Thursday, December 31, 2009

Mzee Kawawa Amefariki!



Waziri Mkuu wa Tanganyika na mpigania huru wa Tanganyika na Muasisi wa Muungano mzee Rashid Mfaume Kawawa amefariki dunia. Mzee Kawawa alikuwa ni swahiba wa karibu zaidi wa baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere.

Mzee Kawawa alizaliwa Mei 27 , 1926 huko Songea kijiji cha Matepwende mkoani Ruvuma. Alianza elimu ya msingi huko Liwale Lindi. Aliendelea na elimu ya kati (middle school) hapo Dar-es-Salaam school ambapo mmojawapo wa wanafunzi wengine ni marehemu mzee Kanyama Chiume mpigania uhuru toka Malawi aliyeishi uhamishoni nchini Tanzania kwa muda mrefu. Wengine katika shule hiyo wakati huo ni pamoja na kina Abdul Sykes, Ali Sykes, Hamza Aziz na Faraji Kilumanga.

Aliendelea na masomo yake huko Tabora Boys kati ya 1951-1956. Alikuwa ni Waziri Mkuu wa Tanganyika mwaka 1962 wakati Mwalimu Nyerere alipoamua kwenda mikoani kujenga chama na kufanya shughuli za kisiasa. Baadaye aliteuliwa tena kuwa Waziri Mkuu mwaka 1972-1977 na akawa miongoni mwa wahamasishaji wakubwa wakati wa vita ya kumng'oa nduli Idi Amin ambapo alitembelea wapiganaji wetu waliokuwa mstari wa mbele kule Uganda. Hii ilimpatia jina la "Simba wa Vita" jina ambalo lilimkaa vyema kwa muda mrefu.

Kabla ya kuingia katika harakati za kupigania Uhuru Mzee Kawawa alikuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa Shirikisho la Wafanyakazi mwaka 1955 ambapo alichaguliwa kuwa Katibu wake Mkuu wa kwanza. Ni katika nafasi hii ndiyo aliweza kuanza kushiriki kwa nguvu zaidi katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika akihamasisha wafanyakazi. Kabla ya hapo alikuwa ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi wa Serikali.

Februari 1956 Mzee Kawawa aliacha kazi yake ya Shirikisho la Wafanyakazi kutokana na kuwa mwajiriwa wa serikali kitu ambacho kilimkataza kuhusisha na siasa na kuamua kuingia katika harakati za kudai uhuru kupitia TANU. Alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya TANU mwaka 1957, Makamu mwenyekiti wa TANU mwaka 1960.

Mwaka 1964 baada ya Muungano Mzee Kawawa alikuwa ni Makamu wa Pili wa Rais akiwa ni msaidizi wa Rais wa Muungano kwa upande wa mambo ya Bara.

Katika siasa amewahi kushika nafasi mbalimbali ikiwemo ile ya Ukatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi na Makamu Mwenyekiti wa CCM na amekuwa mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya CCM.

Mzee Kawawa alikuwa ni mtoto wa kwanza kati ya watoto nane na mojawapo ya kazi zake za awali ilikuwa ni uchezaji wa filamu za uhamasishaji na akawa ndiye mcheza filamu wa kwanza kiongozi mweusi (lead actor).

Mzee Kawawa alikimbizwa hospitali hapo jana kutokana na hali yake kuwa mbaya na kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi; ambapo mapema leo asubuhi alifariki dunia. Mipango ya mazishi inaandaliwa.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Pema Peponi, Amina.

Imeandikwa na: Mwanakijiji

Wednesday, December 30, 2009

Mzee Kawawa alazwa Hospitali ya Muhimbili



Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali Mzee Rashid Mfaume Kawawa aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili leo jioni(picha na Freddy Maro)

MAKAZI YA GAVANA WA BENKI KUU TAARIFA KUHUSU UJENZI WA MAKAZI YA VIONGOZI WAKUU WA BENKI KUU YA TANZANIA


GAVANA WA Benki Kuu na manaibu wake kwa mujibu wa mikataba ya kazi zao, wanastahili kupewa nyumba ya kuishi kila mmoja. Hapo awali Gavana alikuwa anaishi Barabara ya Mahando kiwanja namba 387Masaki na Naibu Gavana Barabara ya Msese kiwanja Namba 43.

Awali Benki Kuu ilikuwa na viongozi wakuu wawili, Gavana na Naibu wake mmoja. Baada ya mabadiliko ya Sheria ya mwaka 2006, Benki Kuu ina viongozi wakuu wanne; Gavana na Manaibu wake watatu. Kila mmoja wao, kwa mikataba iliyowekwa anastahili kupata nyumba ya kuishi.

Mwaka 2006, kabla ya uteuzi wa viongozi wa sasa wa juu, Benki Kuu ilifanya uamuzi wa kujenga nyumba mbili zaidi kwa makazi ya viongozi walioongezeka. Iliamuliwa nyumba hizi zijengwe kiwanja namba 57 Barabara ya Mtwara Crescent na kiwanja namba 12 Barabara ya Tumbawe maeneo ya Oysterbay.Viwanja vyote viwili vilikuwa ni mali ya Benki Kuu vilivyokuwa na magofu yaliyopigwa marufuku kuishi wanadamu (condemned).

Timu ya wataalamu waelekezi ikiongozwa na M/S SKY Architects Consultants iliajiriwa kutengeneza michoro na ramani za nyumba hizo. Michoro miwili ilichaguliwa, moja kwa kila nyumba ili wataalamu hao watengeneze ramani kamili ya ujenzi. Nyumba zote mbili zilipangwa ziwe za ghorofa moja, vyumba vitano vya kulala, wenyeji na wageni, sebule ya wageni, sebule ya familia, mahali pa kulia na vyoo na mabafu yanayoendana na idadi ya vyumba. Majengo ya nje ni pamoja na nyumba ya kuishi watumishi, gereji ya magari, bwawa dogo la kuogelea, ukuta na vyombo vya usalama na kibanda cha walinzi.

Huduma zilizogharimiwa katika ujenzi wa nyumba hizi ni pamoja na mashine ya umeme (generator), mashine ya kupoza hewa na matenki ya kuhifadhi maji. Wakati huohuo, shughuli zingine zilizofanyika ilikuwa ni kutengeneza mahali pa kuegesha magari pamoja na bustani.

Wataalamu hawa baada ya uchoraji huu walifanya tathmini ya vifaa vinavyohitajika na maelekezo kwa wazabuni ili itumike kualika zabuni. Taratibu zote za manunuzi zilifuata sheria ya manunuzi katika kuwaalika wazabuni na kuteua wakandarasi. Kila nyumba ilikuwa ni mradi unaojitegemea na kila moja ilifanyiwa zabuni peke yake.

Izingatiwe kuwa ujenzi wa nyumba hizi ulipangwa na kuamuliwa kabla ya uteuzi wa Profesa Benno Ndulu kujiunga na Benki Kuu Septemba 2007.

Tangazo la kuwaalika wazabuni kwenye kiwanja namba 12 Barabara ya Tumbawe lilichaapishwa katika gazeti la Daily News la Februari 26,2008.Wakandarasi wote wa daraja la pili au la juu zaidi walialikwa kuwasilisha zabuni na walitakiwa kulipa ada ya shilingi 50,000. Wakandarasi 12 walituma maombi na kuchukua hati za zabuni.Lakini kati ya hao 10, waliwasilisha maombi yao kabla ya kufikia tamati ya kupokelewa maombi hayo Machi 25,2008.

Zabuni hizi zilifunguliwa na Bodi ya Zabuni ya Benki Kuu na kufanyiwa tathimini ikishirikisha mtaalamu mwelekezi wa mradi huo na Idara ya Miliki ya Benki Kuu. Mapendekezo kutoka kwa wakandarasi yalikuwa na viwango vya gharama kuanzia Shilingi 1,399,184,549.00 hadi shilingi 1,847,763,537.00 kwa kiwango cha juu. Baada ya tathmini ya zabuni hizo na kufanya masahihisho ya tarakimu zilizowasilishwa, mzabuni aliyeshinda kwa kuwa na gharama ya chini kuliko wote alikuwa ni M/S Eletrics International Co. Limited. Gharama yake baada ya masahihisho ilikuwa ni Shilingi 1,274,295,025.26.

Taarifa ya tathimini hiyo ilipitia tena kwenye Bodi ya Wazabuni na ndipo ilipofikia uamuzi wa kumteua M/S Eletrics International Co. Limited kwa bei ambayo haitabadilika (fixed price) ya Shilingi 1,274,295,025.26 ya kukamilisha ujenzi huu katika wiki 32.Mkataba wa ujenzi na mkandarasi huyo ulitiwa sahihi Juni 03,2008 na kazi ya ujenzi ikaanza mara moja. Mkandarasi huyu aliteuliwa na Bodi Zabuni (DSM) ya Benki Kuu ikaridhia kuwa M/S Remco (International) Limited ishughulikie maswala aya vipoza hewa; M/s Ginde EAP Services Ltd ishughulikie maswala ya maji safi, mabomba na maji taka na M/s Pomy Engineering Co.Ltd ishughulikie maswala ya umeme. Makampuni yote hayo yamesajiliwa Tanzania.

Wazabuni wa nyumba Namba 57 Mtwara Crescent nao pia walialikwa kwa mfumo huohuo wa ushindani wakianza na wakandarasi watano (5) ambao waliwasilisha maombi yao na kuishia na uteuzi wa M/s Holtan Builders Ltd ambayo gharama yake ya Shilingi 1,272,348,512.00 (fixed price) ilikuwa ni ya chini kuwashinda wengine na makubaliano ya kukamilisha ujenzi katika muda wa wiki 24. Mkandarasi huyo alitumia kampuni zifuatazo kwa shughuli zingine: M/s Jandu Construction & Plumbers Ltd kwa shughuli za mabomba, maji safi, na maji taka, M/s Barkley Electrical Contractors Ltd kwa maswala ya umeme na M/s Remco (International) Ltd kwa shughuli za vipoza hewa. Mkandarasi ndiye mlipaji wa gharama za shughuli hizi zote zinalipiwa kutokana na gharama ileile iliyokubalika kwa mkandarasi mkuu.

Watendaji wote wa miradi hii wanaonyeshwa kwenye mabango ambayo bado yapo kwenye viwanja hivyo. Uteuzi wa Gavana Ndulu, Manaibu Gavana, Dkt. Enos Bukuku na Bw.Lila Mkila ulifanyika wakati mipango ya awali ya kujenga nyumba hizi

ilikuwa imeshaanza. Benki Kuu ilikodisha nyumba mbili, mojakiwanja namba 480 Barabara ya Bray, Masaki na nyingine kiwanja namba 591,Msasani Peninsular kwa matumizi ya viongozi hao wawili ambao walikuwa bado wanaishi kwenye nyumba zao mbali na ofisi.

Kati ya Oktoba 2007 aliporipoti kazini kama Naibu Gavana hadi Aprili 2008, Profesa Ndulu aliishi kwenye nyumba yake iliyoko Mbezi Beach, na Naibu Gavana Mkila naye pia aliishi nyumbani kwake kabla ya kuhamia kwenye nyumba hizi zilizokodishwa.

Benki Kuu iliamua kumhamisha Naibu Gavana Juma Reli kwenda Barabara ya Mahando Masaki ili kuruhusu matengenezo ya nyumba aliyokuwa anaishi Kinondoni Barabara ya Msese. Naibu Gavana Dkt.Bukuku anaishi kwenye nyumba yake na Benki Kuu inatoa posho ya nyumba kulingana na mkataba.

Nyumba hizo mbili zilizojengwa chini ya miradi iliyotajwa, sasa hivi zimekamilika.Gavana wa Benki Kuu, Profesa Ndulu alihamia nyumba namba 12 Barabara ya Tumbawe Desemba 17,2009 na Naibu Gavana Mkila alihamia nyumba namba 57 Mtwara Crescent Desemba 4,2009

Kama ilivyo kiutaratibu, ukaguzi wa mahesabu yanayohusu miradi hiyo utafanyika kisheria. Kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006, Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) ndiye mkaguzi wa mahesabu ya Benki Kuu; ambaye ameanza kufanya kazi hii tangu mwaka 2007. Yeye ameiteua kampuni ya Ernst & Young kama wakaguzi wa kumsaidia kutekeleza jukumu hili.

IMETOLEWA NA IDARA YA UHUSIANO NA UMMA NA ITIFAKI
BENKI KUU YA TANZANIA
SEPTEMBA 30, 2009

Magari na Makontena bandari ya Dar es Salaam




Magari yakionekana yamejazana ndani ya eneo la Bandari ya Dar es Salaam yakisubiri kutolewa. Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, TPA wamesema kuwa wameanzisha mpango wa dharura wa kuondosha msongamano wa mizigo bandarini hapo.

Tuesday, December 29, 2009

Mnigeria chupchup kulipua ndege





Maafisa nchini Yemen wamesema raia wa Nigeria anayetuhumiwa kutaka kulipua ndege ya Marekani siku ya Krismasi alikuwa akiishi nchini Yemen hadi mwanzo wa mwezi huu.

Shirika la habari la Yemen, Saba News, limekariri taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Yemen ikisema Umar Farouk Abdulmutallab, alikuwa nchini Yemen kuanzia mwezi Agosti hadi mwanzo wa Disemba.

Taarifa hiyo inasema Bw Abdulmutallab alikuwa na kibali kinachomruhusu kujifunza kiarabu katika chuo kimoja katika mji mkuu, Sanaa.

Awali, rais wa Marekani Barack Obama alisema atafanya kila awezalo kuhakikisha wote waliohusika na kupanga njama za kulipua ndege hiyo wachukuliwe hatua za kisheria.

Bw Obama ameahidi kutumia 'nguvu zote za serikali kutibua, na kutokomeza mipango ya watu wenye itikadi kali'. kwa taarifa zaidi soma

Maafa ya mafuriko





Pichani baadhi ya wakazi wilayani Kilosa mkoani Morogoro wakivuka katika eneo lililokumbwa na mafuriko yaliyoikumba wilaya hiyo kutokana na mto Mkondoa kufurika maji.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametuma salamu za pole kwa wakuu wa mikoa minne ambayo imekumbwa na maafa yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Aidha, Rais Kikwete amepongeza jitihada zinazofanywa na uongozi katika mikoa hiyo kukabiliana na maafa yanayosababishwa na mvua hizo.

Rais Kikwete ametuma salamu hizo za pole leo, Jumanne, Desemba 29, 2009, kwa wakuu wa Mikoa ya Dodoma, Morogoro, Ruvuma na Rukwa.

Katika mikoa hiyo, baadhi ya watu wamepoteza maisha kutokana na mafuriko, wengine wamejeruhiwa kutokana na radi, na kumekuwepo na upotevu wa mali, na mamia ya watu kukosa mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuezuliwa na upepo ulioambatana na mvua kubwa.

Katika salamu hizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhandisi Dkt. James Alex Msekela, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Luteni Kanali (mst) Issa Saleh Machibya, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mheshimiwa Christine G Ishengoma, na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mheshimiwa Daniel Ole Njoolay, Rais Kikwete amesema kuwa amesikitishwa na upotevu wa maisha, upotevu wa mali na hasara ya watu kuezuliwa nyumba zao.

“Nimesikitishwa na kuhuzunishwa na maafa ambayo yameambatana na mvua zinazoendelea kunyesha katika Mkoa wako. Nakupa salamu za pole wewe binafsi Mkuu wa Mkoa, na kupitia kwako, natoa mkono wa pole kwa watu wote waliopatwa na maafa kutokana na mvua hizo,” amesema Rais Kikwete katika sehemu ya salamu zake kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kanali Machibya.


Rais ametuma salamu zenye ujumbe kama huo kwa Mhandisi Dkt. Msekela, Mheshimiwa Ishengoma na Mheshimiwa Njoolay.

Katika Wilaya ya Kongwa ya Mkoa wa Dodoma watu 220 hawana mahali pa kuishi wakati idadi ya wasiokuwa na mahali pa kuishi katika Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro imefikia 2, 152 kufuatia nyumba zao kuezuliwa ama kuharibiwa na upepo ama mafuriko. Katika wilaya hiyo hiyo ya Kilosa, nyumba 922 zimefurika maji.

Katika Mkoa wa Rukwa, watu 27 wamelazwa katika Kituo cha Afya cha Kakese baada ya kuwa wamepigwa na radi katika tukio ambako mtu mmoja amepoteza maisha.

Katika salamu zake, Rais Kikwete amewaelekeza wakuu hao wa mikoa kuendelea kuchukua hatua za dharura kukabiliana na maafa yanayotokana na mvua hizo na kuahidi kuwa Serikali yake iko pamoja na wananchi waliopatwa na maafa katika mikoa hiyo.


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

29 Desemba, 2009

Dar es Salaam Bongo



Hebu ndugu msomaji nieleze hii ni sehemu gani ya jiji hili la dar es Salaam , mambo yanabadilika kila kukicha majengo yanaota kama uyoga, ingawa watu wanalalamika kuwa hawana hela, lakini hela ipo nyingi na inamilikiwa na watu wachache mno.

Monday, December 28, 2009

uzinduzi bodi ya Ngorongoro


Waziri wa Maliasili na Utalii , Shamsa Mwanguga akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa bodi ya Wakurugenzi wa Hifadhi ya Ngorongoro kulia ni Mwenyekiti wa bodi hiyo Pius Msekwa . PHOTO/SILVAN KIWALE

Mambo ya Twanga


Wanenguaji wa bendi ya Twanga Pepeta International ‘Wazee Wa Kisigino’ wakitoa burudani kwa mashabiki wao wakati wa sikukuu ya Krismasi kwenye ukumbi wa Landmark hotel jijini Dar es Salaam.Picha na Silvan Kiwale

Sunday, December 27, 2009

Yanga bingwa Tusker






Yanyakuwa Mil 40

TIMU ya Yanga imefunga mwaka kwa 2009 kwa kishindo baada ya kutwaa ubingwa wa michuano ya Kombe la Tusker kwa kuichapa Sofapaka kwa mabao 2-1 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Yanga walilazika kusubili hadi dakika tano za mwisho kuanza kusherekea ubingwa wao kwa mabao yaliyofungwa na Mrisho Ngassa (90 dk), na Boniface Ambani (85dk).

Mabingwa hao wa Tanzania wamefanikiwa kujinyakulia shilingi milioni 40, huku ndugu zao Simba wakijinyakulia nafasi ya tatu Mil 10 na Wakenya hao Sofapaka washindi wa pili walijinyakulia Mil 20.

Mshambuliaji Jerryson Tegete alikabidhiwa zawadi yake ya ufungaji bora Mil 2 baada ya kufunga jumla ya mabao 6 kwenye michuano hiyo, huku Mafunzo ya Zanzibar imepata tuzo ya timu yenye nidhamu.

Katika mchezo huo mabingwa wa Kenya, Sofapaka walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 34 kupitia kwa Wanyama Thomas kwa mpira wa adhabu ukiwa nje kidogo ya 18 baada ya Mohamed Bakari kumwangusha Humphrey Ochieng uliokwenda moja kwa moja wavuni na kumwacha kipa Obren asijue la kufanya.

Katika kipindi cha pili wachezaji wa Sofapaka wakionekana kuanza kuchoka na kutoa nafasi kwa Yanga waliokuwa wakicheza soka safi ya kuona na kupanga mashambulizi wanavyota.

Dakika 82, Ngasa alitumia kasi yake na kuwazidi mbio mabeki kwenye eneo la hatari na kupiga shuti lilomgonga Ambani na kuokolewa na mabeki.

Mkongwe huyo Ambani alijirekebisha na kuifungia Yanga bao la kusawazisha zikiwa zimebaki dakika 85 kwa kumalizia mpira uliomgonga kipa na kurudi uwanjani. Imeandikwa na Sosthenes Nyoni wa Mwananchi.

Buriani mke wa Herman


Mwandishi wa Habari na Mpiga Picha wa gazeti la Citizen, Emmanuel Herman akiwa amesimama mbele ya kaburi la mke wake mpendwa Mary Hyera muda mfupi baada ya mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam jana, pamoja naye ni ndugu na marafiki zake akiwamo Father Kidevu( Mrocky Mrocky) wa pili kushoto, wa kwanza kushoto ni mtoto wa Marehemu, anayyeitwa Elizabeth Emmanuel. Picha ya Zacharia Osanga.

Spika Sitta ataka wanamuziki wa injili wasaidiwe


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samwel Sitta akizindua albamu ya kundi la Kijitonyama upendo Group (KUG) katika tamasha lililofanyika siku ya Krismas kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Picha na Elias Msuya.

Friday, December 25, 2009

Papa aangushwa chini na mwanamke



Sherehe za Krismasi mwaka huu kwenye makao makuu ya kanisa Katoliki huko Vatican zilitiwa dosari wakati Baba Mtakatifu alisukumwa chini na mwanamke.

Taarifa zasema mwanamke huyo ambaye jina lake halijulikani na ana matatizo ya akili amekamatwa na polisi.

Papa Benedict XVI alikuwa akijiandaa kuongoza misa maalum ya kusherehekea Krismasi wakati mwanamke huyo alivuka mpaka wa ulinzi.

Baba Mtakatifu hakuonyesha ishara zozote za kujeruhiwa kwa kuwa alinyanyuka huku akisaidiwa na msimamizi wa sherehe hizo.

Misa ya Krismasi mwaka huu iliandaliwa saa mbili kabla ya muda wa kawaida ili kumwezesha Papa kupumzika.

Taarifa zasema Askofu Mkuu Roger Etchegaray ambaye pia alisukumwa chini na mwanamke huyo alikimbizwa hospitalini kupimwa iwapo alijeruhiwa.

Yanga washerehekea Xmass kwa bao 2-1




MSHAMBULIAJI Shamte Ally aliyeingia akitokea benchi aliibuka shujaa kwa kufunga bao dakika ya 118 na kuipa Yanga ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Shamte aliyeingia dakika 95 akichukua nafasi ya Abdil Kassimu 'Babi' alipokea pasi nzuri kutoka kwa Ngasa akiwa nje ya eneo la penalti alipiga shuti lilomshinda kipa Juma Kaseja na kutinga wavuni.

Katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote ulishudia dakika tisini zinamalizika kwa timu hizo kwenda sare ya bao 1-1 na kulazisha mchezo huo kuongezwa dakika 30.

Mshambuliaji Jerry Tegete alifungia Yanga bao la kuongoza dakika ya 60 akipokea pasi ya Abdil Babi na kupitisha mpira juu ya kipa Juma Kaseja.

Hillay alifunga mabao la kusawazisha kwa Simba kwa mkwaju wa penalti baada ya beki Bakari Mohamed kumwangusha kwenye eneo la hatari mshambuliaji Emmanuel Okwi dakika ya 79.

Katika dakika ya 110, Simba ilipata pigo kubwa kwa kutolewa kwa kiungo wake Haruna Moshi Boban aliyepewa kadi nyekundu na mwamuzi Denis Batte kutoka Uganda kwa kitendo cha kutumia maneno machafu kwa mwamuzi msaidizi John Kanyenye.

Kwa matokeo hayo sasa Yanga itacheza fainali Jumapili dhidi ya Sofapaka, wakati Simba watawania mshindi wa tatu dhidi ya Tusker kesho.

Mwanzoni wa kipindi cha pili timu zote zilirudi kwa kasi ya kutafuta mabao ya mapema lakini hali ya kosa kosa iliendelea vile vile hadi pale Tegete alipofunga bao lake la sita kwenye michuano hiyo.

Yanga iliwatoa kipa Mghana Yaw Berko aliyeumia baada ya kugongana na Mgosi na kumwingiza Obren Cuckovic, pia walimtoa Kigi Makasi kuingia Godfrey Bonny. Huku Simba wakimpumzisha Mgosi na kumwingiza Mike Baraza mchezaji wa zamani wa Yanga.

Muda mfupi baada ya kuingia Baraza alipiga shuti lilopanguliwa kwa ufundi mkubwa na kipa Cuckovic dakika 77.

Kiungo Abdil Kassimu alipiga shuti akiwa katikati ya uwanja, lakini hakulenga goli dakika ya 48, naye Mgosi alikosa nafasi ya wazi baada ya kupewa krosi safi na Kanoni, lakini shuti lake likapaa juu akiwa yeye na goli.

Hadi timu hizo zinahenda mapumziko hakuna aliyebahatika kuziona nyavu za mwenzake, licha ya Yanga kutetawala zaidi katika kipindi hicho.

Mchezaji wa kimataifa wa Kenya, Jerry Santo alitolewa nje dakika 36 baada ya kugongana na Nadir na nafasi yake kuchululiwa na Ramadhani Chombo 'Redondo'.

Kinara wa ufungaji katika michuano hii alipoteza nafasi ya kufunga dakika ya 33 aliposhindwa kumalizia pasi aliyopewa na Nurdin Bakari akiwa yeye na goli.

Simba walirudi mchezoni na kufanya shambulizi la kushitukiza katika dakika 26 pale mabeki wa Yanga walipozani wametegea mtego wa kuotea, lakini Nadir Canavaro alikuwa makini kuokoa hatari hiyo. Imeandikwa na
Sosthenes Nyoni, Vicky Kimaro

Gavana: Tumejenga nyumba mpya



Ramadhan Semtawa

GAVANA wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndulu amekiri benki hiyo kutumia zaidi ya Sh1 bilioni za walipa kodi kwa ajili ya kutengeneza makazi yake.

Prof Ndulu, ambaye alikuwa akitoa ufafanuzi wa habari iliyochapishwa na Mwananchi kuwa taasisi hiyo kuu ya fedha ilikarabati nyumba hiyo kwa Sh1.4 bilioni, alihusisha taarifa hizo za ubadhirifu huo wa fedha za walipa kodi na mtandao wa wafanyakazi wake ambao alisema una lengo la kumchafua.

Lakini Ndulu alisema pamoja na kutokuwepo na usahihi kwenye taarifa kwamba nyumba anayoishi ilikarabatiwa kwa kiasi hicho cha fedha, makazi anayoishi yalijengwa upya baada ya nyumba zilizokuwepo awali kubomolewa na akadokeza kuwa gharama zinaweza kuwa kubwa zaidi.

“Nyumba haijakarabatiwa, imejengwa from the ground (kutoka chini)... ni tofauti kukarabati na kujenga nyumba mpya huu ni upotoshaji wa wazi na kujaribu kuchafua mema,” alilalamika gavana huyo.

“Napenda taarifa sahihi ambazo hazipotoshi ukweli, kwa maana taarifa kama hizo zinaharibu kila kitu kizuri na kujengwa taswira mbaya kwa wananchi, kitu ambacho si sahihi.

“Pia si kweli kuhusu hizo gharama kwani hakuna tathimini kamili ambayo imekamilika hadi sasa.”

Mwananchi iliripoti kuwa nyumba anayoishi sasa gavana huyo ilikarabatiwa kwa takriban Sh1.4 bilioni na kwamba zote zilikuwa kwenye mradi wa kukarabati nyumba za vigogo wanne wa BoT; ya Ndulu na manaibu wake watatu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, nyumba nyingine ni pamoja na aliyokuwa akiishi gavana wa zamani, marehemu Daudi Balali ambayo Prof Ndulu alidaiwa kuikataa kwa kuwa haina bwawa la kuogolea.

“Nashangaa kuambiwa nimekataa kuhamia kwenye nyumba; kisa haina bwawa la kuogolea, huu ni upotoshaji. Kama ni kuogelea, mimi niliogelea hadi kwenye mito, sasa sijui hili linatoka wapi,” alihoji Profesa Ndulu.

“Kwanza hiyo nyumba wanayosema ilikuwa kwa ajili ya kuishi mimi nikaikataa kwa sababu haina bwawa la kuogolea, ni uongo kwani ile alikuwa akiishi marehemu Ballali na ilikarabatiwa kwa ajili ya (Naibu Gavana Juma) Reli... sasa sijui mimi nimeingiaje,” alihoji.

Akitoa ufafanuzi wa maeneo halisi ya nyumba hizo, Profesa Ndulu alisema makazi yake hayako karibu na katibu mkuu mstaafu wa CCM na kwamba anayeishi huko ni Naibu Gavana (Taaasisi za Fedha na Mabenki) Rila Mkila.

Alisema Naibu Gavana (Uchumi), Dk Enok Bukuku hajahamia kwenye nyumba yoyote ya BoT na kwamba anaishi kwake hadi sasa.

Prof Ndulu, ambaye taasisi yake imelalamikiwa kwa kujiidhinishia mamilioni ya fedha za mikopo yenye tofauti kubwa ya viwango baina ya wafanyakazi wa chini na vigogo, alilalamika kuwa taarifa za ufujaji wa fedha katika ukarabati wa nyumba hizo zinamuweka katika kundi la mafisadi na kwamba ni mkakati wa mtandao huo alioutuhumu kuwa unaundwa na watumishi wa BoT na baadhi ya watu walio nje.

Alidai kuwa miongoni mwa watu walio nje ambao wanaeneza sifa mbaya dhidi yake ni mwanasheria maarufu ambaye anadaiwa kutangaza vita naye baada ya kuzuia mianya ya ufisadi.

Gavana Ndulu, ambaye aliteuliwa baada ya Balali kuachishwa kazi, alisema kamwe hatasita kutekeleza majukumu yake kwa ajili ya kufurahisha au kuhofu watu wenye dhamira ovu.

“Najua, kuna watu wanafikiri watanitisha au kunikatisha tamaa. Nasema nitaendelea kushikilia uzi ule ule kusimamia sheria na taratibu katika kuongoza benki na si vinginevyo,” alisema.

Alilalamika kuwa kuna watu wanataka kuzorotesha juhudi za kujengea nidhamu ndani ya taasisi hiyo na kwamba kwa dhamira zao wanaweza kukaa na kupotosha mambo kwa makusudi.
Kuhusu tuhuma nyingine kwamba, viwanja hivyo vilinunuliwa, Ndulu alisema vyote vimekuwa mali ya BoT kwa muda mrefu na hakuna hata kimoja kilichonunuliwa karibuni.

BoT imekuwa ikiangaliwa kwa karibu tangu kuibuka kwa kashfa ya wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), kashfa ambayo ilihusisha wizi wa zaidi ya Sh133 bilioni.

Taasisi hiyo pia imekumbwa na kashfa nyingine kama za bima ya maghorofa yaliyo jijini Dar es salaam na Zanzibar, kuongeza gharama katika uchapishaji wa noti na matumizi mabaya ya madaraka katika ujenzi wa maghorofa pacha.
Wafanyakazi wa benki hiyo wamejikuta kwenye kashfa za kufanikisha njama za wizi, kuajiriwa kwa kutumia vyeti vya kughushi na tuhuma za watoto wa vigogo kupewa ajira za upendeleo.

Thursday, December 24, 2009

Dk Kigoda, Zitto kuishtaki NSSF


*WADAI SHIRIKA HILO LINAUZA NYUMBA WANAZOPANGA KWA NJIA YA KIFISADI

Exuper Kachenje

WAPANGAJI zaidi ya 100 wa nyumba za Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF),Tabata jijini Dar es Salaam akiwamo Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zitto Kabwe na Naibu Waziri wa Afya Dk Aisha Kigoda, wameazimia kuliburuza shirika hilo mahakamani kupinga hatua yake ya kutangaza kuuza nyumba wanazoishi bila kuwashirikisha.

Aidha, wapangaji hao wanaowakilisha familia zao zenye watu 500 wameitaka NSSF kusitisha hatua hiyo ndani ya siku saba wakieleza kuwa imewaathiri kisaikolojia.

Hatua ya wapangaji hao wanaowakilisha familia za watu 500 wanaoishi kwenye nyumba hizo za ghorofa maarufu kama 'Tabata Phase II Housing Project' inafuatia mkutano wao walioufanya hivi karibuni.

Zitto na Dk Kigoda ni miongoni mwa wapangaji walioorodhesha majina yao na kusaini barua iliyoandikwa Desemba 10 mwaka huu, kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhan Dau baada ya maazimio ya mkutano wao, ambapo nakala yake imepelekwa kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mbunge wa Jimbo la Ukonga Dk Makongoro Mahanga, zilipo nyumba hizo.

Katika mkutano huo wa kujadili hatua hiyo ya NSSF, wapangaji hao walisema wao ni wapangaji halali wenye mkataba unaodumu hadi mwaka 2012.

NSSF ilitangaza zabuni ya kuuza nyumba hizo za ghorofa zilizopo wilayani Ilala kupitia gazeti la Daily News toleo la Desemba 4 na 7 likieleza nia yake ni kuziuza nyumba hizo kwa mteja mmoja.

Baadhi ya wapangaji waliozungumza na Mwananchi walisema, kitendi cha NSSF kutaka kuuza nyumba hizo kwa mtu mmoja kinaonyesha dalili za ufisadi, huku wakieleza kuwa wana fununu kuwa shirika hilo lina mpango wa kuuza nyumba hiyo kwa Mtanzania mmoja mwenye asili ya kiasia.

Wamedai kuwa mtu huyo anayetajwa kuwa NSSF ipo mbioni kumuuzia nyumba hizo zinazokaliwa pia na baadhi ya vigogo, anatajwa katika kashfa mbalimbali za ufisadi nchini.

Baadhi ya vigogo wanaoishi katika nyumba hizo mbali na Zitto na Dk Kigoda ni Jaji Sumari, Balozi mstaafu Nhigula, Habbi Gunze ambaye ni Mkurugenzi wa Utangazazi katika Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA).

Zitto Kabwe, wala Mbunge wa Ukonga hawakupatikana kuzungumzia sakata hilo, lakini naibu Waziri wa Afya Dk Aisha Kigoda alikiri kuwa mmoja wa wapangaji katika nyumba hizo na kueleza kuwa hawezi kupingana na uamuzi uliotolewa katika kikao cha wapangaji kwa kuwa na yeye unamhusu.

“Mimi ni mpangaji kama wengine pale, kama kuna maamuzi yametolewa na kikao au katibu ameandika barua kwenda NSSF au kwingine huo ndio uamuzi wa wapangaji wote,” alisema Dk Kigoda na kuongeza:

Kama ni maamuzi ya kikao hayo ni ‘collective’ (shirikishi), yamekuja kwa niaba ya wapangaji wote, ‘otherwise I have no comment’.”

Mpangaji mwingine Nganga Mlipano aliliambia gazeti hili kuwa hatua hiyo ya NSSF ni kukiuka taratibu, sheria na mkataba baina yao na NSSF hivyo wao kwa umoja wao hawakubaliani na hatua hiyo wakianza mchakato wa kisheria kuupinga na kudai fidia.

"Sisi ni wapangaji wa NSSF, ni kweli, lakini kimsingi unapotaka hata kufanyia marekebisho nyumba zako ni lazima umshirikishe mpangaji wako, kinyume cha hapo ni kuvunja sheria na kumsababishia usumbufu," alisema Mlipano na kuongeza:

"Wote tumekutana, tumejadili na kuandika barua kwenda kwa mkurugenzi wa NSSF nakala tumepeleka kwa Waziri Mkuu na mbunge wetu Makongoro Mahanga tukieleza mambo manne tunayotaka NSSF itekeleze."

Kwa mujibu wa mapendekezo hayo ambayo Mwananchi imeyaona wapangaji hao wanataka NSSF kusitisha mara moja nia yake kuuza nyumba hizo kwa kufuta zabuni iliyotangaza, ikiwa pamoja na kuzuia kufanyika kwa shughuli yoyote inayohusu uuzaji nyumba hizo zenye wapangaji bado.

Pia wameitaka NSSF kuomba radhi bila masharti kwa wapangaji hao kutokana na kuwasababishia matatizo ya kisaikolojia kwa kutangaza zabuni hiyo kinyume cha sheria, na kwamba wapangaji hao wana haki ya kuzuia uuzwaji nyumba hizo kwa kuzingatia sera ya taifa inayozuia uuzaji wa makazi ya watu na kuitaka NSSF kutekeleza mapendekezo hayo kama jambo la dharura ndani ya siku saba.

Mambo ya Krismass


Wafanyabiashara wa kuku wakisafirisha kukuu tayari kwa kuwauza kwa wateja katika maeneo ya Ubungo jijini Dar es Salaam jana . Biashara ya kuku imechangamka katika kipindi hiki cha sikukuu ya Krismass. PHOTO/SILVAN KIWALE

TANGAZO LA KIFO

MPIGAPICHA WA MAGAZETI YA MWANANCHI COMMUNICATION, WACHAPAJI WA MAGAZETI YA THE CITIZEN NA MWANANCHI BWANA EMANUEL HERMAN WA KIMARA BONYOKWA ANASIKITIKA KUTANGA KIFO CHA MKEWE, MARIA BENDERA, KILICHOTOKEA LEO DESEMBA 24, 2009 ASUBHI KATIKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI.

MIPANGO YA MAZISHI INAFANYIKA NAMANGA MSASANI KWA MAMA WA MAREHEMU NA MAZIKO YANATARAJI KUFANYIKA JUMAMOSI DESEMBA 26 JIJINI DAR ES ES SALAAM.

MAREHEMU AMEACHA MUME NA MTOTO MMOJA ELIZABETH HERMAN.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA MUNGU LIHIMIDIWE.

Wednesday, December 23, 2009

Waziri Burian na mambo ya Copenhagen



Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais(Mazingira)Dkt.Batilda Burian(Kulia)akiongea na waandishi wa Habari(hawapo pichani) jana jijini Dar es salaam kuhusu masuala mbalimbali yaliyojili katika mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi uliomalizika tarehe 18,Desemba 2009 mjini Copenhagen,Denmark.Mkutano huo pamoja na mambo mengine ulizitaka nchi zilizoendelea kupunguza uzalishaji wa gesi joto angalau kwa asilimia 40 chini ya viwango vilivyokuwa vikizalishwa mwaka 1990.

MATAPELI WA STAILI MPYA WAIBUKA DAR


Msemaji wa Jeshi la Polisi Kamishna Msaidizi wa Polisi Abdalah Mssika akiwaonyesha waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Polisi jijini Dar leo madawa ya feki ya kuhifadhia nafaka zisiharibiwe na wadudu ambayo kuna kundi la matapeli lililoibuka linawauzia madawa hayo ambalo linawadanganya wananchi kuwa madawa hayo yanahitajiwa kutumika na Shirika la Chakula la Kimataifa Duniani WFP.


Abdalah Mssika akielekeza waandishi wa habari jinsi ya kuweka nembo za kofia za polisi maana baadhi ya waandishi wanakosea kuweka nembo hiyo kulia sahihi ni kuweka nembo kushoto. Na Upendo Ramson wa Jeshi la Polisi.

Tuesday, December 22, 2009

Hoteli ya 'JK" iliyobomolewa







PICHANI WAKIONEKANA WAFANYAKAZI WA HOTELI YA KITALII YA SNOWCREST YA MJINI HAPA WAKIONDOA MABAKI MARA BAADA YA KUVUNJWA KWA UZIO WA HOTELI HIYO NA WAKALA WA BARABARA(TANROADS) MKOANI HAPA,HOTELI HIYO ILIZINDULIWA NA RAIS JAKAYA KIKWETE IJUMAA WIKI ILIYOPITA(PICHA NA MOSES MASHALLA)

Albino meeting


Mwenyekiti wa Chama Cha Maalbino Tanzania, Ernest Kimaya akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano mkuu wa uchaguzi wa chama hicho mjini Dodoma jana.
Mbunge wa Viti Maalum Al-Shymaa Kway-Geer akizungumza na mjumbe wa mkutano mkuu wa Chama Cha Maalbino Tanzania Mzawa Nyagame (kulia) baada ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa uchaguzi wa chama hicho mjini Dodoma jana.

Baadhi ya wajumbe wa Mkutano mkuu wa Chama Cha Maalbino Tanzania, wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano mkuu wa uchaguzi wa chama hicho mjini Dodoma jana. Picha zote na Jube Tranquilino

Major Works Contract for Tanga – Horohoro Road Upgrade Signed




Senior representatives from the Millennium Challenge Account – Tanzania (MCA-Tanzania) and the Resident Country Mission of the Millennium Challenge Corporation (MCC) in Tanzania announced that the first major road construction contract under the MCC Compact was signed today. The competitively awarded contract is for the rehabilitation and upgrading of the 65 km Tanga – Horohoro road to bitumen standard. The total value of the contract was nearly TZS 69.9 billion (US$ 53.8 million) and the winning firm was Sinohydro Corporation Ltd.

This award is the first of six different works contracts for the rehabilitation and upgrading of several Mainland Trunk Roads project under the Compact. Other road segments that will be upgraded include: Tunduma to Laela; Laela to Sumbawanga; Perimho Junction to Mbinga; and Songea to Nantumbo. The award for the Tanga – Horohoro construction work also follows the award of three construction supervision contracts in September 2009. The procurement process for construction of all of the other road segments is now underway simultaneously. Top quality firms from around the world have already passed the first procurement phase and been pre-qualified to participate in the second and final bidding stage, which is expected to result in the award of all five remaining construction contacts for the Mainland Trunk Roads project over the next few months.

MCC Resident Country Director Karl Fickenscher said, “This is truly great news to receive just before the start of the holidays. MCC and our MCA-Tanzania colleagues have been working very hard all year to reach this important project milestone. Up until now, we have been focused on all the necessary preparations, making sure that we have proper technical designs, running a full, open and transparent competition, and working directly with the people who will be affected by the construction to ensure that their views are heard and appropriate compensation and resettlement are arranged. All of this hard work should pay off well in the new year as we launch the construction phase of the Compact.”

The Mainland Trunk Roads project is one of several important transport sector activities underway under the MCC Compact between the Governments of the United States of America and the United Republic of Tanzania that went into effect in September 2008. Other projects in the transport sector include an upgrading of up to 36 kms of rural roads in Pemba and the improvements to Mafia island airport. The MCC Compact also includes major components that will provide significant assistance in the energy and water sectors. The American people will provide a total of $698.1 million in U.S. assistance under the Compact through September 2013.

Tuesday, December 08, 2009

Big Brother Revolution FINAL: Images from Day 91 - Sunday December 6, 2009


After 91 days Nigerian Kevin is voted the winner of M-Net’s hit continental reality series BIG BROTHER REVOLUTION walking away with a whopping USD 200 000! For more information log on to

10th anniversary of the nile basin initiative dinner


Sudan's Minister for Water Resources
Hon. Kamal Ali Ahmed is happy with his gift

Minister for Water and Irrigation Professor Mark Mwandosya speaks ahead of a dinner he hosted for delegates to the 10th Anniversary of the Nile Basin Initiative last night at the Movenpick hotel in Dar es salaam

Friday, December 04, 2009

Balozi wa Rwanda nchini katika ziara na vyombo mbalimbali


Balozi Mpya wa Rwanda Nchini Bi.Fatuma Ndagiza akimweleza Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta baadhi ya Mambo ambayo nchi yake ingependa kujifunza kutoka Bunge la Tanzania wakati alimpomtembelea kujitambulisha Ofisi kwa Spika jana . Balozi huyo wa Rwanda alimweleza Spika wa Bunge kuwa pamoja na mambo mengine Nchi yake inatarajia kuleta ujumbe Tanzania kwa lengo la kujifunza maswala ya Ushirika Nchini.
Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge.