Thursday, August 30, 2007

Uwanja wa Taifa




mechi itapigwa hapa

Sh 3,000 ya zamani, sasa ghorofani

MASHABIKI watakaotaka kuona mechi ya kirafiki baina ya Tanzania na Uganda kesho wametakiwa kuwa makini wakati wa kukata tiketi ili kujua maeneo wanayotaka kukaa na nambari za viti, huku wakikumbushwa kuwa wale waliokuwa wakilipia Sh 3,000 na kusota juani, sasa wataona mechi wakiwa juu ghorofani.
Mkurugenzi wa michezo, Henry Ramadhan aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa uwanja mpya, ambao unajulikana kwa muda kama Uwanja Mkuu wa Taifa wa Tanzania, umejengwa kwa njia ambayo itatoa nafasi kwa kila mtu kuona michezo vizuri kulingana na kiasi atakacholipia.
"Kama kule (uwanja wa zamani) mtu alikuwa anasimama wakati wote wa mchezo na kupigwa na jua, kwenye uwanja mpya atakaa ghorofani sehemu ya juu kabisa na hatadhurika na jua wala mvua," alisema mkurugenzi wa michezo, Henry Ramadhan wakati akiwaonyesha wahariri wa michezo utaratibu wa kuingia uwanjani hapo jana.
"Tena ajabu ni kwamba yule atakayelipia Sh 3,000 na kukaa juu kwenye viti vya kijani, karibu na eneo la VIP, ataona mpira vizuri kabisa sawa na yule aliyelipia Sh 30,000.
"Sasa hapa tuwape nini. Huyu wa 3,000 ni sawa kabisa na yule wa Jukwaa la Kijani la Uwanja wa Taifa. Hawa watakaolipia Sh 3,000 ni theluthi moja ya mashabiki wote watakaoingia uwanjani.
"Lakini naomba muwaambie kuwa wale wenye mshawasha wa kushangilia, basi wachague sehemu ya upinde (iliyo nyuma ya maeneo ya goli yenye viti vya rangi ya machungwa) kwa kuwa huko ndiko hasa kwa washangiliaji, hata vikundi vya ngoma vitakuwa huko."
Ramadhan aliwataka mashabiki kuwa makini kununua tiketi kulingana na sehemu wanazotaka kukaa na kuzisoma vizuri kujua milango watakayoingilia, akibainisha kuwa wale watakaoingia kupitia lango kuu ni wale tu ambao watakuwa na tiketi za VIP.
"Wale watakaokuwa hawaelewi vizuri, au wataenda sehemu ambazo si zao, watakutana na watu ambao wamepangwa kuwaelekeza," alisema. "Naomba tu wawe wastaarabu wakati watakapoelekezwa la sivyo watasaidiwa na wanausalama watakaokuwepo."

Mechi ya Taifa Stars/ Uganda hapa



cheki uwanja unavyoonekana kwa sasa.

Monday, August 27, 2007

Mwalimu na mwanafunzi



mwalimu akimfundisha mtoto wa madrasa hapa ni Bweleo Zanzibar

Neptune



Utunzaji wa mazingira ni kitu kimoja na uwekezaji ni kitu kingine hebu cheki hapa hoteli Neptune Zanzibar wanavyofanya mambo

Mazingira hayo unayapata wapi?



Utunzaji wa mazingira ni kitu kimoja na uwekezaji ni kitu kingine hebu cheki hapa hoteli Neptune Zanzibar wanavyofanya mambo

Tuesday, August 21, 2007

Zee la Nyeti ndani ya nyumba

Kwa hakika mnaweza kusema sasa pele limepata mkunaji, maana kaingia ndani ya nyumba mzee mwenyewe machachari, kama mnamkumbuka huyu jamaa mkongwe katika fani hii tangu enzi za Kasheshe, amekuwa akijiita Zee la Nyeti sasa kaingia kwenye kijiji chetu kwa hakika sasa waweza kumpata kupitia hapa au unaweza kumcheki Mdimu

Afrika Mashariki sarafu moja 2012



MARAIS wa nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) jana walikubaliana kuwa na sarafu moja na soko la pamoja kwa nchi za jumuiya hiyo ifikapo mwaka 2012.

Sambamba na uamuzi huo marais hao pia wamesogeza mbele uamuzi wa uharakishwaji wa kuanzishwa kwa Shirikisho la Afrika ya Mashariki.

Akisoma taarifa ya pamoja ya Marais hao mara baada ya kumalizika kwa mkutano wao katika Hoteli ya Ngurdoto jana, Katibu Mkuu EAC, Balozi Juma Mwapachu alisema wakuu hao wamefikia maamuzi hayo kutokana na maoni yaliyotolewa na wananchi wa nchi hizo na pia kuingizwa kwa Rwanda na Burundi kwenye jumuiya hiyo. Bonyeza hapa usome habari hii kwa kina katika gazeti letu la Mwananchi

Monday, August 20, 2007

Nani kasema kwamba nyinyi wasafi?

WAVUJA Jasho bwana tuna staili zetu za maisha tofauti kabisa na nyinyi mnaojifanya mna uwezo mkubwa wa maisha, nasema mnajifanya mna uwezo mkubwa wa maisha sababu mnatudhulumu kile ambacho na sisi tulistahili kuwa nacho.

Ingekuwa ni halali yenu basi nasi tusingekuwa na budi kukubali na kuwasifieni kwa hicho mlicho nacho, japo kuna wachache mno wenye halali, lakini kwa mtizamo wetu wavuja jasho, tunajua hicho mlicho nacho aidha mmekiiba au kukidhulumu kutoka kwetu bila ya sisi kujua.

Ndiyo maana maisha yetu ni magumu yataendelea kuwa magumu kwasababu hata wanaojidai kuwa wana lengo la kutusaidia wanafanya hivyo ili kusudi wapate wingi wetu ili wakaombee misaada.Bonyeza hapa

Saturday, August 18, 2007

Zitto Kabwe atikisa Dar





MAELFU ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam leo walijitokeza katika mapokezi na maandamano ya kumpokea Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) Zitto Kabwe, (pichani) aliyesimamishwa ubunge hadi Januari mwakani.

Maandamano hayo, ambayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka kambi ya upinzani, yalianzia eneo la Ubungo, baada ya Zitto Kabwe kuwasili akitokea mjini Dodoma. Maandamano hayo yalipitia Barabara ya Morogoro na kuishia katika viwanja vya Jangwani ambako Kabwe alihutubia wananchi na kufafanua juu ya kile kilichotokea bungeni baada ya kuwasilisha hoja yake binafsi na baadaye kusimamishwa.

Katika hotuba yake kwa wananchi hao waliokusanyika Jangwani, Kabwe alisema iwapo mkataba wa madini wa mradi wa Buzwagi ungesainiwa nchini Uingereza ndani ya ubalozi wa Tanzania nchini humo, kusingekuwepo na tatizo. Picha hii ni ya Mpoki Bukuku.

RICHARD BEZUIDENHOUT AKIWA HOME



Hapa Mwakilishi wetu Richard akimlisha dadake keki huku mkewe akishuhudia


Richard mwenyewe akiwa katika pozi la kawaida tuu


Richard akuwa na dadake

Katika harakati za harusi yake yuko na dadake pamoja na babake.

Bonyeza hapa utaona mapicha kibao ya familia yao yeye pamoja na dada na babake.

Thursday, August 16, 2007

Mtukufu Aga Khan




KIONGOZI wa kidini wa Jumuiya ya Ismailia duniani Imam Aga Khan ameleezea nia yake ya kutaka kujenga Chuo kikuu kipya hapa nchini.

Akizungumza na Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein jana Ikulu Jijini Dar es Salaam Imam Aga Khan alisema chuo hicho kitajengwa mkoani Arusha na kwamba kitakuwa cha aina yake katika Afrika kutokana na kuhusisha masomo ya taaluma muhimu pekee.

Mara baada ya ndege aina ya LX-PAK kutua katika viwanja hivyo kwenye saa 12:30 mlango ulifunguliwa na kisha kiongozi mwakilishi wa Mtandao wa Maendeleo ya Aga Khan aliingia ndani ya ndege hiyo kwa ajili ya kumuongoza Aga Khan aweze kushuka.

Mara baada ya kushuka, Aga Khan alipokelewa na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya ndani, Joseph Mungai.

Kisha wimbo maalumu wa jumuiya yao ulipigwa na Brass Bendi ya polisi na baada ya wimbo huo kiongozi huyo alipata fursa ya kuangalia ngoma ya asili yao, sarakasi pamoja na ngoma ya kimasai iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili yake.

Akizungumza mara baada ya mapokezi hayo, Mungai alisema ujio wa kiongozi huyo ni kwa ajili ya kusherehekea miaka 50 ya uimamu wake katika madhehebu ya kiismailia.

Mungai alisema, Aga Khan ameweza kuwa na ushirikiano mkubwa katika nyanja ya kimaendeleo hususani kwenye sekta ya Eimu na Tiba.

“Nataka niwahakikishieni kuwa katika hili la Elimu, shule ya kwanza ya wasichana iliyoko kule Zanzibar ilianzishwe na babu yake huyu Aga Khan, pia anaendelea na juhudi kubwa za kuendeleza Elimu katika taifa letu,” alisema Mungai. Mdau Mpoki Bukuku alikuwako huko na picha hii ni kwa hisani yake.

Mafisi



Oparesheni inayofanywa na magari haya ni ya kawaida mno katikati ya jiji la Dar es Salaam. Magari haya maarufu kama mafisi yanasifika kwa ubovu na uchafu na taka usitake yatakuwapo waliyapiga marufuku lakini wapi, hebu tafakari mgari huu wa gharama namna hii unaburutwa na gari la Sh 800,000.

Wednesday, August 15, 2007

Timu ya Muafaka



Hawa ndiyo mainjinia wa siasa ya muafaka tunaowategemea kutoka katika vyama vya siasa vya CUF na CCM. Bila shaka watafikia muafaka kama muheshimiwa Rais wetu anavyojitahidi kuhakikisha iwe.

Zitto Kabwe



Wachimbaji wadogo wa mgodi wa Mererani wametoa ahadi ya kumlipa mshahara na marupu rupu ya kipindi chote atakachokuwa amefungiwa wakati huo huo chama cha demokrasia na maendeleo Chadema leo mchana kimetoa tamko kupinga kufungiwa kwa mbunge wake Zitto Kabwe kwa madai ya kukiuka kanuni za bunge kufuatia hoja yake binafsi kuhusu kusainiwa mkataba wa madini na Waziri Karamagi huko ughaibuni hivi karibuni.



Zitto mwenyewe amesema hakubali anakata rufaa, yapo mengi ya kujiuliza kabla ya kuchukua maamuzi kama haya. Moja kwanini Kabwe adanganye, na kama kweli kadanganya kwa maslahi ya nani, na kama Waziri ni mkweli kwanini anaogopa kuchunguzwa. Hivi Polisi halali wakija kwako na vibali halali wakasema ndani mwako kuna mali za wizi na wewe ukaamini kweli hakuna mali za wizi kwanini usikubali kukaguliwa ili usichafuliwe? Tujadili

Tuesday, August 14, 2007

Mutoto wa Moro



Sijui hii ni ajira mbaya kwa watoto au ni mtoto anajitahidi kujikimu, tafsiri ya hii term ajira kwa watoto inanisumbua mno. Mtoto huyu alikutwa Moro na Mdau Ashton Balaigwa akidunda mzigo kwa kwenda mbele.

Monday, August 13, 2007

Kilwa Kivinje



Tunazo sehemu nyingi sana za kujivunia hapa klwetu bongo mathalani magofu haya ya Kilwa Kivinje ambayo mdau Hussein Issa alikuwako huko na kuyaona, yanasemekana yalikuwako katika karne ya 15.

Sunday, August 12, 2007

Mambo ya Lindi hayo



Barabara ya Lindi mjini kuelekea Mtwara ikiwa katika final touches, mambo huku ni mswano, Mdau Hussein Issa alikuwako na ana habari chungu mzima mtafute.

Mapango ya Kilwa




Historia ni jambo muhimu mno pichani unaweza kuyaona magofu yaliyopo huko Kilwa ni kivutio muhimu cha utalii.

Wafanyakazi wamtikisa JK wampa siku 30





Katika kuonyesha kweli wamekereka na ahadi wanazodai hazitekelezeki wafanyakazi mkoani Dar es Salaam, wamempa siku 30 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Tucta), Nestory Ngulla, kufikisha malalamiko yao kwa Rais Jakaya Kikwete na kurejeshewa majibu, kuhusu nyongeza duni ya mishahara, ili kuepusha hatua nyingine watakazotumia kudai mishahara.

Tamko hilo lilitolewa na wafanyakazi hao kupitia risala yao iliyosomwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam baada ya kuhitimisha maandamano ya amani yaliyoandaliwa na vyama 18 vya wafanyakazi nchini kupinga kima cha chini cha mshahara wa serikali, kilichopitishwa na bunge hivi karibuni.

Baadhi ya vyama hivyo, ni pamoja na cha Walimu (CWT), Sekta ya Afya (Tughe), Migodi, Nishati, Ujenzi (Tamico), Serikali za Mitaa (Talgwu), Mabaharia (Tasu), Walinzi binafsi (Tupse), Mashambani (Tpawu), Shughuli za Meli (Dowuta), Mawasiliano (Tewuta), Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti (Raawu), Waandishi wa Habari (TUJ) na Chodawu. Picha ya Mpoki Bukuku

Wapiga debe



Pichani jamaa anaonekana akiendelea na shughuli yake ya kupiga debe, shuguli ambayo imepigwa marufuku kwa muda sasa, lakini bado ipo, tujiulize hivi wanaosababisha hawa jamaa kuwapo ni kina nani?

Muzeee



Babu ameishi maisha yake hadi kafika umri huu, amepitia magumu machungu na kila liwalo, kazi kwetu vijana hii ni kama ndoto vile bila shaka baada ya miaka 10 ijayo mtu mwenye miaka 33 ndo ataonekana babu.

JIJI LA DODOMA?????



Imekuwa kama ndoto vile kila siku, wanasiasa wanadai watahamia Dodoma, wakahamishia bunge, baadhi ya wizara, miundombinu, taasisi na hali kadhalika, lakini haiwi, hebu cheki huu ni mojawapo ya ujenzi mpya unaofanywa na serikali jijini humo nyumba hizi zimetimilika na zinatarajiwa kutumika na wananchi wote. Picha hii ni ya Mpoki Bukuku

Tuesday, August 07, 2007

Mshiriki wa Tanzania ana aibu

Kila suala analoulizwa jibu ni my wife, my wife, my wife, hawezi kujibu swali bila ya kumtaja mkewe... kama vile ni wa kwanza kuoa duniani, mdau Masaki kaligusia hili.

Suala hili linamfanya aanze kuonekana kama mtu anayeboa kuliko wote ndani ya nyumba, hata Watanzania nadhani wanaweza kuchoshwa na hali hii inabidi abadilike. Anatajwa mara chache mno na umaarufu wake miongoni mwa wenzie uko chini.

Katika siku yao ya pili, alfajiri mameti wa jumba la Big Brother wanaonekana kuondokewa na ujasiri waliokuwa nao siku ya jana walipokuwa wakiingia ndani ya jumba hilo, sababu Big Brother tayari keshawapiga mkwara mzito.

Wakati wa kuoga asubuhi ya leo kuna mambo kadhaa yalichomoza kuhusiana na joto la maji ya kuoga. Mameti wanagundua haraka kwamba kuna ujanja alioucheza Big Brother.

Meryl kwa mara nyingine tena anafanya kituko anavua nguo na kubakia mtupu, katika tukio hilo anafuatiwa na Tatiana, ambaye anaonekana kujawa na aibu tele kuonyesha mwili wake.

Pamoja na kuinyesha utundu na mara kadhaa kuwa karibu sana na wanaume,
, Lerato anaamua kuoga na nguo yake. Inawezekana hii ni mbinu yake ya kuwatia kiu mashabiki wake ili kusudi wawe na uchu wa kuona mwili wake.

Monday, August 06, 2007

Mshiriki wa Big Brother 2 mtanzania huyu hapa



Kama akishinda donge nono la dola za Marekani 100 000, Mtanzania, Richard Buzidenhout anasema atazitumia kununua vifaa vya kupigia picha za filamu . Mwakilishi huyo wa Big Brother kutoka Tanzania, mwenye umri wa miaka 24 na mwanafunzi wa fani ya filamu ana matarajio makubwa ya kuwa mtaalamu mahiri katika fani ya filamu na binafsi anamhusudu sana mtengenezaji filamu, Peter Jackson kwa umahiri wake.

Richard ambaye ni mshiriki pekee wa shindano hilo aliyeoa anasema kuwa anatamani sana kutembelea nyumbani kwao mkewe huko nchini Canada katika mji wa Brandon uliopo katika jimbo la Manitoba, Canada kushuhudia sehemu aliyokulia mkewe.

Anajielezea kama mtu anayependa mzaha, na kwamba ni mgumu sana kukasirishwa, lakini anasema tabia yake moja inayokera ni usumbufu na kelele nyakati za alfajiri, kabla wengi hawajaamka.

Anapanga kushinda Shindano hilo la Big Brother Africa 2 bila kushusha hadhi yake. Anapenda mazingira asili ya Afrika Mashariki, anasema kitu kinachomvutia zaidi ni kuendesha gari kupitia kreta ya Ngorogoro huku akishuhudia wanyama pori mbalimbali. 

Pia anasema eneo analolihusudu kulitembelea ni Serengeti na maeneo ya Pwani hasa Zanzibar.

Tafadhalini Watanzania tumpigieni kura Richard ili aweze kushinda kitita na hatimaye kupandisha chati Tanzania kimataifa.

Bonyeza hapa au Bonyeza hapa

Ukitaka kumuona cheki Richard hebu Bonyeza hapa

wengine wanaoshiriki Big Brother Africa ni hawa



Bertha Miaka: 28 Nchi: Zimbabwe Mji anaotoka: Harare Kazi: Mwanasheria/mshauri wa Uhusiano na mawasiliano.



Code Sangala Miaka: 31 Nchi: Mali Mji anaotoka: Blantyre Kazi: Mtangazaji/ DJ



Jina Jeff Miaka: 23 Nchi: Kenya Mji anaotoka: Kisumu Kazi: mtunzi wa vitabu, mshauri na mjasiliamali



Justice Motlhabani Miaka: 23 Nchi: Botswana Mji anaotoka: Serowe Kazi: Mwandishi wa kujitegemea/Mwanafunzi




Kwaku Miaka: 30 Nchi: Ghana mji anaotoka: Kumawu Kazi: Mjasiliamali.



Lerato Miaka: 23 Nchi: Afrika Kusini Mji anaotoka: Soweto Kazi: Mratibu wa matukio



Maureen Miaka: 27 Nchi: Uganda Mji anaotoka: Entebbe Kazi: Mbunifu wa mitindo




Maxwell Miaka: 26 Nchi: Zambia Mji anaotoka: Lusaka Kazi: Opareta wa simu



Meryl Miaka: 21 Nchi: Namibia Mji anaotoka: Windhoek Kazi: Mhudumu wa Mapokezi



Ofunnekama Miaka: 29 Nchi: Nigeria Mji anaotoka: Lagos Kazi: Katibu Muhtasi.



Tatiana Miaka: 26 Nchi: Angola Mji anaotoka: Luanda Kazi: Msanii/mwanamitindo

 

Sunday, August 05, 2007

Olga Zarubina awa Miss Tourism Queen International 2007

Unaweza usiwe unajua jina hili Olga Zarubina. Hata unapotafuta katika injini ya kusaka ya Google, hupati kitu kinachomuhusu Olga Zarubina. Lakini huyu ndiye amekuwa mshindi wa taji la Miss Tourism Queen International 2007 lililokuwa likiwaniwa huku nchini China. Ingawa hata unapotafuta katika tovuti rasmi ya Miss Tourism Queen International bado halijapachikwa tangazo rasmi. Hata hivyo, habari hizi zipo katika tovuti ya Global Beauties ambayo ni chanzo mahsusi cha masuala ya urembo.



Kwa maana hiyo Mrembo wetu Sophia Kapama kaambulia patupu, lakini si mbaya amejitahidi saana dada yetu tumpongeze.

Hebu cheki hapa.

Bonyeza hapa au hapaupate taarifa kwa kina zaidi. Utakuta mambo kama haya. Good thing is that by the time, I was writing this entry, I found the official announcement about winner of Miss Tourism Queen International 2007 in its official website.


In the official website of Miss Tourism Queen International, I could find that Olga Zarubina is 24 years old and her height is 1.78 meter. So, you can imagine that she is very tall. Well, I don’t think that she is beautiful but my opinion does not matter. The funniest thing is that there is absolutely no information about Olga Zarubina except that she is a model. I wonder what kind of model she is!


The picture that I have given her has been taken from the official website of Miss Tourism Queen International 2007.



If you want to see Olga Zarubina’s picture then you should visit the following entry:


Miss Russia is Miss Tourism Queen International 2007!

Wednesday, August 01, 2007

Mlima Oldonyo Lengai unavyoonekana sasa



Siku chache zilizopita kulikuwa na hofu kuu ya kuibuka kwa tetemeko katika Mlima wa Mungu maarufu kama Oldonyo Lengai, hebu jionee mandhari. Picha hii ni ya Mussa Juma.

Mama anafikiria nini?



Mwana Mama akiwa amekalia mzigo wake wa Makabichi katika kituo cha basi cha Clinic barabara la Makongoro jijini Mwanza jana. Abiria wengi wanalalamikia kutokuwepo kwa vibanda vya kupumzikia wakati wanasubili usafi na shida kubwa inakuwa kipindi cha mvua. Picha hii imepigwa na Edwin Mjwahuzi