Tuesday, June 19, 2012

Mnyika atimuliwa Bungeni

 

Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akitoka katika ukumbi wa Bunge la Tanzania leo mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea.
(Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dodoma)

 
Mbunge wa Jimbo la Ubungo John Mnyika akiteta na Mbunge wa jimbo la Wawi Hamad Rashid Mohamed (kushoto) na Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo mara baada ya kuondolewa Bungeni leo mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea.

Monday, June 11, 2012

KIkao kazi cha maafisa habari na mawasiliano na serikali

Waziri wa Habari, vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiongea na maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali leo jijini Mwanza.Pamoja na mambo mengine amewataka maafisa hao kuielimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo yanayofanywa na serikali kupitia vyombo vya habari.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Seith Kamuhanda (mstari wa kwanza) akifuatilia mada kuhusu changamoto zinazoikabili Tanzania katika kuhama kutoka mfumo wa Analojia kwenda Digitali kufikia mwaka 2012 katika Kikao kazi cha Maafisa habari na Mawasiliano wa Serikali leo jijini Mwanza. Wengine wanaoonekana nyuma ni maafisa habari na Mawasiliano wa Serikali.
Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo leo jijini Mwanza. Waziri wa Habari, Vijana na Utamaduni Dkt. Fenella Mukangara (mstari wa kwanza katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Wizara hiyo na maafisa habari na Mawasiliano wa Serikali mara baada ya kufungua kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano leo jijini Mwanza. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.