Sunday, June 29, 2008

Mugabe ashinda, aapishwa


RAIS Robert Mugabe wa Zimbabwe, ameshinda na kuapishwa baada ya uchaguzi wa marudio uliofanyika Ijumaa wiki iliyopita, kwa kupata asilimia 85 ya kura zote zilizopigwa.
Afisa Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe (Zec), Lovemore Sekeramyi, alisema kuwa Mugabe alishinda kwa jumla ya kura 2,150,269 huku Morgan Tsvangirai wa Chama cha Movement for Democratic Change (MDC), ambaye pamoja na kutangaza kujitoa jina lake liliendelea kuachwa kwenye karatasi za kupigia kura, alipata kura 233,000.
Alisema kuwa katika matokeo hayo yaliyotangazwa jana, yalionyesha kuwa Rais Mugabe ameshinda katika majimbo yote 10 nchini humo, kupitia uchaguzi huo ambao alisimama peke yake.

Kwa taarifa zaidi soma
cheki Shirika la Utangazaji la BBC

Kilimanjaro Music Award







WASANII kumi wamechaguliwa kuingia katika shindano la kumsaka Mfalme wa hip hop hapa nchini baada ya mashabiki kupiga kura zao kutoka sehemu mbalimbali nchini.
Wasanii ambao wamechaguliwa katika shindano hilo ni Kalapina wa kundin la Kikosi cha Mizinga, Chid Benz kutoka La Familia, Fid Q, Kala Jeremiah, Joe Makini, Langa, Lord Eyez kutoka Nako2Nako, Rado, Black Rhino na Profesa Jay maarufu kama Daddy.
Akizungumza na Mwananchi, Mratibu wa Shindano hilo, Charles Mateso alisema lengo la kaunzisha shindano hilo ni kuleta changamoto kwa mashabiki na hata wasanii wenyewe.
"Kilichofanyika tuliendesha zoezi la kuwataka wasomaji wetu wachague ni wasanii gani wanaofaa kuingia katika shindano hilo, ambapo baada ya majumuisho ya kura zote walipatikana wasanii kumi na hao ndiyo watakaoliwania taji hilo," alisema.
Alisema mshindi wa shindano hilo atapatikana kutokana na kura za wasomaji wa ambao ndiyo watakaomchagua yule wanayemuona anafaa kuwa Ijumaa King Of Hip Hop. "Litakuwa ni shindano la wazi na hakuna kumpendelea mtu, ila mashabiki ndiyo watakaoamua nani anastahili."
“Ili kumpata mshindi wasomaji wanatakiwa kupiga kura kwa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kwa kuandika neno HP (acha nafasi), andika jina la msanii unayeona anastahili kushinda taji hilo na kutuma kwenda namba 15551,” alisema.
Kuhusu zawadi alisema mshindi atapata zawadi kubwa itakayotangazwa hapo baadaye, huku yule aliyeshiriki kupiga kura naye akiwa katika nafasi ya kujishindia zawadi kemkem zilizoandaliwa kwa ajili yao. Picha zote kwa hisani ya mdau wa blogu hii Deus Mhagale ambaye alikuwamo ukumbini.

Werrason anatisha si mchezo








Mwanamuziki nyota kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Ngiama Makanda 'Werrason' akionyesha umahiri wake wa kucheza wakati wa onyesho lake lililofanyika Dar es Salaam juzi Picha zote kwa hisani ya Emmanuel Herman.

Friday, June 27, 2008

Maisha ya Mtanzania halisi


Msichana wa kabila la Wabarbeig wa kitongoji cha Maramboi akiwa
machungaji katika eneo ambalo wametakiwa kuondoka kutokana na serikali ya kijiji
chao cha vilima viwili kulikodisha kwa mwekezaji wa kifaransa En Un Lodge. Picha na mussa juma

Thursday, June 26, 2008

Amanda wetu yuko juu miss Universe


Miss Universe Tanzania, Amanda Ole Sulul ameingia kwenye 20 bora kati ya warembo 80 wanaowania taji la mashindano hayo yanayoatarajia kufanyika Vietnam Julai 14.
Amanda ameingia hatua hiyo pamoja na mrembo wa Afrika Kusini, Tansey Coetzee ambapo warembo wa Misri, Ghana, Mauritius na Nigeria hawapo katika orodha hiyo.
Miss universe Venezuela Diana Mendoza anashika nafasi ya kwanza katika orodha hiyo akifuatiwa na mrembo wa Marekani, Puerto Rico, Panama, Trinidad and Tobago, Mexico, Ireland, Australia, Colombia, na Thailand.
Pia wapo India, Monteneegro, China, Kosovo, Belgium, Japan, Curacao, Tanzania, Afrika Kusini na Italia.
Amanda ambaye alishinda taji la Miss Universe Tanzania Mei 29 mwaka huu, alitayarishwa na wataalam mbalimbali hapa nchini chini ya usimamizi wa kampuni ya Compass Communications.

Picha mpya ya Rais


Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Kassim Mpenda, akiwanyesha jana waandishi wa habari picha mpya ya Rais iliyopo kushoto itakayotumika rasmi kitaifa na kulia ni ya zamani ambayo haitatumika tena.

Kilimo cha umwagiliaji


Wallahi jitihada kama hizi zingelisambaa Tanzania nzima kwa wakulima kutumia njia za kisasa kama hizi nina uhakika tungekuwa tumepiga hatua kali sana ya maendeleo bila shaka tungefanana na Malaysia na Indonesia lakini hebu nambie kilimo chetu kilivyo noma.

Tuesday, June 24, 2008

Maweeeee Flaviana


"Namshukuru Mungu sijaharibu kwa kweli ingawa wakati mwingine waandishi wa habari huwa wanaandika mambo yasiyokuwa na ukweli ndani yake.Hata hivyo mimi husema pengine hiyo ni moja ya kazi yao.Kimsingi, vyombo vya habari ndio vinavyonyanyua na kuchafua pia.Hivyo ni ngumu sana kuelezea ingawa nina imani hili linafahamika.

Jambo ambalo ningependa kuliweka sawa ni kuhusu kilichotokea siku ya uzinduzi wa upimaji ukimwi pale Mnazi Mmoja.Jamani mimi hamna mtu aliyenilazimisha kwenda pale siku ile. Niliamua mwenyewe na nilikuwa najiamini. Sasa nilisikitika pale nilipozirai(faint) watu wakaandika habari tofauti.Mimi ni binadamu, pale kulikuwa na jua kali na msongamano wa watu mkubwa kiasi kwamba hewa ikawa haitoshi.

Ile ni hali inayoweza kumtokea mtu yeyote.Hivyo basi nakanusha usemi uliovuma eti nilizirai kutokana na hofu ya kupima",Hayo is maneno yangu Wadau, na maneno ya Mlimbwende Flaviana Matata alipofanya mahojiano ya kina na wanja la kaka Jeff kupitia cheki Bongo Celebrity ,ukitaka kufahamu zaidi kuhusu flavi na harakati zake za kimaisha ingia hapo
 

Sunday, June 22, 2008

Tsvangirai ajitoa uchaguzi Zimbabwe




MGOMBEA wa kiti cha urais kwa tiketi ya upinzani nchini Zimbabwe, Morgan Tsvangirai ameamua kujitoa katika marudio ya uchaguzi yanayotarajiwa kufanyika Ijumaa wiki hii.

Akitangaza uamuzi huo mjini Harare jana, Tsvangirai alisema hakuna maana ya kushiriki katika uchaguzi ambao kuna uhakika kuwa hauwezi kuwa huru na wa haki ambao matokeo yake yako mikononi mwa Rais Robert Mugabe.

Tsvangirai alisema kwua yeye pamoja na chama chake cha Movement for Democratic Change (MDC) kwa sasa wanaelekeza nguvu zao katika kuiomba jumuya ya kimataifa kuingia nchini humo kwa ajili ya kuwalinda raia wake.

Uamuzi huo uliotangazwa muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao cha dharura cha Baraza Kuu la MDC jana ni hatua inayomaanisha kuwa kwa sasa ushindi ni wa bure kwa Rais Mugabe ambaye ataendelea kubaki madarakani. Habari zaidi hebu soma cheki BBC upate habari hii kwa kina.

Miss Universe Tanzania


Amanda Ole Sulul Miss Universe TANZANIA 2008 baada ya kufika katika mavazi ya ufukweni huko HoChi Ming City, Vietnam. Amanda Ole Sulul yuko nchini Vietnam akishindana na warembo 80 kutoka nchi mbalimbali duniani kuwania taji la Miss Universe 2008.

Ghorofa laporomoka





Kifusi cha jengo la Gholofa 10 lililokuwa likijengwa katika mtaa wa Mtendeni linavyonekana baada ya kuporomoka jana pia Waokoaji, wakimbeba mmoja wa majeruhi kati ya wanne walionasa katika jingo moja lillilopo mtaa wa mtaa wa Mtendeni Dar es Salaam jana, baada ya hilokuporomokewa na jengo jipya la Gholofa 10 lililokuwa kikijengwa.

Friday, June 20, 2008

Watoto hawa bwana!!!


Hii ndiyo bongo bwana mambo yetu yanakwenda tambarare si mchezo lakini kuna kona zingine mambo hayaendi sawa, maji tatizo na kila kitu ni balaa.

Iddi Amin




Kundi zima maigizo likiwa katika kujitangaza leo hii hapa jijini Dar es Salaam Msanii Lumole Matovolwa anayeigiza kama, Iddi Amini-Dadaa akiwa na wenzake walipozungumzia uzinduzi wa mchezo wa kuigizo waliouipa jina la Juliana. Mchezo huo, unatarajiwa kuzinduliwa Juni 26 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

Wednesday, June 18, 2008

Hyenas Square



Unaujua huu uwanja hebu cheki mambo yanavyokwenda hapa Habari zaidi hebu soma cheki Uwanja wa Fisi upate habari kwa kina.

Monday, June 16, 2008

Vipanya marufuku Dar


Hawa jamaa nuksi sana mmesikia hilo balaa yaani kiufupi ni kwamba Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini, (Sumatra), imesema daladala aina ya Hiace, maarufu kama "Vipanya", hazitaruhusiwa kutoa huduma ya kusafirisha abiria jijini Dar es Salaam, ifikapo Agosti Mosi, mwaka huu.

Badala yake, Sumatra imesema huduma hiyo itatolewa na magari makubwa yenye uwezo wa kuchukua abiria zaidi ya 25, badala ya "Vipanya", ambavyo vina uwezo wa kuchukua abiria 18 tu walioketi.

Hata hivyo, Sumatra imesema magari yatakayoruhusiwa kutoa huduma hiyo, lazima yawe ni mapya na yasiwe yametumika zaidi ya miaka mitano, kama inavyofanyika hivi sasa. Mpango huu bila shaka utafanya jiji la Dar es Salaam lisikalike kwa kuwa na vibaka..

Mkurugezi Mkuu wa Sumatra, Israel Sekirasa alisema uamuzi huo unatokana na kanuni mpya za viwango vya magari ya usafiri wa umma ambayo inazuia magari yenye uwezo wa kuketisha abiria chini ya 25 kutoa huduma za usafiri huo mijini.

Sekirasa alisema hayo kwenye mkutano wa wadau wa kukusanya maoni, kuhusu maombi ya wamiliki wa mabasi ya kuongeza gharama za usafiri Dar es Salaam, uliofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini.

"Kwa mujibu wa kanuni mpya za viwango vya magari ya usafiri wa umma, magari yenye uwezo wa kuketisha abiria chini ya 25 hayafai kutoa huduma za usafiri wa umma," alisema Sekirasa. Habari zaidi hebu soma cheki Mwananchi upate habari hii kwa kina

Mzee ruksa ashindwa kukwea mlima Kilimanjaro


INAWEZEKANA ushauri wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kumtaka Rais Mstaafu, Alhaji Alli Hassan Mwinyi asifike kileleni umefanyiwa kazi baada ya Rais huyo mstaafu kuishia urefu wa meta 3,000 kutoka usawa wa bahari.

Mlima huo mrefu kuliko yote barani Afrika una urefu wa meta 5,896 na kama Alhaji Mwinyi angefika kileleni basi angweka rekodi ya kuwa kiongozi wa ngazi ya Juu kabisa Serikalini kuwahi kufika kileleni.

Alhaji Mwinyi ambaye alianza safari ya siku sita ya kupanda mlima huo Jumamosi iliyopita saa 3:15 asubuhi kupitia lango kuu la Machame na kufika kituo cha kwanza cha Machame Camp saa 10:00 Jioni.

Hata hivyo, Rais huyo mstaafu hakuendelea kupanda Mlima huo na kurejea juzi saa 4:00 asubuhi na hii imetadsiriwa kuwa huenda alisikiliza wosia wa Waziri Mkuu Pinda wakati akimuaga hiyo juzi.

Meneja uhusiano wa Kampuni ya Geita Gold Mine(GGM), Ahmed Merere alilithibitishia Mwananchi jana kurejea kwa Rais Mstaafu, lakini akasema kurejea kwake si kwamba ameshindwa kuendelea bali ni uamuzi binafsi. Habari hii ya mdau
Daniel Mjema aliyekuwapo Hai, Kilimanjaro.

Hali si shwari Baktata



WALIOKUWA viongozi waandamizi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), wamekutana kujadili hatua ya Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Issa bin Shaaban Simba kuwavua uongozi katika mazingira ya kutatanisha.

Viongozi waliovuliwa uongozi ni aliyekuwa Naibu Mufti, Sheikh Abubakar Zubeir, Katibu wa Mufti ambaye na Naibu Katibu wa Baraza la Ulamaa la Bakwata Taifa, Sheikh Abdushakur Omar.

Wengine ni Katibu wa Baraza la Ulamaa, Sheikh Hassan Chizenga, Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu Taifa, Sheikh Khamis Mataka na wajumbe wawili wa Baraza la Ulamaa, Sheikh Suleiman Kilemile na Sheikh Hamid Jongo.

Habari zilizopatikana jana zinaeleza kwamba, baadhi ya viongozi hao, kuanzia juzi na jana, wamekuwa wakifanya vikao jijini Dar es Salaam, wakijadili hatua hiyo ya Mufti Simba na hatma yao Bakwata. Habari ya Muhibu Said.

Sunday, June 15, 2008

Mwanza tambarare


Mambo ya Mwanza si mchezo sasa kuna majengo makali ile mbaya yanayolifanya jiji la Mwanza kubadilisha sura hili jengo limejengwa kwa ushirikiano na Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF)

Mzee Mwinyi kiboko


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi (kulia kwake) wakiwa na baadhi ya washiriki wa safari ya kupanda mlima Kilimanjaro kuanzia geti la Machame, Juni 14,2008 . Matembezi hayo yaliyoanzishwa na Waziri Mkuu yameandaliwa na mgodi wa Dhahabu wa Geita n yamelenga kuchangia mapambani dhidi ya ukumwi.

CCM wakaangana


Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mawaziri wakuu wastaafu, Cleopa Msuya (katikati), Fredercick Sumaye (kulia) na Edward Lowassa (kushoto) wakiwa katika mkutano wa wabunge wote wa CCM na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM ulioongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kwenye ukumbi wa African Dream mjini Dodoma Juni 15,2008.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akijiandaa kufungua mkutano wa Wabunge wote wa CCM na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM uliofanyika kwenye ukumbi wa African Dream, Area D mjini Dodoma Juni 15, 2008.
Viongozi wengine kutoka kushoto ni Spika wa Bunge Samwel Sitta, Makamu Mwemyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar, Aman Karume na kulia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.



Mwenyekiti wa CCM,Rais, Jakaya Kikwete na viongozi wengine wakiwa kwenye ukumbi wa African Dream, Area D mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa mkutano wa wabunge wote wa CCM na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM juni
15,2008. Viongozi hao kutoka kushoto ni Spika wa Bunge, Samwel Sitta, Katibi Mkuu wa CCM Mstaafu, Rashidi Kawawa, Mamamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar Aman Karume, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Stars yaishangaza Cameroon



Rais Kikwete akiongoza maelfu ya wadau kuishangilia taifa stars mara baada ya kipyenga cha mwisho kulia. japokuwa kila mmoja alitamani kuchukua pointi zote tatu muhimu, lakini hako kamoja ka sare na moja ya timu kali kuliko zote barani afrika si haba ati. wadau mwasemaje?




LICHA ya kuwa na wachezaji mahiri na wanaocheza klabu kubwa za Ulaya, Cameroon imepunguzwa kasi na kuduwazwa na timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' katika mchezo wa kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia na Mataifa ya Afrika mwaka 2010.
Ikiwa na majina makubwa kama Samuel Eto'o wa Barcelona, kiungo wa Arsenal Alexander Song na Geremi Njitap wa Newcastle, Cameroon ilijikuta ikipigiwa pasi mfululizo na vijana wa Marcio Maximo katika mechi hiyo iliyofanyika jana kwenye Uwanja Mkuu wa Tanzania na kushuhudia matokeo ya suluhu na kosa kosa kadhaa.
Matokeo hayo yameifanya Cameroon kuwa na pointi saba, huku Taifa Stars ikiwa na pointi mbili, lakini ina matumaini ya nafasi ya pili iwapo itazifunga timu za Cape Verde na Mauritius katika mechi za marudiano.
Cameroon ambao waliingia uwanjani na kuanza kucheza soka la mipango zaidi walijikuta wakipigwa na butwaa baada ya mipango yao kutofanikiwa na kujikuta wakipata upinzani mkali kutoka kwa vijana hao wa Maximo. Picha za Mdau Mpoki Bukuku.

Friday, June 13, 2008

Mufti apasua jipu



Watu wengine wamesema maneno mabaya na wengine wakatangaza amekatwa mguu, na maneno kibao ya kashfa yamemwagwa dhidi ya Mufti, lakini inshaalah Mwenyezimungu kamjaalia Mufti Issa Bin Shaaban bin Simba ambaye amesema leo alichofanyiwa hospitali nchini India, ni upasuaji mkubwa baada ya mguu wake wa kulia kuoza kutokana na kushambuliwa na bakteria, ambao awali alisema hajui namna walivyoingia mguuni.

Hata hivyo, baadaye alisema ana wasiwasi huenda bakteria hao waliingia kupitia majeraha mengi aliyokuwa nayo mguuni.

"Nimerudi, ni mzima, nina afya njema, nina uwezo wa kula na madaktari wana matumaini," alisema Mufti Simba ambaye alikanusha uvumi kwamba, amekatwa mguu, ingawa hakuuonyesha mguu huo kwa viongozi wala waandishi wa habari waliohudhuria mapokezi hayo ili kuufuta kabisa uvumi huo.


"Nimepewa miezi mitatu ya mapumziko nisifanye kazi ngumu, baadaye nitarudi India," alisema Mufti Simba.

Bajeti kwapukwapu



SERIKALI imeshindwa kupunguza bei ya petroli na dizeli katika bajeti yake ya mwaka 2008/2009, badala yake imewabana wavuta sigara na wanywaji wa bia na soda kwa kupandisha kodi ya bidhaa hizo.

Pamoja na kutoongeza ushuru katika bidhaa za petroli, bado wachambuzi wa masuala ya uchumi wanaona hali itaendelea kuwa ngumu katika sekta za uzalishaji na usafirishaji kutokana na kuongezeka kwa kasi bei ya nishati hiyo katika soko la dunia, hivyo wananchi kuendelea kuishi katika hali ngumu katika kipindi cha mwaka huu wa bajeti.

Bajeti hiyo pia imeongeza ushuru wa bidhaa katika huduma za simu za mkononi kutoka asilimia saba ya gharama ya matumizi ya huduma hadi asilimia 10. Kwa mantiki hiyo, gharama za matumizi ya simu zitaongezeka kwa watumiaji.Hebu soma cheki FULL DOCUMENT YA HOTUBA YA BAJETI YA WAZIRI BUNGENI

Wednesday, June 11, 2008

Cameroon ndani ya nyumba



Sam Eto'oo akiwa Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam jana kwa ajili ya kuivaa Stars.

CAMEROON jana iliwasili nchini na kikosi chake kamili, huku nahodha wake Rigobert Song akisema: "Tunaihofia Tanzania.Alisema baada ya kuona mikanda ya mechi mbili wanajua kuwa wamekuja kucheza na timu nzuri na isiyotabirika".

Cameroon, ambayo ilikosa fainali zilizopita za Kombe la Dunia nchini Ujerumani mwaka 2006 baada ya kutibuliwa na Misri katika mechi ya mwisho, imewasili nchini siku nne kabla ya mechi dhidi ya Taifa Stars itakayofanyika kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa, Jumamosi.

"Kuja kwetu mapema ni sehemu ya mikakati yetu ya kupata matokeo mazuri kwenye kundi letu, ili tuwe na nafasi nzuri kwenye mashindano makubwa duniani," alisema beki huyo wa zamani wa Liverpool.

"Tumeiona Tanzania mapema, lakini haina tatizo kwetu kwa kuwa kikosi chetu pia kimeteuliwa kwa kuzingatia ukubwa wa mashindano."

Cameroon inaongoza Kundi la Kwanza la michuano ya awali ya Kombe la Dunia baada ya kushinda mechi mbili za kwanza dhidi ya Cape Verde na Mauritius kwa matokeo sanjari ya mabao 2-0 na 3-0 na inataka kumaliza hatua hiyo bila ya kupoteza mchezo.

MAwaziri wafa ajalini

Lorna Laboso1961 — 2008.
Kipkalya Kones: 1952 — 2008.

Ms Aurelia Langat, a sister-in-law of Assistant minister Lorna Laboso overcome by grief on receiving the news of her death

Prime Minister Raila Odinga consoles the family of Roads Minister Kipkalya Kones at their home in Nairobi, on Tues


NDEGE ndogo ya abiria aina ya Cessna 210 imeanguka nchini Kenya na kusababisha vifo vya watu wanne, akiwemo Waziri wa Barabara Kipkalya Kones na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Lorna Laboso.

Ajali hiyo ambayo ilitokea kilomita 120 (maili 75), Magharibi mwa jiji la Nairobi pia imesababisha kifo cha Ofisa wa Polisi, Kenneth Bett na Rubani Schner Christopher.

Vifo vya mawaziri hao kutoka Chama cha Orange Democratic Movement (ODM), vimefanya hadi sasa chama hicho kupoteza wabunge wanne tangu kufanyika Uchaguzi Mkuu wa Desemba mwaka jana ambao ulifuatiwa na ghasia kabla ya mkataba wa amani kusainiwa Februari 28 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka gazeti la Daily Nation na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) na Shirika la Habari la Uingereza (Reuters), ndege hiyo iliyokuwa na namba 5Y BVE ilianguka katika Wilaya ya Narok.

Taarifa kutoka gazeti la Daily Nation ambazo zilinukuuu duru za vyombo vya usalama nchini humo, zilisema ndege hiyo ilikuwa ikienda Kericho ndipo ajali ilipotokea mnamo saa 9 alasiri jana. Hebu soma cheki East Africa Standard