Friday, February 29, 2008

Mambo sasa shwari Kenya




Rais Mwai Kibaki (kushoto) na Kiongozi Mkuu wa chama cha Upinzani nchini Kenya cha
ODM Raila Odinga(kulia) wakitia saini baada ya kufikia muafaka ambao waziri mkuu wa kenya sasa atatoka chama kikuu cha upinzani nchini humo ambacho ni ODM kinachoongoza na Raila Odinga, Muafaka huo umefikiwa chini ya Mpatanishi wa kimataifa na katibu mkuu mstaafu wa umoja wa mataifa Koffi Annan wa pili kushoto mstari wa nyuma, Rais Jakaya Kikwete wa kwanza mstari wa nyuma kushoto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Africa Union,na Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa kwa kulia mstari wa nyuma..

Wednesday, February 27, 2008

ATC yaingiza nchini ndege mpya

SHIRIKA la ndege nchini (ATC) limeingiza nchini ndege moja kati ya mbili ilizonunua Canada kwa jumla ya dola milioni 16.2. ya kwanza iliyowasili jana ni aina ya Bombadier Dash 8 Q300 yenye kubeba abiria 50. Jumapili itawasili Bombadier Dash 8 Q400 yenye kubeba abiria 74.

Kwa mujibu wa bosi wa ATC, Daudi Mattaka ambaye alianza kushika nafasi hiyo mwezi February mwaka jana, ndege hizo zitaanza na safari za ndani kwenda Kigoma, Tabora, Shinyanga, Zanzibar na Dar na baadaye zitaenda Dodoma, Songea na Sumbawanga.

Mattaka alisema lengo la shirika ni kuwa na ndege 9 zake lenyewe ifikapo mwaka 2012, ikiwa ndege tano kubwa kwa safari za masafa marefu na nne ndogo za masafa ya kati. Hivi sasa shirika lina Boeing 737-200 mbili za kukodi, na inatarajia kukodi zingine mbili mwezi ujao kwa safari za Dubai kupitia Muscat na Afrika Kusini, pamoja na China. Picha ya mdau Muhidin Issa Michuzi.

Jakaya Kikwete yuko Kenya

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Jakaya Kikwete akipokewa na Rais Mwai Kibaki wa Kenya akikaribishwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi jana jioni. JK yupo jijini Nairobi kwa ajili ya mazungumzo ya amani.

Tuesday, February 26, 2008

Wakuu wa vyuo wachimba mkwara

WAKUU wa Vyuo Vikuu vya Umma nchini wamelaani vurugu zilizofanywa na wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na kusababisha kifo cha mwanafunzi mmoja na kuazimia kuwa watakaobainika wafukuzwe, wasiruhusiwa kusoma kwenye chuo chote nchini wala kupewa mkopo na serikali.

Sambamba na hilo, wakuu hao wametaka wanafunzi wote watakaopatikana na hatia ya kuhusika na vurugu hizo wasimamishwe kuendelea na chuo na kutoruhusiwa kuendelea na masomo katika chuo chochote cha umma nchini, pamoja na kutolewa katika mpango wa serikali wa kuwakopesha wanafunzi wa vyuo vikuu nchini.

Vurugu hizo zilizofanyika Ijumaa usiku pamoja na mambo mengine wanafunzi hao sehemu ya Mlimani, walivamia nyumba ya Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala, na kuvunja geti wakishinikiza wapatiwe maji.

Soma hapa kupata habari ya kinailiyoandikwa na Tausi Mbowe wa Mwananchi http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=4696

Mtanzania Osama bin London anaswa kwa ugaidi

By Duncan Gardham, Security Correspondent

The missed opportunities in relation to the July 21 bombers can be disclosed today following the conviction of one of the most senior terrorist recruiters in Britain - a man who called himself "Osama bin London".

'Osama bin London's' years of terror training
Mohammed Hamid 'is evil personified'
Cameron: Sharia law 'would undermine British society'

Street preacher Mohammed Hamid - who once told young Muslims the 52 deaths in the July 7 attacks on London were "not even breakfast to me" - groomed the would-be suicide bombers under the noses of watching police, security services and even the BBC.

Hamid, 50, who is believed to have met senior al-Qa'eda figures in Afghanistan, organised a series of training camps in the New Forest, the Lake District, and Scotland and paintballing sessions in Berkshire and Kent to train his followers.

Unaweza kuisoma kwa kina hapa http://www.telegraph.co.uk/news/main.jhtml?xml=/news/2008/02/26/nterror526.xml

TRL yakodisha injini tisa za treni


Na Jackson Odoyo wa Mwananchi

KAMPUNI ya Reli Nchini (TRL) imeingiza injini tisa za gari moshi za kukodi kutoka India.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Narasimhaswami Jayaram alisema injini hizo si mpya bali wamezikodisha kutoka katika kampuni ya reli ya nchi hiyo na zimetumika miaka kumi iliyopita.

Jayaram alisema TRL inalipa kiasi cha dola za Marekani milioni 60 kwa mwaka kwa kukodisha injini hizo ili iweze kutekeleza malengo yake.

“Injini hizo siyo mpya ila ziko katika hali nzuri na bado zitaweza kutumika kwa kipindi kirefu na ni kubwa mara mbili zaidi ya zilizopo."

Hata hivyo alisema kwamba kuwasili kwa injini hizo zitaiwezesha shirika hilo kurahisisha safari za Kanda ya Ziwa inyaounganisha mikoa ya Mwanza na Kigoma.

“Injini hizo ziliwasili nchini tangu Januari 23 mwaka huu na leo zinashushwa kutoka kwenye meli na baada ya kushushwa zitapelekwa moja kwa moja katika karakana ya Morogoro kabla hazijaanza kazi kwa ukaguzi wa kiufundi,” alibainisha. (Picha ya Deus Mhagale)

Mazungumzo Kenya yasimama

MSIMAMIZI Mkuu wa mazungumzo ya pande mbili zinazovutana nchini Kenya, Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan amesimisha mazungumzo ya kutafuta amani.

Akizungumza na vyombo vya habari jana katika Hoteli ya Serena, jijini Nairobi alisema kamati yake imeamua kusimamisha mazungumzo hayo ili kujikita zaidi katika mashauriano na kila upande kwa kina, baada ya kuona hatua ya sasa haizai matunda.

Annan alisema kinachoonekana kwa sasa Kamati hiyo ya usuluhishi inahitaji kukutana na wakuu wa pande hizo mbilI, Rais Mwai Kibaki na Raila Odinga wa ODM kuliko kuendelea kuzungumza na wawakilishi wao, ambao mara kwa mara wamekuwa wakibadilika.

Alisema kwamba mazungumzo hayakusimamishwa bali wanatafuta njia muafaka zaidi, ambayo itakuwa ya kudumu.

"Bado hatujakata tamaa, tunachokitafuta ni suluhu ya kudumu kuliko ilivyo sasa," alisema.

Monday, February 25, 2008

Matokeo rasmi ya uchaguzi wa Kiteto

HABARI zilizotufikia hvi punde zinaeleza kwamba Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kiteto, Benedict Nangoro ameibuka mshindi baada ya kuzoa kura nyingi katika uchaguzi ulofanyika juzi na kura kuanza kuhesabiwa juzi hiyo hiyo hadi jana mchana.

Akitangaza matokeo ya Uchaguzi huo jana jioni, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo, Festo Kang'ombe alisema kuwa Nangoro ambaye ni mgombea wa CCM ameibuka mshindi kwa kupata kura 21,506, wakati mgombea wa Chadema, Victor Kimesera alipata kura 12,561, mgombea wa Sauti ya Umma (Sau) Mashaka Fundi alipata kura 300 na mgombea wa PPT-Maendeleo, Juma Saini aliambulia kura 110.





Kang'ombe alisema kwamba idadi ya watu waliojiandikisha ni 74, 626, lakini waliokwenda kupiga kura ni 35, 261, idadi ambayo karibu ya nusu hawakwenda kupiga kura.

Hawa jamaa hawakuamini kabisa nini kimetokea (Picha zote za Mpoki Bukuku)

CCM yanyakua Kiteto

Matokeo ya awali ya Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Kiteto mkoani Manyarayanaonyesha kuwa mgombea bunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Benedict Ole Nangoro ameshinda.

Habari za uhakika zilizokusanywa na gazeti la Tanzania Daima jana usiku baada ya kura kuhesabiwa katika kata zote 15 (ukiacha maeneo machache ambayo alikuwa hajakamilika) yalikuwa yakionyesha kuwa, Nangoro alikuwa amevuna takribani kura 15,000 dhidi ya 11,000 alizokuwa amepata mshindani wake mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Victor Kimesera.

Habari zaidi ambazo Tanzania Daima ilikuwa imezipata majira ya saa 5:00 usiku wa kuamkia leo zilikuwav zikionyesha kuwa Nangoro alikuwa ameshinda katika takribani kata 11 kati ya kata zote 15 zilizokwishakusabiwa huku mpinzani wake akishinda katika kata nne tu.

Sunday, February 24, 2008

Matokeo ya Kiteto njiani

Kwa mujibu wa habari tumlizozipata hivi punde Matokeo ya jimbo la uchaguzi Kiteto yameanza kutoka ambapo CCM inagaragazwa ile mbaya, kwa kuanzia tu katika vituo kadhaa Chadema iko juu, huko Kibaya na kwingineko any way tusubiri tutakuwa tukiwaleteeni matokeo stay tuned


Jamaaa wakiwa wamejirundika katika lorri



Wananchi wakijipanga kwenda kupiga foleni leo asubuhi

Hawa wanapiga kura katika kituo

Wengine hawa waliamua kuleta vurugu tuuu lakini lilizimwa

Leo ni Leo Kiteto


Tambwe Hizza akifanya mambo

Wana mgambo wakiwa tayari kudhibiti vurugu.

FFU wamemwagwa kibao jimboni Kiteto, sijui CCM wanahofia nini??

Kapteni Komba akishuka katika helikopta waliyoikodi kutoka Kenya.



Eti CCM walisema matumizi ya Helikopta ni ufisadi sasa leo imekuwaje wanatumia helikopta maji yamefika shingoni nini???

Friday, February 22, 2008

Lowassa kuwasha moto Monduli

WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, Edward Lowassa kesho anatarajiwa kurejea jimboni kwake Monduli ambako atahutubia wapiga kura wake na kuwaeleza hali iliyosababisha akachukua uamuzi wa kujiuzulu.

Kwa mujibu wa habari kutoka kwa viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa wilaya ya Monduli Lowassa anatarajiwa kuwasili katika uwanja wa ndege wa Arusha uliopo Kisongo saa tatu asubuhi.

Mara baada ya kutua muda huo katika uwanja huo na kupokewa na vikundi vya ngoma, msafara wa magari ya waliokuja kumpokea utakwenda katika jimbo lake.

Habari kutoka katika vikao vya chama wilayani Monduli zilisema kuwa uamuzi wa kumpokea Lowassa ambaye ni mbunge wa jimbo hilo kwa zaidi ya miaka 15 uliamuriwa katika vikao hivyo na mbunge huyo kujulishwa na siyo uamuzi wake.

“Sisi ndio tulioamua katika vikao kumpokea kwa maandamano ya magari na hata kwa miguu kwani amefanya uamuzi wa kidemkrasia ambao ni viongozi wachache tu wa kiafrika wenye moyo huo,’’ alisema kiongozi mmoja wa CCM.

Inaaminika Lowassa atatumia muda wa wiki nzima kufanya mikutano ya hadhara katika jimbo hilo kuelezea mstakabali mzima kwa wapiga kura wake ambao wengi wao bado hawajafahamu kilichofanya achukue uamuzi wa kujiuzulu Uwaziri mkuu.

Katibu wa CCM wa wilaya ya Monduli Allan Kingazi hakuweza kupatikana kuelezea hali halisi ya mapokezi hayo.

mambo ya Kiteto


Mwenyekiti wa Chadema akihutubia mkutanoi mjini Kiteto leo.

Kapteni Komba aliyesshushwa jukwaani baada ya kudaiwa kuvamia mkutano wa Chadema.

Mbowe akishuhudia Helikopta ya Chadema iliyoujumiwa na kushindwakuruka toka Dodoma (Picha kwa hisani ya Chadema)

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimekodi helikopta itakayokisaidia kupambana na ile ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo katika kampeni za uchaguzi wa jimbo la Kiteto unaotarajiwa kufanyika kesho.

Helikopta hiyo iliyokodiwa kutoka Kenya , iliwasili kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro, majira ya saa 3:20 asubuhi na kuanza kazi ya kupiga kampeni katika maeneo ya vijiji takribani vyote vilivyopitiwa na helikopta ya Chadema Juzi.

Mpaka jioni ya juzi taarifa zinaeleza kwamba CCM ilikuwa haijawasilisha baria ya maombi ya vibali kadhaa vikiwamo vya usjili, leseni ya Kapteni, mkataba wa kukodisha, kibali cha jeshi na maliasili, ingawa inaelezwa kwamba vibali hivyo vilitolewa uwanja wa ndege wakati ndege ikiwa imeshawasili.

Wednesday, February 20, 2008

Dingi kakabidhi ofisi kimya kimya

Duhhh sisi tumestukia picha tu zinatufikia kwamba Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa anamkabidhi ofisi kimya kimya Waziri Mkuu mpya, Mizengo Pinda tunajiuliza Whyyyy ??? Kwanini??? mbona haya mbambo yanakuwa hivi ??? Picha ni ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Kalonzo aja Bongo

Musyoka: Usuluhishi Kenya umefikia hatua nzuri

Na Mwandishi Wetu

MAKAMU wa Rais wa Kenya Kalonzo Musyoka amesema pande mbili katika mgogoro wa kisiasa nchini Kenya zimefikia hatua nzuri ya kuelekea kupata ufumbuzi kamili wa mgogoro huo.

“Hata jana (juzi)Rais Kibaki alikukutana na Koffi Annan na kujaribu kumwarifu vile hali ilivyo ya mazungumzo, kwa sasa hatujafikia maelewano ya mwisho mwisho, lakini hatua kabambe kusema kweli zimefanyika,” alieleza

Musyoka aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam akitokea Nairobi, Kenya ambapo alipokelewa uwanjani hapo na Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein.

Musyoka yuko nchini kwa ziara ya siku mbili kwa ajili ya kuleta ujumbe maalum kwa Rais Jakaya Kikwete kutoka kwa Rais Mwai Kibaki wa Kenya .

“Ujumbe ninao kutoka kwa Rais Kibaki wa Jamhuri ya Kenya kwa rafiki yetu, rafiki yake Jakaya Kikwete na huku tukileta pongezi nyingi sana tukijua kwamba kitendo ambacho kimetokea Kenya kimewakera sana ndugu zao Watanzania,” alidokeza. (Taarifa hii ya Ofisi ya Makamu wa Rais)

Tuesday, February 19, 2008

Rais Bush awasili Rwanda

Jamaa keshafika Rwanda hapa akipokewa na kikundi cha ngoma jijini Kigali,

Karibu Rwanda ndivyo asemavyo Jenerali Paul Kagame

Joji Kichaka aondoka nchini

Eeee Bwana kazi ilikuwa ngmu si mchezo, sasa twaweza kupumua kidogo maana geni mzito ule , ndivyo wanavyoonekana kusema viongozi hawa wa Tanzania.
Msafara wa Bush ukiingia uwanjani kupitia kambi ya Jeshi la anga sijui ni sababu za kiusalama ama utaratibu wa kisasa, tuliozoea tunajua viongozi huingilia geti la mashariki.

Benzi ya Ikulu yetu wamo si mchezo

Dege la Rais Bush wa Marekani likipaa kuelekea Rwanda hiyo ilikuwa mitaa ya saa mbili kasrobo leo hii.


Kwaherini Watanzania, tumeuona ukarimu wenu, ndivyo wanavyoonekana wakisema mama na baba Bush baada ya kusaini mikataba na serikali yetu, yailahi sijui kama kuna usalama, Wamarekani hawana rafiki wa kudumu.


Gari aina ya Cardillac ambalo amelitumia Rais wa Dunia wakati wote akiwamo nchini mpaka anaondoka, si mchezo nadhani ndo hilo atalitumia Rwanda.



Msafara wa rais Joji Kichaka ukiwa unaingia uwanja wa zamani wa ndege ambao kwa uhakika ndo hutumika mahss kwa vingozi.





Monday, February 18, 2008

Hospitali ya Mount Meru







Rais Geoge Bush wa marekani akiwa akiwa amemshika mama mjamzito baada ya kumkabidhi chandarua kwa ajili ya kujikinga na mbuu muda mfupi uliyopita alipotembelea hospitali ya wilaya ya Meru mkoani arusha , kushoto kwake ni Dr Aziz Msuya wa hospitali hiyo.


Ziara ya Bush

Dinner Ikulu jana..













Shughuli ya utiaji saini Ikulu asubuhi


Hahaahahahaaaa ndivyo wanavyoonekana wanajeshi hawa wawili wa zamani wakicheka kwa pamoja.
Jamaaa kafuraaaahi kinoma huenda hakuwahi kupata generosity ya aina hii ya watu kuacha kazi na kisha kumpokea yeyetu.
Hii furaha ya hawa Marais inaashiria mambo fulani makubwa ambayo bila shaka hatuyajui na hatutayajua mpaka yatakapofunuliwa, haiwezekani Marekani ikawa rafiki ghafla, hawanarafiki hawa jamaa anyway we just wait and see.


Kama vile anamuambia ebwaana mambo vipi, unaonekana uko fiti Kanali, mwenzio mimi nilikimbia jeshi kule Marekani, vipi wwewe unaendelea.

Makamanda wawili wa jeshi wakiwa wanatoa speech hawa jamaa, nadhani wanapatana sababu ya ujeshi, nani kamanda mkubwa kuliko mwingine kati yao.


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bi Condoreza Rice akiwasalimia wananchi alipoingia Ikulu Dar jana. Alikuwa na mvuto wa kipekee sijui kwakuwa ni bomba ama kw akuw ani black?

Askari wa Marekani akipita na mbwa ili kuhakikisha kuwa maeneo hayo ni salama kwa wazee kuingia.









Mama Bush na mama Kikwete







Pichaa za juu ni Rais George Bush wa Marekani wakitia saini msaada mkubwa wa $ 700 Million kutoka serikali ya Marekani , Mkataba huo umekusudia kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa barabara tatu ambazo ni barabara ya Tunduma hadi Sumbawanga,Tunduru Songea hadi Mbambabay na barabara ya Horohoro hadi Tanga na pia msaada huo mradi wa umeme katika mkoa wa Kigoma, mara baada ya kutia saini mlataba huo Rais Bush na Rais Kikwete walitembelea hospitali ya Amana iliyopo wilayani Ilala imepata mafanikio makubwa katika mradi wa mapambano dhidi ya Ukimwi ambap pia umedhaminiwa na serikali ya Marekani.









Rais Bush anatarajia kwenda mkoani Arusha na kufanya shughuli ambako atalala na kurejea Dar es Salaam siku inayofuata na kuhitimisha Ziara yake nchini Tanzania na kuelekea Kigali nchini Rwanda.
(Picha Mpoki Bukuku na Reuters)