Friday, September 28, 2012

TASWIRA ZA JINSI WAMACHINGA WALIVYOVAMIA NA KUGAWANA NA KUJENGA VIBANDA VYA KUENDESHA BIASHARA ZAO MJINI ARUSHA JANA

Vibanda vya wafanyabiashara wadogo (Wamachinga) walivyojenga baada ya kuvamia na kujipimia maeneo. Hapa vibanda hivyo vinaonekana kuwa tayari kwa biashara zao.
Wanamama wanaouza mboga mboga ambao walikuwa sehemu ya Wamachinga waliovamia uwanja huo, wakiendelea na biashara zao baada ya kujigawia maeneo.
Wamachinga jiji la Arusha waliokosa eneo kwenye uwanja wa NMC jana wakigawana maeneo baada ya kuvunja uzio wa bati uliokuwa umezungushiwa kwenye uwanja ambao awali ulikuwa unamikiwa na Manispaa ya Arusha kabla ya kuuzwa kwa mtu binafsi karibu na Soko la Kilombero, Kata ya Ngarenaro.
 Wamachinga jiji la Arusha waliokosa eneo kwenye uwanja wa NMC jana wakigawana maeneo baada ya kuvunja uzio wa bati uliokuwa umezungushiwa kwenye uwanja ambao awali ulikuwa unamikiwa na Manispaa ya Arusha kabla ya kuuzwa kwa mtu binafsi karibu na Soko la Kilombero, Kata ya Ngarenaro.
 Wamachinga jiji la Arusha waliokosa eneo kwenye uwanja wa NMC jana wakigawana maeneo baada ya kuvunja uzio wa bati uliokuwa umezungushiwa kwenye uwanja ambao awali ulikuwa unamikiwa na Manispaa ya Arusha kabla ya kuuzwa kwa mtu binafsi karibu na Soko la Kilombero, Kata ya Ngarenaro.
 Polisi wakiwa kwenye magari yao baada ya kufika, kuegesha magari yao upande wa pili wa barabara kwenye kituo cha mafuta kwa muda, kisha kuondoka bila kutawanya wafanyabiashara wago (Wamachinga) waliovamia na kujitwalia eneo hilo.
Polisi wakiwa kwenye magari yao wakifika na kuyaegesha magari yao upande wa pili wa barabara kwenye kituo cha mafuta kwa muda kabla ya kuondoka bila kufanya juhudi zozote za kuwazuia machinga hao kujitwalia eneo hilo.Picha na Grace Macha-
----
Na Mahmoud Ahmad-Arusha

 Hali si shwari katika jiji la Arusha na viunga vyake baada ya wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga kuzua tafrani mara walipovamia eneo la kiwanja cha Ermoil lililopo mkabala na soko la Kilombero na kisha kuanza kugawana maeneo ya kufanyia biashara kwa kujipimia.

Vurugu hizo zimetokea jana wakati Rais Jakaya kikwete akiwa jijini Arusha kufungua mkutano mkubwa wa mapinduzi ya kijani ambao umehudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka nchi za Afrika,Amerika,Ulaya na Asia. Hatahivyo,katika vurugu hizo mfuasi mmoja wa chama cha     wananchi(Cuf),Athuman Abrahaman alishambuliwa kwa mawe na kisha kujeruhiwa eneo la usoni na watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa Chadema huku gari la matangazo la Cuf nalo likijikuta likipopolewa kwa mawe na spika zake kuharibika vibaya. Askari wa jiji la Arusha walionekana majira ya saa 3;30 asubuhi akipita na gari lao katika maeneo mbalimbali ya jiji hapa huku wakiwatangazia wamachinga wote kuondoka katika maeneo ambayo hayajatengwa kufanyia biashara zao. 

Askari hao walikuwa wakiwatangazia wamachinga hao kuondoka katika maeneo ambayo hayajatengwa kufanyia biashara huku wakitamka ya kwamba endapo wakikahidi watachukua bidhaa zao kwa nguvu na kuwachukulia hatua za kisheria. Hatahivyo,baada ya muda mfupi ndipo askari hao wali anza kutekeleza majukumu yao ya kusomba bidhaa hizo na kisha kuzipakia ndani ya gari lao huku wakivipeleka katika ofisi za manispaa ya Arusha. 

Hatua hiyo iliwapelekea wamachinga hao kujikusanya kwa pamoja na kisha kuvamia ghafla eneo la wazi wa Ermoil kwa kuvunja uzio wa mabati uliokuwepo na kisha kuanza kujigawia maeneo kwa kuyapima kwa kamba. Wamachinga hao zaidi ya 200 walivamia huku wengine wakitumia nafasi hiyo kupora mali mbalimbali zilizopo ndani ya eneo hilo kama mabati,nondo na saruji zilizokuwa ni mali za mtu anayedaiwa kumiliki eneo hilo. Katika heka heka za kugawana viwanja ndani ya eneo hilo wamchinga hao walikata miti iliyokuwemo ndani na kisha kuanza kuichoma kwa moto hali ambayo ilisababisha wingu zito la moshi kutanda hewani.

 Hatahivyo,wakati tafrani hiyo ikiendelea polisi waliokuwa wamesheheni kwenye magari yao walikuwa wakipita mara kwa mara kuzunguka eneo hilo lakini hawakuonekana wakifanya udhibiti wowote zaidi ya kuwaangalia wamachinga hao. Kitendo cha askari wa jeshi la polisi mkoni hapa kushindwa kuwadhibiti wamachinga hao kimetajwa kimetokana na uhaba wa askari kutokana na ugeni wa mkutano wa jana pamoja na kuhofia hali ya amani kuharibika jijini Arusha.

Mkuu wa wilaya ya Arusha,John Mongella alilaani tukio hilo na kusema kwamba wamachinga hao wamevamia eneo hilo kimakosa kwa kuwa si la kwao huku akikitupia lawama chama kimoja cha siasa hapa nchini kwamba kimehusika katika kuhamasisha vurugu hizo. Alisema kwamba kwa sasa watakutana kujadili tukio hilo kwa undani kwa kuwa wana ugeni mkubwa lakini alisema kwamba kitendo cha wafuasi wa Chadema kupiga mawe gari la Cuf na mfuasi wake si cha kiungwana. 

Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya jiji la Arusha,Omary Mkombole alisema kwamba kitendo cha wamachinga hao kuvamia eneo hilo ni kuvunja sheria na wataondolewa hapo hivi karibuni. Mkombole,mbali na kulaani tukio hilo alisema kwamba uongozi wa jiji umepanga maeneo mbalimbali ya kufanyia biashara na eneo hilo ni mali ya mtu binafsi ambapo alikuwa ameanza jitihada za kuliendeleza.

WARSHA YA UMUHIMU WA ALAMA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA KWA VIZIWI YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari( MAELEZO)Assah Mwambene  kushoto akifungua Warsha kuhusu umuhimu wa Lugha ya Alama katika Utoaji  huduma  kwa Viziwi kwenye Ukumbi wa World Family of  Radio Maria,Regency Estate mjini Dar es Salaam na kulia ni Mkalimani wa Lugha ya Alama.
(PICHA NA ANNA ITENDA WA MAELEZO)
 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Ndugu Assah Mwambene Kushoto akibadilishana  mawazo na  Deputy Chief Executive Officer  wa (CCBRT) Mama Susan Boon kwenye Warsha ya kuhusu Umuhimu wa Lugha ya Alama katika utoaji  huduma kwa Viziwi kwenye Ukumbi wa world Family  of  Radio Maria ,Regency Estate mjini Dar es Salaam leo.
 
Mkuu wa wa Idara ya Wanawake Chama Cha Viziwi Tanzania( CHAVITA)Lupi Maswanya Mwaisaka akitoa neno la Shukrani kwa Mgeni  Rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Ndugu Assah Mwambene wakati wa kufungua Warsha kuhusu Umuhimu wa  Lugha ya Alama katika utoaji  huduma kwa Viziwi kwenye Ukumbi wa World Family of Radio Maria uliopo Regency Estate  mjini Dar es Salaam leo.
 
Baadhi ya Washiriki kutoka Vyama na Asasi za Viziwi nchini ,Serikalini na kutoka Mashirika mengine ya kiraia wakimsikiliza Mkurugenzi  wa Idara ya Habari  (MAELEZO )Ndugu Assah Mwambene (hayupo pichani )akifungua Warsha  kuhusu umuhimu wa Lugha ya Alama katika Utoaji huduma kwa Viziwi kwenye Ukumbi  wa World Family of Radio Maria mjini Dar es Salaam leo.
 
Baadhi ya Washiriki kutoka Vyama na Asasi za Viziwi nchini ,Serikalini na kutoka Mashirika mengine ya kiraia wakimsikiliza Mkurugenzi  wa Idara ya Habari  (MAELEZO )Ndugu Assah Mwambene (hayupo pichani )akifungua Warsha  kuhusu umuhimu wa Lugha ya Alama katika Utoaji huduma kwa Viziwi kwenye Ukumbi  wa World Family of Radio Maria mjini Dar es Salaam leo. 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari ( MAELEZO)Ndugu Assah Mwambene  wa kwanza kushoto akiangalia baadhi ya kazi zinazotengenezwa  na Viziwi wakati wa warsha kuhusu umuhimu wa lugha ya alama katika utoaji wa huduma kwa viziwi kwenye Ukumbi wa world Family  of  Radio Maria ,Regency Estate mjini Dar es Salaam leo.
 
Baadhi ya washiriki wa Warsha kuhusu Umuhimu wa Lugha ya Alama katika utoaji  huduma kwa Viziwi kwenye picha ya pamoja na mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Ndugu Assah Mwambene  wa sita kushoto (aliyevaa suti) kwenye Ukumbi wa World Family of  Radio Maria ,uliopo  Regency Estate mjini Dar es Salaam leo.

Rais Kikwete afungua mkutano wa kimataifa wa African Green Revolution mjini Arusha

 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mwenyekiti wa Alliance for a Green Revolution in Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mwenyekiti wa Alliance for a Green Revolution in Africa Dkt.Kofi Annan(kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Bill and Melinda Gates, Bibi Melinda Gates wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa” Africa  Green Revolution Forum 2012,” uliofanyika katika ukumbi wa Ngurdoto mountain Lodge mjini Arusha leo.
 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa wa”African Green Revoultion mjni Arusha leo(picha na Freddy Maro)
 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa wa”African Green Revoultion mjni Arusha leo(picha na Freddy Maro)

Thursday, September 27, 2012

Bendi mbalimbali kukamua kukamua tamasha la Tanzania Live Music Festival kesho Leaders


 
Balozi wa tamasha la Tanzania Live Music Festival Jackline Wolper akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Leaders leo wakati wandaaji wa tamasha hilo walipozungunzia kukamilika kwa maadalizi  katika picha wanaofuatia ni Mzee King Kikii, Tarsis Masela  wa Akudo Impact na Jamwaka kutoka Sikinde
……………………………………….
Tanzania Live Music Festival imewadia! ambapo kuanzia kesho tarehe 28/29 mashabiki wote wa muziki wa dansi jijini  Dar es saalam wanakaribishwa kuburudika na muziki wa wa dansi bila kikomo,katika viwanja vya Leaders jijini  ikijumuisha bendi zaidi ya kumi ambazo zitakuwa zikiimba live.
Bendi zitakazo tumbuiza ni Sikinde, Msondo, B Band Mashujaa Band, Akudo, FM Academia, Wazee Sugu na wengine kibao!
Lakini pia kutakuwa na bendi zitakazosindikiza onesho hilo  kama vile Khadija Kopa malikia wa Mipasho na Mashauzi Classic chini ya Isha Mashauzi.
Lengo kubwa la Tamasha hili ni kusaidia Chama cha Dansi Tanzania CHAMUDATA ili kuboresha na kuendeleza chama hicho.
waandaajiwa tamasha hilo wametoa shukurani kwa  Kampuni zote ambazo zimekuwa zikiunga mkono maadalizi yote  ili kufanikisha  Tamasha hili.
Kampuni hizo ni
TIMES FM, GLOBAL PUBLISHERS, MAJIRA, WHINDHOEK, REAL STAR, FLY 540, FACE TO FACE BAR and RESTAURANT, PUSH MOBILE
Wapenzi wote wa muziki wa dansi mnakaribishwa kujiunga pamoja na kupata burudani. Kiingilio ni 20,000 kwa VIP na 5000 kwa tiketi za kawaida. Wote mnakaribishwa.

Majina ya makada wa CCM walioteuliwa kuwania nafasi mbalimbali za uongoz

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), jana kimetangaza majina ya makada wake walioteuliwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi, ambapo vijana wameonekana kupewa nafasi kubwa zaidi za kuwania fursa ya kukiongoza Chama hicho kikongwe nchini.
Vijana wengi wameonekana kuchomoza katika nafasi za uenyekiti, makamu mwenyekiti, itikadi na uenezi, uchumi na fedha na zile za ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC).
Miongoni mwa vijana mahiri na wenye uwezo mkubwa katika uongozi walipata fursa ya kupitishwa na NEC ni pamoja na Paulo Herman Kirigini, ambaye ameteuliwa kuwania ujumbe wa NEC kupitia viti vitatu bara kwa kundi la Wazazi, ambako atachuana na wakongwe kadhaa wakiwemo mawaziri na wabunge.
Vijana wengine waliochomoza katika kuwania nafasi mbalimbali ni Christopher Pallangyo (Mwenyekiti wilaya ya Meru), Latifa Ganzel (Morogoro Mjini), Harold Lyimo (Arusha), Peter Mushao (Longido), Nanai Konina (NEC- Monduli), Patrick Myovela (Iringa Vijijini), Muhaji  Bushako, Alice Mjula (Muleba) na Asad Salum Kikule (Kilolo).
Wengine ni Murdhid Ngeze (Bukoba Vijijini), Revocatus Babeiya, Editha Kokutona Rwezaula, Alistides Mujwahusi, Lucas Zakaria, Janes  Darabe.
Vijana wengine ni Dk. Sebastian Ndege (NEC-K-ndoni), Thabiti Ntuyabaliwe (NEC-Kndoni), Saidi Omar (NEC-K-ndoni).
Wengine ni Issa Mangungu (31) Phares Magesa (33) NEC Temeke,  Leonard Bugomola (27),
Malugu Mwendesha (33) nafasi ya katibu uchumi mkoa wa Geita, Christian Sinkonde (31) NEC Kisarawe.
Vijana wengine waliochomoza kwenye nafasi ya NEC, Morogoro Vijijini Omari Mgumba (36)
Robert Selasela (28), Zuberi Mfaume (39) na Morogoro Mjini ni Robert  Makorere (32),Kelvin Mutatila Njuwa (33 na Amina  Mhina (36).
Kuteuliwa kwa idadi kubwa ya vijana kunaashiria kuwa CCM imeanza kutekeleza mikakati yake ya kuendelea kukisuka upya na kuingiza damu changa kwa ajili ya kuendeleza mapambano ya kisiasa na kuwadhibiti wapinzani.

MISS EAST AFRICA 2012,TANZANIA KUPATA MWAKILISHI WAKE MWEZI UJAO




Mrembo atakaeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya mwaka huu ya urembo ya Miss East Africa atatangazwa rasmi tarehe 14/10/2012 katika hotel ya Serena Jijini Dar es salaam.
 Jumla ya warembo 148 wameomba kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss East Africa mwaka huu lakini ni Mrembo mmoja tu atakaechaguliwa kuiwakilisha Nchi katika mashindano hayo makubwa ya urembo katika ukanda huu wa Africa na yanayosubiliwa kwa hamu na wapenzi wa fani hiyo ndani na Nje ya Africa Mashariki
 Aidha maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri ambapo yatafanyika tarehe 07 December, 2012 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam
 Wakati huohuo Nchi ya Burundi imebadili mwakilishi wake ambapo sasa itawakilishwa na mrembo Ariella Kaneza (23), Mwanafunzi wa mwaka wa pili wa chuo kikuu cha Universte De Lumiere akichukua Degree ya marketing.
 Taarifa kutoka Burundi iliyosainiwa na Mratibu wa Mashindano ya Miss East Africa Nchini humo, Serge Nkurunziza, zimeeleza kwamba Burundi imeamua kubadili mwakilishi wake ili kuhakikisha kwamba Nchi hiyo inashinda Taji hilo kwa mara ya pili tangu mashindano hayo yalipoanzishwa mwaka 1996 baada ya kugundua kwamba mwakilishi wake wa awali anapungukiwa baadhi ya sifa chache za kuweza kunyakua taji hilo. (Burundi imewahi kushinda Taji hilo mara moja mwaka 2008 kupitia kwa mrembo wake Miss Claudia Niyonzima)
Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yanatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake na yatashirikisha warembo kutoka Nchi 16 za ukanda wa Afrika Mashariki.
 Nchi zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine zilizoalikwa kushiriki ni pamoja na Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Southern Sudan, Malawi, pamoja na visiwa vya Seychelles, Madagascar, Reunion, Comoros, na Mauritius.
Mashindano ya Miss East Africa yanalenga kukuza ushirikiano na kutangaza utamaduni wa Afrika Mashariki, pamoja na kutangaza utalii wa Tanzania kama Nchi wenyeji wa mashindano hayo makubwa katika ukanda huu wa Afrika
Mashindano ya Miss East Africa yanamilikiwa na kuandaliwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam,.

Wednesday, September 26, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA MAOFISA WA JWTZ IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba (kulia) kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu leo jijini Dar es salaam. Meja Jenerali Ndomba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Abdulrahaman Shimbo aliyestaafu utumishi jeshini kwa Umri.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga (kulia) kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na walioapishwa leo.
 Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Ulinzi na Maofisa wa JWTZ na Jeshi la Kujenga Taifa leo mara baada ya hafla fupi ya kuwaapisha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Samuel Ndomba na Mkuu wa JKT Meja Jenerali Raphael Muhuga.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Devis Mwamunyange (kushoto) akimweleza jambo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam.Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (katikati).
 Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa leo jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Maofisa waandamizi wanawake wa JWTZ leo Ikulu jijini Dar es salaam. Kulia ni Meja Jenerali Lilian Kingazi (Kulia) na Meja Jenerali Grace Mwakipunda (kulia).

REDDS MISS TZ YATANGAZA TAREHE NA UKUMBI WA FAINALI YA KITAIFA 2012 NA SIKU YA KUANZA KAMBI







Mkurugenzi wa LINO AGENCY Hashim Lundenga katika akizungumza na waandishi wa habari.

Mashindano ya Redds Miss Tanzania kwa sasa yamekamilika katika hatua zote na hatua ya mwisho ilikuwa hatua ya kanda ambayo kwa sasa imekamilika na kufanikiwa kuwapa warembo jumla ya 30 .
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa LINO AGENCY Hashim Lundenga alisema mashindano kiujumla katika ngazi zote hadi kanda yamekuwa na mafanikio makubwa na kuonyesha kuwa fainali ya Taifa ya mwaka huu itakuwa na ushindani wa hali ya Juu.
 
Washiriki wengi wa mwaka huu kwa asilmia 90   ni wasomi  wanafunzi wa Vyuo Vikuu na wengine wanatarajia kujiunga na Vyuo Vikuu, jambo ambalo litaleta hamasa kubwa katika shindano la mwaka huu.
 
Baada ya kukamilika kwa mashindano hayo ya Kanda kwa sasa tunatangaza rasmi kuwa warembo wote 30 walioshinda na kuingia katika kinyang,anyiro cha Redds Miss Tanzania 2012 wataingia kambini siku ya jumanne October 2,2012 katika Hotel yenye hadhi ya kitalii ya GIRAFFE HOTEL  Iliyopo hapa Jijini Dar Es salaam,Washiriki hao watakuwa kambini kwa muda wa mwezi mmoja.
Tunapenda kuwajulisha wadau wa tasnia ya urembo kwamba shindano la REDDS MISS TANZANIA 2012 litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 03 November 2012 katika Ukumbi wa Hotel ya Blue Peal (Ubungo Plaza).
 
Kwa Upande wake Meneja wa Kinywaji cha Redds Original Victoria Kimaro alisema wao kama wadhamini wakuu wa Redds Miss Tanzania wamejipanga kwa nguvu kubwa kutoa burudani ya aina yake kwa wadau wote wa tasnia ya urembo hapa nchini sambamba na kuhakikisha warembo wote waliofanikiwa kuingia hatua ya fainali watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali.
 
Kwa kuzingatia mabadiliko ya Kalenda ya Mashindano ya urembo ya Dunia, Mrembo wa Tanzania atakuwa na muda  mrefu wa maandalizi kwani atatakiwa kuripoti katika Fainali za Mashindano ya urembo ya Dunia katikati ya mwaka ujao. 2013.

CHIKAWE ALONGA UMOJA WA MATAIFA


Waziri wa Katiba na Masuala ya Sheria, Mhe. Mathias Chikawe ( Mb ) akipitia kwa mara ya mwisho hotuba yake kabla ya kuisoma, wakati wa mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa uliokuwa ukajadili Utawala wa Sheria katika Ngazi ya Kimataifa na Kitaifa, katika hotuba yake katika mkutano huo ambao ulifunguliwa na Katibu Mkuu, Ban Ki Moon, na kuhutubiwa na Viongozi wakuu wa nchi na serikali wakiwamo Mawaziri kutoka nchi 80, alielezea namna ambavyo Jamhuri ya Muungano imekuwa ikizingatia utawala wa sherika katika ngazi ya taifa, kanda na kimataifa na akaelezea pia mchakato unaoendelea wa maandalizi ya Katiba mpya. wengine katika picha kuanzisha kulia ni Mhe. Abubakari khamisi Bakari,(Mb) Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe, Musa Hassan Mussa ( Mb) kutoka Zanzibar na waliokaa nyuma ni wataalam wa sheria.

Mhe. Mathias Chikawe ( Mb) akihutubia Mkutano wa Kilele wa Umoja wa Mataifa uliokuwa ukijadili ajenda ya Utawala wa Sheria katika ngazi ya Kitaifa na Kimataifa. Mkutano huo wa Siku Moja ulifanyika siku ya Jumatatu hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. 

Na Mwandishi Maalum 

Waziri wa Katiba na Masuala ya Sheria Mathias Chikawe ( Mb) amesema, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejidhatiti ipasavyo katika utekelezaji na uzingatiaji wa utawala wa sheria kuanzia ngazi ya taifa, kanda na kimataifa. Chikawe ameyasema hayo jana jumatatu hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, katika Mkutano wa kilele ambao ajenda yake kuu ilikuwa ni Utawala wa Sheria kitaifa na Kimataifa”. 

Mkutano huo ambao umeandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa, Ban Ki Moon, umehudhuriwa na kuhutubiwa na viongozi wakuu wa nchi na serikali na mawaziri zaidi ya 80 wanachama wa Umoja wa Mataifa. 

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Umoja wa Mataifa kuandaa mkutano wa aina hii ambao ulijikita katika kuzungumzia utawala wa sheria kama kiungo muhimu kati ya ngazi ya kitaifa na kimataifa na ukuaji wa uchumi, maendeleo endelevu na kuondoa umaskini na njaa Aidha mkutano huo pia umetoa fursa kwa nchi kuelezea namna gani zimekuwa zikizingatia au kutekeleza utawala huo katika ngazi ya kimataifa na kimataifa.

 Mkutano huu umefanyika siku moja, kabla ya kuanza kwa majadiliano ya Mkutano wa 67 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, mkutano utakaofunguliwa leo siku ya Jumanne, utahutubiwa na viongozi mbalimbali akiwamo Rais wa Marekani Barack Obama. 

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huu wa 67 unaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe(Mb) akimwakilisha Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete. 

Waziri Mathias Chikawe ni miongoni wa wajumbe wanaohudhuria mkutano huu akiwamo pia Mhe. Abubakari Khamis Bakali (Mb), Waziri wa Katiba na Masuala ya Sheria kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Vita Kawawa ( Mb) na Mhe. Musa Hassan Musa ( Mb) kutoka Zanzibar Akizungumzia utawala wa sheria katika ngazi ya kitaifa, Waziri Mathias Chikawe amewaeleza wajumbe wa mkutano huo kwamba, utawala wa sheria ni sehemu ya makubaliano ya kijamii kati ya taifa na mtu binafsi.

 “ Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imekuwa nguzo muhimu katika kutoa mwongozo na kipimo cha utawala bora. Na kwa sababu hiyo misingi ya usawa mbele ya sheria, uwajibikaji kwa sheria na mgawayo wa madaraka vimezingatiwa katika utawala wa sheria” akasema na kuongeza “ Kwa kuzingatia kwamba Katiba inatokana na wananchi na inazingatia kile ambacho wananchi wanataka, Tanzania hivi sasa iko kazi zoezi linalohusisha kila mtu kupitia Katiba ya sasa kwa alengo la kuanda katiba mpya baada ya Katiba ya sasa kuitumikia Tanzania kwa miaka 50 iliyopita”.

 Ameeleza. Aidha Waziri Chikawe amesema Katiba ya Tanzania pia imetoa nafasi ya kuanzishwa kwa taasisi za kitaifa zenye wajibu wa kuhakikisha kwamba utawala wa sheria siyo tu unafuatwa lakini pia haki za wananchi zinalindwa Akabainisha kwamba baadhi ya taasisi za aina hiyo ni Kamisheni ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, taasisi ambayo kwa miaka mingi imeendelea kufanya kazi nzuri. 

Akaongeza kwamba uzingatiaji wa misingi ya ulinzi na uhifadhi wa haki za binadamu, fursa ya kupata haki na uasawa, utawala bora na utawala wa sheria nchini ni mambo ambayo yamezingatiwa vema katika Dira ya taifa ya mwaka 2025 na Mpango wa Taifa wa Kukuza uchumi na Kupunguza Umaskini.

 Katika hatua nyingine, Waziri wa Katiba na Utawala wa Sheria amesema, uimarishaji wa mfumo wa sheria ni moja yamambo ambayo yamepewa kipaumbele katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano. Na kwamba serikali imefanya jitihada za makusudi za kuongeza idadi ya majaji, mahakimu, ujenzi wa mahakama mpya na kuzikarabati za zamani. 

 Akaeleza pia kwamba kumekuwa na mikakati ya kuboresha huduma za mahakama kwa kuanzisha huduma itakayojulikana kama tele justice. Aidha akauelezea umma huo wa Umoja wa mataifa, kwamba Tanzania imejipanga kupambana kikamilifu na rushwa ili kuwa na jamii huru. Awali akufunguaa mkutano huo ambao mwishoni ulipitisha Andiko, Katibu Mkuu Ban Ki Moon alitoa mwito kwa jumuia kushirikiana na kwa kutumia sheria ya kimataifa, kutatua migogoro kwa njia ya zamani na kuhakikisha kwamba mgogoro hiyo haitokei tena. 

Aidha Katibu Mkuu amezitaka nchi kuimarisha utawala wa sheria ikiwa ni pamoja na kuwapatia mafunzo ya polisi na kuimarisha idara ya mahakama hususani katika nchi zile ambao hali ya amani ni tete na zimekuwa zikikumbwa na migogoro. Kwa upande wake, Rais wa Baraza Kuu la 67 la Umoja wa Mataifa Bw. Vuk Jeremic ameonya dhidi ya kuona sheria ya kimataifa kama nyenye umuhimu mdogo na inamadhara kwa uendeshaji wa masuala ya dunia Akasisitiza kwamba kama nchi na watawala watakuwa madhubuti na kuzingatia utawala wa sheria ni wazi hakuta kuwapo na ushawishi wa kukimbilia vita. 

Akasisitiza umuhimu wa uwepo wa Makama ya Makosa ya Jinai (ICC) na kuzitaka nchi ambazoa hazijaitambua mahaka hiyo au kuiona kama si sehemu ya Umoja wa Mataifa kuachana na dhana hiyo Akasema kazi ya ICC ni pamoja na kuhakikisha kwamba haki inatendekea kwa kuwafikisha mbele ya mahakama hiyo watuhumiwa wa makosa ya jinai na kuzuia kutoa jirudia kwa mauaji ya kimbari. 

 Aidha mkutano huo pia ulihutubiwa na viongozi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa kama vile Kamisheni ya Haki za Binadamu, Rais wa Mahakama ya Kimataifa ) ICJ Bw Petro Tomka ambaye alibainisha kwamba ni nchi 67 tu kati ya Nchi 193 za Umoja wa Mataifa, sawa na asilimia 34 ikiwa ni pamoja na mwanachama mmoja tu wa Baraza kuu la Usalama ambazo zimeikubali na kuitambua ICJ.

Mwandishi Agnes Yamo aaga dunia


Wednesday, September 19, 2012

CUF wachangisha fedha kujipanga na uchaguzi 2015


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) akichangia pesa kwenye harambee iliyoambatana na matembezi ya hisani kuanzia Buguruni hadi kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam leo ambapo zaidi ya Sh 129 milioni zilichangwa. Pesa hizo ni kwaajili ya kueneza kampeni yao ya dira ya mabadiliko mikoani kote kujiandaa na uchaguzi 2015.



Profesa Lipumba akimuangalia Mwenyekiti wa  chama hicho wilaya ya Ilala Saidi Rico alipokuwa akichangia.



Msongamano wa wanachama wa chama hicho kwenye foleni ya kwenda kuchangia fedha