Sunday, October 31, 2010

ELVAS MUSIBA AFARIKI DUNIA!


Hayati Elvis Musiba.

Aliyekuwa Rais wa Chama Cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda nchini Tanzania (TCCIA), Elvis Musiba, amefariki dunia leo jijini Dar es salaam. kwa mujibu wa taarifa fupi iliyotolewa na ITV jioni hii, taarifa kamili na mipango ya mazishi itatolewa baadae na msiba uko nyumbani kwa marehemu, Mikocheni. Kwa wapenzi wa hadithi za vitabu, watamkumbuka marehemu kwa zile novo zake maarufu za Kikosi Cha Kisasi cha Willy Gamba na Njama zilizotamba nchini Tanzania katika miaka ya 80. Mungu alilaze roho ya marehemu peponi - Amin!

Wednesday, October 27, 2010

Madaktari wakiteta uwanja wa ndege Dar


Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia) akizungumza na Mgombea urais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, walipokutana uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere wa Jijini Dar es Salaam leo mchana wakati Dk. Shein, akiondoka kuelekea Visiwani Zanzibar na Dk. Bilal, akiwasili jijini kutoka Visiwani humo kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni leo Okt 27.

Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia) akisalaimiana na Mgombea urais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, walipokutana uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere wa Jijini Dar es Salaam leo mchana wakati Dk. Shein, akiondoka kuelekea Visiwani Zanzibar na Dk. Bilal, akiwasili jijini kutoka Visiwani humo kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni leo Okt 27. Kuliani ni mke wa Dk. Bilal, Bi Zakia Bilal.


Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia) akizungumza na Mgombea urais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, walipokutana uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere wa Jijini Dar es Salaam leo mchana wakati Dk. Shein, akiondoka kuelekea Visiwani Zanzibar na Dk. Bilal, akiwasili jijini kutoka Visiwani humo kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni leo Okt 27. Kushoto ni mke wa Dk. Shein, Tunu Shein, akizungumza na mke wa Dk. Bilal, Zakia Bilal.


Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia) akisalaimiana na Mgombea urais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, walipokutana uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere wa Jijini Dar es Salaam leo mchana wakati Dk. Shein, akiondoka kuelekea Visiwani Zanzibar na Dk. Bilal, akiwasili jijini kutoka Visiwani humo kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni leo Okt 27. Picha zote na Muhidin Sufiani.

Tuesday, October 26, 2010

Shinda mkoko Vodacom bado siku 15 tu


Magari aina ya Hyundai I10 yanayotolewa na kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania katika shindano lake la kila siku la Shinda Mkoko yakiwa katika msururu wakati yalipokuwa yakipelekwa katika maegesho yaliyopo kwenye kampuni ya kuuza magari ya FK Motors iliyopo barabara ya Nyerere.

Monday, October 25, 2010

Kampeni mgombea urais wa TLP


Katibu Mkuu wa TLP Rajabu Tao (kulia) akimnadi mgombea Urais wa chama hicho Mutamwega Mgahywa, kwa wananchi waliohudhuria mkutano wa mgombea huyo eneo la Manzese viwanja vya Bakhressa jijini Dar es Salaam juzi, ambapo walitangaza kumalizia kampeni zao Mkoani Mwanza.

Mgombea urais kwa tiketi ya TLP Mutamwega Mgahywa, akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria mkutano wa mgombea huyo eneo la Manzese viwanja vya Bakhressa jijini Dar es Salaam juzi, ambapo wanatarajia kufungia kampeni zao Mkoani Mwanza. Picha zote na Said Powa

Ujumbe wa Tanzania waondoka kwenda Miss World


Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania,Ankal Hashim Lundenga akiwa katika mazungumzo na wazazi wa Genevieve Emmanuel mrembo anaeiwakilisha Tanzania katika masindano ya Dunia,katika uwanja wa ndege wa J.K. Nyerere leo.

Ujumbe wa watu 5 ukiongozwa na Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania bw. Hashim Lundenga umeondoka nchini leo kuelekea Sanya China katika kuhudhuria mashindano ya urembo ya dunia yaliyopangwa kufanyika Jumamosi Tarehe 30 Oktoba 2010.

Katika ujumbe huo yupo pia Katibu Mkuu wa Kamati bw. Bosco Majaliwa, Miss Tanzania Mshindi wa 2 Glory Mwanga, na Miss Temeke mshindi wa 2 Anna Daudi ambaye pia alifanikiwa kuingia katika 10 bora ya Fainali za Miss Tanzania 2010.

Mama Mzazi wa Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel, Mrs. Mary E. Mpangala pia yumo katika msafara huo ili kushuhudia Fainali hizo za kumtafuta Mrembo wa dunia ambazo zitafanyika Jumamosi hii katika kisiwa cha Hainan huko Sanya China.

Msafara huo unatarajia kurejea nchini Tarehe 3 Novemba 2010.

Z connect promotion


Un identified Motorcyclist showing a different style of driving motorcycles in Arusha during the Z connect promotion offered by mobile phone company, Zantel. Photo/Courtesy.

Jeshi la Kenya wamshukuru Mungu


Kikosi cha Misitu pamoja na familia zao wakiingia katika kanisa la Romani Catholic upande wa the holy family Minor Basilica kwaajili ya kuanza ibada ya shukrani kwa Mungu iliyofanywa jana na askari Polisi na familia zao nchini Kenya.

Rais Mwai kibaki akikata keki baada ya kumalizika kwa ibada ya shukrani kwa Mwenyezi Mungu iliyofanywa jana na askari Polisi wa Kenya pamoja na familia zao katika kanisa la Roman Catholic upande wa the holy family Minor Basilica huku Askofu wa kanisa hilo pamoja na makamanda wa Jeshi hilo wakishuhudia. Picha zote na Anna Nkinda - Nairobi.

Dk Slaa akibonyeza kizenji





Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema Dk Willibroad Slaa, akaihutubia mkutano wa Kampeni, uliofanyika katika viwanja vya Garagaza,vilivypo Mtoni, Unjuja, Zanzibar jana. Picha na Emmanuel Herman

Sunday, October 24, 2010

Mashabiki saba wafariki uwanjani Nairobi



Mashabiki saba wamekufa katika uwanja wa soka wa Nyayo, mjini Nairobi, kufuatia mkanyagano katika uwanja wa Nyayo.

Habari za awali zilikinukuu kituo cha matangazo cha Jambo FM.

Hayo yalitokea katika mechi ya ligi kuu ya Kenya, kati ya timu za Gor Mahia na AFC Leopards.
Kulingana na kituo hicho ambacho kwa kawaida hutangaza moja kwa moja mechi za soka, watu hao saba walikufa baada ya mashabiki kujaribu kuingia uwanjani kwa kutumia mabavu, ili kutizama mechi hiyo ya vilabu hivyo vikongwe, ambavyo ni kati ya vilabu maarufu zaidi vya soka nchini Kenya.

Kituo cha matangazo cha Jambo FM kilielezea kwamba licha ya vifo hivyo vya mashabiki hao saba kutokea, mwamuzi hakusitisha mechi hiyo. Mechi hiyo pia ilichezwa katika mazingira ya mvua kubwa.

Habari kwa hisani ya www.bbcswahili.com

Saturday, October 23, 2010

Rais Kikwete aitikisa Gairo



Mgombea urais kwa tiketi ya CCM Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia
maelfu ya wananchi katika mkutano mkubwa wa Kampeni uliofanyika mjini
Gairo mkoani Morogoro leo mchana(picha na Freddy Maro)

Breaking Newzzz Dk Slaa: Huwezi kumtaja rais kwenye ufisadi ukawa salama


Nimemsikiliza live Dk Slaa katika mdahalo wake uliomalizika muda mfupi uliyopita, miongoni mwa aliyoyasema ni haya, "Huwezi mtaja raisi kuwa ni fisadi lakini bado unaishi!!!! sibaatishi!!! kunywa chai na Obama halafu hamna hela.



Nyingine amesema kama urais ni kumwaga damu hautaki, na kwamba akasema “mtu akikupiga kofi mgeuzie, wametuchafua mnooo... ukiona refarii anasema mpira ukiisha matokeo ni draww ogopa


‎" Siyo TRA peke yake uchafu uko kila kona nikiingia madarakani sitakuwa na msamaha na mtu, nimewaambia huko katika kampeni, warudishe fedha walizoiba...nimepita pale muheza nikaambiwa kuna nyumba ya dk wa wilaya imejengwa kwa milioni 70, ukiangalia ni aibu wananchi wakaja kwenye gari yangu wakaninong'oneza wakasema hiyo nyumba tumejenga sisi kwa michango yetu , imekamatwa mifugo yetu.. fedha kumbe zimeliwa huu ni mfano wa wizi uliopo kila kona,"Dk Slaa anasisitiza


‎"Tuna taarifa mabango yaliyobandikwa kote nchini na hata katika nyumba mbovu za nyasi huko vijijini nimepita nimeshuhudia nyumba zinataka kuanguka lakini zina mabango ya bure, mabango haya yametengenezwa Canada kwa gharama ya dola zaidi ya milioni moja, na yalipofika hapa nchini hayakulipiwa kodi, halafu CCM wanasema hawawezi kusomesha watoto bure huuu ni ufisadi!!!,"Dk Slaaa ananena!




Tuesday, October 19, 2010

Mwenyekiti wa wazee ajisalimisha



Mwenyekiti wa wazee waliokua wafanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Nathaniel Mlaki akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam baada ya kujisalimisha katika ofisi ya kamanda wa Kanda maalum, Suleiman Kova (kulia). Ndugu Mlaki alitakiwa kujisalimisha baada ya kutoa taarifa za uongo kwenye vyombo vya habari za kufa kwa mzee mwenzao, Anderson Msuta wakati wazee hao walipofunga barabara ya kivukoni na kuondolewa na polisi. Mzee Msuta alijitokeza juzi na kukanusha uvumi wa kufa kwake.( Picha Na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi).

Monday, October 18, 2010

School of Law kutanuliwa



Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Oliver Mhaiki (kulia) wakitiliana saini mkataba wa ujenzi wa majengo ya kudumu ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) na Meneja Mkuu wa Kampuni ya ujenzi ya BCEG ya China Bw. Jia Jianhui mara baada ya kutiliana saini makataba huo jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Oktoba 18, 2010). Katikati ni Afisa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Benas Mayogu.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Oliver Mhaiki (katikati) akibadilishana mkataba wa ujenzi wa majengo ya kudumu ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) na Meneja Mkuu wa Kampuni ya ujenzi ya BCEG ya China Bw. Jia Jianhui mara baada ya kutiliana saini makataba huo jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Oktoba 18, 2010). Kulia ni Kaimu Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Gerald Ndika.
Picha zote na Mohammed Mhina.

Wizara ya Katiba na Sheria leo imetiliana saini na kampuni ya Beijing Construction Engineering Group Company Ltd kutoka China kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya kudumu ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST).

Ujenzi huo wenye thamani ya aidi ya shilingi bilioni 16 unafanyika jijini Dar es Salaam kupitia Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria (LSRP) kwa thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 16.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Oliver Mhaiki alisema ujenzi huo unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 15.

Katibu Mkuu huyo aliitaka kampuni hiyo kuhakikisha kuwa ujenzi huo unakamilika kwa wakati na kiwango kama ilivyokusudiwa ili kuondokana na changamoto zinazoikumba Taasisi hiyo kutokana na kutokuwa na majengo ya kudumu.

Kwa sasa Taasisi hiyo inaendesha mafunzo yake kwa kutumia majengo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati ikisubiri ujenzi wa majengo yake ukamilike.

Akiongea katika hafla hiyo fupi, Kaimu Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Gerald Ndika alisema ujenzi huo unatarajiwa kujumuisha majengo ya kisasa vikiwemo vyumba vya madarasa, maktaba, nyumba za watumishi, hosteli na vyumba vya mahakama vya mazoezi.

“Hii itaifanya taasisi kutoa mafunzo ya vitendo kwa wahitimu wa shahada ya kwanza ya sheria sheria kwa ufanisi zaidi na hivyo kutimiza ile azma ya kutoa mafunzo sahihi ya vitendo,” alisema Dkt. Ndika.

“Baada ya kukamilika, wanafunzi wetu wataruhusiwa kutoa huduma za kisheria Mahakamani kwa wateja chini ya usimamizi wa wanasheria wazoefu,” alisema za Dkt. Ndika na kuongeza kuwa udahili wa wanafunzi unatarajiwa kuongezeka kutoka wastani wa 300 wa sasa hadi 1,000 kwa mwaka, alisema.

Mshindi wa Big Brother All Stars

It’s day 91 on M-Net’s Big Brother All Stars --- and Nigeria’s Uti was chosen by Africa as the winner of M-Net’s Big Brother All Stars during Sunday night’s spectacular live Finale Show. Pictured here: Uti
Munya akishika kichwa kama vile anasema "mama yangu" hii ni mara ya pili anaikosa kosa tuzo ya kwanza


Uti toka Nigeria akifurahia ushindi wake waBig Brother Africa All Stars usiku huu huko Sauzi
Munya toka Zimbabwe akikubali matokeo ya kuwa wa pili kwa saluti kali
Mwakilishi wa Tanzania Mwisho Mwampamba akihojiwa na mshereheshaji Ike baada ya kushika nafasi ya nne
Mwisho akitoka katika mjengo wa Big Brother baada ya kuibuka wa nne

Friday, October 15, 2010

JK ahitimisha kilele mbio za mwenge


kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka huu 2010 Dr.Nassoro Ally Matuzya akimkabidhi mwenge wa Uhuru Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa sherehe za kilele cha mbio hizo kilichofanyika katika uwanja wa michezo wa Lake Tanganyika mjini Kigoma leo mchana.

Wednesday, October 13, 2010

CCM, Chadema wakatana kwa mapanga




WATU watatu wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Mara, wawili
wanachama wa Chadema na mmoja wa CCM akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kushambuliana katika Mtaa wa Kigera mjini Musoma.

Tukio hilo la kusikitisha linadaiwa kusababishwa na ukosefu wa uvumilivu wa kisiasa, lilitokea Oktoba 11, mwaka huu, kati ya saa 1:00 na saa 2:00 usiku katika mtaa huo.

Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Mara Benedictor Mwijarubi aliwataja majeruhi hao kuwa ni Mapambano Malima (30) ambaye amekatwa upande wa kushoto wa uso , Sele Mwita (27) amekatwa mkono na mguu, wakazi wa Kigera na wafuasi wa Chadema.

Alimtaja majeruhi aliyechini ya ulinzi wa polisi kuwa ni Kapuru Charles (44) mwanachama wa CCM ambaye anadaiwa kukodiwa kufanya tukio hilo.


Muuguzi huyo, aliliambia Mwananchi kuwa majeruhi hao walikuwa wakitoka Kwangwa kuelekea mjini na kukutana na kundi lililokuwa na silaha za jadi na kuanza kurushiana maneno kabla ya kuwashambulia na kuwajeruhi vibaya watu hao.Kamanda wa polisi Mkoa wa Mara Robert Boaz hakutaka kuzungumza lolote kuhusu tukio hilo.


“Nina jambo muhimu sana nalishughulikia ndiyo maana sijapokea simu yako, hilo suala naomba unitafute kesho nitakuwa na nafasi ya kulizungumzia, maana nimebanwa sana,”alisema na kukata simu.

Mgombea ubunge wa Jimbo la Musoma kwa tiketi ya CCM, Vedastus Mathayo alipotafutwa kwa njia ya simu yake ya mkononi, licha ya kupokea hakuweza kuzungumza lolote.

Naye Katibu Mwenezi wa CCM, Mkoa wa Mara Maximillian Ngesi alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo alisema; “niko kwenye kikao nitakupa majibu,”alisema na kukata simu.

Habari kutoka kwa vyanzo mbalimbali zinadai wanachama wa Chadema walikuwa wakitoka kwenye mkutano na wanaCCM wakawavizia kwa ajili ya kuwapiga.

Mgombea wa Chadema jimbo hilo Visenti Josephat Nyerere alipotafutwa katika simu ya mkononi hakuweza kupokea licha ya kuita.

Mwananchi lilielezwa kuwa wagombea wote waliitwa na kamati ya ulinzi na usalama ili kuzungumzia suala hilo ambalo inalenga kuvunja amani nchini.

Hivi karibuni Chadema waliwatuhumu CCM kwa kuandaa vijana kwa ajili ya kufanya vurugu na walisema walikuwa wakifanya mazoezi mazito katika Shule ya Mshikamano na ofisi ya chama hicho.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mara Ndegaso Ndekubali akijibu tuhuma hizo
alisema wao wanawafundisha vijana wao ukakamavu.

“Tunawafundisha ukakamavu ili kulinda mikutano yetu, lakini ili tukichokozwa tutajibu, maana Chadema ndiyo wamejiandaa kwa fujo,”alisema.

Kutokana na tuhuma hizo Kamanda wa polisi Mkoa wa Mara, Boaz alisema hakuna chama kinachoruhusiwa kuandaa vijana kwa ajili ya kulinda mikutano na kwamba polisi ndio wana wajibu wa kulinda mikutani na wala si vijana wa chama chochote. “Kazi ya ulinzi kisheria ni ya polisi na atakayeinua pembe tutaikata bila kuangalia chama ,”alisema. Imeandikwa na Anthony Mayunga-Mara. SOURCE MWANANCHI OKTOBA 12.

Tuesday, October 12, 2010

Mmea huu una jina hiloooo


Mimea hii hupatikana sana katika maeneo yenye hali ya hewa ya jangwa hususani maeneo ya mkoa wa Shinyanga na mengine yenye sifa kama mkoa huo, majani yake huwa ni mapana na ina matunda yanayofanana na mambo fulani hivi, wataalamu wanasema ni dawa ya magonjwa kadhaa jina lake la kisayansi au botanical name ni Calotropis procera kiswahili chake Mpumbula

Friday, October 08, 2010

Happybirtday Mr President

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimlisha kipande cha keki Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa sherehe ya kumpongeza Rais Kikwete kwa kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa kwake jana jioni.Sherehe hizo zilifanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlisha kipande cha keki mkewe Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe ya kuadhimisha kuzaliwa kwake miaka 60 iliyopita.Sherehe hizi zilifanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata keki wakati wa sherehe ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuzaliwa kwake pembeni yake ni Mama salma Kikwete na mjukuu wao Karima wakishuhudia.(picha na Freddy Maro)

Redet: Kikwete aongoza kura za maoni


MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete amewaacha mbali wapinzani wake kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kupata asilimia 71.2 ya kura za maoni katika utafiti uliofanywa na Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia (Redet).

Matokeo hayo yamekuja katika kipindi ambacho kuna mzozo mkubwa baina ya taasisi nyingine inayofanya utafiti wa masuala ya kijamii, kisiasa na kiuchumi ya Synovate na Chadema ambayo inadai kuwa mgombea wake wa urais, Dk Willibrod Slaa aliongoza kwenye kura ya maoni iliyofanywa na taasisi hiyo.

Synovate imekana kufanya utafiti wa aina hiyo na kwamba hadi sasa imefanya utafiti kuhusu mwenendo wa vyombo vya habari katika kuripoti habari za uchaguzi mkuu, lakini Chadema imesema inao ushahidi kuwa taasisi hiyo iliendesha utafiti ulioonyesha kuwa Dk Slaa alipata asilimia 45 dhidi ya 40 za Kikwete.

Jana, Redet ilitangaza matokeo ya utafiti wake ambayo yanaonyesha kuwa Kikwete bado anaongoza, licha ya umaarufu wake kushuka kwa asilimia chache.

"Tukianzia uchaguzi wa rais wa Serikali ya Muungano, asilimia 71.2 ya wahojiwa wote walisema watamchagua mgombea urais wa CCM. Ilifuatiwa na Chadema ambayo asilima 12.3 walisema watamchagua mgombea wa Chadema na asilimia 10.1walisema watamchagua mgombea wa Cuf," alisema Dk Benson Bana ambaye ni mwenyekiti mwenza wa mpango huo.
Hata hivyo Kikwete anaonekana kupata kura nyingi zaidi kuliko asilimia za kura za wabunge ambazo ni 66.7 zikipungua kwa asilimia 4.5 kwa kulinganishwa na za kura za urais, huku madiwani wakipata asilimia 66.

Kwa mujibu wa Redet, matokeo yangekuwa hivyo iwapo uchaguzi mkuu ungefanyika kati ya Septemba 20 hadi 28 mwaka huu.

Akitoa matokeo ya utafiti huo wa 17 uliofanyika katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na Visiwani katika kipindi hicho cha Septemba, Dk Bana alisema jana kuwa waliohojiwa walitakiwa kutoa maoni kuhusu uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani.

Alisema katika utafiti huo wahojiwa waliulizwa: "Mwezi Oktoba mwaka huu utafanyika uchaguzi mkuu.
Kama uchaguzi huo ungefanyika leo, je wewe ungemchagua mgombea wa chama gani?"
Alifafanua kuwa kutokana na swali hilo vyama vitatu vya CCM, CUF, Chadema vilipata alama nyingi kwa wagombea wake wa urais, wabunge na madiwani.

Hata hivyo, Dk Bana alisema kiwango cha asilimia za kura kimepungua kwa mgombea wa CCM kulinganisha na utafiti uliofanywa na Redet mwezi Machi wakati matokeo yalipoonyesha kuwa asilimia 77.2 wangemchagua mgombea urais wa CCM na tofauti na asilimia 71.2 alizopata safari hii.

"Itakumbukwa kwamba matokeo ya utafiti wa Redet wa hapo Machi mwaka 2010 yalionyesha wengi wangemchagua mgombea urais wa CCM asilimia 77.2. Katika utafiti CCM bado inaongoza, hata hivyo kiwango cha asilimia kimepungua," alisema Dk Bana.

Dk Bana alisema utafiti huo wa Redet ulifanywa kwa kuwahoji watu 2,600 katika wilaya 52 na kwamba watu 1,849 ndio waliosema watamchagua mgombea wa CCM, 263 wa CUF na 319 mgombea wa Chadema.
Ikilinganisha na utafiti wake wa mwezi Machi mwaka huu, Redet ilisema kuwa katika kipindi cha miezi sita kilichopita, idadi ya watu ambao wangemchagua mgombea wa Chadema imeongezeka kwa asilimia nane (8) kutoka 4.2 za mwezi Machi hadi 12.3.

Redet ilitaja pia kuongezeka kwa asilimia 0.9 kwa kura za urais wa CUF, asilimia 02 kwa TLP na 0.1 kwa NCCR-Mageuzi huku ikitaja sababu kuwa ni kampeni za uchaguzi zinazoendelea.

Lakini, taasisi hiyo ilisema mgombea urais wa CCM anaongoza kwa kutajwa jina lake kama mtu ambaye wangependa awe rais wa Tanzania na asilimia 68.5 ya wahojiwa wote akifuatiwa na Dk Slaa wa Chadema aliye na asilimia 11.9 huku Profesa Lipumba wa CUF akiwa wa tatu kwa asilimia 9.3 ya wahojiwa.


Dk Slaa
Taasisi hiyo ya utafiti wa kitaalam ilisema kuwa katika kura za urais, CCM itapata kura kidogo zaidi katika Jimbo la Kigoma Vijijini ambako atapata asilimia 28 huku Jimbo la Nkasi akipata asilimia zote 100.

Kwa mujibu wa utafiti huo kwa upande wa wabunge wa Jamhuri ya Muungano, pia asilimia ya watakaochagua mgombea wa CCM imepungua kwa asilimia 1.3, huku ikiongezeka kwa vyama vya upinzani, vikiongozwa na Chadema ambayo imeongezeka kwa asilimia 2.9, CUF 1.5, TLP na NCCR-Mageuzi asilimia 0.8 kila kimoja.

Kwa mujibu ya Dk Bana asilimia 66.7 ya waliohojiwa walisema watamchagua mgombea wa CCM huku asilimia 11.7 wakitaja mgombea wa CUF na asilimia 11.5 wa Chadema huku vyama vingine vikitajwa na idadi ndogo ya wahojiwa katika nafasi hiyo na ile ya urais.

Utafiti huo unaonyesha kuwa TLP katika urais itapata asilimia 0.4 na ubunge asilimia moja wakati NCCR-Mageuzi ikipata 0.3 urais na 1.1 ubunge na UDP iliambulia sifuri.

Kwa mujibu wa Redet matokeo ya utafiti huo kwa nafasi za udiwani katika vyama hivyo yanakaribia kufanana na nafasi za ubunge na uraisi. habari imeandikwa na Exuper Kachenje na Zulfa Msuya: Source :MWANANCHI.

Wednesday, October 06, 2010

RAIS JAKAYA AMTEUA PROFESA WANGWE KUWA MWENYEKITI WA BODI



Benjamin Sawe

Maelezo

Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Samwel Wangwe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Elimu Kibaha.
Taarifa iliyotumwa Kwa vyombo vya habari kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu na Serikali za Mitaa Bibi Maimuna Tarishi imesema Profesa Wangwe ameteuliwa kutokana na Sheria aliyopewa Rais Kikwete katika Sheria ya Mashirika ya umma namba 17 ya mwaka 1969.
Sambamba na uteuzi wa Profesa Wangwe,Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda pia amewateua Wakurugenzi wa Bodi ya Shirika la Elimu Kibaha.
Kutokana na Mamlaka aliyopewa Waziri Mkuu katika Sheria ya Umma namba 17 ya mwaka 1969 wakurugenzi wa bodi walioteuliwa ni pamoja na Bibi Fatma Kiongosya ambaye ni Mwakilishi wa Wizara ya Afya na Uchumi,Dr Magreth Mhando,Mwakilishi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Wengine ni Bibi Salock Musese kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Bwana Apenda William Mrinji,kutoka Wizara ya Kilimo,Chakula na Ushirika na Bibi Halima Kihemba ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha.
Uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi pamoja na Wakurugenzi hao umeanza rasmi tarehe 1/9/2010 na itamaliza muda wake tarehe 31/08/2013

Tuesday, October 05, 2010

Siku wa waalimu duniani


Mwanafunzi wa shule ya msingi Samora mjini Songea mkoani Ruvuma akimkaribisha Rais Dk Jakaya Kikwete kwa saluti maalumu muda mfupi kabla ya Rais Kikwete kufungua rasmi jingo la Chama Cha waalimu mkoa wa Ruvuma leo asubuhi(picha na Freddy Maro)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia baadhi ya watoto waliomlaki muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa songea ambapo alikuwa mgeni rasmi katika maadhimnisho ya sherehe ya siku ya mwalimu duniani.(Picha na Freddy Maro)

Serengeti yazindua kampeni ya saidia taifa stars ishinde leo jijini dar



Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Muhammed Seif Khatib akibandika stika kwenye ramani ya Tanzania kuashiria kuwa kampeni kubwa ya kuhamasisha watanzania waweze kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu ya taifa katika mchezo wake muhimu dhidi ya timu ya timu ya Taifa ya Morocco hapo jumamosi,Oktoba 9 2010 imezinduliwa rasmi.kati ni Meneja Mkuu wa Uhusiano, mawasiliano na Jamii kutoka kampuni ya bia ya Serengeti Dada Teddy na Rais wa TFF, Leodga Tenga wakishuhudia tukio hilo mchana huu.

Sunday, October 03, 2010

Balozi Maajar akabidhi hati ya utambulisho kwa Obama


Balozi wa Tanzania nchini Marekani,Mwanaid Maajar akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Marekani, Barack Obama mara baada ya kupokea hati ya utambulisho wa Balozi wetu huyo nchini humo.

Friday, October 01, 2010

Dk Slaa afunika Songea


Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Songea na vitongoji vyake, wakati wa mkutano wake wa kampeni, kwenye Uwanja wa Majengo jana. (Picha na Joseph Senga)

Jk afunika Tabora


JK akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Igunga,Rostam Aziz katika uwanja wa SabaSaba mjini Igunga mchana huu.

Umati mkubwa ulijitokeza uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora kumsikiliza JK