Tuesday, December 30, 2008

huu mchezo wa mafuta tumeuchoka



Pichani unaweza kumuona askari anayelinda kituo cha mafuta kinachodaiwa kufungwa kutokana na kukosa mafuta lakini waagizaji wakubwa wa mafuta nchini wamewakana wamiliki wa vituo vya kuuza nishati hiyo na kushangazwa na kitendo cha kupandisha bei kiholela wakati wa Sikukuu ya Krismasi kwa kisingizio cha uadimu wa mafuta baada ya meli kuzuiwa na maharamia wa Kisomali.

Kauli ya waagizaji hao imekuja siku moja baada ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima kueleza kuwa akiba ya mafuta iliyopo ni kubwa ya kuweza kutosheleza mwezi mzima na kushangazwa na hatua ya wafanyabiashara hao kupandisha bei ya mafuta kwa madai kuwa ni adimu.

Bei ya mafuta ilipanda ghafla usiku, siku moja kabla ya Krismasi huku baadhi ya vituo vikifungwa kwa maelezo kuwa kuongezeka kwa vitendo vya maharamia wa Kisomali kuteka meli za mizigo kwenye pwani ya Somalia kumefanya meli zilizobeba shehena za mafuta yanayokuja nchini kushindwa kupita na hivyo kusababisha uhaba wa nishati hiyo muhimu.

Monday, December 29, 2008

Kubenea akiwa na Paschal


MKURUGENZI Mtendaji wa gazeti la MwanaHALISI (ambalo liko kifungoni), Saed Kubenea mwenye miwani, akimjulia hali mwanahabari Pascal Mayala jana katika hospitari ya Apollo Indraprastha, mjini Delih nchini India.

Mayala amelazwa hopitari hapo akipata matibu yaliotokana na ajali ya pikipiki miezi mitatu iliyopita ambapo alijeruhiwa vibaya mguu wa kushoto, mkono wa kushoto na bega la kushoto.

Kwa upande wake, Kubenea yupo nchini India kwa takribani mwezi mmoja sasa, akipata matibabu ya macho yaliotokana na kuvamiwa na kumwagiwa tindikali, ofisini kwake Januari 05 mwaka huu.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PPR, Pascal Mayala akiwa amelazwa katika Hospitali ya Apollo Indraprastha, mjini Delhi nchini India anakotibiwa baada ya kujeruhiwa vibaya katika ajali ya pikipiki iliyotokea hivi karibuni nchini.

Picha na (mpiga maalum)

Friday, December 26, 2008

jamaa na mambo ya krismasi


Mkazi huyu wa mkoa wa Arusha alikutwa akiwa amelala ndani ya mtaro huku akiwa
hajitambui jirani na kituo kikuu cha polisi mkoani hapa.Wapita njia walisema kuwa
mtu huyo alikuwa amelala baada kunywa pombe akisherehekea sikukuu ya krismas.(picha
na Hemed Kivuyo)

Friday, December 19, 2008

Kijarida Cha Cheche Mitaani-Jinsi walivyoitafuna ATCL


Je ATCL imefikaje hapa hadi kujikuta inasimamisha huduma yake? Ni kwanini shirika la IATA liamue kuisimamisha ATCL? Je ni kweli tatizo la ATCL ni fedha! Umesikia kuhusu Dowans na jaribio lililofeli la kujaribu kuitengenezea mshiko licha ya kampuni hiyo kurithi mkataba usio halali wa Richmond?
Umewahi kusoma maoni ya Rev.Kishoka (Waumini wake wako kwenye mtandao!)? Vipi kuhusu hoja za nguvu zisizo na kigugumizi za mwanakijiji na mawazo ya kina ya Dada Jessy? Kama umejibu "hapana" kwenye swali lolote hapo juu basi wewe ni miongoni mwa watu ambao hawajapata nafasi ya kusoma kijarida cha bure, huru, na kinachotubutu zaidi cha "Cheche za Fikra". Unaweza kujisomea kwenye mtandao wa habari wa
http://www.forums.mwanakijiji.com/forumdisplay.php?f=62 au unaweza kujiandikisha kupata kijarida hicho kwenye email yako kila wiki kwa kuomba kutumiwa kijarida hicho kwa kutuma ombi la kuandikishwa kupitia klhnews@gmail.com
Na sisi tunaweza!
Twende na tuwe "Cheche"Mhariri!

Mgonja atoka lupango





Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Gray Mgonja, leo alifikishwa tena Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mbele ya Mheshimiwa Henzroni Mwankenja kushughulikia suala la dhamana ambalo ilifanikiwa baada ya mawakili wake kuwasilisha hati ya nyumba sita pamoja na Hati ya kusafiria ya mshitakiwa, pichani Mgonja akiwasalimia ndugu zake wakati akiingizwa mahakamani hapo.Picha za http://www.globalpublisherstz.com

Miss East Africa Bujumbura leo





Picha kwa mujibu wa Mpoki Bukuku

Herry Makange aagwa



Ndugu jamaa na marafiki wakimfariji mjane wa marehemu

KWA MUJIBU wa taarifa ambazo tumezipata Mwili wa Marehemu Herry Makange umeagwa leo hapa jijini Dar es Salaam nyumbani kwa Mzee Mponzi ( Baba Mkwe wake) Oysterbay Mtaa wa Msasani nyumba N0 35 saa 6 hadi saa 8 mchana na baadae mwili wa Marehemu utasafirishwa hadi Kibaha Vigaeni nyumbani kwao kwa maazishi yatakayo fanyika huko huko Kibaha. (Picha ya Mrocky Mrocky)

Deus Malya ndani ya mahakama




Deus Malya (left) in consultations with his advocate Godfrey Wasong a.k.a White before the proceedings of a traffic case against him at the Dodoma Resident magistrate court yesterday. Photo/Jube Tranquilino

Thursday, December 18, 2008

Herry Makange afariki dunia




HAYATI HERRY MAKANGE

Habari tza kusikitisha tulizozipoke hivi punde kutoka kwa issamichuzi.blogspot.com zinasema kuwa HERRY MAKANGE, MPIGANAJI WA CHANNEL TEN NA DTV, HATUNAYE TENA BAADA YA KUFARIKI KATIKA AJALI HAPA DAR JANA MCHANA.

HABARI ZILIZOPATIKANA JANA USIKU NA KUTHIBITISHWA ASUBUHI HII NI KWAMBA HERRY ALIKUTWA NA MAUTI AKIELEKEA MJINI KUTOKEA KAWO KIBAHA AKIWA ANAENDESHA PIKIPIKI. ALIKUWA NDIO KWANZA AMEREJEA TOKA TABORA KIKAZI NA ALIKUWA AKIENDA KURIPOTI KAZINI.
IKUMBUKWE KWAMBA HERRY ALIKUWA MMOJA WA WAPIGANAJI WALIONUSURIKA KATIKA AJALI YA GARI HUKO KIBITI ILIYOMHUSISHA PIA MPIGANAJI ATHUMANI HAMISI AMBAYE HADI LEO YUKO SAUZI AKITIBIWA SHINGO NA MGONGO. KURASA YA AJALI HIYO YA KIBITI BOFYA HAPA
TUTAENDELEA KUFAHAMISHANA KILA KINACHOJIRI BAADAYE IKIWA NI OAMOJA NA MIPANGO YA MAZISHI.
MUNGU AILAZE ROHO YA MPIGANAJI MWENZETU MAHALI PEMA PEPONI
-AMINA

Wednesday, December 10, 2008

Huduma za ndege ATCL zasitishwa ndani, nje ya nchi


Moja ya ndege za Shirika la Ndege Tanzania ambalo sasa huduma zake zimesimamishwa.

SHIRIKA la Ndege la Tanzania (ATCL), ambalo limekuwa na matatizo makubwa tangu ndoa yake ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) ivunjike, limenyang’anywa cheti cha kuruka angani na Mamlaka ya Anga (TCAA) baada ya kukosa viwango vya ubora kuruka angani.

Taarifa kutoka ndani ya ya ATCL zimeeleza kuwa shirika hilo limenyang’anywa cheti hicho tangu Desemba 8 mwaka huu na hivyo litashindwa kusafirisha abiria hadi hapo litakapokidhi masharti ya usalama wa anga na kurejeshewa cheti hicho.

Miongoni mwa viwango hivyo vya usalama ni ukaguzi wa mara kwa mara wa ndege zake, kuwa na wataalamu wa kutosha kama marubani na wahandisi, vitu ambavyo vimeonekana kukosekana kwenye shirika hilo la serikali.

Kufungiwa huko kumekuja huku kukiwa na uwezekano wa shirika hilo kufungiwa na Chama cha Kimataifa cha Usafiri wa Anga (IATA) kufanya safari zake baada ya kubaini zaidi ya makosa 500.

Mwishoni mwa wiki iliripotiwa kuwa ATCL ilikaguliwa mwezi Oktoba na kubainika na makosa hayo ya usafiri wa anga, lakini ikashindwa kuyarekebisha na ndipo IATA ilipoanza mchakato wa kutaka kuizuia kufanya safari.

“Ni kweli ATCL imenyang’anywa cheti cha viwango kwa kukosa ubora wa kuruka angani hivyo haitafanya safari za nje wala ndani ya nchi,” alisema mmoja wa watu wa ndani TCAA alipohojiwa na Mwananchi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, ndege za ATCL zilizokuwa zikifanya safari zake ndani na nje ya nchi haitaweza kufanya tena safari hizo na vigogo wa ATCL jana walikuwa na vikao na TCAA kuzungumzia suala hilo.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo katibu mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Omar Chambo alisema hana taarifa kuhusu kunyang’anywa cheti kwa ATCL na kudai kuwa mkurugenzi wa shirika hilo, David Mataka ndiye anayeweza kueleza suala hilo.

“Sina taarifa kuhusu suala hilo... hayo ni mambo ya ATCL na anayeweza kukueleza ni Mataka, hivyo wasiliana naye... haiwezekani toka tarehe nane hadi leo mimi sijui,” alisema Chambo.

Tuesday, December 09, 2008

Mchezo wa bao


Nimaarufu saana mchezo huu ukichezwa na watu wa rika mbalimbali na katika nyakati tofauti, ni mchezo wa kijadi na aliupendelea sana hayati Mwalimu Julius kambarage Nyerere, hebu cheki watoto sijui wanacheza au wanazuga!

Miaka 47 ya uhuru wa tanzania




MAMA Maria Nyerere na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, jana walikuwa kivutio katika maadhimisho ya Sherehe za Uhuru yaliyofanyika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam baada ya kushangiliwa na umati wa watu waliohururia sherehe hizo huku viongozi wengine wakiingia kimya kimya.

Kitendo cha wananchi kuwashangilia viongozi hao kwa nderemo na vifijo bila hata kuhamasishwa ilileta utofauti mkubwa kati yao na Rais Jakaya Kikwete ambaye alishangiliwa na baadhi ya makundi hasa baada ya kutangaziwa na mwongoza sherehe.

Akitangaza wakati msafara wa rais unakaribia kuingia uwanjani huku watu wakiwa kimya, mwongoza sherehe huyo alisema: “Mabibi na mabwana tunayemtarajia kuingia uwanjani hivi sasa ni Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Jakaya Kikwete, hivyo atakapoingia uwanjani ninaomba tumshangilie kwa nguvu zetu zote.”

Hata hivyo, muda mfupi baada ya tangazo hilo Rais Kikwete akaingia uwanjani kwa kutumia geti kubwa na kuzunguka uwanja akiwa katika gari la wazi la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ndipo makundi hayo yakijaribu kushangilia kwa sauti ya chini huku baadhi yao wakipeperusha bendera ya Taifa.

Watoto bwana


Watoto wakiwa katika michezo yao bwana huwawezi ni ma expert wa michezo yao hebu wacheki hawa watoto wamebuni mchezo wao, hii ilikutwa na mdau wetu Juma Uledi wa Morogoro

Monday, December 01, 2008

Jupiter, Venus, mwezi zakutana


VITU vitatu jana vilikuwa viking'aa angani vikiwa vimejipanga pamoja; ni sayari za Jupite na Venus ambazo ziliuzunguka mwezi uliokuwa ukionekana kama mithili ya ukucha uliokatwa.

Ni tukio lisilo la kawaida kutokea, lakini hutokea kila baada ya miaka kadhaa. Baada ya tukio la jana, sayari hizo na mwezi zitakaribiana tena Novemba 18 mwaka 2052.

Jupiter na Venus zilianza kusogea kuelekea karibu na mwezi juzi jioni na ilipofika jana zilionekana zikiwa umbali wa digrii 2, ambazo ni sawa na kidole kilichonyooshwa kwenye mkono, anasema Alan MacRobert, mhariri mwandamizi wa jarida la Sky and Telescope alipoongea na AP.

Tofauti na hali inavyokuwa wakati jua likikamatwa na mwezi, jana haikuhitaji kiona mbali kushuhudia tukio hilo kutokana na vitu hivyo vitatu kutoa mwanga mkali, mwezi ukionekana kuwa mkubwa zaidi na kufuatiwa na Jupiter, ambayo ilionekana upande wa kushoto, huku Venus ikionekana kuwa ndogo kuliko zote.

Vibaka wawapa polisi kibarua kizito Mtoni Kizinga



Hebu cheki wananchi wa Mto Kizinga wanavyopata shida kuweza kupita kwenda au kurudi kutoka kwao Mbagala ni karaha kubwa mno, jana jeshi la polisi lilimwaga askari wake katika daraja la Mto Kizinga lililopo Mtongani jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kudhibiti vibaka walioanza kutumia fursa ya adha ya kuvuka mto huo kuwapora watu mali zao.

Daraja la mto Kizinga limefunikwa na maji baada ya mvua kubwa iliyonyesha juzi maeneo ya Kisarawe hali ambayo imewalazimisha watu kuvuka mto huo kwa miguu baada ya magari kushindwa kupita.

Vibaka hao walikuwa wakijibanza pembeni mwa daraja hilo lilofunikwa na maji na kuwapora watu wanaopita eneo hilo kwa miguu vitu mbalimbali na kusababisha uvunjifu wa amani.

Polisi hao wamemwagwa eneo hilo baada ya malalamiko kadhaa ya watumiaji wa njia hiyo kutaka polisi wadhibiti vitendo hivyo kwa ulinzi wa silaha.

“Kwa kweli hali ilikuwa mbaya sana katika daraja hili tulikuwa hatupiti kwa raha yaani Jana na juzi ikifika saa moja asubuhi au jioni hujavuka katika daraja hili basi ujue lazima utakabwa,” alisema Irene John wakati akiongea na Mwananchi na kuongeza kuwa

“Jana mama mmoja alikuwa akipita eneo hili alipigwa na kuporwa pochi pamoja na simu na vibaka na polisi walifika mara moja na kumkamata tunashukuru kwani polisi wamefika na hali ni shwari kabisa hakuna tena matukio ya uporaji” . Habari imeandikwa na Christina Kabadi.