

 Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa, David Misonge Shambwe (kulia) akizungumza kwenye uzinduzi wa nyumba za kuuza za makazi za Mindu zilizopo jijini Dar es Salaam leo mchana huu, kulia kwake ni Meneja wa Masoko na Utafiti wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Itandula Gambalagi.
Meneja wa Masoko na Utafiti wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Itandula Gambalagi (kushoto) akibadilisha mawazo na bwana Stanley wa Aggrey and Clifford ambao ni wadau wakubwa wa matangazo na utafiti wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye uzinduzi wa nyumba za kuuza za makazi za Mindu zilizopo jijini Dar es Salaam leo mchana huu.
 Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa, David Misonge Shambwe (kulia) akizungumza na vyombo vya habari kwenye uzinduzi wa nyumba za kuuza za makazi za Mindu zilizopo jijini Dar es Salaam leo mchana huu.

Baadhi ya watu waliofika kushuhudia  uzinduzi wa nyumba za kuuza za makazi za Midu zilizopo jijini Dar es Salaam leo mchana huu.
 Nyumba hizo za makazi zinavyoonekana kwa ndani
  Wadau muhimu wa sekta ya habari wakifuatilia kwa kina maelezo ya Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa, David Misonge Shambwe (hatyupo pichani) wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa nyumba za kuuza za makazi za Mindu zilizopo jijini Dar es Salaam leo mchana huu. (Picha zote kwa hisani ya SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA)



RAIS JK AKUTANA NA MWALIMU WAKE

 










PICHANI NI MATUKIO MBALIMBALI YA RAIS JAKAYA KIKWETE ALIPOKUTANA NA MMOJA WA WALIMU WALIOMFUNDISHA UDSM MIAKA YA 1970, PROF. ABDUL AZIZ JALLOH. WAWILI HAO WALIKUTANA BAADA YA MIAKA MINGI WAKATI RAIS AKIZINDUA ZOEZI LA TATHMINI YA UTAWALA BORA CHINI YA MPANGO WA AFRIKA KUJIPIMA KIUTAWALA BORA (APRM) MACHI, 2012 IKULU DAR ES SALAAM. PROF. JALLOH ALIKUWA NCHINI AKIWA MMOJA WA WATAALAMU BINGWA WALIOKUJA KUHAKIKI HALI YA UTAWALA BORA NCHINI. MWENYE 'FRENCH TIE' NI WAKILI (BARRISTER) AKERE MUNA ALIYEKUWA KIONGOZI WA JOPO LA WAHAKIKI HAO.